Jumanne, 24 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mtoto Huyu Aliyeungua Anapenda Moto

(Imetafsiriwa)

Habari:

Siku ya Pakistan iliadhimishwa mnamo Jumatano tarehe 23 Machi. Vikosi vya jeshi vilionyesha nguvu zao katika gwaride la kijeshi la kila mwaka jijini Islamabad huku viongozi wakuu walioshiriki katika Kikao cha 48 cha Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) wakitazama kama wageni wa heshima. (Dawn)

Maoni:

Kila mwaka Pakistan huadhimisha Machi 23 kama siku ya Pakistan kwa kutangaza sikukuu. Katika siku hii, vikosi vya jeshi huonyesha ustadi wao, ndege za kivita hutengeneza mawingu ya rangi tofauti angani kwa kutumia pesa tulizochuma kwa bidii. Ijapokuwa, utaalamu huu hujaribiwa vyema zaidi katika uwanja wa vita na kwa kukabiliana na adui, si kwa kuita kundi la marafiki wa OIC na kufurahia mbwembwe za ndege. Upinzani wa kisilaha wa 1857 ulionyesha umoja wa ajabu wa Mabaniani, Waislamu na Makalasinga, na hili liliwatikisa Waingereza. William Russell, mwandishi wa habari wa vita, aliyetumwa na The Times anaandika: “Machifu wote wakuu wa Oudh, Mussalman na Hindu, wako pale, na wameapa kumpigania mfalme wao mchanga, Birjeis Kuddr [sic], hadi mwisho. Usaidizi ni mwingi, jiji limejaa watu, kazi zinaimarishwa daima. Oudh yote iko mikononi mwa adui, na tunashikilia tu ardhi tunayofunika kwa vyembe vyetu." Hatua za haraka zilichukuliwa ili kujenga uadui kati ya Waislamu na Mabaniani. Mara tu baada ya kuangamiza vita hivi vya ukombozi, Rais wa wakati huo wa Bodi ya Udhibiti Sir Charles Wood, akiwa ameketi jijini London, alikiri: "Tumedumisha mamlaka yetu nchini India kwa kuuhujumu upande mmoja dhidi ya mwengine na lazima tuendelee kufanya hivyo." Iliwachukua Waingereza zaidi ya miaka 200 kuwapokonya silaha Waislamu wa India, na kujaribu kuwapa tena silaha kama watumwa na wafanyakazi wao wenyewe. Adui hangeweza kuukamata Umma pasi na usaidizi wa vibaraka wao, wanaojifanya kama Waislamu wenye ushawishi na kupenya ndani ya sababu na kuanzisha mawazo ambayo yangewapotosha watu kutoka kwenye jambo hilo.

Leo, mwaka wa 2022, miaka 82 imepita tangu kupitishwa kwa azimio la Lahore. Azimio hili liliwasilishwa kama tiba ya uchungu mkubwa wa kiakili, hali ya kunyimwa haki na kukata tamaa baada ya Waislamu wa bara hilo kusukumizwa ukutani katika suala la muozo wa kifikra, kisiasa, kiuchumi na kielimu. Azimio hili lilitupeleka kwenye sehemu ndogo ya ardhi, iliyosheheni maiti milioni moja za ndugu na dada zetu Waislamu, na mkusanyo huu wa wafu bado unaendelea. Wakati huo huo wenye nguvu, ambao wamefikia nafasi zao kwa kusimama juu ya vichwa vyetu, wanasherehekea tarehe hizi kama mafanikio kwa kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwenye sherehe hizi ambapo silaha zetu zinawekwa katika maonyesho; ndege za kivita kufanya mbwembwe huku ndugu na dada zetu Waislamu wanyonge wanaohitaji wanajeshi hawa na nguvu hizi wakiendelea kuteseka.

Umefika wakati sasa wa sisi Waislamu kukataa kuongozwa hadi machinjioni na wachinjaji hawa, na tusimame sio tu sisi wenyewe pekee bali kwa ajili ya Ummah mzima. Kelele hizi za sherehe zisizuie kelele za ndugu zetu na dada zetu. Tunatakiwa kujielekeza kwenye lengo tulilopangiwa na Mwenyezi Mungu (swt). Ufalme wa Mbinguni na ardhini ni Wake Yeye. Tunawataka wajinga hawa waasi wenye kiburi kuondoka kwenye nyadhifa walizozinunua kwa kuwatumikia makafiri. Umma wa Kiislamu, chini ya kivuli cha Khilafah Rashida, utayachukulia mambo haya jinsi yanavyostahiki kuchukuliwa. Nguvu zote zitatumika tu katika kumtumikia Wenye uwezo wote. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«مَنْ رَأَى مِنْكُمْ مُنْكَرًا فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِلِسَانِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِقَلْبِهِ، وَذَلِكَ أَضْعَفُ الْإِيمَانِ»

“Yeyote anayeuona uovu basi na auondoe kwa mkono wake, na ikiwa hawezi basi kwa ulimi wake, na ikiwa hawezi basi (achukie) kwa moyo wake, na hiyo ndio imani dhaifu zaidi.” [Muslim]

Kwa Muumini, neno la Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake ndilo linalobeba hazina za ulimwengu  huu na Akhera na Mwenyezi Mungu pamoja na Rehma yake hunyanyua viwango vya waja wake na huwaongoza kwenye yale wanayoyatafuta (yaani radhi za Mwenyezi Mungu (swt)).

Mtume (saw) amesema, «لاَ يُلْدَغُ الْمُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ» “Muumini hang'atwi kutoka kwenye tundu moja mara mbili.”

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu