Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mazungumzo ya Vienna na Maslahi ya Amerika

(Imetafsiriwa)

Mnamo Juni 13, 2021: “Mazungumzo yasio ya moja kwa moja baina ya Tehran na Washington juu ya kufufua mkataba wa nuklia wa Iran wa 2015 yalianza tena mjini Vienna siku ya Jumamosi huku Muungano wa Ulaya ukisema majadiliano hayo yalikuwa “magumu” na Ujerumani ilitaka maendeleo ya haraka… Ujumbe wa Amerika katika mazungumzo hayo, ujulikanao kama Tume ya Pamoja ya Mpango Kazi Mpana wa Ushirikiano (JCPOA), iliyo na makao yake katika hoteli moja iliyo upande wa pili wa barabara huku Iran ikikataa mikutano ya ana kwa ana.”

Matukio ya Awali: 

- Mwaka 2015, Iran na mataifa kadhaa (ikiwemo Amerika) yalisaini Mkataba wa Nyuklia wa Iran. Mkataba uliipa Iran unafuu wa vikwazo, na kuweka vizuizi kwenye mpango wa nyuklia wa Iran.

- Wakati huo mnamo 2018, Raisi Trump aliitoa Amerika kwenye mkataba, akidai kuwa umeshindwa kuzuia mpango wa makombora ya Iran na ushawishi wake kwenye eneo.

- Mwaka mmoja baadaye, Iran ilianza kupuuza vizuizi kwenye mpango wake wa nyuklia.

- Wakati wa uchaguzi wa Uraisi wa Amerika, Biden alisema kuwa atairudisha Amerika kwenye Mkataba wa Nyuklia wa Iran. Na mnamo Oktoba 2020, Amerika ilishindwa kutanua vikwazo na kuweka vikwazo vya kimataifa juu ya Iran kwa kuitumia njia ya JCPOA ya kisheria ya kuvirejesha tena vikwazo.

- Mnamo mwezi Aprili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Saeed Khatibzadeh, alisema kuwa Iran itarejea kwenye vikomo vya nyuklia vya 2015 pindi Amerika itakapoondoa vikwazo vyote, vilivyoongezwa na vilivyopachikwa tena.” Na afisa wa Wizara ya Kigeni ya Amerika, Ned Price alisema kuwa “uondoshwaji vikwazo hauambatani na JCPOA, huku akisisitiza hatotoa sura na aya kamili juu ya vipi hayo yanaweza kuwa.” (Chanzo)

- Kwa sasa, mazungumzo ya Vienna yameanza tena, baada ya kutofikia maelewano ya mwisho yalipomalizika mnamo Mei 19. Yanakusudiwa kuiruhusu Amerika na Iran kurejea kujifunga na mkataba wa nyuklia wa Iran wa 2015. Na viongozi wa kisiasa wanasema kuwa watafikia makubaliano lakini wanahitaji muda. Utawala wa Biden pia umesema kuwa unajukumu la ‘kufuatilia’ makubaliano hayo au msururu wa makubaliano. (Chanzo)

Mkataba wa Nyuklia wa mwanzo umeainisha vikomo juu ya mipango ya nyuklia pamoja na vikwazo ambavyo Amerika inapaswa kuviondoa. Lakini Amerika ‘imefanya mambo kuwa magumu’, wakati utawala wa Trump ulipoweka vikwazo kadhaa teule vinavyopishana chini ya makombora ya balistik, ugaidi na mamlaka za haki za binaadamu. Joe Biden amesema kuwa ana “jukumu lisiloyumba” kuizuia Iran kutokana na kumiliki silaha za nyuklia wakati pia wakiahidi kuipatia Tehran “njia ya kuaminika ya kurejea kwenye diplomasia.” (Washington post)

Kuhusiana na msimamo wa Iran katika mazungumzo – vyombo vya habari hivi sasa vinajadili athari ambayo chaguzi zitakuwa nazo juu ya nafasi ya Iran katika mkataba. Wanaweza kuitumia hali ya ndani kuhalalisha, au kuwafikiana, katika hitimisho lolote litakalofikiwa katika mazungumzo hayo. Lakini katika hali halisi, haitobadilisha chochote. Sera za nje hazitawaliwi na Raisi – zinatawaliwa na Kiongozi Mkuu, Ali Khamenei, ambaye yupo madarakani tokea 1989. Kwa hali hiyo, Iran haibadilishi “mkakati wake mpana kwa ghafla, hata katika kutowafikiana na utambulisho wa raisi mpya aliye chaguliwa.” (Chanzo) Usisitizaji wao unaelekea kuwa ni juu ya vikwazo ambavyo Amerika imewawekea – na hitajio lao la kuondolewa.

Ndio, Amerika inafuata maslahi yake – daima imefanya hivyo.

Unaposoma habari na uchambuzi jumla wa kisiasa, kuna maoni kuwa Iran na Amerika ni maadui, zikiwa nchi zote mbili zimesimama kidete na kusukuma ajenda zao binafsi. Kile ambacho ripoti hizo hazizungumzii ni namna Amerika inavyoitumia Iran kuzisukuma ajenda zao katika eneo, na Mkataba wa Nyuklia wa Iran, uondoaji wa (vikosi) uliofuatia wa Raisi Trump na mazungumzo ya sasa ya Vienna, yote yanatokea ndani ya muktadha huu.

Kwa miaka michache iliyopita, vyombo vya habari na tabaka la wanasiasa nchini Amerika wamemkosoa Donald Trump, wakitilia mkazo namna ya pupa yake. Wamejadili makosa aliyoyafanya wakati Amerika ilipojitoa kwenye Mkataba wa Nyuklia. Wakipuuza ukweli kuwa yeye bado ni sehemu ya muundo wa siasa za Amerika – Raisi wa Amerika hatekelezi kibinafsi, anatekeleza ndani taasisi za nchi, ambazo zote zimeundwa kuunga mkono maslahi ya kitaifa ya dola hiyo. Hivyo, wakati Amerika ilipojitoa katika Mkataba wa Nyuklia wa Iran, na kuweka vikwazo, ilikuwa ni katika maslahi yao kuyatekeleza hayo.

Haya yako wazi katika maamuzi kadhaa ambayo Amerika imeyafanya wakati wa uraisi wa Donald Trump – ambapo walificha maamuzi yao mengi yenye utatanishi nyuma ya shakhsia yake na mbinu zake. Mifano inajumuisha kuzuia wakimbizi, kuidhibiti China, kuziondoa kampuni za Amerika na kuzirudisha nyumbani. Zimefaidika hata kutokana na bei kubwa ya mafuta, walipoweka mbinyo kwa Iran, kama ilivyofaidisha makampuni ya mafuta ya Amerika yalipokimbilia kuzalisha mafuta zaidi ya mwambatope (shale oil).

Hivi sasa, Amerika na vyombo vya habari wanashajiisha sura ya kwamba Amerika iko tayari kujifunga na ‘kanuni’ za mfumo wa Kimataifa; kushiriki au kufuata makubaliano kama ya Mkataba wa Paris, kupiga hatua kujiunga tena na Baraza la Haki za Binaadamu na Ushirikiano wa Kati ya Maeneo ya Pasifiki (TPP). Hivyo, inaonekana kwamba Joe Biden anafanyia kazi muktadha huo – athari ilionayo haya juu ya Mazungumzo ya Vienna itabaki kusubiriwa. Lakini Amerika imekuwa muda wote, na itaendelea kufuata maslahi yake katika eneo (kwa njia ya wazi au fiche).

Mahitaji ya Amerika kwa Iran yamebadilika ndani ya muda… ambapo imepelekea mabadiliko katika mahusiano yake na Iran.

Mwaka 2015, Iran ilisaini Mkataba wa udhalilifu wa Nyuklia na hivyo Amerika ikaiondoshea vikwazo ilivyoiwekea nchi hiyo. Hii ikakazia mahusiano ya wazi baina ya Iran na Amerika. Wakaendelea kuchukua jukumu katika eneo ambapo iliiruhusu Amerika kudhibiti ubwana wake wa kiulimwengu na kuipunguzia mzigo wa dola kuu (ilioubeba) huku ikijificha kwa michezo ya kisiasa inayoicheza katika eneo.

Dori ya Iran katika kuunga mkono mizozo mbali mbali (kama ile ya Afghanistan, Syria, Iraq na Lebanon) imeliyumbisha eneo – dori ambayo Amerika iliwahitajia kuifanya. Ukolezaji wa kitisho cha mipango ya nyuklia ya Iran kimeipa Amerika sababu iliyoihitaji kuongeza mshikamano wa mafungamano yake ya kijeshi na ‘Israel’ na nchi za Ghuba. Huku ikiendeleza maafikiano yao katika Mashariki ya Kati kuyadhibiti mafuta ya eneo la Mashariki ya Kati.

Wakati Raisi Trump wa Amerika alipojitoa kwenye mkataba, ilikuwa ni kufinika ukweli wa kuonekana kuwa ni kosa lakini haikuwa hivyo. Kupitia hali hiyo, nafasi ya Bashar Al-Assad iliongezeka Syria. Hawakuihitaji Iran kufuatilia dori ya moja kwa moja katika eneo, na kwa kujitoa kutoka kwenye mkataba kuliwawezesha kujitayarisha na masharti mapya ya kupunguza dori ya Iran katika eneo wakati huo huo pia kuisukuma Iran kusaini mkataba mpya wa nyuklia, ambao utayanufaisha makampuni ya Amerika kwa kuyapatia fursa mwanana katika masoko ya Iran.

Inaweza kuonekana hivi sasa kuwa, Amerika itaihitajia Iran kuendelea kucheza dori katika eneo. Lakini huku ikiwa bado hawajatoa ripoti yoyote juu ya maamuzi yanayofanywa, kwa namna gani na katika uwezo upi ni jambo la kusubiriwa kutokea kwake. Wakati Joe Biden akivitoa vikosi vyake kutoka katika eneo hilo – na kuangalia njia mbadala za kuimarisha ushawishi wa Amerika, watahitaji kuzingatia ni dori gani wanayoihitaji Iran kuicheza.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Fatima Musab

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu