Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hotuba ya Pili Katika Kongamano: ‘Vijana Waislamu …Waanzilishi wa Mabadiliko Msingi’

Kuwafanya Vijana Waislamu kuwa Masekula kupitia Mitaala ya Elimu

Thaqafa ya watu wowote huwakilisha uti wa mgongo wa uwepo wao na kudumu kwao. Juu ya thaqafa, hadhara yake hujengwa, dhamira na malengo yake hufafanuliwa, mpangilio wa maisha yao huwa wa kipekee kwake, watu wake huyeyushwa ndani ya chungu kimoja ili watafautishwe kupitia hiyo na mataifa na watu wengine. Njia ya kuhifadhi thaqafa ya Ummah ni elimu inayofanya kazi kujenga aqliya na nafsiya, na kukuza maadili, fikra na misingi ambayo kwayo utambulisho wa mtu huundwa katika mustakbali. Na kwa kuwa uhusiano kati ya udhibiti na elimu ndio msingi wa Magharibi, wamefanya kazi kuzidhibiti biladi za Kiislamu na kuzitawala kupitia kuifanya elimu kuwa ya kisekula, kama walivyo fanya kazi kuwaweka mbali Waislamu kutoka katika Dini ya Uislamu ili kuzuia uzalishaji wa utambulisho wa Kiislamu uliobeba hamu kwa Ummah na kadhia yake nyeti. Kwa sababu hii, wamejitokeza kukarabati mitaala ya elimu kwa mujibu wa mtazamo wao wa utandawazi na mielekeo ya kisekula. Hivyo, mitaala ya elimu sio tena jambo la kindani katika biladi hizi bali limekuwa ni jambo la kiulimwengu lenye lengo la kumomonyoa Itikadi (Aqeedah) ya watu wake na kuwasafisha mabongo yao kutokana na fikra na maadili. Na hilo limefanya mitaala hii ijengwe juu ya msingi mwengine usiokuwa Aqeedah ya Ummah. Bali imejengwa juu ya Itikadi (Aqeedah) ambayo inagongana nayo, ambayo kwayo inataka kugurisha thaqafa ya Kimagharibi kwa vijana na mabinti wa Ummah huu, tofauti na thaqafa ya Ummah wao ambapo ni njia hii ndio inayo dhamini utiifu kwao … Kasisi Dkt. Samuel Zwemer, akielekeza hotuba yake kwa wamishenari, alisema, “Mumewatayarisha vijana katika biladi za Waislamu ambao hawajui tena fungamano na Mwenyezi Mungu na hawangependa kulijua. Mumewatoa Waislamu kutoka katika Uislamu huku mukiwa hamkumsababisha kuingia kwao katika Ukristo. Zaidi ya hayo, yule aliyelelewa katika Uislamu amejitokeza kwa mujibu wa vile ukoloni ulivyotaka awe; hajali juu ya majanga na anapenda starehe na uvivu huku hamu yake maishani ikiwa haifuati isipokuwa matamanio yake”.         

Katika mchakato huu wa kuingiza usekula wametumia njia kadhaa ikiwemo kuangazia juu ya kupuuza lugha ya Kiarabu, na kuwaweka wanafunzi mbali nayo, huku wakiufanya ufundishaji wa lugha za kigeni sawa au hata juu kuliko Kiarabu. Hilo lilikuwa ni kwa ajili ya kuwaondoa ufahamu wa Ahkam za Qur’an (katiba yao) kwa njia ambayo ingeangazia kufikiria kwao na kuwafanya kutia bidii kwa ajili ya mwamko. Walifanya vivyo hivyo katika masomo ya Kiislamu kupitia kuyafanya kuwa ni masomo ya upili badala ya kuwa ni masomo ya msingi. Na huku ufundishaji wake ukiwa katika muundo wa kazi ya ziada ya nyumbani, kaida na kuwa somo linalo hitajika tu kupita mitihani kabla ya hatimaye kusahauliwa, badala ya kuwa liwe ndio msingi wa kujenga utambulisho wa Kiislamu kwa vijana. Na usisahau mtego wa elimu ya Kimagharibi na shule za kigeni, ambapo wamishenari wa Kikristo au wa kisekula, ambao kihakika ni kama vyombo vya kutia sumu yao hatari katika Dini, fikra, fahamu na tabia … Hivyo basi, matunda ya yote haya, yalikuwa ni kujenga msingi juu ya fikra huru, ambazo zilikuwa si za Kiislamu. Yote haya, huku Uislamu ukitazamwa kana kwamba ni dini ya kikasisi tu iliyotenganishwa na maisha na ambayo ilihusishwa na ibada pekee na sio katiba na njia ya maisha, kuongezea na kutokuwa na uhusiano au umuhimu kwake na maisha yao ambayo ina athari juu ya fahamu na tabia zao … Mwanamke alikuwa na mgao wake kuhusiana na mabadiliko haya ndani ya mtaala huo; walifanya bidii kubadilisha sura na dori yake msingi ndani ya mujtama, ambayo waliita ‘Kubadilisha Unyanyapaa Wake!’ kupitia kumfanya ang’ang’ane kuwa mwanamke mchapakazi pekee na sio mke nyumbani. Hivyo basi wakalitoa somo la usimamizi nyumbani nje ya mtaala huo, ambalo linajumuisha ndani yake mada ambazo zingemsaidia msichana kupata elimu kuhusu dori yake msingi. Pia wakatangaza vita dhidi ya kile wanachokiita ‘ndoa ya mapema’ huku wakiimba kuhusu umakinifu wake wa kiuchumi na uhuru wake. Wakawashajiisha wanafunzi kujihusisha katika amali, safari, miradi na vyama ndani na nje ya shule kama vile matukio na sherehe zisokuwa za Kiislamu, ambazo aghalabu huhusisha kuchanganyika baina ya wanaume na wanawake, zikionyesha miili na ukiukaji wa hukmu za sheria.

Ndio, dada zangu … Wanataka kudhamini kukuuza kizazi ambacho kwa jina ni cha Waislamu lakini kidhati na kimsingi ni cha kimagharibi. Kizazi ambacho kitaishi katika biladi ya Kiislamu lakini kitamiliki ada na maadili ya mujtama wa kimagharibi. Kizazi ambacho ni watoto wa ‘Umar, Ali na Salahuddin lakini chenye kuamini kuwa kila ulinganizi wa kurudisha Uislamu halisi una wakilisha ulinganizi wa ugaidi, urudishaji nyuma, na upotofu, na wala sio ulinganizi wa mwamko. Na ili wasimame wenyewe kuwa kizingiti mbele ya kurudi kwa Uislamu na dhati yake.

Dada zangu waheshimiwa:

Wakoloni wamezikadiria sera za elimu kuwakilisha moja ya sehemu muhimu ambazo ni lazima wazidhibiti juu yazo. Hivyo wanaingilia mitaala, shule na sera za elimu katika biladi kadhaa kama Misri, Pakistan, Saudi Arabia na Yemen. Kwa mfano, usaidizi mkubwa ambao Amerika imetoa kwa serikali ya Musharraf nchini Pakistan ili kuzifuatilia madrassa na kuvipiga marufuku vitabu vya shule katika masomo yote kutokana na uhusiano wake wowote na Uislamu. Hii ikiwemo kufuta mada ya Al-Walaa’ Wa-l-Baraa’, Ayah za Jihad na kuchafua baadhi ya ufafanuzi wa Itikadi (Aqeedah) ndani ya sayansi ya Shari’ah nchini Saudi Arabia. Yote hayo, kwa mujibu wa madai yao na visingizio vyao, yanafanywa ili kuzuia ‘ugaidi’ kuibuka katika madrassa hizo!! Vile vile, nchini Palestina na baada ya kuwasili kwa yale yanayoitwa ‘Mamlaka ya Palestina’ mitaala imebuniwa inayofanya kazi kuuvunja Uislamu ndani ya nafsi za vijana Waislamu na kuwabadilisha kuelekea ukafiri wa usekula kupitia kuzivuruga akili zao kwa fahamu zilizo mbali na Uislamu. Ama kwa Misri Al-Kinanah, wamefuta nususi zote zinazo husiana na vita kwa Mayahudi huku zikitukuza amani na maelewano. Pia wamefuta masomo yanayo jadili watu wenye utambulisho wa Kiislamu kama Salah ud-Deen Al-Ayubi na ‘Uqbah Bin Naafi’ wakidai kuwa masomo haya yanachochea misimamo mikali na ghasia huku wakifuta zaidi Hadith za Mtume (saw) zinazo shajiisha Jihad. Hii ni ikiongezewa na kurudia hadhara ya Kifirauni kama mwakilishi wa historia ya Misri huku wakipuuzia kwa ukamilifu ufunguzi wa Uislamu katika historia yake yote.

Ama kwa hapa Tunisia, Bourguiba alikipiga marufuku Chuo Kikuu cha Zaytuna na kubuni shule ambazo mwelekeo wa kisekula wa kimagharibi umetawala. Aliingiza ufundishaji wa lugha za kigeni katika umri mdogo, huku akiwaweka mbali wanafunzi kutoka na elimu ya Kiislamu akiibadilisha kwa thaqafa ya kijamii ambayo kwayo mwanafunzi atafunzwa sheria za kibinadamu na mafungamano fisidifu kama uzalendo na utaifa.

Kamwe hatutadharau dori ya mashirika ya vijana, vyama vya wanawake na taasisi za kimagharibi kama USAID, UNICEF, UNESCO na Baraza la Uingereza, ambayo upande mmoja yanatoa usaidizi kwa wanafunzi na elimu na ustawi, huku kindani (na kwa uhalisia) yakiwa na sumu hatari kupitia kutia usekula fikra na fahamu. Hii ni kiasi kuwa mazingira na anga jumla ndani ya shule hizo yawe ya kikafiri na haswa yawe ya kisekula, ambapo Magharibi inapewa sura nzuri na ya kuvutia huku Uislamu ukionyeshwa kuwakilisha mafungamano na mipaka inayozuia uhuru, kuregesha nyuma na ni kikwazo kwa maendeleo na mwamko. Sura inayotolewa ni Magharibi inawakilisha maendeleo, ufanisi na hadhara tajiri ambayo inapaswa kufanya bidii kuwa kama wao na kuendelea mbele kupitia njia yake!! Hivyo tunawaambia kuwa Mwenyezi Mungu Ta’ala amesema:    

وَلاَ تَرْكَنُواْ إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُواْ فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللّهِ مِنْ أَوْلِيَاء ثُمَّ لاَ تُنصَرُونَ]

“Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa” [Hud: 113].

Dada zangu waheshimiwa:

Hii ndio hali ya sasa ya elimu ndani ya biladi za Waislamu na hivyo tufanye nini kuhusiana na vijana na wanafunzi wetu?! Ni ipi njia sahihi ili tuwafunze watoto na wanafunzi wetu Uislamu ima kama wazazi au walimu?

Kama tulivyo taja, hatupaswi kuingiliana na Uislamu wa sasa juu ya msingi kuwa ni somo tu la kusomwa au kupata maalumati yanayo jaza karatasi za mtihani na mwanafunzi kupata shahada kupitia kwayo, huku ikiishia hapo. Bali, ni lazima tukuze fahamu zinazo pelekea mabadiliko ya kifikra na baada ya hapo mabadiliko ya tabia na mwenendo. Ni lazima tuwaunganishe na uhalisia ili uwaguse na kuufahamu ili kuharakisha utekelezaji wake … Hivyo tunapowapa somo lolote kama ‘Ibaadat (vitendo vya kiibada) au Akhlaq (maadili), ushairi, historia au sayansi, sio mujarrab tu wa kupeanwa kama elimu ya nadharia pekee.  Bali tutaiunganisha na uhalisia na Ahkam Ash-Shari’ah ambazo zitawanufaisha katika kujenga fahamu na tabia au mwenendo wao.   

Hivyo kwa mfano, tunapo ifafanua Swala, hatuwafunzi tu ni Rakaa ngapi, tunasema na kufanya nini, bali kuwa ni nguzo (Rukn) ya Dini na kuwa kupitia kutengea kwake kitendo hutengea na kwamba ni lazima iwe yenye kukataza na kukinga kitendo chochote kiovu na kichafu. Na tunapo wafunza usomaji wa Qur’an, tunapanda ndani yao kuwa inawakilisha katiba (Dustoor) ya maisha ya kujifunga na kuitekeleza, na kwamba sio tu ya kusomwa wakati wa Ramadhan, mazishini au kabla mitihani. Kwa kuwa inawakilisha Ahkaam Shariah zinazotakiwa kujifunga kwazo na kuzitekeleza katika ngazi ya mtu binafsi na dola… Hivyo hivyo pia kuhusiana na mambo ya kimaumbile yanayo somwa katika sayansi ambapo kwa mfano hatutayaunganisha tu kwa matendo ya kimada pekee bali pia tutawasilisha upande wa Kiimaani kwa kuyaunganisha na Muumba wake (swt) kama yalivyo jitokeza katika Ayah za Kitabu chake Kitukufu. Hivyo hivyo pia kwa Akhlaq, Muamalaat, historia, fizikia na teknolojia miongoni mwa masomo mengine kupitia kuyaunganisha kwa njia ya kuendelea na thaqafa ya Kiislamu, Aqeedah na Ahkam, na fahamu na tabia…   

Najua dada zangu kuwa jambo hili si rahisi kiuhalisia kwamba tunakabiliwa na vita dhidi ya Uislamu na waumini wake. Lakini, ni wajib juu yetu kupunguza madhara yanayo tokana na vita hivi. Najua kuwa utekelezaji wa Uislamu unakosekana kutokana na kukosekana dola ya Kiislamu inayo utabikisha kwa upana na ukamilifu… Ni dola hii ndiyo itakayo dhibiti ndani yake elimu ambayo mtu anaihitaji katika uwanja wa vita vya kimaisha kama wajib. Ni jukumu lake kutoa elimu bila ya malipo kwa kila mtu, mume au mke, katika viwango vya msingi na upili. Hii ni huku ikifungua fursa kwa elimu ya zaidi na ya juu bila malipo kwa wote kwa kadri ya uwezo wake… Sio kama hali ilivyo sasa ambapo watu wakati mwengine hujinyima chakula chao ili waweze kuwapa watoto wao elimu!! Ni dola ambapo lengo la elimu liko juu ya mambo mawili:

La kwanza ni kujenga utambulisho wa Kiislamu, aqliya na nafsiya, na hilo ni kupitia kukuza thaqafa ya Kiislamu kama Aqeedah, fikra na tabia ndani ya akili za wanafunzi na nafsiya zao za ndani. Kwa sababu hiyo, wale wanao andaa mitaala na kuitekeleza ndani ya dola ya Khilafah watakuwa makini kufikia lengo hilo…

Jambo la pili ni utayarishaji wa watoto wa Kiislamu ili watoke miongoni mwao wasomi wanao chukua taaluma katika kila nyanja ya maisha ima iwe katika sayansi za Kiislamu (kama Ijtihad, Fiqh na Mahakama miongoni mwa nyanja nyenginezo) au katika sayansi za kiutafiti (kama uhandisi, kemia, fizikia, utabibu na nyenginezo), wasomi wenye uwezo watakao ibeba dola ya Kiislamu na Ummah wa Kiislamu mabegani mwao ili ichukue nafasi ya kwanza ya uongozi miongoni mwa mataifa na dola za ulimwengu. Hapo ndipo itakapo kuwa dola inayo ongoza, dola iliyo barabara na mfumo wake, na sio dola ya kitumwa na kibaraka katika fikra na uchumi wake kama hali ilivyo sasa katika ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu… Itakuwa ni Dola ambapo shule itakuwa ndio chimbuko la kwanza la ujenzi wa watu wenye utambulisho wa kipekee wa Kiislamu, katika nyanja za Usool ul-Fiqh, lugha na Tafseer. Kama itakavyo kuwa chimbuko la kwanza la ujenzi wa watu waliomakinika katika nyanja za elimu inayohusiana na chembe (atom), anga na tarakilishi nk…. Ni dola ambayo sote tuna hamu ya kuishi ndani ya boma lake na chini ya kivuli chake…    

Twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kuharakisha kurudi kwa Khilafah kwa njia ya Utume ili watoto wetu waweze kusoma chini ya kivuli chake na kuondolewa fikra za kirasimali pamoja na ufisadi na madhara yake yote… na twataraji kuwa siku itakuwa karibu…

Muslimah (Umm Suhaib) Ash-Shaami

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 07:34

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu