Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 MATUNDA YA HADHARA YA KIKATILI NI JAMII ISIYOSTAARABIKA

(Imetafsiriwa)

MTI HUJULIKANA KWA MATUNDA YAKE

Mwishoni mwa karne ya kumi na nane na kumi na tisa sayansi ilikuzwa kama ufunguo wa maendeleo na baadaye ilinasibishwa na hadhara. Auguste Comte katika kazi yake aliripoti katika ‘The Course of Positive Philosophy’ jamii ililengwa kurekebishwa kwa msingi wa kisayansi. Aliamini kila mtu anapaswa kufundishwa sayansi ya kisasa ili aweze kuunda mitazamo au tabia kama sehemu ya maumbile ya mtu kupitia kujifunza au kujioanisha pasi na kutambua na maadili mapya ya kisayansi maishani mwao. Ingawa, falsafa ya Comte haijajadiliwa kwa upana lakini imeoanishwa pasi na kutambua katika maisha ya vizazi vinavyo kuja mbele. Kwa miaka mingi, malengo na dhana za kisasa, zisizo za kimantiki, zisizo za kimaadili na za kikatili ziliiunda jamii na kusababisha thaqafa inayobadilika kila wakati, yenye uharibifu, katili na ya kimada ndani ya jamii. Hadhara ya kibepari katili na ya uharibifu imeibuka ambapo Jamii haina huruma kwa taabu au mateso ya ulimwengu unaowazunguka.

Samuel Huntington aliandika, “Siasa za ulimwengu zinaingia katika hatua mpya, ambapo migawanyiko mikubwa kati ya wanadamu na chanzo kikuu cha migogoro ya kimataifa itakuwa ya kithaqafa. Katika enzi hii inayoibuka ya mzozo wa kithaqafa, Umoja wa Mataifa lazima uunde miungano pamoja na thaqafa zinazofanana na kueneza maadili yake popote iwezekanavyo" [1].

MATUNDA YA MTI ULIOKUZWA CHINI YA KIVULI CHA JAMII YA KISASA ILIYOSTAARABIKA

Aftab Amin Poonawalla alimuua mpenzi wake Shraddha Walker na kuukata mwili wake vipande 35 kabla ya kuvitupa katika misitu ya Chhatarpur kusini mwa Delhi [2]. Uhusiano wa kuishi kinyumba ndio utamaduni wa siku hizi wa jamii hii inayoitwa iliyostaarabika ambayo ni ngeni kabisa kwa Uislamu. Wenza wanaoishi kinyumba hawana wajibu shirika wa kimaadili, hata hivyo, kwa kuwa sheria zilizotungwa na mwanadamu hufanya ridhaa ya pande zote mbili kuwa ndio sababu ya kisheria chini ya sheria ya kisekula ya nchi. Uhusiano huu unaadhibiwa chini ya utawala wa Kiislamu ambapo jamii imejengwa juu ya mwongozo pekee kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt).

Athari nyengine, ya zama hizi za kisasa, inayohusiana na Aftab ni kukiri kwake kuhusu kupenda kwake kutazama mfululizo wa mtandao na vipindi vinavyohusiana na uhalifu na ni kutokana na maonyesho hayo kwamba aliazima mawazo juu ya kuhifadhi sehemu za mwili zilizokatwa na kuzitupa baadaye [ 2, 3]. Uislamu unajenga shakhsia ya Kiislamu kutoka kwa mtu binafsi mwenye malengo bora katika maisha ambayo kwa kawaida huilinda jamii kutokana na udhalilishaji wowote. Pia alikiri mbele ya polisi kwamba alikuwa amevuta bangi siku ambayo alimuua mpenzi wake Shraddha Walkar. Zaidi ya hayo, alikuwa akivuta bangi, na alikuwa mtumiaji wa kawaida wa dawa za kulevya [3].

TAFAKARI JUU YA TUKIO HILO NA UCHUNGUZE

Kwa kila Shraddha inayounda vichwa vya habari, kuna wanawake elfu moja ambao bado, ima kwa sababu bado hawajauawa, au kwa sababu wamezoea kuishi nayo, kwa huruma ya mnyanyasaji. Katika kesi ya unyanyasaji wa kinyumbani, asilimia kubwa ni ya wanawake, sio tu nchini India, lakini ulimwenguni kote [4]. Matukio hayo yote ambayo yanaendana na ukatili kama huo lazima yatangazwe na kuchunguzwa ili kudhibiti jamii kutokana na kuenea daima kwa utamaduni wa kikatili wa ubakaji, mauaji na mateso. Kimsingi ni muhimu kuwashtaki wahalifu wote wanaofanana na tukio halipaswi kutumiwa kuwapotosha watu.

Akizungumza na ANI, babake Shraddha, Vikas Walker alisema, "Ninashuku upendo wa jihad" [2]. Itakuwa upotovu mkubwa ikiwa vitambulisho vya kupinga Uislamu kama vile 'Upendo wa Jihad' vitatumiwa kwa mtu huyu anayechunguzwa. Huku kutakuwa ni kukengeuka kutoka kwenye mjadala muhimu sana kuhusu sababu ya matukio yote yanayofanana, ambayo idadi yake ni kubwa. Kwa hakika, mielekeo ya kidini ya Kiislamu ya Aftab haiambatani na thaqafa ya kweli ya Kiislamu na mafundisho yake ya kimsingi. Kuulaumu Uislamu katika suala hili mahususi bila shaka kutatoa kiwango kidogo cha hatua za kisiasa na huenda kwa kiasi fulani ikawatenga watu fulani. Mkosaji halisi ni utamaduni wa kisasa usiostaarabika ambao unasimamia uhalifu mwingi kama huo ndani ya jamii. Suluhisho litakuwepo tu pale jamii itakapofichua thaqafa na mfumo wa kibepari uliotungwa na mwanadamu. Mtu anapaswa kutafuta jibu la swali la kimsingi sana kuhusu maisha, yaani, ‘nini kusudio la maisha haya?’ Je, tumewahi kujiuliza kuhusu yale yaliyokuwa kabla ya uhai na yale yatakayokuwa baada yake? Sisi kiuhalisia, ni kama wanyama waliopotea bila lengo pana maishani. Mwenyezi Mungu (swt) anatukumbusha katika Surat Al-Imran Ayah 185:

[كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ]

“Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kaamili Siku ya Kiyama.” [3:185].

Swali ni je, tunatafuta jamii iliyo kamilifu ambayo itaongozwa na yule aliyemuumba mwanadamu, aliyempa uhai na kuumba ulimwengu ili kuendeleza maisha haya? Je, maumbile haya sio ya uhalisia? Uhalisia huu unaweza kuhisika na uko dhahiri kuhusu mwanadamu kwamba ana kikomo, ni mtegemezi na ni dhaifu katika nyanja zote za maisha yake. Hivyo, mwanadamu mwenye mapungufu, utegemezi na kutokamilika kwake anapaswa kutafuta suluhisho kamilifu, la kutegemewa na kamilifu kutoka kwa Muumba wake. Ni juu ya mwanadamu kuchagua baina ya uongofu na upotofu. Mabepari hujitengenezea watumwa wakati Uislamu una hekima ya kushiriki na kuunda uongozi wa Aqida au imani ya Uislamu. Kila kitendo cha mwanadamu kimefungwa kwa muongozo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Hapo tu ndipo mtu anayeweza kupata mafanikio ya kweli maishani. Mwenyezi Mungu (swt) anatuamrisha katika Surah Al Baqara Ayah 208:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ ادْخُلُواْ فِي السِّلْمِ كَآفَّةً وَلاَ تَتَّبِعُواْ خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ]

“Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala msifuate nyayo za Shetani; hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi.” [2:208]

HADHARA ILIYOTUNGWA NA MWANADAMU NA MATUNDA YAKE UCHUNGU

Kumwelimisha mtoto humjenga fikra zake kuhusu maisha. Fikra hizi huendeleza mielekeo katika maisha ya mwanadamu. Mielekeo humpa mtu motisha na nguvu ya kutenda kulingana na fikra zake. Mfumo wa elimu hujenga msingi wa kizazi kijacho. Kwa bahati mbaya, mfumo wa Kibepari umeiweka elimu kama bidhaa ya biashara na kuitumia kama chombo cha kutawala akili. Hili linapaswa kuwa jambo la kutia wasiwasi sana ulimwengu tunaoishi lakini suala muhimu kwa Hadhara ya Kiislamu. Ili kuzikoloni akili za vijana wa Kiislamu katika nchi nyingi za Kiislamu, Magharibi imepandikiza elimu kwa mbinu na nyenzo ambazo zimewaweka Waislamu mbali na Aqidah (itikadi) yao na urithi wao wa thaqafa (utamaduni), na pia kuzuia mwamko na maendeleo yao. Misingi isiyo sahihi ya mfumo wa elimu hukuza mtu mwenye malengo ya ubinafsi na uchoyo. Katika mizizi ya jamii ya sasa, fahamu na imani ya kimsingi ni usekula, uhuru, uliberali, na mawazo mengine yasiyo ya Kiislamu. Fahamu zote hizi zinaitenganisha na kuikataa ‘Dini’, muongozo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) katika mambo ya kidunia Ambaye ndiye Muumba Pekee wa kila kitu ulimwenguni. Fikra ndio msingi wa ukuaji na mporomoka wote.Watoto wa Ummah huu kutoka katika nchi za Kiislamu hasa na nchi nyinginezo kwa ujumla wamekuwa kama nguruwe kwenye maabara ambazo zimetengana na mazingira halisi ya Waislamu.

Katika tukio hili mhalifu, Aftab, alivuka mipaka mingi ya ukatili. Yeye ni tatizo la utamaduni uliopo wa kuchukiza, usioweza kuthaminiwa na usiofaa ambao wanauita kuwa wa kistaarabu. Fahamu na imani za kimsingi katika usekula, uhuru, uliberali, ndio msingi wa utamaduni wa kisasa ambao huunda jamii isiyostaarabika na iliyo poromoka iliyojaa ukatili katika fikra na vitendo.

MATUNDA YA HADHARA YA KIISLAMU NA ZAMA ZAKE ZA DHAHABU

Hadhara ya binadamu chini ya kivuli cha Khilafah iliyotabikisha mfumo wa elimu ya Kiislamu uliokuwa na uwezo wa kulinda kitambulisho cha Waislamu kama Khairu Ummah (taifa bora). Muongozo wa kuregesha zama za dhahabu uko wazi kabisa, hatuna budi tuufuate. Mfano wake wa dhahabu unaonekana kwa sababu ulikuwepo kwa mamia ya miaka. Na kwa kufanya kazi kwa bidii tunaweza kuufanya uwepo tena, na hiyo ni kwa kujenga ufahamu ndani ya Ummah huu kuhusu mfumo mbovu wa kidemokrasia uliotengenezwa na mwanadamu na ubora wa mfumo wa Kiislamu wa Mwenyezi Mungu (swt). Kwa hivyo, Ummah huu hautasita kuitupilia mbali mifumo yao isiyokuwa ya Kiislamu na kudai utabikishwaji wa Uislamu kama mfumo mbadala. Kwa Ummah huu, Mwenyezi Mungu ndiye muongozi pekee kwa kila suala linalohusiana na maisha ya hapa duniani na Akhera. Kiroho ulitawala na kuuongoza Ummah katika zama zake za dhahabu. Kipengele cha kiroho kinamfanya Mwenyezi Mungu kuwa chanzo pekee cha muongozo na muongozo huu ndio chanzo pekee cha vitendo katika maisha ya mwanadamu. Kwa hivyo, hisia ya kiroho inatawala kama vile Hukmu za Mwenyezi Mungu (swt) zinavyo yaongoza matendo ya mwanadamu. Radhi Zake pekee ndiyo lengo. Akili ya mwanadamu huridhika, moyo hupata utulivu na hatimaye ghariza ya uchaji Mungu hushibishwa. Huu ndio msingi wa thaqafa ya Kiislamu unaounda jamii iliyostaarabika kikweli iliyojaa hisia ya kiroho katika fikra na matendo.

Imeadikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ameenur Rehman

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu