Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mhimili wa Marekani, Saudi na Iran

(Imetafsiriwa)

Hatua za hivi majuzi za Saudi Arabia kukataa kuongeza uzalishaji wa mafuta kinyume na utawala wa Biden zimesababisha mtafaruku nchini Marekani kwani ilionekana kama ukaidi wa Saudia kwa mshirika wake wa usalama. Ili kudhihirisha uhalisia wa kisiasa, ni muhimu kuelewa taswira pana ya kieneo. Saudi Arabia, katika miezi ya hivi karibuni, imekuwa ikikabiliana na uwiano wa Urusi na zaidi ya hayo, imekataa kuchimba na kusukuma mafuta zaidi kwenye soko na kusababisha bei ya kawi kubaki juu. Kwa upande wake, ukaidi wa Ufalme huo umesababisha matatizo kwa utawala wa Biden kuongeza zaidi orodha ya masuala yanayoathiri umma wa ndani wa Marekani, huku kawi ikiwa mojawapo yao. Ikiwa tutachunguza mashirika makubwa ya mafuta wao pia, wamekataa kuchimba idadi ya kutosha ya mafuta na gesi ili kupunguza bei inayopanda, na kuhujumu utawala wa Biden.

Kulingana na Bei ya Mafuta, siku kadhaa zilizopita, Rais Biden alizitishia kampuni za mafuta kwa ushuru juu ya faida na "vizuizi vingine" ikiwa hazitaacha kurudisha pesa taslimu kwa wanahisa na kuanza kuwekeza pesa hizi katika uzalishaji zaidi wa mafuta. Sekta hiyo, kupitia Taasisi ya Petroli ya Marekani, ilijibu kwa kukariri tena ukweli kwamba soko la mafuta ni la kimataifa, na wazalishaji hawana udhibiti kamili wa bei kwa sababu pia ni soko huria. Wazalishaji wa mafuta, wakubwa na wadogo, hawakujibu shambulizi la hivi punde la Rais wa Marekani dhidi yake. Sekta hii iliendelea tu kile ambacho imekuwa ikifanya tangu bei ya mafuta ilipopanda tena: kurudisha pesa taslimu kwa wanahisa na kupanga matumizi yake kwa uangalifu.

La kwanza ni kwa sababu big oil ndio wafadhili wa Republican na kwa kuwa ni dhidi ya Big Tech- wafadhili wa Democrat- na ajenda ya tabianchi. Big oil wanatamani ama kushawishi wimbi la mabadiliko ya tabianchi na rasilimali zenye uwezo wa kurudiwa matumizi yake na kama haiwezekani, inapendelea kulizimua. Kufikia sasa, big oil imefanikiwa kwani imeweza kubadilisha nguvu zake kupitia mawakala wake wa kisiasa ndani ya serikali- wakiwa Republican- na kuwalazimisha Democrats kufuata sera zao. Kwa kufanya hivyo, Big Tech pia imeshutumiwa kwa kuisaidia big oil kuzalisha mafuta zaidi, hatua ambayo inaonekana kwenda kinyume na ahadi ambazo makampuni ya teknolojia yalikuwa yametoa kuhusu kupunguza utoaji gesi hewani. Haya yote yamedhuru utawala wa Biden na chama cha Kidemokrasia na zaidi ya hayo, wafadhili wao.

Tukirudi kwa Saudi Arabia, iko kitandani na chama cha Republican cha Amerika na pia ina nia ya kuudhuru utawala wa Biden na kuisaidia Republican kushinda uchaguzi wa katikati ya muhula kwa sababu ikiwa GOP itashinda, Democrats itakuwa katika tishio kubwa ambapo Republicans daima wataweza kuzuia karibu kila mswada kupitishwa Bungeni. Mbali na hilo, miongo kadhaa iliyopita Aramco ilikuwa inamilikiwa na big oil na hadi wa leo Aramco imewaajiri Wamarekani 40,000 kuanzia wakuu, wanajiolojia, na washauri ambao wana historia ya kuajiriwa na big oil hapo awali! Kuanzia sasa, haishangazi kwa nini Saudi Arabia inaambatana na msimamo wa kihafidhina/big oil badala ya democrats na wafadhili wao. Hivyo, Saudi Arabia haiendi mbali kutokana na kuwa kibaraka wa Marekani badala yake inachagua kuwa upande wa bwana tofauti kutoka nyumba hiyo hiyo moja! Zaidi ya hayo, Saudi Arabia haitaki mshindani wake Iran kuwa na nguvu chini ya Democrats.

Hili linatuleta kwa Iran na dori yake ya sasa katika mgogoro huu. Hivi sasa, Iran inapitia msukosuko wa ndani kutokana na utawala wao wa kikatili usiokuwa wa Kiislamu dhidi ya watu wa Iran. Magharibi kwa jumla imetumia suala hili kupindisha suala hilo na kuushambulia Uislamu. Hata hivyo, utawala wa Biden hadi sasa, haujakanusha kwa uthabiti ufufuo wa JCPOA na wala Iran haijakanusha, jambo ambalo linadhihirisha kwamba mataifa yote mawili yananuia kutekeleza mapatano hayo katika siku zijazo. Ikiangazia unafiki kutoka pande zote mbili ambapo pande zote mbili zinakataa kushikamana na maadili na vima vyao.

Zaidi ya hayo, katika mwezi uliopita Iran iliweza kuipa Urusi droni kadhaa katikati ya vita vya Ukraine, Amerika iliamua kuiwekea Iran vikwazo katika jaribio la kuzuia usambazaji wa droni kuelekea Urusi. Hii inazua shaka kwa nini Amerika haikuweka vikwazo mara moja lakini mwezi mmoja baada ya Iran kupeleka droni za kutosha kwa Urusi? Kwa mara nyingine tena, inaonyesha kwamba Marekani inaitumia Iran kusimamia mpango wa Marekani kwa Urusi nchini Ukraine.

Ili kuangaza picha hii, tutaangalia matukio yafuatayo ili kuona ni kwa nini Biden alitoa kauli kama hizi: Joe Biden alisema hivi majuzi, "Musijali, tutaikomboa Iran," Biden aliwaambia wafuasi katika hotuba ya kampeni jijini California. Kisha Saudi Arabia ikakimbilia Marekani ikilalamika kuhusu Iran kuhatarisha  ufalme huo. Kisha, Iran ilirusha kombora ambalo Marekani ililitaja kama "la uhasama na uvunjifu wa amani" kwa eneo hilo. Kisha ndege za Marekani zilijaribu kuhangaisha juhudi za Iran ili kuzuia shambulizi lililokaribia dhidi ya ufalme huo. "Tuna wasiwasi na picha ya tishio, na tunaendelea kuwasiliana mara kwa mara kupitia njia za kijeshi na kijasusi na Wasaudi," Baraza la Usalama la Kitaifa la Amerika lilisema wakati huo. "Hatutasita kuchukua hatua katika kutetea maslahi yetu na washirika wetu katika kanda hiyo." Ili kufanya mambo yawe ya kuvutia zaidi, Seneta wa Republican Joni Ernest alisema kuwa, "Huku Iran ikijiandaa kwa mashambulizi dhidi ya washirika wetu, picha za kidijitali za eneo hilo (DEMS) zinazoongoza zinatetea kuondolewa kwa vitengo muhimu vya ulinzi wa anga na makombora, na kuhatarisha maisha ya raia wa Marekani na vikosi vyetu vilevile." alisema. Aliongeza zaidi, "Saudi Arabia ni mshirika wa muda mrefu wa usalama wa Ghuba na hilo halijabadilika. Utawala wa Biden ulipunguza uzalishaji wa kawi wa Marekani na umelaumu OPEC+ kwa bei ya juu ya gesi. Watu wa Marekani hawainunui."

Kumalizia, vyama vyote vya kisiasa ndani ya Amerika vinatumia mamlaka mbili tofauti zinazopingana katika eneo hilo kwa maslahi yao binafsi. Kwa upande mmoja, mafuta ya Republican na Big oil wanaitumia Saudi Arabia kuvuna faida na kudhoofisha upinzani kisiasa ili kuweza kupata ushindi katika uchaguzi wa katikati ya muhula, ambao ungewanufaisha sana. Kwa upande mwingine, Democrats wanaitumia Iran kuitisha Saudi Arabia ili iweze kufikiria upya sera zake za sasa zenye kuegemea Republican na pia kuweza kukabiliana na juhudi za Republican ili waweze kudumisha nguvu ya Democrat bungeni.

Hili ndilo umbile la mfumo uliojengwa juu ya utenganishaji Muumba na mambo ya maisha. Na nidhamu (Uhuru, Urasilimali na Demokrasia) zinazochipuza kutokana na itikadi hii batili husababisha kuleta si chengine isipokuwa uharibifu, ufisadi na machafuko. Wakati mataifa ya kigeni yanapoanza kuiga au hata kushirikiana na mataifa hayo ya Kimagharibi ya Kisekula hata umbile lao la utawala huchafuka na kufisidika kama tunavyoona kwa Iran na Saudi Arabia ambazo zimeshughulika kuunga mkono nguzo ya dunia (Marekani) ya ufisadi na ukafiri kwa maslahi yao ya kibinafsi, ambayo haisaidii watu wao wala katika kutatua matatizo yao kwa muda mrefu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mohammed Mustafa

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu