Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kwa Hakika Pamoja na Uzito upo Wepesi!

Mapambano baina ya Haki na Batil yamekuwepo tokea Adam (as) alipoumbwa na yatakuwepo hadi Siku ya Hukumu. Baadhi ya wakati Batil huonekana kama imeshinda na kutowezekana kusimamishwa hadi msaada wa Mwenyezi Mungu (swt) uje kwa watu wanaoendeleza vita vyao upande wa Haki. Hutekeleza mapambano haya na huwa ndio watu bora zaidi ya viumbe na huwa ni mfano kwa watu wanaokuja kushiriki katika mapambano baada yao. Mwenyezi Mungu (swt) amewataja katika Quran,

(كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِٱلْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ ٱلْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ)

“Nyinyi mmekuwa bora ya Ummah waliotolewa watu. Kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.” [TMQ 3:110].

Watu hawa wamechukua uongozi kwa Mtume Muhammad (saw) na kufuatiwa na Maswahaba (ra) na waumini baada yao waliobeba ujumbe wa kuamrisha mema na kukataza maovu ambao Mwenyezi Mungu (swt) amewaamrisha. Wamepitia ugumu usioelezeka hadi kufikia ushindi. Makafiri kutokana na chuki zao dhidi ya Uislamu na Waislamu, wametumia kila njia iliowezekana na mbinu katika muda wote wa historia kuzima kuibuka kwa Uislamu na kuwa wenye kutawala. Lakini kila mara kwa msaada wa Mwenyezi Mungu (swt) Aliye na Nguvu, Mtukufu, na juhudi zisizochoka za Waumini, Waislamu wanaibuka kuwa washindi dhidi ya Makafiri. Na huu ni ukweli usiopingika ambao Waislamu wanauthamini sana hivi sasa wakati wanaishi katika hali ambapo upande wa Batil ndio unaotawala na huku wakikumbana na dhulma katika mikono ya Makafiri. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

(كَتَبَ ٱللَّهُ لَأَغْلِبَنَّ أَنَا۠ وَرُسُلِىٓ إِنَّ ٱللَّهَ قَوِىٌّ عَزِيزٌ“Mwenyezi Mungu ameandika: Hapana shaka Mimi na Mtume wangu tutashinda. Hakika mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.”  [TMQ 58: 21].

Wakati wa zama za Mitume, Waislamu waliwashinda madhalimu kama Nimrod, Fir’awn, Abu Jahl, Abu Lahab, Walid bin Mughirah na wengineo waliojitahidi sana wakiwa upande wa uovu kuizuia Haki isienee, wakiona kama hawatoshindwa lakini hatimaye, walikabiliana na kushindwa kwa udhalili.

Baada ya zama za Mitume na wakati wa Khilafah ya Kiislamu uovu ulijaribu kueneza mbawa zake katika namna ya uvamizi wa Makruseda na Wamongolia kwa zaidi ya karne moja.

Kipindi cha karne hii Waislamu walikabiliana na matatizo mengi kiasi ambacho waliachwa bila chochote bali kama watazamaji wa uovu unaofanywa na Makafiri, ikiwemo kukatwa kichwa kwa Khilafah ndani ya ngome yake. Wakati huo mbawa za uovu zilikatwa na watu kama Salahuddin Ayyubi na Allaudin Zhingi waliobeba jukumu mabegani mwao dhidi ya uovu. Walikuwa na matumaini makubwa katika msaada wa Mwenyezi Mungu (swt) wakati wakikimbilia kwenye mapambano yao, wao na hasa Salahuddin Ayyubi aliwaunganisha Waislamu chini ya kivuli cha Khilafah na akawashinda Makafiri katika Vita vya Hattin. Kupitia hili kwa mara nyengine imeonyesha kwa dunia kuwa ushindi mara zote huwa kwenye Haki.

Kwa mara nyengine katika karne ya 18 na 19 mabaki ya maadui wa Uislamu yameendeleza mapambano yao wakati wa Khilafah ya Uthmaniya. Kipindi hiki waliushambulia Uislamu kwa aina ya uvamizi wa Kithaqafa na Kisiasa pamoja na uvamizi wa Kijeshi na waliweza kuivunja Khilafah mnamo 28 Rajab 1342, ikiwa imetimia miaka 100 kamili ya Hijri iliouacha Ummah wa Kiislamu ukikumbana na mashambulizi ya maadui bila ya mlinzi wao. Tokea muda huo, Makafiri wameonekana kutawala dunia kwa kiwango ambacho Waislamu walianza kufikiria kuwa hawatoweza kuwashinda. Hii ilipelekea wengi wao kusubiria matokeo ya kimiujiza kama kuja kwa Mahdi na Issa (as) kuushinda uovu kwa mara nyengine.

Uovu hivi leo ambao umetawala na kupigana dhidi ya Uislamu ni mfumo wa dunia wa Urasilimali wa Kisekula wa Kiliberali ambao umeonekana, unaendelezwa, na kuenezwa na Makafiri wa Kimagharibi. Mfumo huu wa dunia wa Urasilimali wa Kisekula wa Kiliberali unamuengua Mwenyezi Mungu (swt) kutokana na mambo ya maisha ya watu na kusababisha maangamizi kila unapotekelezwa kutoka mashariki hadi magharibi. Umeingia kwenye ulimwengu wa Kiislamu kupitia ukoloni ukiongozwa na Uingereza hadi Vita vya Pili vya Dunia, tokea kipindi hicho umekuwa ukisimamiwa na Amerika kupitia taasisi mbali mbali za kimataifa kama UN, IMF na NATO na watoto wake kama GCC, OIC, nk.

Nidhamu iliyoletwa na mfumo huu wa ulimwengu wa urasilimali wa kisekula wa kiliberali umechafua fikra, mawazo na tabia za Waislamu na umepunguza jukumu la Uislamu na kulifikisha kwenye maisha yao ya kibinafsi tu. Pamoja na hayo, Wamagharibi wameendeleza juhudi zao kuwavua Waislamu kutokana na alama zozote zilizobaki za sheria za Kiislamu na kanuni katika masuala ya kijamii, kiuchumi, kisheria na kisiasa za kiutawala katika ardhi za Waislamu kupitia sheria tofauti, mikataba na matamko. Kwa kuwa Waislamu wamekoseshwa utambulisho wao kutokana na kuvamiwa huku, wamekosa uwezo wao wa kufikiri na kujenga fikra zinazotokana na Uislamu. Wengi ya Waislamu hivi leo wanaamini kuwa Mfumo huu wa Kisekula ambao ni muovu zaidi katika historia ya Wanaadamu hauwezekani kubadilishwa na hivyo kuanza kuangalia masuluhisho ya muda ndani ya mfumo wake au kuanza kupatanisha juu ya maadili yao ya Kiislamu na maadili hayo ili kupunguza maumivu yao.

Kibaya zaidi Wamagharibi wamewalea viongozi na wasomi miongoni mwa Waislamu wanaozikuza fikra zake, mawazo, na masuluhisho kwa Ummah wa Waislamu.

Hatimaye, Waislamu wameachana na njia ilioelekezwa na Uislamu kwa ajili ya muamko wao na kuanza kufuata njia ilioagizwa na ‘uovu’ yaani mfumo wa urasilimali wa kisekula wa kiliberali kutokana na ujinga wao juu ya ukweli kuwa masuluhisho haya na njia ni zenye kuleta utatuzi wa muda na wa sehemu tu badala ya utatuzi wa kudumu. Yote hayo yamedhoofisha kujiamini kwa Waislamu katika kukataza uovu na wameachana na jukumu la kupeleka mbele mapambano haya. Inaonekana wamesahau kuwa wakati msaada wa Mwenyezi Mungu (swt) unapokuja madhalimu kama Firawn, Nimrod au Abu Jahl hawataweza kusimama mbele ya ‘Haki’ na mwisho wao watakabiliana na kushindwa kwa udhalili.

Ili tuweze kubadilisha hali ya sasa ilivyo ya ubwana wa Makafiri, Waislamu lazima waondokane na hali ya kukata tamaa na waweze kujiamini kwa kuacha fikra na mawazo yanayopigiwa debe na Makafiri kama Usekula, Demokrasia, Utaifa, Maslahi, (fikra ya kushikamana na) dhara lililo jepesi lao nk., ambayo kupitia kwake kunapatikana ufisadi, na wajenge fikra na mawazo yao moja kwa moja juu ya Uislamu. Haya ndio mabadiliko ambayo Mwenyezi Mungu (swt) anayataka kutoka kwa Waislamu, Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

(إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا۟ مَا بِأَنفُسِهِمْ)

“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yalioko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao” [TMQ 13:11].

Ili kuweza kufanya mabadiliko ya hali ya sasa ilivyo ya Waislamu na kuuleta tena utukufu wao uliopotea, Mwenyezi Mungu (swt) ametupatia baadhi ya mafunzo makubwa kupitia Surah Ash-Sharh na nyenginezo ili kujenga uaminifu wa Mtume Muhammad (saw) na Waislamu katika Makkah wakati wa mapambano yao dhidi ya Maquraysh. Hata leo, Waislamu wanaweza kupata baadhi ya mafunzo kutoka Aya hizi.

Nayo ni:

1. Utulivu na Ushindi mara zote huja kupitia Shida.

Kwa kweli, mapambano ambayo Ummah wa Kiislamu umetuamuru sio mapambano ya kawaida, wale ambao wanaendesha mapambano wanapaswa kuwakabili madhalimu wa muda wao. Mwanzoni mapambano haya yametekelezwa na Mitume hadi Mtume Muhammad (saw) na kisha Maswahaba wa Mtume Muhammad (saw) na waumini baada yao. Hivi leo, jukumu la kuendeleza mapambano haya limevikwa kwetu waumini. Kama ilivyo, mapambano haya hayatokuwa rahisi na wale wanaobeba mapambano haya hivi leo lazima wayakabili mataifa yenye nguvu ya leo yanayoongoza mapambano (dhidi yetu) kama Amerika, Ufaransa, Urusi, China na madhalimu vibaraka kama Bashar al-Assad, Al-Sisi, Muhammad Bin Salman na serikali nyengine zinazohangaika mchana na usiku kutetea mfumo wa urasilimali wa kisekula wa kiliberali. Hivyo, ugumu usiwe sababu ya kujiengua kutoka kushiriki katika mapambano haya. Waislamu lazima waelewe muda wote kuwa ushindi siku zote huja na ugumu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

 (أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا۟ ٱلْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُم مَّثَلُ ٱلَّذِينَ خَلَوْا۟ مِن قَبْلِكُم)

“Mnadhani kuwa mtaingia Peponi bila kukujieni kama yaliyowajia wale waliopita kabla yenu”? [TMQ 2: 214].

Tunaweza kuchukua mazingatio kutoka kwa maisha ya Abdullah ibn Umm Makhtum, “Anas ibn Malik amesema, ‘Katika vita vya al-Qadisiyyah, Nilimuona Abdullah ibn Umm Makhtum amevaa ngao ncha zake zikiwa zinanin’ginia. Ameshika bendera nyeusi mkononi mwake. Alipoulizwa, “Je, Mwenyezi Mungu hajakupatia udhuru [kutokana na mapigano]?” [Alikuwa kipofu] Alijibu, “Bila shaka, lakini ninataka kuongeza idadi ya waumini pamoja nami.” {Tafsir Al Qurtubi}. Ikiwa yeye (ra) ameshiriki katika mapambano kwa ajili ya Uislamu huku akiwa mlemavu, basi sisi tuna udhuru gani? Kila mtu ana jambo la kutekeleza kwa ajili ya Uislamu.

2. Uungaji mkono wa Mwenyezi Mungu (swt) na msaada wake muda wote uko pamoja na waumini

Uimara mkubwa wa muumini huja wakati anapotambua kuwa uungaji mkono na msaada wa Mwenyezi Mungu (swt) uko pamoja naye katika kila mapambano. Yule mwenye msaada wa Muumba wake huweza kukabiliana na kila changamoto. Haya yamehakikishwa muda baada ya muda katika maisha ya watu wanaomuamini Yeye (swt). Mwenyezi Mungu (swt) huondosha khofu na uzito kutoka kwa wale wanaomtegemea Yeye tu (swt). Tunajua namna Yeye (swt) alivyoondosha uzito kutoka kwenye nyoyo za Waislamu katika Vita vya Badri na kuwapa ushujaa wa kupigana dhidi ya maadui zao. Wakati wa harakati zake katika Makkah, Mwenyezi Mungu (swt) alimtuliza Mtume Muhammad (saw) kwa kusema, (وَوَضَعْنَا عَنكَ وِزْرَكَ) “Na tukakuondoshea mzigo wako” [TMQ 94: 2]. Hii inatuonyesha kuwa Yeye (swt) mara zote anaondosha mazito kutoka kwenye vifua vya watu wanaofanya kazi kwa ajili ya njia Yake (swt). Hivyo sisi tukiwa Waislamu hatutakiwi kusitasita katika njia Yake (swt). Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

(يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِن تَنصُرُوا۟ ٱللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ)

“Enyi mlioamini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na kuithibitisha miguu yenu” [TMQ 47: 7].

3. Usijisalimishe kutokana na shutuma. Mwenyezi Mungu (swt) ameinyanyua hadhi ya Waumini.

Moja ya sababu ya Waislamu kusitasita kuitikia wito wa Uislamu ni khofu ya shutuma, wanahofia kupigwa chapa ya wenye msimamo mkali, siasa kali nk. makafiri wa Kimagharibi hawapotezi muda katika kuwachora picha hasi Waislamu kupitia njia na namna yoyote wanayoipata. Muislamu hatakiwi kusalim amri kabisa kwa aina hizi zinazokaririwa kwao kwa sababu Mwenyezi Mungu (swt) amewasifu na kuwapa cheo kikubwa wale wanaofanya bidii kulifanya neno la Mwenyezi Mungu kuwa juu. Mtume (saw) amesema,

لاَ تَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِى قَائِمَةً بِأَمْرِ اللَّهِ لاَ يَضُرُّهُمْ مَنْ خَذَلَهُمْ أَوْ خَالَفَهُمْ حَتَّى يَأْتِىَ أَمْرُ اللَّهِ وَهُمْ ظَاهِرُونَ عَلَى النَّاسِ

“Kutabakia na kundi kutoka Ummah wangu litalosimama juu ya haki,  halitodhuriwa na wale wenye kuwapinga au kuwadhihaki hadi ije amri ya Mwenyezi Mungu na hali wao wako dhahiri mbele ya watu” (Muslim). Mtume Muhammad (saw) alishutumiwa na Maquraysh kuwa ni muongo, mshairi, mchawi, mwenda wazimu lakini shutuma hizo hazikumzuia katika kufanya jitihada dhidi ya Maquraysh. Kwa hakika, alisifiwa kwa kiwango kikubwa na Mwenyezi Mungu (swt) na Yeye (swt) aliwaagiza Malaika na Waislamu wote kumsifu. Hivi leo, tunaona kila ambapo jina la Mwenyezi Mungu (swt) linapotajwa, jina la Mtume (saw) pia linatajwa pamoja naye hapa duniani na pia, amepewa hadhi kubwa katika maisha ya Akhera. Mtume Muhammad (saw) amesema,

«من التمس رضى االله بسخط الناس رضي االله عنه وأرضى الناس عنه ومن التمس رضا الناس بسخط االله سخط االله عليه وأسخط عليه الناس»

“Yeyote anayetafuta radhi za Mwenyezi Mungu japokuwa ni kwa kuwachukiza watu, basi Mwenyezi Mungu atakuwa radhi naye, na atawaridhisha watu naye. Na yeyote anayetafuta radhi za watu japokuwa kwa kumchukiza Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu atachukizwa naye na kuwafanya watu wachukizwe naye.” (Ibn Hibban/Tirmidhi)

Hivyo wale wanaotaka radhi kwa Mwenyezi Mungu hawatojali juu ya shutuma za watu.

4. Muda wote kuna wepesi (mara mbili) baada ya uzito.

Mwenyezi Mungu (swt) anasema, (فَإِنَّ مَعَ ٱلْعُسْرِ يُسْرًا) “Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi” Kupitia Aya hii, Mwenyezi Mungu (swt) amemtia moyo Mtume Muhammad (saw) na Waislamu kuwa kwa kila ugumu anaoupata katika mapambano kwa ajili ya Haki (Uislamu), Yeye (swt) pia hutoa ushindi kwa waumini: mara mbili, mmoja ni katika hii dunia kwa kuifanya ishinde na mwengine ni katika siku ngumu zaidi ambayo lazima mtu afaulu yaani Akhera. Hivyo, hii lazima imshajiishe kila Muislamu apanie kuifuata njia ya Mwenyezi Mungu (swt) ili awe mshindi duniani na Akhera. Ugumu ambao Waislamu wanakabiliana nao katika mapambano haya hauwezi kulinganishwa na malipo atayoyapata Akhera. Pia, ushindi unaokuja baada ya uzito uliotajwa katika Aya hii inaonyesha kuwa kazi kubwa ya kusimamisha Uislamu haitofanyika kupitia miujiza kama kuja kwa Mahdi (as) nk, bali kupitia mazito anayokabiliana nayo Muislamu.

5. Njia tunayolazimika kuifuata ni njia ilioelekezwa kwetu na Mwenyezi Mungu (swt)

Mwenyezi Mungu (swt) baada ya kuwafariji Waislamu kupitia Mtume Muhammad (saw) kwa maelezo ya kujiandaa kutekeleza kazi muhimu sana ya kusimamisha Uislamu yenye ugumu mkubwa, lakini pia, Yeye (swt) amesema kuwa msikhofu juu ya ugumu kwa kuwa atauondosha kutoka kwenye vifua vyao, na kuwa wasikhofu juu ya shutuma zinazofanywa dhidi yao kwa kuwa Atanyanyua hadhi zao na kuahidi ushindi kwao duniani na Akhera. Baada ya kuwaliwaza waumini kwa maneno yote haya, Mwenyezi Mungu (swt) ametaka kutoka kwa Waumini kusimama kidete kwenye Njia Yake ya kusimamisha Uislamu kwa kushiriki kwenye mapambano haya na kuomba msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu tu na sio kutoka kwa Makafiri, wanafiki na maadui wa Mwenyezi Mungu. Kutaka msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) pia inajumuisha njia ya kuurejesha tena Uislamu kama Mwenyezi Mungu (swt) alivyotuelekeza. Kutekeleza mapambano ya kurejesha Uislamu katika njia iliofunzwa na kisichokuwa Uislamu kama Usekula au mfumo mwengine wowote uliobuniwa utapelekea Waislamu kushindwa na pia itapelekea kukabiliana na udhalili katika dunia hii na mbele ya Mola wao Siku ya Kiyama kama Umar (ra) alivyosema, “Tulikuwa watu madhalili sana duniani na Mwenyezi Mungu ametupa heshima kupitia Uislamu. Tutapotaka heshima kwa chengine chochote, Mwenyezi Mungu atatudhalilisha.” Ili tubadilishe hali ya sasa ya udhalili ambayo Ummah wa Kiislamu unakabiliana nayo hakuna budi kuungana mkono na Hizb ut Tahrir ambayo inafanya kazi bila kuchoka kurejesha njia ya maisha ya Uislamu kupitia kuirejesha tena Khilafah kwa njia ya Utume kwa kuomba Nusra na usaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) pekee. Ili usiendelee kuishi chini ya udhalilifu hata kwa sasa.

أقيموا_الخلافة#
#ReturnTheKhilafah
#YenidenHilafet
خلافت_کو_قائم_کرو#

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Syed ibn Buhari

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu