Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 “Mwanzo wa Mwisho wa Jaribio la Kiamerika”

Na: Dkt. Abdullah Robin

Waamerika wamefungiwa katika majumba yao kwa kuogopea kirusi kipya ambacho kimeuwa zaidi ya Waamerika 100,000 mwaka huu, lakini kifo cha mwanamume mmoja pekee mnamo Mei 25 kimewatoa barabarani kufanya maandamano, kupora na kuwasha moto kukileta hofu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

George Floyd mwenye umri wa miaka 46 aliuwawa na polisi katika mji wa Minneapolis. Alikuwa amenunua sigara kwa kutumia bili ya dola 20 ambayo muuza duka aliishuku kuwa ghushi, lakini kosa lake ni kuwa alikuwa mtu mweusi. Hakukataa kukamatwa, lakini afisa wa polisi mwenye ngozi nyeupe, Derek Chauvin, akapiga goti juu ya shingo ya Floyd kwa takriban dakika 9 licha ya mwathirika kulalamika kuwa hawezi kupumua na kulilia mama yake kabla kunyamaza. Akawa hafurukuti katika dakika tatu za mwisho kabla ya polisi kuenua goti lake kutoka katika shingo ya mtu huyo mweusi aliyepoteza uhai, hata ingawa watu wengi katika eneo hilo la tukio walimuomba afisa huyo wa polisi kuondoa goti katika shingo ya mwanaume huyo. Maafisa wengine watatu polisi walikuwa wakitazama, lakini George Floyd alilala kwa kuzuiliwa vibaya shingoni na Derek Chauvin hata wakati kikosi cha maafisa wa gari la wagonjwa walipokuwa wanamuangalia mapigo yake ya moyo, kabla ya kupelekwa hospitalini ambapo alitangazwa kufariki. Watu weusi nchini Amerika wamepata shida sana na vurugu la ubaguzi wa rangi na unyanyasaji kwa zaidi ya miaka 200, lakini tukio hili limevutia hisia za watu nchini Amerika kwa njia ya kihistoria na maandamano kuzidi kila kukicha.

Ubalozi wa Amerika umelengwa jijini London, Paris, Berlin, Copenhagen na Mexico huku Amerika ikigeuka kuwa ishara ya unyanyasaji kote ulimwenguni. Trump ameshajiisha vurugu, akiitisha waporaji kupigwa risasi na vikosi vya majimbo ya Amerika kuchukua udhibiti licha ya uhalisia kwamba kila jimbo liko na jeshi lake la polisi na Ulinzi wa Taifa. Trump ametangaza kwamba yeye ni “rais wako wa sheria na utangamano” na lakini vikosi vyake vya usalama viliharibu maandamano ya amani nje ya Ikulu yake kwa kutumia vitoa machozi, risasi za mpira na vilipuzi vya sauti ili kwamba Trump apate fursa ya kupiga picha huku ameshikilia bibilia nje ya kanisa karibu na Waziri wake wa Usalama akiwa amevalia sare za kijeshi.

Washiriki wa zamani wamejitenga na Trump. John Allen, generali mstaafu wa kikosi cha Baharini cha nyota nne alijibu akisema “kwamba hiki ndicho kinachotokea katika tawala za kimabavu. Hiki ndicho kinachotokea katika tawala zisizokuwa huru. Hakitokei Amerika, na Hatupaswi kukivumilia.” Akaendelea kusema kwamba matendo haya “yanaweza kuashiria mwanzo wa mwisho wa jaribio la Kiamerika.” Aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Trump, James Mattis, amesema, “Donald Trump ni rais wa kwanza katika maisha yangu ambaye hajaribu kuunganisha watu wa Amerika – hajaribu hata kujifanyisha. Badala yake anajaribu kutugawanya…. Nilipojiunga na jeshi, takriban miaka 50 iliyopita, nilichukua kiapo cha kusaidia na kulinda Katiba. Sikuwahi kufikiria kwamba vikosi vinavyo chukua kiapo sawia vitaamrishwa kwa hali yoyote kuenda kinyume na haki za kikatiba za raia wenzao – kando na kuonyesha vurumai kwa ajili ya Kamanda Mkuu wa majeshi aliyechaguliwa na raia kupata fursa ya kupiga picha huku uongozi wa kijeshi ukisimama pamoja naye". Seneta mmoja wa Republican amesema, “Nilipoona maoni ya Jenerali Mattis jana, nilihisi kama pengine tunaelekea katika hatua ambayo tunaweza kuwa wakweli zaidi na wasiwasi ambao tunaobeba kindani na tukawa na ujasiri wa imani zetu wenyewe kuuzungumzia.” Jibu la Trump kwa seneta huyu kutoka chama chake mwenyewe ambaye anatafuta kuchaguliwa tena mnamo 2022 lilikuwa la kawaida, “Eka mgombeaji yeyote tayari, mzuri au mbaya, hilo sijali, nitamuidhinisha. Kama una mapigo, niko na wewe! ” Trump anakabiliwa na uchaguzi mwingine mnamo Novemba, lakini aliyekuwa mkuu wake wa Ikulu ya White House, John Kelly, alisema, “Nadhani tunahitaji tumuangalie kwa makini yule tunayemchagua,” na akakinzana na baadhi ya madai ya Trump kuhusu James Mattis.

Kile kinacho endelea sasa Amerika ni zaidi ya mwamko wa nchi dhidi ya ubaguzi wa rangi. Kuna uasi dhidi ya utawala wa Trump. Mmoja wa washirika wa karibu wa Trump, Senata Lindsey Graham wa Carolina Kusini, alimtetea Trump: “Kutoka wakati rais Trump anapoamka mpaka anapoenda kulala kunajitihada za kuharibu urais wake”. Kinacho fanya hii hali kuwa hatari sana kwa Amerika ni kwamba Trump yuko na msaada thabiti maarufu kutoka kwa wapiga kura wengi ambao wanajihisi wenyewe kuwa kama wametelekezwa na kuhiniwa kama wale wanaoteseka na ukatili wa askari na ubaguzi wa rangi, na Trump anaonekana kama bingwa wao.

Kwa ajili ya kutuliza taharuki, polisi na idara ya haki zimewaadhibu na kuwashtaki maafisa waliohusika katika mauaji ya George Floyd na matendo mengine ya kikatili kote nchini, na wakati hatua hizi zilipokosa kuwaridhisha umati wa watu, hatua dhidi ya maafisa zimeongezwa. Hata hivyo, utoaji majibu umeanza. Maafisa wa polisi hamsini na saba eneo la buffalo, New York, wamejiuzulu kutoka katika kitengo cha msaada wa dharura katika jeshi hilo baada ya kusimamishwa kazi kwa maafisa wawili ambao walinaswa katika video inayoonekana wakimsukuma mwandamanaji mzee mwenye umri wa miaka 75 mpaka chini ambaye alikuwa akiandamana baada ya amri ya kutotoka nje usiku kuamrishwa. Mwanamume mmoja aliyekamatwa kwa kuvamia wasichana wawili ambao waliunga mkono maandamano hayo na mwanamume mwengine akichomelea minyororo na akitoa matusi ya kiubaguzi wa rangi ni ushahidi wa namna hisia zilivyo kita katika pande zote mbili. Amerika imegawanyika kwa uchungu sana, na sasa haina hakika kwake yenyewe au haina hakika ya nafasi yake ulimwenguni.

*Imeandikwa kwa Ajili ya Gazeti la Ar-Rayah – Toleo la 290

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu