Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Utafutaji wa Shahada (Kifo katika Jihadi)

Utafutaji wa shahada imekuwa daima ni fahamu msingi ndani ya elimu ya kijeshi enzi za Uislamu. Pamoja na masomo juu ya zana za vita, mikakati na mbinu, utafutaji wa shahada ulitizamwa kama msingi wa fahamu za masomo, uelewaji na ujengaji wa nafsiyya. Utafutaji wa shahada ndio uliotia nishati majeshi ya Kiislamu katika vita, ukiwawezesha kufikia yale ambayo wengine walishindwa kuyafikia na wasingejaribu kuyafikia. Huku majenerali wa majeshi ya makafiri wakiwa wamejifunga na dunia, wakipanga mikakati yao kuhakikisha kuna majeraha kidogo, majenerali wa majeshi ya Kiislamu walikuwa wamebarikiwa wanajeshi ambao waliona kifo katika uwanja wa vita kama mlango wa kupata zawadi kubwa kwa roho yoyote inayotaka.

Utafutaji wa shahada uliwaruhusu wanajeshi Waislamu kusimama kidete pasi na wasiwasi wowote dhidi ya majeshi makubwa ukilinganisha idadi yao na kuyashinda baadaye. Maafisa wa enzi za Kiislamu hawakuchukulia kufanya kazi ndani ya vikosi vya jeshi kama njia ya kupata ajira, usafiri, nyumba na elimu kwa watoto wao kama ilivyo sasa kwa maafisa wa vikosi vya jeshi ndani ya dola za Waislamu leo. La, macho yao daima yalikuwa yamefungika tu kwa zawadi kubwa ya milele ambayo hawawezi kuipata duniani humu wanamoishi tena kwa muda mfupi.

Katika zama zetu, baada ya kuangushwa utawala wa Kiislamu, matamanio ya Waislamu ya utafutaji shahada yanaendelea kuwatia tumbo joto wanamikakati wa majeshi ya Kimagharibi na kuwakatisha tamaa. Msukumo wa kufikia shahada unaangaliwa kama uboreshaji wa kikosi ki aina yake. Umewaruhusu Waislamu pasi na kuwa na kikosi cha jeshi kilichoandaliwa vyema kuweza kupeana kipigo na kuyatia hasara kubwa majeshi ya kiuvamizi kama inavyoonekana ndani ya Afghanistan na Kashmir. Imewalazimisha Wamagharibi kusoma kwa makini somo la mbinu za kivita zisizokuwa kawaida, ambazo zimewashangaza kumuona mwanajeshi Muislamu akitamani shahada. Na kuwatia uoga wakuu miongoni mwa Wamagharibi kila wanapofikiria uunganishwaji wa vikosi vya majeshi ya Waislamu dhidi yao, ambalo ni jambo lisiloepukika kutokana na kurudi tena kwa Khilafah kwa Njia ya Utume. 

Utafutaji shahada ni fahamu msingi ndani ya Uislamu na ambayo inaelezea sifa za Ummah wa Uislamu. Mwenyezi Mungu (swt) Asema:

وَلاَ تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُواْ فِى سَبِيلِ اللَّهِ أَمْوَتاً بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ - فَرِحِينَ بِمَآ ءَاتَـهُمُ اللَّهُ مِن فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُواْ بِهِم مِّنْ خَلْفِهِمْ أَلاَّ خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلاَ هُمْ يَحْزَنُونَ﴿

“Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi. Wanafurahia aliyo wapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake, na wanawashangilia wale ambao bado hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwamba haitakuwa khofu juu yao wala hawata huzunika." [Aali Imran 3:169-170]. Hapa Mwenyezi Mungu (swt) Anasema kwa yakini kuwa licha ya kwamba mashahidi wameuawa katika maisha haya, roho zao ziko hai na zinaendelea kupokea mahitaji yao Katika Maisha ya Milele. Katika Sahihi Muslim amerikodi kuwa Masruq alisema, "Tulimuuliza `Abdullah kuhusiana na Ayah hii,

وَلاَ تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُواْ فِى سَبِيلِ اللَّهِ أَمْوَتاً بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ﴿

“Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi.”

Alisema tulimuuliza RasulAllah (saw) suali hilo hilo na (saw) alisema:

«أَرْوَاحُهُمْ فِي جَوْفِ طَيْرٍ خُضْرٍ، لَهَا قَنَادِيلُ مُعَلَّقَةٌ بِالْعَرْشِ، تَسْرَحُ مِنَ الْجَنَّةِ حَيْثُ شَاءَتْ، ثُمَّ تَأْوِي إِلَى تِلْكَ الْقَنَادِيلِ، فَاطَّلَعَ إِلَيْهِمْ رَبُّهُمُ اطِّلَاعَةً فَقَالَ: هَلْ تَشْتَهُونَ شَيْئًا؟ فَقَالُوا: أَيَّ شَيْءٍ نَشْتَهِي وَنَحْنُ نَسْرَحُ مِنَ الْجَنَّةِ حَيْثُ شِئْنَا؟ فَفَعَلَ ذَلِكَ بِهِمْ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، فَلَمَّا رَأَوْا أَنَّهُمْ لَنْ يُتْرَكُوا مِنْ أَنْ يُسْأَلُوا، قَالُوا: يَا رَبِّ نُرِيدُ أَنْ تَرُدَّ أَرْوَاحَنَا فِي أَجْسَادِنَا حَتَّى نُقْتَلَ فِي سَبِيلِكَ مَرَّةً أُخْرَى، فَلَمَّا رَأَى أَنْ لَيْسَ لَهُمْ حَاجَةٌ، تُرِكُوا»

“Roho zao zimo ndani ya ndege wa kijani ambao wana taa, ambazo zinalewalewa chini ya Arshi ya Mwenyezi Mungu, na wanazunguka ndani ya Pepo popote wanapotaka. Kisha wanarudi katika taa hizo. Mwenyezi Mungu huwatizama na kusema, 'Je mnatamani chochote?' Wao husema, 'Tutamani kipi zaidi, wakati tunatembea popote tunapotamani ndani ya Pepo.' Mwenyezi Mungu akawauliza tena suali hili mara tatu, na walipoona kwamba Ataendelea kuwauliza mpaka watoe jibu, wakasema, 'Ewe Mwenyezi Mungu! Tunatamani roho zetu zirudishwe katika miili yetu ili tuuliwe tena kwa ajili Yako.' Mwenyezi Mungu alijua hawana matamanio mengine, kisha wakawachwa."

Kwa hiyo ni muhimu kwa afisaa Muislamu kutafakari cheo cha ndugu yake mwanajeshi aliyepata shahada akiwa Uhud. Autafakari kwa kina ujumbe waliomuachia miaka yote hiyo. Imamu Ahmad alirekodi kuwa Ibn `Abbas alisema kuwa Mtume (saw) alisema,

«لَمَّا أُصِيبَ إِخْوَانُكُمْ بِأُحُدٍ، جَعَلَ اللهُ أَرْوَاحَهُمْ فِي أَجْوَافِ طَيْرٍ خُضْرٍ، تَرِدُ أَنْهَارَ الْجَنَّـةِ، وَتَأْكُلُ مِنْ ثِمَارِهَا، وَتَأْوِي إِلى قَنَادِيلَ مِنْ ذَهَبٍ فِي ظِلِّ الْعَرْشِ، فَلَمَّا وَجَدُوا طِيبَ مَشْرَبِهِمْ وَمَأْكَلِهِمْ، وَحُسْنَ مُتَقَلَّبِهِمْ قَالُوا: يَا لَيْتَ إِخْوَانَنَا يَعْلَمُونَ مَا صَنَعَ اللهُ لَنَا، لِئَلَّا يَزْهَدُوا فِي الْجِهَادِ، وَلَا يَنْكُلُوا عَنِ الْحَرْبِ، فَقَالَ اللهُ عَزَّ وَجَلَّ: أَنْا أُبَلِّغُهُمْ عَنْكُم»

“Ndugu zenu walipouliwa katika Uhud, Mwenyezi Mungu aliziweka roho zao ndani ya ndege wa kijani walioelekea katika mito ya Pepo na kula kutoka katika matunda yake. Kisha wanarudi katika taa za dhahadu zinazolewalewa katika kivuli cha Arshi. Walipoonja utamu wa chakula chao, vinywaji na makaazi yao, walisema kuwa, 'Tunatamani ndugu zetu wangelijua yale ambayo Mwenyezi Mungu aliyotupa ili wasiweze kuachana na Jihadi au vita.' Mwenyezi Mungu alisema, 'Nitawafikishia habari zenu.'

Mwenyezi Mungu akateremsha Ayah ifuatayo:

وَلاَ تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُواْ فِى سَبِيلِ اللَّهِ أَمْوَتاً بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ﴿

“Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi.”

Hivyo basi, afisaa wa enzi ya Kiislamu alikuwa si tu ana hamu ya malipo ya Tahajjud na kuswali Msikitini, alikuwa Analia na huku silaha yake ikiwa mikononi mwake madhubuti huku akiomba Dua, akitamani kupata shahada. Hakika, dua ya afisaa Muislamu au mwanajeshi sio tu kwa ajili ya majumba, magari na elimu nzuri bali ni kwa ajili ya shahada. Mu’adh bin Jabal (ra), mwanamikakati shupavu aliyemshauri RasulAllah (saw) katika Vita vya Badr, alisimulia kuwa RasulAllah (saw) alisema,

«مَنْ سَأَلَ اللَّهَ الْقَتْلَ فِي سَبِيلِهِ صَادِقًا مِنْ قَلْبِهِ أَعْطَاهُ اللَّهُ أَجْرَ الشَّهِيدِ»

“Yeyote anayemuomba Mwenyezi Mungu ili auliwe katika njia Yake kwa dhati kutoka moyoni, Mwenyezi Mungu atampa zawadi ya shahada." [Tirmidhi].

Afisaa Muislamu hajali hadhi wala cheo katika dunia hii lakini anatafuta hadhi ya shahada na cheo kinachotokana nayo. Imamu Ahmad alirekodi kuwa Anas alisema kuwa RasulAllah (saw) alisema:

«مَا مِنْ نَفْسٍ تَمُوتُ، لَهَا عِنْدَ اللهِ خَيْرٌ، يَسُرُّهَا أَنْ تَرْجِعَ إِلَى الدُّنْيَا، إِلَّا الشَّهِيدُ، فَإِنَّهُ يَسُرُّهُ أَنْ يَرْجِعَ إِلَى الدُّنْيَا فَيُقْتَلَ مَرَّةً أُخْرَى، لِمَا يَرَى مِنْ فَضْلِ الشَهَادَة»

“Hakuna roho ambayo imeridhiwa na Mwenyezi Mungu na ikafa itatamani kurudi katika maisha haya, isipokuwa ya shahidi. Atatamani kurudishwa katika maisha haya ili aweze kuuliwa tena, ili aweze kuonja cheo cha kupata shahada."

Shahada ni kitendo kimoja ambacho kitamfanya mtu kutamani kutoka Jannah kwa fursa ya kufa tena na wakati utajiri wa dunia nzima utakapojaribu kumzuia utashindwa. Imesimuliwa kutoka kwa Anas b. Malik RasulAllah (saw) alisema,

«مَا مِنْ أَحَدٍ يَدْخُلُ الْجَنَّةَ يُحِبُّ أَنْ يَرْجِعَ إِلَى الدُّنْيَا وَأَنَّ لَهُ مَا عَلَى الأَرْضِ مِنْ شَىْءٍ غَيْرُ الشَّهِيدِ فَإِنَّهُ يَتَمَنَّى أَنْ يَرْجِعَ فَيُقْتَلَ عَشْرَ مَرَّاتٍ لِمَا يَرَى مِنَ الْكَرَامَةِ»

“Hakuna atakayeingia Peponi atatamani kurudishwa tena duniani lau hata angelipewa kila kitu juu ya mgongo wa ardhi (kama kishajiisho) isipokuwa shahidi ndiye atakayetamani kurudishwa tena katika ardhi hii na auliwe mara kumi kwa ajili ya cheo kitukufu ambacho amepewa." [Muslim]

Afisaa Muislamu hayafungi macho yake juu ya kuwapa umadhubuti wa kifedha familia yake bali anakwenda mbio kuwafungulia njia ya kuingia Jannah, iliyojaa mazuri yasiyokuwa na mwisho. Imesimuliwa na Abu al-Darda', RasulAllah (saw) alisema,

«يُشَفَّعُ الشَّهِيدُ فِي سَبْعِينَ مِنْ أَهْلِ بَيْتِهِ»

“Shahid atapewa nafasi kuwaombea watu sabini wa familia yake." [Abu Dawud].

Afisaa Muislamu haendi mbio kuchuma mali nyingi ambazo wanaomtegemea waweze kustarehe nazo baada ya kifo chake, kwa kuwa anajua kuwa shahada ni manufaa makubwa kwa wanaomtegemea. Abu Bakr Ibn Marduwyah amerekodi kuwa Jabir bin 'Abdullah alisema, "Mtume wa Mwenyezi Mungu aliniangalia siku moja na akasema, 'Ewe Jabir! Kwa nini nakuona una majonzi?" Nikasema, 'Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Babangu alipata shahada na kuniachia madeni na watoto.' Akasema,

«أَلَا أُخْبِرُكَ؟ مَا كَلَّمَ اللهُ أَحَدًا قَطُّ إِلَّا مِنْ وَرَاءِ حِجَابٍ، وَإِنَّه كَلَّمَ أَبَاكَ كِفَاحًا .قَالَ سَلْنِي أُعْطِكَ. قَالَ أَسْأَلُكَ أَنْ أُرَدَّ إِلَى الدُّنْيَا فَأُقْتَلَ فِيكَ ثَانِيَةً، فَقَالَ الرَّبُّ عَزَّ وَجَلَّ إِنَّهُ قَدْ سَبَقَ مِنِّي الْقَوْلُ إِنَّهُمْ إِلَيْهَا لَا يَرْجِعُونَ. قَالَ أَيْ رَبِّ فَأَبْلِغْ مَنْ وَرَائِي»

“Nikwambie kuwa Mwenyezi Mungu hakuwahi kuzungumza na yeyote isipokuwa nyuma ya pazia. Lakini, Alizungumza na babako moja kwa moja." Akasema, 'Niombe na Nitakupa.' Akasema, 'Naomba nirudishwe hai ili ni uliwe katika njia Yako tena.' Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, akasema, 'Nimezungumza neno kuwa hawatorudishwa tena katika (haya maisha).' Akasema, 'Ewe Mwenyezi Mungu! Basi nifikishie habari zangu kwa nilio wawacha nyuma."

Afisaa Muislamu yuko makini na sehemu yake ya mwisho, uchungu wa kifo, adhabu ya kaburi na uoga wa kupindukia unaotokana na kutosamehewa Siku ya Hesabu. Kwa hiyo anatizama fadhila tukufu za Mwenyezi Mungu (swt) zinazotokamana na shahada. Imesimuliwa kutoka kwa Abu Hurairah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) alisema,

«مَا يَجِدُ الشَّهِيدُ مَسَّ الْقَتْلِ إِلاَّ كَمَا يَجِدُ أَحَدُكُمْ مَسَّ الْقَرْصَةِ»

“Shahidi hahisi kitu chochote anapouliwa zaidi ya mmoja wenu anavyohisi anapoumwa na (chungu)." [Ibn Majah]

Imesimuliwa kutoka kwa Rashid bin Sa'd, kwamba mwanamume mmoja miongoni mwa Maswahaba wa Mtume alisema, "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa nini waumini watapewa mitihani katika makaburi yao isipokuwa shahidi? Mtume (saw) alisema,

«كَفَى بِبَارِقَةِ السُّيُوفِ عَلَى رَأْسِهِ فِتْنَةً» “Kupambana kwa panga juu ya kichwa chake ni mtihani tosha." [an-Nisai].

Mtume (saw) alisema,

« يُغْفَرُ لِلشَّهِيدِ كُلُّ ذَنْبٍ إِلاَّ الدَّيْنَ »

“Mwenyezi Mungu humsamehe kila dhambi shahidi, isipokuwa deni lake." [Muslim].

Na imesimuliwa kutoka kwa Miqdam bin Ma’dikarib kwamba Mtume (saw) alisema,

«لِلشَّهِيدِ عِنْدَ اللَّهِ سِتُّ خِصَالٍ يُغْفَرُ لَهُ فِي أَوَّلِ دَفْعَةٍ مِنْ دَمِهِ وَيُرَى مَقْعَدَهُ مِنَ الْجَنَّةِ وَيُجَارُ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ وَيَأْمَنُ مِنَ الْفَزَعِ الأَكْبَرِ وَيُحَلَّى حُلَّةَ الإِيمَانِ وَيُزَوَّجُ مِنَ الْحُورِ الْعِينِ وَيُشَفَّعُ فِي سَبْعِينَ إِنْسَانًا مِنْ أَقَارِبِهِ»

“Shahidi ana mambo sita (amewekewa) na Mwenyezi Mungu: Ana samehewa kuanzia kudondoka kwa tone la damu yake inapomwagwa; anaonyeshwa sehemu yake ndani ya Pepo; ana epushwa na adhabu za kaburi; ana wekwa salama na Hofu Kubwa, ana vishwa vazi la imani; ana ozeshwa (wake) miongoni mwa wenye macho mapana; na anaruhusiwa kuwaombea watu sabini wa familia yake." [Ibn Majah].

‏Na Afisaa Muislamu wa kuigwa, kusifiwa na kuonewa wivu ni yule ambaye sifa yake imejengwa na Uislamu, na kilele chake ni moto wa matamanio ya kupata shahada. Kwa hiyo, lazima ayatafakari maneno ya Umar al-Farooq (ra) aliyechagua majenerali baada ya majenerali waliopata ushindi baada ya ushindi. Imamu Malik amesimulia kutoka kwa Yahya ibn Saeed kuwa Umar ibn al-Khattab (ra) alisema, 

كَرَمُ الْمُؤْمِنِ تَقْوَاهُ وَدِينُهُ حَسَبُهُ وَمُرُوءَتُهُ خُلُقُهُ وَالْجُرْأَةُ وَالْجُبْنُ غَرَائِزُ يَضَعُهَا اللَّهُ حَيْثُ شَاءَ فَالْجَبَانُ يَفِرُّ عَنْ أَبِيهِ وَأُمِّهِ وَالْجَرِيءُ يُقَاتِلُ عَمَّا لاَ يَؤُوبُ بِهِ إِلَى رَحْلِهِ وَالْقَتْلُ حَتْفٌ مِنَ الْحُتُوفِ وَالشَّهِيدُ مَنِ احْتَسَبَ نَفْسَهُ عَلَى اللَّهِ

"Utukufu wa Mu'min ni uchajimungu. Dini yake ndiyo ukoo wake. Uume wake ni katika tabia yake nzuri. Ujasiri na uoga ni ghariza ambazo Mwenyezi Mungu ameziweka pale Anapotaka. Muoga ni yule ambaye ana shindwa hata kumtetea babake na mamake, na jasiri ni yule anayepigana kwa ajili ya vita sio ngawira. Kuuliwa ni njia moja ya kukutana na kifo, na shahidi ni yule anayejitoa muhanga akitarajia zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu." [Muwatta]

Ni starehe na fadhila aina gani zilizoko mbele ya Afisaa Muislamu anayetafuta shahada! Nyuma yake ni kudhilalishwa kwa Ummah huu mikononi mwa makafiri katika ardhi za karibu na mbali, Ardhi Tukufu –Palestina, Afghanistan, Kashmiri, Myanmar (Burma), Syria, Mashariki Turkestan na Iraq. Kati yake na shahada ni kurudisha tena enzi ya Kiislamu wakati ambapo simba kwa mara nyingine watafunguliwa na kuachwa kuwashughulikia maadui waoga, ambao watakimbia kama fisi kama walivyofanya kabla yao. Na kwa dharura iliyoko mbele yake ni kutoa Nussrah yake ili kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Mtume (saw) ili aweze kupata moja kati ya Husnain, ushindi au shahada.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na 

Musab Umair – Pakistan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 06:49

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu