Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Umbile la Kiyahudi Linaweka Kielelezo Hatari - lakini kwani ni wa Kwanza Kufanya Hivyo?

(Imetafsiriwa)

Matendo ya umbile la Kiyahudi yanatia wasiwasi wachambuzi kote ulimwenguni ambao wanashangaa kutojali kwao waziwazi sheria ya kimataifa kunamaanisha nini kwa mustakabali wa maadili yote ambayo wanayaenzi mno. Sababu ya hii ni kwa sababu ya umuhimu ambao ‘kielelezo’ kinashikilia katika sheria ya Kimagharibi. Inastahili kusaidia kuhakikisha kuwa kuna uthabiti, kutegemewa, na kutabirika katika maamuzi ya mahakama ili kuongeza imani katika mfumo wa mahakama.

Kupitia mara kwa mara, utegemezi, kutabirika na kwa uwazi kuonyesha kutojali kila kipengee muhimu cha sheria zao za kimataifa, umbile la Kiyahudi limefanya watu kuogopa mustakabali wa mfumo.

Hivi majuzi zaidi, wakati wabunge wa Kiyahudi walipopitisha sheria mbili za kukata mafungamano na UNWRA, wakitishia shirika hilo linaotoa misaada kwa watu wa Gaza kwa kulizuia kufanya kazi katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya Palestina. Chini ya sheria ya kwanza, shirika la Umoja wa Mataifa, lingepigwa marufuku kufanya “shughuli yoyote” au kutoa huduma yoyote ndani ya umbile la Kiyahudi. Sheria ya pili ingekata mafungamano ya kidiplomasia ya umbile la Kiyahudi na shirika hilo. Linalibandika shirika hilo la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) kuwa ni kundi la “kigaidi” na kulipiga marufuku shirika hilo la kibinadamu kufanya kazi katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya Palestina.

“Sheria tuliyopitisha sasa sio mswada mwingine tu. Ni wito wa haki na wito wa mwamko,” alisema mbunge Boaz Bismuth, ambaye alidhamini moja ya miswada hiyo. “UNRWA sio shirika la msaada kwa wakimbizi. Ni shirika la misaada kwa Hamas.”

Mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini, wakati huo huo, alisema hatua ya Knesset iliweka “kielelezo hatari” kwani “inapinga Mkataba wa Umoja wa Mataifa na kukiuka majukumu ya Dola ya ‘Israel’ chini ya sheria ya kimataifa”. (Chanzo)

Uamuzi huu unaashiria hatua ya hivi punde zaidi ya umbile la Kiyahudi ya kutojali Umoja wa Mataifa na mashirika yake mbalimbali. Pia ni moja tu ya hatua katika kukataa waziwazi kwa umbile la Kiyahudi kutii sheria ya kimataifa. Wamepuuza sheria za haki za binadamu, wamepuuza uharamu wa kuikalia kwa mabavu Gaza na Ukingo wa Magharibi, wametumia silaha haramu za fosforasi nyeupe, na wamekataa kuruhusu msaada kuwafikia watu wa Palestina. Wameshajiisha makaazi haramu katika maeneo yote ya Wapalestina, wamehalalisha kupuuza kwao sheria zinazosimamia vita, na wameanzisha mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari na wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa, na kuanzisha mashambulizi ya droni katika maeneo yaliyotengwa na Umoja wa Mataifa huko Gaza. Na kisha kuna mashambulizi ya Lebanon na kushambuliwa kwa ubalozi wa Iran nchini Syria.

“Madhara ya kitendo hiki ni makubwa, sio tu ya kisiasa lakini pia kisheria. Shambulizi hili linakinzana waziwazi na kanuni zilizowekwa za kinga ya kidiplomasia, kanuni ambayo imekuwa msingi wa sheria ya kimataifa kwa karne nyingi. Kwa kuchukua hatua hii kali, uongozi wa Israel umeonyesha kutojali waziwazi viwango hivi vya kisheria vya kimataifa.” Chanzo

Wamefanya vitendo hivi vyote chini ya kivuli cha ‘haki ya kujilinda’, wakifinika kila aina ya vitendo vinavyodaiwa kuwa haramu chini ya sheria ya kimataifa na kupuuza pingamizi za UN na mashirika ya haki za binadamu kote ulimwenguni.

Kilio cha kimataifa kimekuwa kikubwa. Kwa hivyo kwa nini Marekani na maafisa katika mataifa mengine ya Magharibi wamekanusha kwa kudumu, kutafsiri vibaya au kukataa kukubali ukweli ambao sisi sote tunashuhudia? Je, hawana akili au wamedanganywa tu?

Ni salama kwa salama, kwamba katika hali nyingi, sio sawa hivyo. Suala ni kwamba hawawezi kukiri kile kinachotokea - kwa sababu hapo watapaswa kuchagua kati ya sheria ya kimataifa inayowaruhusu kudumisha udhibiti juu ya ulimwengu mzima na hamu yao ya kuliunga mkono umbile la Kiyahudi, na hawawezi kufanya hivyo hadi mpango wao wa eneo uzae matunda.

Lakini pia wanapaswa kuzingatia mstari kwa uangalifu, kwa sababu ikiwa wanakiri waziwazi kwamba wanaruhusu uvunjaji mkubwa wa sheria ya kimataifa (bila hoja ya kisheria) wanawezaje kumhisabu mtu mwengine yeyote katika siku zijazo? Na ndiyo maana kila mtu hutembea akishangaa kwa kile kinachoonekana kama ujinga mtupu.

Tukiangalia nyuma katika chaguo la Netanyahu tukilinganisha 9/11 na Oktoba 7, sio chaguo dogo, ingawa labda itakuwa sahihi zaidi kulinganisha na Vita vya Iraq, angalau katika muktadha wa makala haya, kwa sababu sheria ya kimataifa, na uchambuzi wa kisiasa, ilikuwa ndio nukta ya mabadiliko katika historia. Marekani haikukaidi tu sheria ya kimataifa, kukiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa (UN) na kanuni zinazosimamia utumiaji nguvu, pia walibadilisha jinsi dola zinavyotafakari vitisho, jinsi zinavyohalalisha hatua za kijeshi, na jinsi sheria za vita zinavyobadilika kuendana na ongezeka la watendaji wasio wa kiserikali mithili ya makundi ya kigaidi. ‘Vita dhidi ya Ugaidi’ vilivyofuata vilibadilisha sheria ya kimataifa na kuweka msingi wa uwezo wa umbile la Kiyahudi kuhalalisha mashambulizi yao dhidi ya Gaza kwa hoja kwamba kihakika ni vita dhidi ya Hamas.

Sasa, kwa mujibu wa sheria ya Kimataifa, Vita vya Iraq vilikuwa haramu. Lakini wakati huo, hakukuwa na matokeo, Marekani haikuwajibishwa, na hivyo chaguo la dunia la ‘kulaani’ tu kitendo hicho ulitupatia Vita dhidi ya Ugaidi ambavyo vimedumu kwa zaidi ya miongo miwili. Na sasa, miaka 23 baadaye, tumekuwa tukitazama kwa hofu na kuchukizwa huku umbile la Kiyahudi likifanya vitendo mithili ya hivyo mjini Gaza.

Inakufanya ujiulize, kwa vielelezo hivi vilivyowekwa, je, mustakabali utaleta nini? Amerika ilianzisha uhalali wa kisheria kwa kuvamia dola halali ili kukomesha dhidi ya maslahi yao ya kitaifa. Umbile la Kiyahudi limechukua uhalali huo wa kisheria na kuupanua kwa viwango vya kutisha.

Na bado, kwa mara nyengine tena, tunachoona ni marudio ya shutma na ukanushaji. Je, tunafikiri kwamba mambo yatakuwa mazuri? Hayakuwa hapo awali, kwa kweli ni mabaya zaidi. Viongozi wa dunia wameshindwa kuiwajibisha Marekani - na umbile la Kiyahudi – kuliwajibisha tena, hilo lenyewe linaweka kielelezo kwa hatua zozote za siku zijazo ambazo dola yoyote itazichukua.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fatima Musab
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu