Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 [إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ]    

“Wewe tu Tunakuabudu, na Wewe tu Tunakuomba Msaada” [Al-Fatiha: 5]

(Imetafsiriwa)

Kila siku, katika kila swala, ya faradhi au nafila, Waislamu wanasoma kauli ya Mwenyezi Mungu (swt), aya katika Surat Al-Fatiha:

[إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ]

“Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada”

Hivyo, Waislamu wanakiri na kutangaza kujisalimisha kwao kwa Mwenyezi Mungu (swt), na watakuwa na Tawhid, watamtii Yeye, watamuabudu Yeye Peke Yake na kutaka msaada kutoka Kwake (swt) katika kuabudu kwao, utiifu wao katika mambo yao yote. Imeelezwa kwenye tafsiri ya Ibn Kathir: “Hatumuabudu yeyote isipokuwa Wewe, na hatumtegemei yeyote isipokuwa Wewe, na huu ndio ukamilifu wa utiifu.” Dini inaegemea juu ya maana hizi mbili, na baadhi ya waliotangulia wamesema: al-Fatiha ndio siri ya Qur’an, na siri yake ni tamko hili:

[إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ]

“Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada” [Al-Fatiha: 5].

Kipande cha kwanza kinakataa kumshirikisha Mwenyezi Mungu (swt), na cha pili kinakataa uweza na nguvu, na kinayapeleka mambo kwa Mwenyezi Mungu (swt). Maana hii inapatikana kwenye zaidi ya aya moja ya Qur’an, Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

[فَاعْبُدْهُ وَتَوَكَّلْ عَلَيْهِ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ]

“Basi Muabudu Yeye na umtegemee Yeye. Na Mola wako Mlezi haghafiliki na yale mnayoyatenda” [Hud: 123]

[قُلْ هُوَ الرَّحْمَنُ آمَنَّا بِهِ وَعَلَيْهِ تَوَكَّلْنَا]

“Sema, Yeye ni mwingi wa Rehema; tunamuamini Yeye, na juu Yake tunategemea” [Al-Mulk: 29]

[رَّبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ فَاتَّخِذْهُ وَكِيلاً]

“Mola Mlezi wa mashariki na magharibi, hapana mungu isipokuwa Yeye, basi mfanye awe mtegemewa wako.” [Al-Muzzammil: 9]. Pamoja na aya hii tukufu:

[إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ]

“Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada” [Al-Fatiha: 5].

Ni sharti kwa ibada ili ikubaliwe na Mwenyezi Mungu (swt) ni kuwa ifanywe kwa ajili Yake tu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

[قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ اللَّهَ مُخْلِصاً لَّهُ الدِّينَ]

“Sema: Hakika mimi nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumsafishia  Dini Yeye tu.” [Az-Zummar: 11].

Na Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

[وَمَا أُمِرُواْ إِلَّا لِيَعْبُدُواْ اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُواْ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُواْ الزَّكَاةَ وَذَلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ]

“Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Swala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini Madhubuti.” [Al-Bayyina: 5].

Unyenyekevu ni kumchagua Mwenyezi Mungu (swt) kwa nia ya kuabudu na kutegemea malipo kutoka Kwake Pekee.

Kutoka kwa Abu Huraira (ra), kuwa Mtume (saw) amesema:

«قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: أَنَا أَغْنَى الشُّرَكَاءِ عَنِ الشِّرْكِ، مَنْ عَمِلَ عَمَلاً أَشْرَكَ فِيهِ مَعِي غَيْرِي تَرَكْتُهُ وَشِرْكَهُ»

“Mwenyezi Mungu aliyetukuka amesema: Mimi nimejitosheleza kiasi kuwa sihitaji mshirika. Atakayefanya amali kwa ajili ya mwengine pamoja nami, nitamuachia na washirika wake.” [Ameipokea Muslim].

Pia inatakiwa ibada iwe kwa namna na njia ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ametuagiza na kutufundisha Mtume Wake (saw). Kutekeleza ibada kunahitaji elimu juu ya ibada na elimu ya hukmu zake na namna ya kuzitekeleza kabla ya utekelezaji wake.

Kuwa mja wa Mwenyezi Mungu (swt) kuna maanisha kutekeleza maamrisho Yake na kujifunga na hukmu Zake katika kila kitu alichokiamrisha na alichokikataza. Ibada katika maana yake ya jumla haijajifunga katika kutekeleza matendo ya kibinafsi tu yanayoambatana na mahusiano yake na Mola Wake, kama swala, funga, zaka na Hajj, bali imekusanya matendo yanayohusisha mahusiano ya mtu na nafsi yake mwenyewe kama vyakula na nguo, na mahusiano yake na watu wengine kama miamala, ujenzi wa ardhi na urithi ndani yake na kufanya kazi kutekeleza sheria Zake (swt) katika ardhi na kubeba ujumbe wa Uislamu na ulinganizi wake ulimwenguni.

Kuwa mja wa Mwenyezi Mungu (swt) maana yake ni kutaka msaada Wake kutenda matendo ya utiifu na ibada, na kutaka msaada Wake katika kujiweka mbali na makatazo Yake pamoja na kuushinda ushawishi wa Shetani na minong’ono ya nafsi inayoamrisha uovu.

Imepokewa na Mu’adh bin Jabal (ra) kuwa Mtume (saw) ameniambia,

 «أُوصِيكَ يَا مُعَاذُ، لَا تَدَعَنَّ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلَاةٍ أَنْ تَقُولَ: اللَّهُمَّ أَعِنِّي عَلَى ذِكْرِكَ وَشُكْرِكَ وَحُسْنِ عِبَادَتِكَ» “Nakuusia ewe Mu’adh, Usiwache kusema katika kila mwisho wa swala: ‘Ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie katika kukukumbuka, na kukushukuru, na kukuabudu kwa vizuri.” [Imepokewa na Abu Dawud na wengineo]

Hii ina maana kuwa tunahitaji msaada Wake katika mambo yetu yote ya maisha na kuwa tunarejea Kwake na kumtaka msaada Wake katika madhara yote yanayotupata na katika madhara na mazito yanayotupata katika kulingania Uislamu na katika juhudi zetu katika kusimamisha dini yake juu ya ardhi, na tukilenga juu ya kauli ya Mwenyezi Mungu (swt):

[وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً]

“Na anayemtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.” [At-Talaq: 3].

Ina maana kuwa hatujisalimishi kwa madhalimu na maadui wa Dini, na hatuwarudii na kutaka msaada kwao, kwani Mwenyezi Mungu (swt) yuko pamoja nasi, na nguvu zao na ufalme wao utaondoka bila kujali muda utakaochukua. Mwenyezi Mungu (swt) bila shaka atatusaidia, na yeyote anayemtegemea Mwenyezi Mungu (swt) hatojuta, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Mwezi wa Ramadhan ni fursa kubwa kuifanya upya ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt), na kukubali kutii kwetu kujisalimisha Kwake (swt), na hukumu Zake; na kutupatia utiifu na kuabudu, kufanya kazi ya kubadilisha hali hii fisidifu, kutaka msaada wa Mwenyezi Mungu (swt), kumuamini Yeye, na kuamini ushindi Wake, basi na tusonge mbele katika njia hii na tusimame kidete na kufanya kazi kwa bidii.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Bara’ah Manasrah

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu