Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kutokana na Sera Yake Dhaifu ya Kigeni, Urusi Inaendelea Kukaza Kitanzi cha Amerika Shingoni Mwake Yenyewe

(Imetafsiriwa)

Japan itasambaza gesi yake asili myayuko kwa Ulaya: wawakilishi wa Muungano wa Ulaya (EU) na Amerika wameielezea Tokyo juu ya ombi hilo. Japan yenyewe inaagiza rasilimali ya nishati, lakini katika hali ya sasa, imeamua kuonyesha uungaji mkono wa kisiasa. Shehena ya kwanza itawasili Ulaya mnamo mwezi Machi. (ru.euronews)

Tokea 2008, wakati Raisi wa Shirikisho la Urusi alipotoa “hotuba yake ya Munich”, Urusi imekuwa ikijaribu kuonyesha madaraka yake katika jukwaa la ulimwengu, ikiikabili dunia ilioelemea ncha moja chini ya uongozi wa Amerika.

Lakini kwa miaka 14 iliyopita, Urusi imekumbana na kushindwa kuliko wazi kabisa. Uoni mfupi wa kisiasa, ambao ni matokeo ya kushindwa kwa mfumo wake, kumeifanya Urusi kuwa sanamu la kimataifa, ambapo matendo yake ya kifedhuli yanatumiwa na Amerika kuendelea kuubana urithi wa USSR na kuzidi kuiunganisha jamii ya ulimwengu kuwa upande wa Amerika, hasa kwa nchi ambazo ni wanachama wa EU na NATO.

EU, licha ya kutokubaliana kwa wafadhili wake wakuu – Ujerumani na Ufaransa, inalazimika kuifuata Amerika, kwa sababu Urusi chini ya Putin inakemea wazi wazi “maadili ya Ulaya” yalio na sifa mbaya. Kwa hiyo katika hali hii, kwa upande wa EU, maadili ya pamoja na Amerika ni muhimu zaidi kuliko manufaa ya kiuchumi ya urafiki na Urusi.

Katika hili, Amerika inaungwa mkono sio tu na nchi za Ulaya, bali pia na nchi zote za dunia, hasa Japan, iliyopo upande mwengine wa dunia, ambayo Waziri wake wa Biashara ameelezea maamuzi yake ya kusambaza gesi myayuko Ulaya kama ifuatavyo: “Japan inapaswa kuziunga mkono nchi za G7, hasa zile zenye maadili ya pamoja na Japan.”

Baada ya maamuzi ya kijasiri ya Shirikisho la Urusi mnamo 2014 ya kuunganisha Crimea na kuzusha hali ya kutotengemaa katika Ukraine ya Mashariki, katika Donbas, sera ya kigeni ya Urusi imekuwa na udhaifu mkubwa, ufa mdogo ambao Amerika pamoja na washirika wake, wanashambulia mara kwa mara.

Kwa hivyo, uongozi wa Ukraine mara kwa mara umeonyesha dhamira yake ya kujitoa kutoka makubaliano ya Minsk na hata, ikiwezekana, kuanza usafishaji wa nguvu wa Donbass kutoka kwa wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi na wanaotaka kujitenga.

Urusi, imetambua kuwa muda unakwenda dhidi yake katika Donbass na inaelekea kwenye kushindwa kwa majivuno katika eneo hili, ikifuatiwa hata na msukumo mkubwa wa kuunganika kwa Crimea, inajaribu kuongeza hatari kwa mara ya pili mwaka jana kwa kuharakisha silaha katika mipaka ya Ukraine.

Huenda mtu asikubaliane na hitimisho hilo na kuhoji kuwa kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita Urusi ilizidisha sera yake ya kigeni na ilijitangaza sana katika medani ya kimataifa, ikiendesha juhudi za busara za kisiasa. Lakini hilo si jengine isipokuwa ni ndoto za propaganda za Warusi.

Katika miaka 10 iliyopita, Urusi ilikabiliana na kile kiitwacho “mapinduzi ya rangi” mipakani mwake, kwa kweli imeshaipoteza Ukraine, katika mzozo wa Karabakh ulilazimisha kusalimisha mshirika wake wa Transcaucasia katika CSTO Armenia. Hata Kazakhstan, ambayo ni eneo jirani  linalohusiana na Shirikisho la Urusi na eneo lake la kuishi, hivi leo, kwa mujibu wa propaganda ya vyombo vya habari vya Urusi, imekuwa ni muathiriwa wa majaribio ya Magharibi ya kuzalisha tena mapinduzi ya rangi ndani yake.

Euronews inaeleza:

“Wiki hii, Washington imeangalia njia mbadala ya kusambaza nishati Ulaya nyuma pazia la mzozo unaozunguka Ukraine. Kiongozi wa diplomasia wa Ulaya, Josep Borrell, alikuja kwa mshirika wake wa Amerika Anthony Blinken. <…> Pia mnamo siku ya Jumatatu, raisi wa Amerika Joe Biden, aliyemkaribisha Chansela wa Ujarumani Olaf Scholz jijini Washington, aliahidi wazi kabisa juu ya “kuachana” na mradi wa bomba la mafuta la Nord Stream 2.

Hebu fikiria, upande wa pili wa Atlantiki, walikuwa wakiangalia juu ya njia mbadala za kusambaza nishati Ulaya, na Biden aliahidi kumaliza majaribio ya ushirikiano wa kiuchumi baina ya EU na Urusi.

Baada ya hayo, vipi kwa mwenye akili timamu atadai juu ya kuhuika na kukua kutoka kwenye kupiga magoti kwa Shirikisho la Urusi? Uoni mfupi wa kisiasa wa Urusi umetumia vibaya vitisho vya kijeshi na kauli zake za mwisho kwa karne kadhaa, ikiathirika kutokana na kushindwa katika matumizi ya uwerevu wa kisiasa.

Hakuna kinachoelezea utovu wa uzoefu wa sera za kigeni za Urusi kama maneno yafuatayo ya mmoja wa watawala wake, Mrusi Tsar Alexander III (r.1881-1894): “Urusi ina marafiki wawili tu – jeshi lake la nchi kavu na jeshi la majini.”

Baada ya kuvunjika kwa USSR na kukataliwa kwa ukomunisti, wakati Urusi ilipopoteza msingi wake wa kimfumo, ijapokuwa sio sahihi, maneno ya Alexander III yamekuwa ni msingi wa sera yake nzima ya kigeni. Hivi sasa Urusi ina hiyari kutojisumbua yenyewe na mipango na ujanja wa kisiasa, badala yake kuchukua nafasi ya usaliti na vitisho dhidi ya majirani zake na dunia nzima.

Hivyo, katika kujibu juu ya ucheweleshaji wa utekelezaji wa Nord Stream 2, Urusi imeamua kupandisha bei ya gesi kwa Ulaya katika kipindi hiki cha majira ya baridi, na hivyo kuzidi kuhakikisha hofu ya Magharibi kuwa mradi huu utatumika kwa usaliti. Matokeo yake, Amerika imeongoza “operesheni ya uokozi” wa EU kutoka kipindi cha baridi kali, ikiishirikisha hata Japan, iliyopo upande mwengine wa dunia. Yote haya yatapelekea, kama sio kumaliza kabisa, basi kwa kiwango kikubwa cha ukataaji wa EU wa vyanzo vya nishati kutoka Urusi.

Hata hivyo, hii haimaanishi kuwa Amerika inaongozwa na malengo mazuri ya kipekee katika mgogoro huu, kama inavyodaiwa ya kuwa inazijali Ulaya na Ukraine. Iko mbali na hilo. Amerika inatumia mbwa kichaa wa Urusi aliyeshikwa mnyororo kwenye mipaka ya Muungano wa Ulaya ili kuendelea kuzibana ziwe upande wake.

Kufuatia matamshi ya Seneta Lindsey Graham wa Amerika, aliyoyatamka baada ya hotuba ya Putin ya Munich, hapa ipo fasaha: “Kwa tamko lake moja tu, amefanya zaidi katika kuziunganisha Amerika na Ulaya kuliko yale tuwezayo kuyafanya sisi kwa muongo mmoja.”

Tokea 2014 Urusi imeongeza kasi harakati zake kupitia njia hii ya maafa, kukipatikana muongezeko zaidi wa vikosi vya NATO katika mipaka yake.

Katika sera yake ya kigeni katika Mashariki ya Kati na Afrika, Urusi inaendelea kuhudumia maslahi ya Amerika, ima iwe nchini Syria, Libya, Sudan, na hivi sasa Mali. Haya yanahakikishwa na ukweli kuwa Amerika haikuweka kabisa vikwazo vyovyote dhidi ya Moscow kwa vitendo vyake katika nchi hizi. Amerika imewakilisha kazi chafu kwa Urusi kwa maslahi yake, kama kuiripua kwa mabomu miji ya Syria.

Kwa upande wake, Urusi inategemea kupata tahafifu juu ya mzozo wa Ukraine, pamoja na kutambuliwa kwa utwaaji wa nguvu wa Crimea.

Katika miaka michache iliyopita, kumekuwa na majaribio kwa Amerika kuitumia Urusi kuibana China, ambayo kuinuka kwake kunauhofisha utawala wa White House.

Hivyo, katika makabiliano ya sasa pamoja na Magharibi, Urusi ipo katika kujihami. Kwa mbinyo inaopatiwa, itaweza tu kujibu kwa kushadidisha upande wa kijeshi, ambao kwa nafasi ya kimbinu inaweza bado kuwa mshindi, lakini katika kipindi cha muda mrefu bila shaka itapelekea kushindwa vibaya na udhalilifu.

Inachoweza kufanya Urusi hivi leo ni kuwapiga wanafunzi na vijana wanaoshiriki katika maandamano ndani ya nchi, pamoja na mateso, ukamataji na kuwafunga raia wake Waislamu kwa ajili ya tarakimu mbili, ikiwashtumu kwa siasa kali na ugaidi.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Fazyl Amzaev

Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu