Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Umma wa Kiislamu Unawatazamia Makamanda wake wa Kijeshi Kuzuia Kuteketezwa kwa Quran Tukufu

(Imetafsiriwa)

Baada ya hisia kali za umma, Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif alitoa wito wa maandamano ya nchi nzima mnamo tarehe 7 Julai 2023 ili kutetea utakatifu wa Qur'an Tukufu, na kuandamana dhidi ya tukio la hivi majuzi la kudhalilishwa kwake nchini Uswidi. Mamlaka za Uswidi zilivuka mstari mwekundu tena ziliporuhusu kuchomwa kwa Qur'an Tukufu katika siku iliyobarikiwa ya Idd ul Adha mnamo Juni 28, 2023. Gazeti la DW la Ujerumani liliripoti kwamba wanaume wawili walisimama nje ya msikiti mkuu wa Stockholm mnamo siku ya Jumatano na kuchoma Quran, kufuatia idhini iliyotolewa na mahakama ya Uswidi. Hii si mara ya kwanza kwa Quran Tukufu kuchomwa moto nchini Uswidi. Mapema mwaka huu, mwanasiasa wa siasa kali za mrengo wa kulia wa Uswidi na mchochezi wa chuki dhidi ya Uislamu Rasmus Paludan aliteketeza Qur'an Tukufu mbele ya ubalozi wa Uturuki nchini Uswidi chini ya ulinzi wa serikali ya Uswidi.

Mwitikio rasmi kutoka kwa Uswidi na Magharibi kwa upana umekuwa wa kutabirika: Kuchomwa moto kwa Quran tukufu ni uhuru wa kuzungumza na kwa hivyo maadili haya ya Kimagharibi yatalindwa mbele ya hasira ya Waislamu. Mkuu wa muungano wa vita vya msalaba NATO, Katibu Mkuu Jens Stoltenberg alisema mnamo tarehe 29 Juni 2023 kwamba anaelewa hisia zilizosababishwa na kuchomwa moto kwa nakala ya Quran nchini Uswidi lakini akahimiza kuwepo kwa maridhiano juu ya kujiunga kwa Uswidi katika NATO.

Mwitikio kutoka kwa watawala waoga na vibaraka wa ardhi za Waislamu, zamani na sasa, haukuwa na athari kwa makruseda wa Ulaya. Shutma nusunusu na zisizo na maana zinazotolewa na watawala wa Kiislamu ni jambo la kawaida tu. Hata hazijachukuliwa kwa uzito na Umma wa Kiislamu. Waislamu hawana matumaini kutoka kwa watawala hawa na ile inayoitwa jumuiya ya kimataifa na taasisi zake kama vile Umoja wa Mataifa na mashirika ya Haki za Binadamu. Haya kwa hakika yanalinda unyanyasaji na fedheha ya Aqidah ya Kiislamu na kutoa hifadhi ya kisheria kwa uvamizi wa kikatili wa Kimagharibi na unyonyaji wa ardhi za Kiislamu.

Kitovu cha matumaini ya Ummah kiko kwa watu wa vita. Hawa ndio watu wanaoweza kubadili mkondo katika kuupendelea Uislamu na Umma katika muda wa saa chache, kupitia kuhamasishana kusimamisha ngao ya Waislamu, Khilafah. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam ni ngao watu hupigana nyuma yake na hujilinda kwaye.” [Muslim].

Umma wa Kiislamu unamtafuta Saad ibn Muadh (ra) miongoni mwa makamanda wake wa kijeshi ambaye atasimama na kusimamisha ngao ya Uislamu, Khilafah, ambaye atalipiza kisasi cha kunajisiwa Aqidah yetu na kukomesha utiifu wetu wa kisiasa na kiuchumi kwa Magharibi. Tangazo tu la kuanzishwa kwa Khilafah litawalazimisha makafiri hao waoga kuharakisha kurudi mafichoni. Tunahisi hasira za ndugu zetu katika majeshi ya Pakistan kama vile majeshi mengine kutoka nchi za Kiislamu. Wakati umewadia sasa wa kuzigeuza hasira na nishati hii kuwa amali ya kivitendo kwa kutoa Nusrah kwa ajili ya kusimamisha Khilafah.

Enyi Maafisa Wanyoofu wa Kijeshi wa majeshi ya Pakistan!

Jifungueni kutoka katika minyororo ya watawala hawa vibaraka na muwakanyage kwenye njia yenu ya kuinua Dini hii tukufu katika mamlaka na utawala. Ummah unasubiri kutoa msaada wao wote wa nyenzo na hisia endapo mutasonga ili kuilinda Aqidah ya Kiislamu. Zaidi ya yote, Nusra ya Mwenyezi Mungu (swt) inangoja na ni nani awezaye kusimama mbele ya Muumba wetu?

Makafiri wamevuka mistari mekundu yote na jambo hilo limechemka hadi kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu waziwazi kama vile vibonzo vya Mtume wetu kipenzi (saw) na kuchoma Qur'an Tukufu chini ya ulinzi wa serikali za Magharibi. Ni nini chengine kinachohitajika kukushajiisheni kusonga mbele kuihama  Aqidah ya Kiislamu na Ummah?

Hakika, kuyahami matukufu kunahitaji jibu la kijeshi. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَإِن نَّكَثُوا أَيْمَانَهُم مِّن بَعْدِ عَهْدِهِمْ وَطَعَنُوا فِي دِينِكُمْ فَقَاتِلُوا أَئِمَّةَ الْكُفْرِ ۙ إِنَّهُمْ لَا أَيْمَانَ لَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَنتَهُونَ]

“Na wakivunja viapo vyao baada ya kuahidi kwao, na wakatukana Dini yenu, basi piganeni na waongozi wa ukafiri. Hakika hao hawana viapo vya kweli. Huenda (kwa hayo) wakaacha.” [Surah At-Tawba 9:12]. At Tabari amesema, وقدَحوا في دينكم الإسلام  “Na wameitusi Dini yenu ya Uislamu.” Ibn Kathir amesema, من طعن في دين الإسلام أو ذكره بتنقص  “Yeyote mwenye kuitusi Dini ya Uislamu au kuivunjia heshima.” Imam Qurtubi amesema,  بالاستنقاص والحرب وغير ذلك  “Kupitia kuivunjia heshima, vita, na mengineyo.”

Magharibi kafiri imechukua msimamo wa kimfumo unaotokana na chuki yao ya kihistoria na hisia ya kushindwa kuelekea Uislamu. Huu ni mgongano wa hadhara ambao hauwezi kupatikana ushindi juu yake kupitia kauli zisizo na maana za watawala vibaraka wa Waislamu na hatua tasa. Uislamu unahitaji dola ili kujilinda na kueneza nuru ya Uislamu kwa ulimwengu. Jitokezeni na mutoe Nusrah yenu kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume ambayo itapambana na kudhalilishwa kwa Aqidah kwenye nyayo za Khalifa Abdul Hameed II. Tishio lake tu la Jihad dhidi ya Ufaransa na Uingereza lililazimisha serikali zao kuachana na tamthilia ya kufuru.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Seljuk – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu