Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Njaa Inatumiwa kama Silaha ya Vita

kwa Kukosekana Khilafah

(Imetafsiriwa)

Serikali ya Ethiopia imeitumia njaa kama njia ya kuwamaliza wapiganaji wa upinzani huko Tigray kwa kuzuia chakula na dawa zote kuingia katika eneo hilo.

Asilimia 90 ya watu wako katika hatari ya njaa na vifo kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuilika kutokana na mkakati huu wa kinyama.

Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni Dkt Tedros Ghebreyesus amenukuliwa akisema:

“Hakuna kinachosonga. Nilitarajia chakula na dawa vitaanza kutiririka mara tu baada ya kusitishwa kwa mapigano. Hilo halifanyiki. Watu wanakufa kwa njaa na magonjwa yanayoweza kutibika na watu milioni 6 wamefungiwa kutoka kwa sehemu zengine za ulimwengu kwa miaka miwili kana kwamba hawapo.

Pia aliongeza kuwa huduma za umeme na mawasiliano ya simu zimeregeshwa katika baadhi ya maeneo lakini akatuhumiwa na maafisa wa Ethiopia kwamba alikuwa akiendesha vita vya propaganda akieneza habari za uongo na kujaribu kuhujumu makubaliano ya amani.

Hivi sasa takwimu ni kwamba hadi kufikia mwaka 2022 watu milioni 13 wanakabiliwa na uhaba wa chakula katika eneo hilo na 150,000 - 200,000 wamekufa kwa njaa. 89% wanahitaji msaada wa chakula. Katika ripoti moja iliyochapishwa Juni 2021 zaidi ya watu 350,000 tayari wanakabili hali ya “janga” la njaa na kwa sasa Tigray anashikilia hadhi ya kuwa mwenyeji wa njaa mbaya zaidi katika Afrika Mashariki tangu 2011 na 2012. Ripoti ya gazeti la kimataifa la The Economist inataja kwamba kuna ushahidi wa serikali ya Ethiopia wa kuwanyima chakula na madawa kimakusudi wakazi wa Tigray ili kuzima TPLF (Jeshi la Ukombozi la Watu).

Mnamo tarehe 10 Februari 2021, Abera Tola, mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu cha Ethiopia aliripoti kwamba watu walikuwa wakifika kwenye kambi za wakimbizi kutafuta msaada wakiwa wamedhoofika na "kwamba ngozi yao ilikuwa kwenye mifupa yao". Alikadiria kuwa 80% ya watu hawakuweza kufikiwa na mashirika ya kibinadamu.

Mapema Februari 2021, Muferiat Kamil, Waziri wa Amani wa Ethiopia alikubali kwamba kuwe na usambazaji mkubwa wa chakula katika eneo la Tigray, kulikuwa na dirisha fupi la msaada lakini miezi iliyofuata ya kunyesha kwa mvua duni na uharibifu wa mazao na nzige ulimaanisha kwamba mavuno yalipunguzwa sana na kusababisha uhaba wa chakula. Hivi sasa kati ya watu 400 na 900 wanakufa kila siku kutokana na njaa na hakuna dalili za idadi hiyo kupungua. OCHA, ReliefWeb ilitoa maoni yao kwamba mtu 1 alikuwa akifa kwa njaa kila sekunde 48.

Matendo haya ya kutisha kwa hakika yanapangwa na tawala ovu zinazo angamiza ardhi zetu kwani zinatumikia njama chafu za watawala wa Kikoloni wanaotaka kudhoofisha upinzani wa wananchi katika Pembe hiyo ya Afrika, mojawapo ya maeneo yenye rasilimali nyingi zaidi duniani. Huku wenyeji wakihangaika kwa ajili ya maisha yao ya kila siku, mataifa yanajishughulisha sana kuyaruhusu makampuni na serikali za kigeni kutumia fursa za biashara zinazoletwa na vita, tunachoshuhudia hasa hapa ni utumiaji wa mara kwa mara wa umaskini na njaa ili kuyabakisha mataifa kuwa dhaifu. Uharibifu ambao hili linao kwa mamilioni ya wanawake na watoto walionaswa katika mchezo huu wa kisiasa wa madaraka hauhusiani na ulafi wa kinyama wa mataifa ya Magharibi yanayotafuta mamlaka na pesa. Mnamo tarehe 2 Julai 2021, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilijadili suala hilo na kutangaza kuwa zaidi ya watu 400,000 wanaathiriwa na uhaba wa chakula na kwamba watoto 33,000 walikuwa na utapiamlo mbaya. Ripoti hiyo pia ilisema kwamba watu milioni 1.8 walikuwa kwenye ukingo wa njaa.[26]

Sheria za duni zilizopo katika rekodi za Umoja wa Mataifa kama vile;

Kifungu cha 8(2)(b)(xxv) cha Mkataba wa Roma wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kinachosema “Kutumia njaa ya raia kwa makusudi kama njia ya vita kwa kuwanyima vitu vya lazima kwa maisha yao, ikiwemo kuzuia kwa makusudi misaada kama ilivyotolewa chini ya Mikataba ya Geneva” na Vifungu 270(i) na 273 vya Kanuni ya Kuadhibu ya Ethiopia ya 2004 inayohusiana na sheria za uhalifu kuhusiana na njaa katika Vita vya Tigray havina utekelezwaji wa kweli.

Mnamo Aprili 2021 Wakfu wa Amani ya Dunia ulichapisha ripoti na katika sehemu ya 4 ya waraka huo ushahidi unaoongezeka umeorodheshwa juu ya matumizi ya makusudi ya uhaba wa chakula na matibabu ili kulemaza miundombinu ya eneo la Tigray. Waandishi walihitimisha kwamba serikali za Ethiopia na Eritrea zilihusika na njaa, na kwamba “dhurufu za ushahidi zinaashiria kwamba [njaa hiyo] ilikuwa ya kimakusudi, ya kimpangilio na iliyoenea sana.”

Hakuna shauku kutoka kwa mashirika ya kimataifa katika kutekeleza uingiliaji kati wowote katika uhalisia huu kwani unatumikia maslahi kimkakati. Hali kadhalika ukosefu wa uthabiti wa kisiasa wa Iran juu ya kifo cha mwanamke mmoja unapewa umakini wa kimataifa, wakati wanawake na watoto wanafariki nchini Palestina kwa serikali za Kizayuni kuokoa maslahi na kutotilia maanani tukio hilo.

Mapema Oktoba 2021, Mark Lowcock, ambaye aliongoza OCHA wakati wa Vita vya Tigray, alisema kuwa serikali ya majimbo ya Ethiopia ilikuwa ikiisababishia Tigray njaa ya makusudi, “ikiendesha kampeni ya hali ya juu ya kusitisha misaada kuingia” na "hakukuwa tu na jaribio kuwaacha na njaa watu milioni sita bali jaribio la kuficha kinachoendelea.”

Mnamo Novemba 2021 katika Jografia ya Binadamu, Teklehaymanot G. Weldemichel alisema kuwa “njaa [katika Jimbo la Tigray] tangu mwanzo ilikuwa ni lengo la mwisho la serikali ya Ethiopia na Eritrea”. Teklehaymanot aliorodhesha mbinu muhimu alizoziona zikichochea baa la njaa zikiwemo uporaji na uharibifu wa miundombinu; hatua za benki ambazo zilizuia upatikanaji wa pesa; na mzingiro kuzuia misaada ya kibinadamu.

Jibu pekee la halali kwa jinai hizi dhidi ya wanadamu linaweza kutolewa na mamlaka halali ardhini ambayo liko katika sura ya Mwenyezi Mungu (swt) na amri zake za kusimamisha Khilafah ambayo itawapa wanadamu wote haki yao stahiki ya chakula, mavazi na usalama wa maisha. Imepokewa kutoka kwa Uthman bin Affan (ra) kuwa: Amesema Mtume, rehma na amani zimshukie:

«لَيْسَ لِابْنِ آدَمَ حَقٌّ فِي سِوَى هَذِهِ الْخِصَالِ بَيْتٌ يَسْكُنُهُ وَثَوْبٌ يُوَارِي عَوْرَتَهُ وَجِلْفُ الْخُبْزِ وَالْمَاءِ»

Hapana haki kwa mwana wa Adamu isipokuwa vitu hivi: nyumba anayoishi, nguo ya kusitiri uchi wake, kipande cha mkate na maji.” [Chanzo: Sunan al-Tirmidhi 2341]

Sisi kama Umma wa Kiislamu ambao una udugu mmoja lazima tuzifanyie kazi amri hizi za Mwenyezi Mungu (swt) za kuwafanya wanadamu wote waungane chini ya bendera ya hukmu za Sharia na lazima tuhimizane kufanya kazi bila kuchoka hadi jambo hili la faradhi litimie.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammed
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu