Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Chagua Baina ya Udhaifu na Matumaini

Waislamu wako zaidi ya bilioni mbili duniani. Kwa kuongezea, watafiti wengi wanaasharia kwamba Waislamu watawashinda kiidadi Wakristo kufikia mwaka 2050. [World Population Review, 2023]. Ardhi za Waislamu zimejaa rasilimali tele kama vile asilimia 70 ya mafuta, asilimia 50 ya gesi na rasilimali asili nyingine kando na kuwa rasilimali ya watu wengi. Hata hivyo, suali linalotia kizungumkuti ni kwa nini Waislamu wanataabika duniani kote licha ya kuwa na uwezo huo? Matatizo yanajumuisha si tu umasikini, mpasuko wa kijamii, mizozo ya kijeshi, mgando wa kifikra na kuhamisha wasomi nk.

Ni jambo la kawaida kuendelea kushuhudia fujo na vilio kutoka kila upande ambapo Waislamu walipo. Baadhi ya mifano ya kidhalimu ni Xinjiang (Uchina), Kashmir (India), Gaza (Ardhi ya Baraka ya Palestina), Somalia, Ukraine, Urusi, Afghanistan, Yemen, Libya na Sudan. Je, madhila yanayowakumba Waislamu yanawastahiki au la?

Ili kuweza kujibu hayo hapo juu, ni muhimu kuelekeza akili zetu kwa kauli zifuatazo za Mwenyezi Mungu (swt) na misemo ya Mtume (saw):

Mwenyezi Mungu (swt) alisema yafuatayo: وَمَا خَلَقۡتُ ٱلۡجِنَّ وَٱلۡإِنسَ إِلَّا لِيَعۡبُدُونِ﴿ “Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.” [Adh-Dhariyat:56] وَلَن يَجۡعَلَ ٱللَّهُ لِلۡكَـٰفِرِينَ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ سَبِيلاً﴿ “na wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [An-Nisa: 141] وَمَنۡ أَعۡرَضَ عَن ذِڪۡرِى فَإِنَّ لَهُ ۥ مَعِيشَةً۬ ضَنكً۬ا وَنَحۡشُرُهُ ۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَـٰمَةِ أَعۡمَىٰ * قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرۡتَنِىٓ أَعۡمَىٰ وَقَدۡ كُنتُ بَصِيرً۬ا * قَالَ كَذَٲلِكَ أَتَتۡكَ ءَايَـٰتُنَا فَنَسِيتَہَا‌ۖ وَكَذَٲلِكَ ٱلۡيَوۡمَ تُنسَىٰ “Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu. Aseme: Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona? (Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo vivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na kadhalika leo unasahauliwa”.  [TaHa: 124-126].

Thawban (ra) amesimulia kwamba Mtume (saw) alisema: «يُوشِكُ الأُمَمُ أَنْ تَدَاعَى عَلَيْكُمْ كَمَا تَدَاعَى الأَكَلَةُ إِلَى قَصْعَتِهَا»‏.‏ فَقَالَ قَائِلٌ وَمِنْ قِلَّةٍ نَحْنُ يَوْمَئِذٍ قَالَ «بَلْ أَنْتُمْ يَوْمَئِذٍ كَثِيرٌ وَلَكِنَّكُمْ غُثَاءٌ كَغُثَاءِ السَّيْلِ وَلَيَنْزِعَنَّ اللَّهُ مِنْ صُدُورِ عَدُوِّكُمُ الْمَهَابَةَ مِنْكُمْ وَلَيَقْذِفَنَّ اللَّهُ فِي قُلُوبِكُمُ الْوَهَنَ»‏.‏ فَقَالَ قَائِلٌ يَا رَسُولَ اللَّهِ وَمَا الْوَهَنُ قَالَ «حُبُّ الدُّنْيَا وَكَرَاهِيَةُ الْمَوْتِ» “ Watu hivi karibuni wataitana mmoja baada ya mwengine ili kuja kuwashambulia kama watu ambapo wanakaribisha wengine ili waje kula nao. Mmoja akauliza: Itakuwa ni kwa sababu itakuwa idadi yetu ni chache wakati huo? Akajibu: La, mutakuwa wengi wakati huo: lakini mutakuwa kama povu na takataka zinazobebwa na kimbunga, na Mwenyezi Mungu atauondosha uoga kutoka katika vifua vya adui wenu na kuweka wahn katika mioyo yenu. Mmoja akauliza: Wahn (udhaifu) ni nini. Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw): Alijibu: Kuipenda dunia na kukichukia kifo.” [Sunan Abi Dawud 4297]

Amesimulia Hudhaifa bin Al-Yaman: يَقُولُ كَانَ النَّاسُ يَسْأَلُونَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَنِ الْخَيْرِ، وَكُنْتُ أَسْأَلُهُ عَنِ الشَّرِّ، مَخَافَةَ أَنْ يُدْرِكَنِي فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّا كُنَّا فِي جَاهِلِيَّةٍ وَشَرٍّ فَجَاءَنَا اللَّهُ بِهَذَا الْخَيْرِ، فَهَلْ بَعْدَ هَذَا الْخَيْرِ مِنْ شَرٍّ قَالَ «نَعَمْ»‏‏.‏ قُلْتُ وَهَلْ بَعْدَ ذَلِكَ الشَّرِّ مِنْ خَيْرٍ قَالَ ‏«نَعَمْ، وَفِيهِ دَخَنٌ»‏‏.‏ قُلْتُ وَمَا دَخَنُهُ قَالَ «قَوْمٌ يَهْدُونَ بِغَيْرِ هَدْىٍ، تَعْرِفُ مِنْهُمْ وَتُنْكِرُ»‏‏.‏ قُلْتُ فَهَلْ بَعْدَ ذَلِكَ الْخَيْرِ مِنْ شَرٍّ قَالَ ‏«نَعَمْ، دُعَاةٌ عَلَى أَبْوَابِ جَهَنَّمَ، مَنْ أَجَابَهُمْ إِلَيْهَا قَذَفُوهُ فِيهَا»‏‏.‏ قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ صِفْهُمْ لَنَا‏.‏ قَالَ ‏«هُمْ مِنْ جِلْدَتِنَا، وَيَتَكَلَّمُونَ بِأَلْسِنَتِنَا»‏‏.‏ قُلْتُ فَمَا تَأْمُرُنِي إِنْ أَدْرَكَنِي ذَلِكَ قَالَ «تَلْزَمُ جَمَاعَةَ الْمُسْلِمِينَ وَإِمَامَهُمْ»‏‏.‏ قُلْتُ فَإِنْ لَمْ يَكُنْ لَهُمْ جَمَاعَةٌ وَلاَ إِمَامٌ قَالَ «فَاعْتَزِلْ تِلْكَ الْفِرَقَ كُلَّهَا، وَلَوْ أَنْ تَعَضَّ بِأَصْلِ شَجَرَةٍ، حَتَّى يُدْرِكَكَ الْمَوْتُ، وَأَنْتَ عَلَى ذَلِكَ» “Watu walikuwa wakimuuliza Nabii wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) kuhusu jambo zuri lakini nilikuwa nikimuuliza kuhusu jambo ovu ili nisije nikazama ndani yake. Kwa hiyo nikasema, “Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu (ﷺ)! Tulikuwa tukiishi katika ujahiliya na ndani ya mazingira mabaya (mno), kisha Mwenyezi Mungu akatuleta katika hili zuri (Uislamu); je, kutakuwepo na uovu wowote baada ya zuri hili? Alisema, “Naam.” Nikasema, ‘Je, kutakuwepo uzuri wowote baada ya uovu huo?” Alijibu, “Naam, lakini utakuwa umechafuka (sio msafi).” Nikauliza, “Uchafu wake utakuwa ni nini?” Alijibu, (Kutakuwepo) na baadhi ya watu ambao watawaongoza wengine sio kwa mujibu wa Sunnah yangu. Mutaridhia baadhi ya vitendo vyao na kutoridhia vingine.” Nikauliza, “Je, kutakuwepo na uovu wowote baada ya zuri hilo? Alijibu, “Naam, (kutakuwepo) baadhi ya watu wanaolingania katika milango ya (Jahannam) Moto, na yeyote atakayeitikia ulinganizi wao, watatupwa ndani ya (Jahannam) Moto kutokana nao.” Nikasema, “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Waweza kutuelezea ni kina nani hao?” Alisema, “Watakuwa wanatoka miongoni mwetu na watazungumza lugha yetu.” Nikasema, “Waniamrisha nini lau hali hiyo itatokea katika uhai wangu?” Alisema, “Kuwa pamoja na kundi la Waislamu na Imam (mtawala) wao.” Nikasema, “Lau hakutakuwepo na kundi la Waislamu wala Imam (mtawala)?” Alisema, “Basi jitenge mbali na makundi yote hata kama itakubidi ung’ate (ule) mizizi ya mti mpaka kufa kwako ilhali umebakia katika hali hiyo."” [Sahih al-Bukhari 7080].

Hakika, aya na hadith hizo zinatupa jibu ni kwamba inatustahiki sisi Waislamu kuwa katika hali hii ya maangamivu duniani kote kwa sababu ya udhaifu (wahn) wetu kama inavyothibitishwa:

Kwanza, sisi sio tena watumwa kwa Mwenyezi Mungu (swt) badala yake; ni watumwa kwa Wamagharibi wakoloni. Kwa kujifunga na itikadi yao ya kisekula, mfumo wake wa kirasilimali, nidhamu zake na maadili yake. Kwa upande mwingine, tumetupilia mbali itikadi (aqeedah) yetu ya Kisiasa ya Kiislamu  

Pili, tumekubali na tunaendelea kupigia debe fahamu za kukanganya za kisekula za kirasilimali kama vile uzalendo na utaifa yote eti kwa ajili ya kujikurubisha na mujtama ilhali tumelitupa fungamano na umoja wa Kiislamu.

Tatu, tumewachukua wasioamini (makafiri) kuwa ndio wandani na viongozi wetu dhidi ya

Mwenyezi Mungu (swt), Mtume wake (saw) na waumini ambao wanalingania kujisalimisha kikamilifu kwa Shari’ah. Hivyo basi, tunashiriki katika vikao vyao ili kupanga njama dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Nne, dhamira yetu katika haya maisha ya mpito ya dunia imejikita katika msingi wa lengo huhalalisha njia. Hivyo basi, tunajituma usiku na mchana ili kufaulu hapa duniani lakini kwa gharama ya kuikosa Akhera ya milele! Tumefungamanisha kufaulu na kukusanya utajiri wa kimada na kujifurahisha kihisia. Haishangazi kuona kwamba tumeporomoka kiwango cha wanyama.

Kwa kutamatisha, yote yanategemea na chaguo la mtu binafsi ima kubakia katika hali ya udhaifu au kukumbatia matumaini. Mwenyezi Mungu (swt) alisema: ﴾إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوۡمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنفُسِہِمۡ﴿ “Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao.” [Al-Rad: 11].

Njia pekee ya kuthibitisha kuwa hakika umekumbatia matumaini, ni kwa kujitoa katika minyororo ya ubwana wa Wamagharibi wakoloni. Kwa kutupilia mbali itikadi yao ya kisekula, mfumo wao wa kirasilimali, nidhamu zao na maadili yao. Kisha kupatiliza ulinganizi wa kurudisha tena maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Serikali ya Kiislamu ya kweli kwa maana Khilafah kwa njia ya Utume.

Kwa kuwa na /kukumbatia matumaini, inamaanisha kutumia juhudi zako za mwisho (kimada au vinginevyo) katika kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu (swt) kupitia kujiunga na harakati za kunyanyua utambuzi na maoni ya umma na kuwahesabu watawala Waislamu ndani ya ulimwengu wa Waislamu. Kwamba watawala Waislamu waivunjilie mbali mipango ya Sykes-Picot ambayo iliigawanya dola yetu iliyokuwa Dola Moja ya Khilafah na kuwa vijidola vilivyo na mipaka ya kikoloni na ambayo imesababisha maafa tangu kubuniwa kwao. Hivyo basi, ima waukubali Uislamu ndio msingi wa serikali zao na watawale kwa Shari’ah; au wapinduliwe na nafasi zao zichukuliwe na Muislamu mwanamume kama Khalifah. Hakika, ni kwako wewe ima kuzama ndani ya wahn (kuipenda dunia na kukichukia kifo) au matumaini.

Mwenyezi Mungu (swt) alisema: ﴾وَمَن يَتَوَلَّ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُ ۥ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَإِنَّ حِزۡبَ ٱللَّهِ هُمُ ٱلۡغَـٰلِبُونَ﴿ “Na atakaye fanya urafiki na Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, basi hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kushinda.” [Al-Maidah: 56].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro (Abu Taqiuddin)

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu