Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kumbuka kuwa Kifo ni Hakika na Sababu yake ni Ajal na si Chengine!

Kifo na mwisho wa maisha haya imekuwa ni kitu kisicho cha maumbile na kiko mbali. Akhera na kuendelea kwake kusiko malizika kunaonyeshwa kuwa ni jambo lisilofikirika. Uangalifu wa uhakika huwekwa katika maisha ya sasa. Mwanaadamu hujaribu kutafuta ukomo wa furaha yake na pumziko katika dunia hii na hukifunika kifo na uhakika wa kuwa siku moja hatokuwepo tena katika dunia hii.

Hata hivyo, kwa kutofikiria kuhusu kifo na Akhera kunapatikana baadhi ya athari mbaya kwa tabia za mwanaadamu. Matokeo yake, lengo lake na jitihada yake muda wote huishia kwenye maisha haya ya kidunia. Hivyo, kama hakuna fikra kuhusiana na kifo, mwanaadamu hatoshughulishwa na uwajibikaji wake na kuchagua furaha katika dunia hii kuwa ni msingi wa matendo yake. Mipaka na miongozo ya Muumba yatakuwa na umuhimu mdogo kuliko matamanio yake mwenyewe, tamaa na mapenzi. Mwanaadamu hufanya hadaa ili kupata kufikia lengo lake na hudanganya ili kupata heshima. Ustawi wake binafsi hutangulizwa juu ya kila kitu chengine.

Matajiri huwanyonya masikini na viongozi wanawalaghai watu wao. Utambuzi wa mwanaadamu unamsumbua kidogo na fikra zake zinamuamuru alenge juu ya masuala yake ya kimaisha. Kizazi kinanyanyuliwa na muelekeo huu binafsi na juu ya fikra zilizoshikana na maisha ya kidunia. Haya yote ni matokeo ya kutofikiria juu ya kifo.

كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ وَنَبْلُوكُم بِالشَّرِّ وَالْخَيْرِ فِتْنَةً وَإِلَيْنَا تُرْجَعُونَ

“Kila nafsi itaonja mauti, na tunakujaribuni kwa mtihani wa shari na kheri. Na kwetu Sisi mtarejeshwa” [Quran: 21:35]

Hata hivyo, Quran inaendelea kuwakumbusha wanaadamu kuwa watakumbana na kifo. Ujumbe wa Uislamu ni kuwawacha huru wanaadamu kutokana na kuhangaika kwa ajili ya furaha ya Maisha haya ya dunia, ambayo kuyapata hakuwezekani, na kuwaitia Akhera. Ufunuo wa Mwenyezi Mungu (swt) hufunua kifua cha kila Muumini kwa ajili ya Maisha ya milele na hivyo mtu huwa na tabia ambazo zipo katika dunia hii ya kupita, lakini shauku yao na lengo lao liko Akhera. Hivyo hakuna kumbusho zuri zaidi kwa Akhera kuliko kifo. Lakini kifo hakitokei wakati mtu amekuwa mzee, kuwa mgonjwa, kuwa na mwili dhaifu au kukumbwa na ajali mbaya. Imani kuwa mtu huweza kuchelewa kufa kwa kuwa anakula vizuri, anafanya mazoezi, kuchukuwa hadhari na afya ya mwili wake au kuishi katika nchi ya amani sio sahihi. Sababu halisi ya kifo ni Ajal (mwisho wa muda wa uhai) na sio chengine chochote.

   (وَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَن تَمُوتَ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ كِتَابًا مُّؤَجَّلًا وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ الْآخِرَةِ نُؤْتِهِ مِنْهَا وَسَنَجْزِي الشَّاكِرِينَ)

“Na haiwezi nafsi kuwa ife ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kama ilivyo andikwa ajali yake. Na mwenye kutaka malipo ya duniani tutampa, na mwenye kutaka malipo ya Akhera tutampa. Na tutawalipa wenye kushukuru”. [Quran: 3:145]

Hivyo, mtu asipoteze muda wake kufikiria kuhusu namna ya kuepuka kifo. Badala yake, mtu ajiangalie kwa makini ima jitihada zake zimeelekezwa kwenye ustawi wa dunia hii tu au ustawi wa (maisha) ya Akhera. Fikra kuhusu kifo muda wote iambatane na mtu ili asisahau lengo lake. Utu wake wote katika dunia hii uelekezwe katika kukusanya matunda ya Akhera yake. Kuna matendo tofauti ambayo mwanaadamu huweza kufanya kujiaandaa kwa mauti yake. Anaweza kufuata Sheria za Mwenyezi Mungu (swt) zilizowekwa kwake akiwa mtu binafsi na, kwa hivyo, atapata pia malipo kwa matendo haya. Lakini mwanaadamu muda wote ajitahidi kupata kiwango cha juu zaidi cha malipo katika dunia hii. Kwa hivyo, kuna malipo makubwa katika kufanya kazi pamoja na jamii ya wanaolingania wanaadamu katika Uislamu, katika Kheri na kwa ajili ya Akhera. Katika jamii kama hiyo, kuna udhamini mzuri zaidi kwa kuwa mtu hatovurugwa na dunia danganyifu na kuwa watu muda wote watakumbushana juu ya lengo kuu la maisha haya na uhalisia wa kifo. Jamii kama hiyo ni Hizb ut Tahrir ambayo lengo lake ni kuhuisha njia ya maisha ya Kiislamu, utaratibu wa maisha ambao haushajiishi wanaadamu katika kulenga kibinafsi pekee juu ya ustawi wake mtu binafsi na uchu wa maisha ya kidunia, bali ni kutaka ukuruba wa akili na moyo na kukinaika na Muumba, na kujiandaa katika dunia hii kwa ajili ya maisha ya milele na kwa kukutana na Mwenyezi Mungu (swt).

“Uthman bin Affan (ra), katika hutuba ya mwisho aliyoitoa katika uhai wake, alisema: “Mwenyezi Mungu (swt) amekupeni dunia hii kwa kuitafuta Akhera, na hakukupeni kwa ajili ya kuitegemea, kwani dunia hii inamalizika na Akhera ni ya milele. Hivyo, msikifanye kile chenye kumalizika kuwa ni cha kuzingatiwa wala kukufanyeni mshughulishwe kutokana na kile kinachodumu. Chagua kutaka kile kinachodumu juu ya kile kinachomalizika, kwa kuwa dunia hii itaondoshwa na maregeo yetu ni kwa Mwenyezi Mungu (swt)”.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi ya Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Amanah Abed
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

#FromAffliction2Success          #MihnettenKurtuluşa      #KutokaMatatizoHadiMafanikio       محن_ومنح#

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 16 Mei 2020 06:10

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu