Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Nani Atakaesimama kwa ajili ya Wanaodhulumiwa? Yuko wapi Muislam Shujaa?

(Imetafsiriwa)

Mnamo Disemba 21, 2022 katika tafrija ya kibinafsi kwenye mji mkuu wa Chile Santiago, Raisi Boric alitangaza mipango ya kufungua ubalozi katika maeneo ‘yaliokaliwa kimabavu’ ya Palestina. Alitamka kuwa hii itapeleka ujumbe kuwa “sheria za kimataifa ziheshimiwe”. Wizara ya mambo ya nje ya Mamlaka ya Palestina yaliukaribisha mpango huu.

Hili lilihakikishwa tena na Antonia Urrejola, waziri wa mambo ya kigeni wa Chile, ambaye alisema, “Hakukuwa bado na muda uliowekwa na kwamba Chile inaendelea kuzitambua Palestina na Israel kuwa ni dola halali.”

Kuwaunga mkono watu waliodhulumiwa na kukaliwa kimabavu ardhi yao ni jambo la sawa lakini kuhalalisha uwepo wa dhalimu tokea 1949 sio sawa kabisa. Lakini hakuna anayezungumza kuhusu hili wala ya kwamba hili litatosheleza kuingia katika suluhisho la dola mbili ambalo sisi Ummah wa Muhammad (saw) hatutolikubali.

Tusiwe na haraka katika kumshangilia Raisi Gabriel Boric kana kwamba ameikomboa Palestina kutoka kwa wavamizi. Yeye, Boric atilie maanani kutokana na kauli ya rafiki yake wa Amerika ya Kusini Che Guevara. Guevara aliwaambia wakimbizi wa Palestina kuwa lazima waendeleze mapambano ya kuikomboa ardhi yao. Alisema, hakuna njia isipokuwa kupinga uvamizi, alikiri kuwa suala lao ni “gumu” kwa sababu wakaazi wapya wa Kiyahudi wamekalia majumba yao. “Hatimaye haki lazima irejeshwe” alisisitiza.

Hivyo tumesahau kuwa nchi kadhaa za Amerika ya Kusini ikiwemo Chile ziliwaita nyumbani mabalozi wao kutoka umbile la Kiyahudi mnamo 2014 kupinga vita. Lakini hatimaye Chile na nchi nyengine ziliwarejesha mabalozi wao kipindi kifupi baadaye. Nchi pekee ya Amerika Kusini ambayo hadi sasa haijalitambua umbile la Kiyahudi ni Venezuela.

Boric mapema mwaka huu (2022) alikataa kukubali hati za utambulisho wa balozi wa umbile la Kiyahudi kwa kuuliwa mtoto wa Kipalestina ikiwa ni kupinga lakini wiki mbili baadaye alikubali hati hizo.

Matendo haya ima yawe katika kupinga au kuunga mkono hayaonyeshi mgao wa sehemu mbili. Kile tunachokifahamu ni kuwa licha ya maadili yake ya mrengo wa kushoto aliyo nayo Boric, atakuwa mwenye maafikiano ili afikie malengo yake ya kisiasa. Chile inategemea kwa kiasi kikubwa juu ya mauzo yake ya nje wakiwa wanunuzi wakubwa ni Marekani na China. Kwa bidhaa yake kuu inayosafirisha nje ya shaba inaifanya Chile kuwa ni mzalishaji mkuu zaidi duniani wa madini haya. Kabla ya kushinda uchaguzi wa Chile, Boric alikuwa mkali kwa harakati ya BDS lakini kwa sasa anaonekana kusita kila muda ukisonga, yaani wanasiasa husema jambo moja kabla ya uchaguzi lakini mara tu wanaposhika madaraka hufanya jengine. Kama inavyoendana na msemo, matendo yana nguvu zaidi ya maneno.

Chile ni makaazi ya watu wenye asili ya Palestina kati ya 350,000 – 500,000, raisi aliyepita wa Chile alikuwa ni mjukuu wa wahamiaji wa Kipalestina. Idadi hii inaifanya kuwa kubwa zaidi nje ya ardhi za Kiarabu. Hivyo tunaona kuwa kura za Wapalestina ni muhimu katika Chile na Boric anazitumia lakini hatokuwa na nguvu kiasi hicho kwa kuwa anajua uwepo wake wa muda mrefu madarakani unategemea juu ya uchumi imara. Haya ni majaribio ya kuimarisha hadithi ya suluhisho la dola mbili. Hivyo leo hii tutaendelea kukubali nadharia ya suluhisho la kiakili kwa uvamizi wa ardhi yetu? Hadithi hii haina saruji katika jengo lake isipokuwa mchanga tu ambao utabugujika kwa mbinyo wa muda mfupi tu. Ni unafiki kudhania kuwa ardhi ya Palestina itakombolewa kwa ukamilifu kupitia suluhisho la dola mbili.

Ni nani tunayemfanya mpumbavu kwa kukubali hadithi hii? Ni wewe unayesoma haya, hivyo unakubali kwenda kinyume na kile ambacho Dini yako ya Uislamu imekileta kutoka mbingu ya saba?

Hivyo Dini yetu haikukamilika kiasi cha kuangalia masuluhisho ya kiakili ya kuona kupata kichache ni bora kuliko kukosa kabisa? Namna gani tunaelekea kwenye kufikiri katika njia hii ya kushindwa?

Watawala katika ardhi za Waislamu sio tena mashujaa wa Uislamu. Uungaji mkono wa watu katika mkusanyiko wa Kombe la Dunia Qatar mwezi huu kwa watu madhlumu wa Palestina una uzito mkubwa licha ya sera ya uhalalishaji mahusiano wa watawala. Wachezaji wa timu ya Morocco walionyesha mgawanyiko wa wazi baina ya wananchi na Mfalme wa Morocco aliyekubali uhalalishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi.

Dunia hivi sasa inahitaji wanaharakati watakaofanya kazi kunyanyua Al-liwa (bendera) ya Uislamu. Dunia inakuhitaji wewe kusimama imara na kuhakikisha kuwa Dini yako inaweza kukomboa uvamizi wa ardhi tukufu ya Palestina. Je unaweza kugeukia kwenye kile kitakachokupa uhai?

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا۟ اسْتَجِيبُوا۟ لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا۟ أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ)

“Enyi mlioamini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapokuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake yeye tu mtakusanywa.” [TMQ Al-'Anfāl 8:24]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Nasir Abu Mazin

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu