Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 [وأَحْسِنْ كَمَا أَحْسَنَ اللَّهُ إِلَيْكَ]
“Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe.” [Al-Qasas: 77]
(Imetafsiriwa)

Ihsan – kutafuta ukamilifu na ubora ni kiwango cha juu na hadhi kwa waja wema wa Mwenyezi (swt). Pindi mmoja wetu atakapoifikia, atakuwa karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu, mwenye ikhlasi katika kazi yake, akihamia kwa Mola wake kwa utiifu na akijisalimisha kwa hukmu na sheria Zake, akijitahidi sana kukamilisha ibada kwa njia bora zaidi  yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake, kuwa mpole, mwenye upendo na mwenye urafiki katika kuamiliana kwake. Yenye kumpa mtu utulivu na sakina katika nafsi na roho, na kuwa mwenye upendo na kupendwa, akiwashauri wengine kwa mema, akichukia vitendo viovu.

Wale wanaozingatia Aya za Qur'an Tukufu watazipata nyingi zao zikielezea fadhila ya Ihsan, kama vile kuiamrisha na kuwahimiza wengine kuifanya, na kutaja matendo ya mtenda wema na sifa zake, na jinsi Mwenyezi Mungu alivyowaahidi waja Wake wema malipo, pepo na upendo, ili Muislamu apatilize faida ya tabia hii njema na kheri.

Kwa mfamo, Mwenyezi Mungu Mtukufu asema kuhusu Fadhila Yake kwa watendao wema kwa badali ya malipo ya wema wao:

]هَلْ جَزَاءُ الْإِحْسَانِ إِلَّا الْإِحْسَانُ]

“Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani?” [Ar-Rahman: 60]. Na kuhusu ukaribu wa watendao wema na Mwenyezi Mungu Mtukufu:

]إِنَّ اللَّهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوْا وَالَّذِينَ هُمْ مُحْسِنُونَ]

“Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kumcha, na watendao mema.” [An-Nahl: 128]. Na kuhusu upendo wake kwa watendao wema:

[وَأَحْسِنُوا إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ]

“Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.” [Al-Baqara: 195]. Ama kuhusu malipo mema hapa duniani na kesho Akhera, Yeye (swt) asema:

[فَآتَاهُمُ اللَّهُ ثَوَابَ الدُّنْيَا وَحُسْنَ ثَوَابِ الْآخِرَةِ وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ]

“Basi Mwenyezi Mungu akawapa malipo ya duniani na bora ya malipo ya Akhera. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao mema.” [Aali Imran: 148]. Na Yeye (swt) amewaongezea thawabu zao katika maneno Yake (swt):

[لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَى وَزِيَادَةٌ وَلَا يَرْهَقُ وُجُوهَهُمْ قَتَرٌ وَلَا ذِلَّةٌ أُولَئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ]

“Kwa wafanyao wema ni wema na zaidi. Wala vumbi halitawafunika nyuso zao, wala madhila. Hao ndio watu wa Peponi.” [Yunus: 26]. Kwa sababu hii, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«إِنَّ اللَّهَ كَتَبَ الْإِحْسَانَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ»

“Hakika Mwenyezi Mungu (swt) ameandika ihsan katika kila kitu.”

Ihsan ina vipengee vingi na inajitokeza kwa aina nyingi, na ni katika amali za ibada na miamala, katika mambo madogo na muhimu. Kipengee cha juu kabisa ni Al-Ihsan pamoja na Mwenyezi Mungu, ambayo hupatikana kupitia imani ya Mungu mmoja (Tawhid), kwa Mwenyezi Mungu, na ibada ya ikhlasi Kwake. Vivyo hivyo, ihsan pamoja na Mtume kwa kumwamini yeye na yale aliyokuja nayo na kumtii, kumpenda na kumfuata, kuiga Sunnah yake na kufuata njia na mbinu yake. Vivyo hivyo, kuna ihsan kwa watu, kisha ihsan kwa nafsi, kwa kuitakasa na kujitahidi kupata furaha yake kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu hapa duniani na uokozi wake kesho Akhera.

Mojawapo ya aina za ihsan ambayo hujaza moyo kuridhika na furaha ni ihsan kwa watu na kuwasaidia, katika mambo yanayowanufaisha au kuwaondolea madhara katika mambo ya dini yao au dunia yao.

Ni furaha nzuri ilioje anayoipata mtu wakati anapowafundisha watu mema kwa ajili ya Mola wake, na akaona kati yao athari ya mafundisho yake, mwongozo na ushauri. Vipi isifurahie au kufurahishwa na yule aliyewaonyesha upole watu na kuona athari yake kwao, haswa siku hizi ambazo tunaishi kwa shida, iwe kifikra, kijamii, au kifedha? Huyu alisahihisha njia yake ya kifikra na kumfanya aione njia sahihi ya mabadiliko na maendeleo, na huyu akampa ushauri wa dhati zaidi kwa shida zake, iwe ni katika familia au kazini, na matokeo yake ni utulivu ulioufurahisha moyo. Na mtu huyu mwingine alinyoosha mkono wake kumsaidia kwa pesa zake na akamfuta kutoka kwake vumbi la hitaji na giza la fedheha, na huyo akaondoa dhiki yake au akatimiza deni lake, kwa hivyo akafurahi baada ya kuwa na huzuni na mfadhaiko… Enyi ambao mnataka kujisikia furaha na kujifariji, jitahidi kuwa wapole kwa watu kadiri muwezavyo, ili muwe na furaha katika ulimwengu wenu, na kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, ili mpate kuwa na furaha kesho Akhera.

Mojawapo ya aina kubwa ya ihsan kwa watu ni kwamba mmoja wetu anaacha kuwadhuru wengine kwa njia na aina zote, na kusamehe kutendewa vibaya na kudhuriwa na wengine, na kisha licha ya hayo tunapaswa kuwatendea upole, yaani, kuvunja uadui wao kwa upole, ili hisia za uhasama na chuki ziondolewe na kubadilishwa na hisia za upendo na urafiki.

Na hatusahau kuwa upole kwa wanadamu ni kafara kwa matendo mabaya na kuondoa mateso, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

]إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ]

“Hakika mema huondoa maovu.” [Hud: 114].

Kwani mtenda mema anaweza kuepushwa na misiba, na maafa juu yake kutokana na ihsan yake kwa waja wa Mwenyezi Mungu (swt), na hii imejumuishwa katika hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُسْلِمٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ الدُّنْيَا نَفَّسَ اللَّهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ، وَمَنْ يَسَّرَ عَلَى مُعْسِرٍ يَسَّرَ اللَّهُ عَلَيْهِ فِي الدُّنْيَا وَاالْآخِرَةِ، وَمَنْ سَتَرَ عَلَى مُسْلِمٍ سَتَرَ اللَّهُ عَلَيْهِ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، وَاللَّهُ فِي عَوْنِ الْعَبْدِ مَا كَانَ الْعَبْدُ فِي عَوْنِ أَخِيهِ»

“Yeyote anayemuondolea Muislamu tatizo miongoni mwa matatizo ya dunia, Mwenyezi Mungu atamuondolea tatizo miongoni mwa matatizo ya Siku ya Kiyama. Na yeyote anayemsahilishia mwenye uzito Mwenyezi Mungu atamsahilishia duniani na Akhera, na yeyote anayemsitiri Muislamu Mwenyezi Mungu atamsitiri duniani na Akhera, na Mwenyezi Mungu yuko katika usaidizi wa mja maadamu mja yuko katika usaidizi wa nduguye.” Na yeye (saw) pia amesema:

«صَنَائِعُ الْمَعْرُوفِ تَقِي مَصَارِعَ السُّوءِ»

“Watendaji wema hulinda kutokana na hatima.”

Ama thawabu kamili na malipo makubwa kwa watendao mema, yanawangojea kwa Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema siku atakapokutana nao, anawapenda, anaridhika nao, anawakirimu vizazi vyao, anawasamehe dhambi zao, na kuwaingiza katika pepo ambayo upana wake ni kama mbingu na ardhi; Mwenyezi Mungu (swt) asema:

]لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَى وَزِيَادَةٌ وَلَا يَرْهَقُ وُجُوهَهُمْ قَتَرٌ وَلَا ذِلَّةٌ أُولَئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمْ ففِيهَا خَالِدُونَ]

“Kwa wafanyao wema ni wema na zaidi. Wala vumbi halitawafunika nyuso zao, wala madhila. Hao ndio watu wa Peponi. Humo watadumu.” [Yunus: 26].

Na ikiwa tutatafuta ihsan katika mambo yetu yote, tutaizoea na kutafuta ukamilifu katika ibada zetu na miamala yetu, kwa hivyo mtu atakuwa mzuri katika kumwabudu Mola wake na kuamiliana na viumbe wa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo atakuwa mwema kwa wazazi wake, mkewe, watoto wake, ndugu zake, majirani na marafiki, na kwa kweli ihsan yake inaweza kumfikia yule anayemchukia, ilhali kosa lake likafikiwa na upole, na ihsan inaenea hadi kwa mnyama na mmea «فِي كُلِّ ذِي كَبِدٍ رَطْبَةٍ أَجْرٌ» “Fungamano lolote na kiumbe hai lina ujira.” Mtu wa kwanza kuwa mwema kwake ni yule yule aliye kati ya pande zake, ambaye ataulizwa na kuhesabiwa kwa matendo yake hapa duniani na Akhera. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

]كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَة]

“Kila nafsi imejiweka rehani kwa yale iliyoyachuma.” [Al-Mudathir: 38].

Jifanyie mema, ewe mwanadamu, kwa kutembea katika Njia Iliyo Nyooka. Njia ya wale ambao Mwenyezi Mungu (swt) amewaneemesha miongoni mwa manabii, wakweli, mashahidi na wema. Inakuja ibada, isimamishe kwa ukamilifu, na ifanye bila unafiki na kwa kutafuta kuridhika kwa wanadamu, kwa hivyo kufanya ibada na kuikamilisha ni mojawapo ya aina bora za ihsan.

Lakini ukamilifu huu lazima uunganishwe na hitaji la kufanya mabadiliko ndani yetu, kwa wengine, na hivyo katika Ummah. Hivyo basi, mtu anayefanya matendo mema hutafuta mabadiliko katika kila nyanja ya maisha yake na jamii, akijua njia sahihi ya mabadiliko ambayo itaendeleza Ummah na kuzibadilisha fahamu kutoka mizizi yake na kuunda fahamu safi za Kiislamu ambazo zinatia upatanishi wa sheria na mfumo wa Uislamu hapa duniani.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atufanye miongoni mwa wale wanaomwabudu yeye sawasawa, tuwe wema kwa viumbe vya Mwenyezi Mungu, tuwe wema kwa nafsi zetu, na atubariki na ihsan katika matendo na maadili yetu, na ikhlasi katika maneno na matendo yetu. Yeye anatutosha na Sifa njema zote ni kwake Yeye Mola wa Walimwengu wote.

#رمضان_والإحسان
#Ramadan_And_Ihsan
#Ramazan_ve_İhsan

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Muslimah Ash-Shami (Um Suhaib)

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu