Mgogoro wa Madeni ya Kenya: Wanasiasa Wanatupiana Lawama huku Wakidanganya Watu kwa Kutofichua Hasa Tatizo Msingi Lililoko (Ubepari)
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kenya inagubikwa na wasiwasi wa kiwango chake cha madeni kufikia shilingi 9.1 trilioni. Sajili ya hivi punde ya deni la Hazina ya Kitaifa inaonyesha deni la taifa lilifikia Sh 8.2 trilioni kufikia Disemba mwaka jana. Jumla ya mkopo wa nje ulikuwa Sh 4.174 trilioni huku mikopo ya kimataifa ikiwa Sh1.782 trilioni, kibiashara Sh1.208 trilioni na baina ya Sh1.17 trilioni. Kenya huenda ikalazimika kukagua kikomo chake cha deni angalau mara mbili katika muda wa miezi 24 ili kuunda nafasi ya kukopa kwa serikali itakayokuja baada ya ile ya Uhuru Kenyatta.