Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Khilafah Itawalinda Wanawake Dhidi ya Ukatili Sio Upitishaji wa Sheria za Kisekula

Habari:

Rais wa Amerika Joe Biden mnamo Jumatano, 9 Februari 2022 alitoa taarifa kwa kichwa, “Taarifa ya Rais Biden kuhusiana na Utangulizi wa Uidhinishaji Upya wa Sheria ya 2022 ya Kupambana na Ukatili Dhidi ya Wanawake.” Alihitimisha taarifa yake kwa kusema kwamba, “Kupambana na ukatili wa kinyumbani, unyanyasaji wa kingono, ukatili wa kuchumbiana na uviziaji hautakiwi kuwa ni suala la chama cha Kidemokrasia au Kijamhuri. Ni jambo la haki na kuhurumiana. Nashukuru sana kutokana na mswada huu muhimu ulioleta pamoja vyama viwili unasonga mbele, na natarajia kuwa Bunge litauidhinisha na kuuweka mezani kwangu haraka upesi.” White House

Maoni:

Sheria inayopambana na Ukatili Dhidi ya Wanawake iliandikwa kwa mara ya kwanza na kupigiwa upatu na Rais Biden pale alipokuwa Seneta na kupitishwa kuwa sheria mnamo 1994. Sheria hiyo imerekebishwa takribani mara tatu ili kuzingatia hali iliyoko sasa na maslahi mapya. Ni kinaya kwamba Amerika inajipiga kifua kama ndio mwanga wa demokrasia, lakini inataabika kindani kutokamana na kujisalimisha kwake kwa mfumo wa kirasilimali wa kisekula. Ni muhimu kutambua kwamba mzizi wa misukosuko inayowakabili wanawake na jamii kwa ujumla sio kwa sababu sheria hazijakazwa. Alas! Ni natija ya wanadamu kujitwika nguvu za Muumba, Allah (swt) katika utungaji wa sheria.

Haijalishi ni sheria ngapi zimepitishwa, hazitotatua matatizo ambayo taifa la kisekula inakabiliwa nayo pasina kuzingatia ni Amerika, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uchina, Urusi, n.k. kwa sababu zote zimeasisiwa juu ya itikadi batili ya kisekula. Haishangazi kuona takwimu zikithibitisha hali ya kutamausha iliyoenea duniani. Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni wa nchi hatari zaidi duniani kwa wanawake unaiweka Amerika Na..19! Kwa upande mwingine, nchi kubwa ya kidemokrasia, India kuwa Na.9!  World Population Review

Tiba ya maradhi haifanywi kwa kubahatisha kwa kumuangalia tu mgonjwa na kupendekeza matibabu fulani. Bali, mgonjwa hulazimika kufanyiwa ukaguzi wa kina ili kuweza kutambua na kuwa na yakini kile kinachomsibu mgonjwa. Kufikia sasa wanawake (feminists) na wanaume (manginas) wanaodai kulingania kumwezesha na kumkomboa mwanamke pamoja na mashirika yao ya kieneo na kimataifa wamekata tamaa katika mapambano yao hadaifu. Hii ni kutokana na juhudi zao zimeambulia patupu kwa kuwa nidhamu za kirasilimali za kisekula zilizopo ambazo zipo zinapigia debe udhalilishaji na kuwafanya wanawake kama chombo cha ngono.

Mfumo wa kirasilimali wa kisekula na nidhamu zinazochipuza kutokamana nazo kama vile nidhamu huria ya kijamii ambayo imepelekea ukandamizaji wa wanawake na kusambaratika kwa familia na uwiano wa kijamii; ni maradhi ya muda mrefu ambayo yamepenya katika kila Nyanja ya maisha. Hivyo basi, ni dharura kupatikane suluhisho mbadala ili kuweza kuwanusuru wanawake na jamii kwa ujumla kutoka katika dhiki zinazozidi kila kukicha. Naam! Mbadala unahitajika kwa sababu hivi sasa tumevuka zama za kujaribu na kukosea ambapo akili ya mwanadamu imeganda kifikra licha ya kwamba kiuhalisia anaonekana kuwa hai na anapumua!

Mbadala ni Khilafah, nidhamu ya utawala wa Kiislamu ambayo inaongozwa na mwanamume Muislamu, mtawala Khalifah. Khilafah imeasisiwa juu ya Shari’ah ya Kiislamu na sio uwerevu wa mwanadamu kama vile mifumo ya kirasilimali na kikomonusti na nidhamu zao na tawala zao. Kukosekana kwa Khilafah kwa zaidi ya miaka 101 Hijria tangu kuvunjwa kwake mnamo 28 Rajab 1342 imepelekea dunia kujaa mahangaiko na majanga yasiyoingia akilini yenye kuendelea yakiondosha matumaini ya utulivu na ustawi wa kweli.

Hatima yake, ni kuwa juhudi zinatakiwa kuelekezwa katika kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume. Kurudi kwa Khilafah kutawahakikisha wanawake na jamii kwa ujumla kupata hadhi, usalama na haki za Kishari’ah. Khilafah itakuwa ni mlinzi na ngao kwa walio madhaifu na nguvu pasina kuzingatia dini au hali zao za kijamii na kiuchumi. Kurudi kwake kutadhamini furaha na ustawi wa kweli. ﴿وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ “Na siku hiyo Waumini watafurahi. [Ar-Rum 30: 4].

#أقيموا_الخلافة           #الخلافة_101      #TurudisheniKhilafah #YenidenHilafet

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu