- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Je, Ugaidi ni Quran na Vitabu, Enyi Mliofilisika
(Imetafsiriwa)
Tovuti ya Russia Today ilichapisha ripoti ya habari mnamo tarehe 5/2/2025 ikisema kwamba "Huduma ya Usalama ya Shirikisho la Urusi ilisambaratisha seli ya magaidi yenye mafungamano na Hizb ut Tahrir katika Rasi ya Crimea na kuwakamata watu watano waliokuwa wakisajili wafuasi wa Hizb, ambayo imepigwa marufuku nchini Urusi." Ripoti hiyo ilijumuisha video inayoonyesha operesheni ya ukamataji na uvamizi wa nyumba, ambapo ilionekana wazi kwamba kile ambacho idara ya usalama ya Urusi ilichukua kutoka kwa nyumba za Mashababu ni nakala za Al-Quran Al-Kareem, vitabu, na vijitabu vya kisiasa na kifikra vya Kiislamu - machapisho maarufu ya Hizb ut Tahrir kwa jina pamoja na maalumati yaliyomo.
Hasa, hata katika video ya operesheni ya ukamataji iliyorekodiwa na huduma ya usalama, nyumba za Mashababu zilionekana za kawaida, zisizo na madhubuti, na zisizo na mashaka. Wakaazi wake walifungua milango wakiwa wamevalia mavazi ya kiraia, wengine hata wakiwa wamevalia nguo za kulala, wasioonyesha upinzani, vurugu, au dalili zozote za ugaidi au ujambazi. Baada ya operesheni ya msako huo, ni Quran na vitabu pekee vilivyopatikana—hakuna silaha au zana zozote zinazohusiana na vurugu au ugaidi zilizopatikana.
Hii inaonyesha wazi kwamba kile ambacho Hizb imejitangaza nacho tangu kuanzishwa kwake mwaka 1953 huko Al-Qudsi—kwamba ni chama cha kisiasa ambacho hakikubali vurugu au vitendo vya kimada—ni kweli kama ilivyothibitishwa na video yenyewe ya ukamataji.
Hizb ut Tahrir, si kwa woga au ujanja, bali kwa kufuata mfano wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ni chama cha kisiasa cha Kiislamu ambacho hakichukui vitendo vya kimada kama njia ya kuregesha maisha kamili ya Kiislamu, na wala hakijishughulishi na vurugu au ugaidi ili kufikia hili. Badala yake, shughuli zake zote ni za kifikra na za kisiasa. Historia yake ya miaka 72, iliyoenea katika mabara matano, inashuhudia na kutilia nguvu hili.
Hata hivyo, ni kufilisika kwa polisi na tawala za kidikteta ndizo zinazowasukuma kutunga tuhuma za uongo na kuizushia Hizb na wanachama wake ili kukabiliana nayo na kupunguza kuenea kwake. Hawana uwezo wa kupambana nayo kifikra, hoja, au mazungumzo. Hizb ut Tahrir ina mradi mkubwa wa hadhara—mradi safi na usio na doa wa Kiislamu—ambao hakuna mfumo mwingine unaoweza kupambana dhidi yake. Uislamu na mradi wake unawakilisha haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambao hakuna batili inayoweza kuukaribia kutoka nyuma au mbele. Vipi basi kanuni na mawazo yaliyoundwa na mwanadamu yanaweza kuhimili hoja na utukufu wa Uislamu? Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:
[بَلْ نَقْذِفُ بِالْحَقِّ عَلَى الْبَاطِلِ فَيَدْمَغُهُ فَإِذَا هُوَ زَاهِقٌ وَلَكُمُ الْوَيْلُ مِمَّا تَصِفُونَ]
“Bali tunaitupa kweli juu ya uwongo ikauvunja na mara ukatoweka. Na ole wenu kwa mnayo yazua.” [Al-Anbiya:18].
Mtazamo wa Urusi, kama ule wa madhalimu wote leo, si mpya wala si wa kibunifu; badala yake, ni wa zamani mithili ya pambano kati ya haki na batili, kati ya nuru na giza. Mzingatie Nabii Lut (amani iwe juu yake): watu wake hawakuweza kupata chochote cha kumkosoa isipokuwa wema ambao ulimtofautisha na wao. Badala ya kumheshimu na kumfuata, walitaka kumfukuza. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[وَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلاَّ أَن قَالُواْ أَخْرِجُوهُم مِّن قَرْيَتِكُمْ إِنَّهُمْ أُنَاسٌ يَتَطَهَّرُونَ]
“Na haikuwa jawabu ya kaumu yake isipo kuwa kuambizana: Wafukuzeni katika mji wenu, maana hao ni watu wanao jitakasa.” [Al-A’raf:82]. Hivyo basi, “uhalifu” wake na wa wafuasi wake ni kwamba walijitakasa nasi zao!
Na huyu hapa Firauni ambaye aliwatishia watu adhabu kali na kukatwa mikono na miguu kwa sababu tu ya kuamini haki iliyoletwa na Nabii Musa. "Uhalifu" wao pekee ulikuwa ni kukinaika kwao na imani katika kile walichojua kuwa ni haki. Wachawi wa Firauni walipoitambua haki na kuamini, hakuwa na njia ya kuwaepusha na imani yao isipokuwa kwa mateso. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[قَالَ آمَنتُمْ لَهُ قَبْلَ أَنْ آذَنَ لَكُمْ إِنَّهُ لَكَبِيرُكُمُ الَّذِي عَلَّمَكُمُ السِّحْرَ فَلَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَافٍ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ فِي جُذُوعِ النَّخْلِ وَلَتَعْلَمُنَّ أَيُّنَا أَشَدُّ عَذَاباً وَأَبْقَى]
“(Firauni) akasema: Oh! Mnamuamini kabla sijakupeni ruhusa? Hakika yeye ndiye mkubwa wenu aliye kufundisheni uchawi. Basi kwa yakini nitakukateni mikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakutundikeni misalabani katika vigogo vya mitende, na hapo kwa yakini mtajua ni nani katika sisi aliye mkali wa kuadhibu na kuiendeleza adhabu yake.” [Ta-Ha:71].
Lakini hata miongoni mwa watu wa Farauni mwenyewe, mtu muumini, aliyeficha imani yake, alisema kwa hoja nzuri:
[وَقَالَ رَجُلٌ مُّؤْمِنٌ مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَكْتُمُ إِيمَانَهُ أَتَقْتُلُونَ رَجُلاً أَن يَقُولَ رَبِّيَ اللهُ وَقَدْ جَاءكُم بِالْبَيِّنَاتِ مِن رَّبِّكُمْ وَإِن يَكُ كَاذِباً فَعَلَيْهِ كَذِبُهُ وَإِن يَكُ صَادِقاً يُصِبْكُم بَعْضُ الَّذِي يَعِدُكُمْ إِنَّ اللهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ مُسْرِفٌ كَذَّابٌ]
“Na akasema mtu mmoja Muumini, aliye kuwa mmoja katika watu wa Firauni aliye ficha Imani yake: Mtamuuwa mtu kwa sababu anasema Mola wangu Mlezi ni Mwenyezi Mungu? Na hali naye amekujieni na hoja zilizo wazi? Na akiwa yeye mwongo basi uwongo wake ni juu yake mwenyewe, na akiwa mkweli yatakufikieni baadhi ya hayo anayo kuahidini. Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi apindukiaye mipaka, mwongo mkubwa.” [Ghafir:28].
Na huyu hapa Mtume Muhammad (saw), mkweli na mwaminifu zaidi, anayejulikana kwa tabia yake isiyo na kasoro—sifa ambazo hata watu wake walizikubali. Hata hivyo, madhalimu wa Maquraishi hawakuona budi ila kumkabili kwa nguvu, ukandamizaji, na dhulma. Walimzingira, wakamdhuru, wakawatesa maswahaba zake, na wakawatoa nje ya nyumba zao, licha ya kwamba “kosa” lao pekee ni imani yao kwa Mola wao Mlezi na Dini Yake ya haki. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَن يُؤْمِنُوا بِاللهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ]
“Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa,” [Al-Buruj:8].
Na hii hapa Urusi leo, kama dola zengine za kidikteta na za kipolisi, imeshindwa kupambana na Hizb na wanachama wake kwa mijadala ya busara, badala yake wanatumia nguvu na uzushi. Mashtaka ya Urusi ya ugaidi dhidi ya Hizb ni kushindwa kifikra na kimaadili—uongo mtupu ambao unapaswa kuwaletea aibu. Lau watawala wa Urusi wangekuwa na akili yoyote, wangeruhusu Hizb kujihusisha kwa uhuru na akili za watu, na wao wenyewe wangekubali Uislamu—dini ya haki, rehma, na uadilifu—wakiachana na urasilimali mbovu ambao umefisidi maisha, kuharibu rasilimali, na kuleta mateso kwa ulimwengu mzima.
Ama kuhusu Hizb na wanachama wake, wameweka ahadi kwa Mwenyezi Mungu tangu siku ya kwanza kabisa ya kuwa walinzi waaminifu wa Uislamu, wabebaji wa ujumbe wa Mwenyezi Mungu wa nuru na uongofu, wenye msimamo juu ya haki mpaka Mwenyezi Mungu awape ushindi na hilo litakuja hivi karibuni, kwa idhini yake. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[وَلِيُمَحِّصَ اللهُ الَّذِينَ آمَنُواْ وَيَمْحَقَ الْكَافِرِينَ]
“Na pia ili Mwenyezi Mungu awasafishe walio amini na awafutilie mbali makafiri.” [Aal-i-Imran:141].
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Baher Saleh
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir