Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Je ni kweli wanakataa “ndoa za mapema”?!

Katika Kampeni: Familia: Changamoto na Suluhisho za Kiislamu

(Imetafsiriwa)

“Ndoa ya mapema ni tabia ya aibu." "Ndoa ya mapema ni msiba kwa mvulana na msichana." "Ndoa za mapema hupelekea matatizo ya kiakili, kiafya na kifamilia na kupoteza haki za watoto." Kauli hizo ndizo zinazojirudia mara kwa mara katika semina na makongamano yanayofanywa na taasisi za wanawake au vituo vya haki za binadamu. Na hata katika mabunge ya nchi nyingi wanapotunga sheria za familia mara nyingi huwa wanaongeza umri wa kuoana au wanapendekeza sheria ya kuzuia ndoa kwa vikundi vya vijana kwa umri maalum.

Mashirika ya wanawake – yanayoshirikian na nidhamu zinazowadhamini za Kimagharibi – hupangilia semina ambazo huwaonya dhidi ya ndoa za mapema, wakilingania wazazi wapigane nazo na hata kutaka sheria zinazozuia ndoa za "wasichana waliovunja ungo." Hili lilitokea Misri, ambayo iliweka umri wa ndoa ni kutimu kwa miaka 18 kama ilivyo katika tovuti ya bunge la Misri mnamo 9/9/2017 ambayo inasubiri kujadili sheria itakayowasilishwa Bungeni ili kuzidisha umri wa ndoa kuwa miaka 21. Hili pia limefanyika ndani ya Morocco ambayo iliweka umri kuwa miaka 16 kwa wasichana na miaka 18 kwa wavulana. Kwa hiyo umri wa kisheria imekuwa ni moja ya masharti ya ndoa ambapo ndoa haiwezi kukamilika ikiwa hautimu. Hii ni kwa mujibu wa makubaliano ya Kimagharibi yanayokwenda sambamba na haya kama makubaliano ya CEDAW ambayo yamejifunga juu ya kanuni na sheria zinazohusiana na kanuni za mahusiano ya wanawake na wanaume. Pia yanatakiwa kutekelezwa na dola zilizotia saini na ziweke sheria zinazokwenda sambamba ndani ya nchi hizo. Lakini swali ni: kwani haya makubaliano ya kimataifa yanalenga kuzuia ndoa za mapema na kuzitizama kama uhalifu dhidi ya watoto na ukiukaji wa haki zao ambazo hutekelezwa kiasili?

Kwa mujibu wa Gazeti la "Al-Sharq Al-Awsat" mnamo 18/5/2010 kwa kichwa: Idadi hii kubwa ya watoto wenye mimba" ilitaja "Idadi ya kina mama wenye mimba ambao hawajaolewa ni zaidi ya asilimia 70 kuliko ile ya kina mama walioolewa, Asilimia 55 ya watoto wanawake 1,000 wana mimba. Asilimia 68 ya watoto waliozaliwa UK ni kutoka kwa wazazi ambao hawakuoana. Chaneli ya MBC iliripoti mnamo 23/1/2012 kuhusu ripoti ya mabarobaro wenye mimba kwa kichwa "Kiwango kikubwa duniani na umri wao ni baina ya miaka 15 na 19: Mabarobaro Waamerika wanazaa watoto elfu 400 kwa mwaka nje ya ndoa," ikisema kwamba Amerika ndiyo iliyo na idadi kubwa ya wanaozaa miongoni mwa mabarobaro wasichana ndani ya ulimwengu ulioendelea." MWISHO.

Takwimu zinazofichua idadi ya watoto ambao wanahangaishwa, wanabakwa, mahusiano ya watoto shuleni ndani ya Amerika na wasichana walio na mimba ndani ya shule za Kimagharibi ni kubwa mno na hakuna hakuhitajii kuelezea kwa mapana.

Hivyo basi, makubaliano yote ya kimataifa ambayo yanatekelezwa kwa msaada wa serikali za vibaraka ndani ya ardhi za Waislamu na tukizingatia kuwa ni sheria kamilifu za kupangilia mahusiano ya familia na mahusiano ya Waislamu wanaume na wanawake sio sahihi kwa wale waliotuwekea na sio jambo la kushangaza kwa sababu yule ambaye hana kitu hawezi kuwapa wengine kitu. Inawezekanaje kuchelewesha umri wa ndoa katika nchi zetu ilhali wao wanasambaza tembe za kudhibiti mimba kwa wanafunzi shuleni mwao ili kupunguza viwango vya watoto wanaozaliwa kwa uzinifu?? Au midomo yao inaficha yale ambayo mioyo yao inaficha?

Na wafikishia kauli inayohusiana na mada hii, nikifupisha shambulizi juu ya ndoa za mapema licha ya kuwepo kwa sheria za uhuru wa kibinafsi zilizowekwa na makubaliano hayo hayo yanayofanya ndoa za mapema ni uhalifu. “Sio jambo la mzaha na kuhuzunisha kwa wakati mmoja kuzindua neno "ndoa za watoto" kwa ndoa za wasichana wa umri wa miaka 17 na hata kuzingatia kuwa ndoa hii ni janga kwa msichana na wakati huo huo mwili wa msichana ukazingatiwa kuwa ni wake pekee na kwamba ana uhuru wa kuutumia kivyovyote anavyotaka na kwamba hakuna mtu ana haki –yeyote atakayekuwa- kumdhibiti yeye msichana na mtizamo wake wa kijinsia hata kama ni babake au mamake lakini anayo haki ya kuwalaumu wazazi wake wanapo muudhi na kuingilia uhuru wake binafsi?"

Vita dhidi ya ndoa za mapema sio natija ya leo, bali ni tukio katika msururu wa masuala yaliyobuniwa ndani ya vita dhidi ya Uislamu na hukmu zake. Lakini, tutazitafsiri vipi ndoa za mapema kuwa ni hatari kwa afya ya mtoto wakati anapokuwa ana mimba ilhali ipo sheria chini ya makubaliano ya CEDAW na mengineyo ambayo yanawataka mabarobaro wenye mimba kuendelea na elimu zao pasina kulaumiwa na kubeba mimba za uzinifu pamoja na kupitisha sheria ili kupambana na mimba za uzinifu na kumpa chaguo msichana ima kuiavya mimba au kuibeba?

Mashtaka na majadiliano ya kirongo yanadhihirisha kuwa si sahihi kiutabibu na kiuhakika na kwamba kilichofanywa kuwa batili kwa ushahidi wa kukata na takwimu za viwango vya kujifungua, vifo na umri wa mama sio chochote bali ni kelele za mzaha zinazolenga sio kuwalinda watoto au kuwakomboa wanawake bali ni kuweza kuwarahisisha wanawake. Kwa uwazi zaidi ni juhudi kubwa za kuupiga Uislamu na hukmu zake zinazohusiana na familia na kuulinda mujtama kutokana na majanga ya ufisadi na uchafu. Na kila mtu anayeunga mkono au kuhalalisha sio chochote bali ni kuudunga moyo wa Ummah. Sijawasaza hapa wale wanaojaribu kuoanisha vipengee vya Uislamu au kuvitafsiri ili viendane na sheria za kimataifa. Ndoa za mapema zinaruhusiwa ndani ya Uislamu; ni hukmu ya Mwenyezi Mungu (swt) na haistahili kwa mtu yeyote kuikejeli au kuipima kiakili kwa kisingizio cha kuilinda Dini ya Mwenyezi Mungu (swt)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bayan Jamal

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 06:55

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu