Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Bw. Macron! Waislamu wako Tayari Kupambana katika Vita Vyako vya Kithaqafa vya Kisekula Dhidi ya Uislamu!

Bw. Macron! Umesema kuwa unataka kuanzisha vita vya kifikra dhidi ya Uislamu kwa maadili yako ya kisekula na njia ya maisha ya kiliberali. Sawa, sisi kama Waislamu tuko tayari zaidi kuingia vita hivi vya kifikra!

Hivyo ni silaha gani za kifikra ulizo nazo kutushambulia? Je, utadai kuwa usekula umeweka dola zilizostaarabika zilizojengwa chini ya maadili mazuri…wakati unatetea urushaji wa matusi na kutukana imani takatifu za watu chini ya bendera ya uhuru wa kiliberali? Hili likienda sambamba na kuwanyanyapaa wafuasi wa dini walio wachache na kuwafanya kama wahuni na raia wa daraja la pili kuhusiana na haki zao? Je, unauangalia huu kama ni ustaarabu kuwahangaisha watoto wa Kiislamu kwa kuvamia majumba yao na polisi wenye silaha, kwa sababu tu wamekataa vikatuni vya kumtusi Mtume wao mpendwa (saw) wanayemuenzi … AU kuwatupia lawama wafuasi wa dini walio wachache ili kujikomba kwa wabaguzi, wapigaji kura wenye chuki na wageni kama ni sehemu ya fursa zako za kisekula za mchezo wa kisiasa? Je, hii ni alama ya dola iliyostaarabika kutawala na kupora rasilimali za nchi, na mauwaji na kuyafukarisha mataifa katika mchakato huo. AU kuunga mkono utawala wa madikteta duniani, ikiwemo kuwauzia silaha, kama Saudia Arabia, kutumiwa juu ya raia nchini Yemen na kwengineko? Ni ustaarabu wa aina gani kuwachukulia wahamiaji madhaifu na wasiojiweza na waombaji hifadhi wanaokimbia vita, mateso na udhalimu kuwa kama wanyama waharibifu – kukataa kuwapatia makaazi ya heshima na ulinzi?

Katika vita hivi vya kithaqafa, je unaweza kudai kuwa usekula ndio mfumo na nidhamu pekee inayoweza kuunganisha watu wa makabila, asili na imani tofauti …. wakati mfumo wako umejaa ubaguzi kutokana na imani zako za kitaifa na mapendeleo kwa wazungu? Hii ikijumuisha kujenga khofu, chuki, hasira na mgawanyiko baina ya jamii kupitia tabia ya wanasiasa wa kisekula na vyombo vya habari ya kueneza chuki kwa Uislamu ambao bila kuchoka wanaikashifu imani ya Kiislamu? Vipi unaweza kudai kuwa usekula ni nguvu ya uunganishaji wakati serikali za kisekula zinasema mfumo wa kiulimwengu umeenea ukuaji unaoongezeka na ushawishi wa mrengo wa kulia, ubaguzi, taasisi na harakati za kiimla? Na kwa vipi unakuwa na ujasiri wa kutamka kuwa imani ya Kiislamu inachochea mgawanyiko, wakati ni wewe na wafuasi wako wanasiasa wa kisekula ndio mnaoeneza riwaya za mgawanyiko wa Waislamu wanaojumuisha ‘safu ya 5’ nchini, ‘wengine’ na ‘maadui wa ndani’ kutokana na imani yao ya kidini, na wakati marufuku yako ya hijab na niqab inawatenga wanawake wa Kiislamu kutokana na mtengamano kamili ndani ya jamii? 

Ni Uislamu, kama ambavyo unapaswa kujua, ndio uliounganisha matabaka, makabila, na asili zote kuanzia China hadi Uhispania chini ya mfumo mmoja, dola moja iliotawaliwa na sheria zake, zenye kung'oa ubaguzi kutoka kwenye nyoyo za watu wake – kwani ni itakdi yake hasa inaepusha na kukataa fikra na fahamu hii yenye sumu inayouchochea: utaifa. Kwa hakika, yule mnayemvunjia heshima na kumshambulia – Mtume Muhammad (saw) amesema:

«فَلَيْسَ لِعَرَبِيٍّ عَلَى عَجَمِيٍّ فَضْلٌ، وَلَا لِعَجَمِيِّ عَلَى عَرَبِيٍّ فَضْلٌ، وَلَا لِأَسْوَدَ عَلَى أَبْيَضَ فَضْلٌ، وَلَا لِأَبْيَضَ عَلَى أَسْوَدَ فَضْلٌ، إِلَّا بِالتَّقْوَى»

"Hakuna ubora kwa Mwarabu juu ya asiyekuwa Mwarabu, wala kwa asiyekuwa Mwarabu juu ya Mwarabu; wala kwa mweusi juu ya mweupe, wala kwa mweupe juu ya mweusi, isipokuwa kwa uchaji Mungu.”

Zaidi ya hivyo, alikuwa ni Mtume wetu mpendwa (saw) aliyeufuma mfumo wa utawala mjini Madina ambapo chini ya mfumo huo watu wote walikuwa sawa chini ya sheria na wakifurahia haki sawa na usalama kwa raia bila ubaguzi – mweusi na mweupe, Muislamu na asiye Muislamu, mwanamume na mwanamke, tajiri na masikini. Mfumo huu – ambao unauumbua kwa vibandiko vya siasa kali na msimamo mkali – uliuonyesha dunia namna ya kusimamia kwa ukweli mahitaji na haki za wale wenye imani tofauti. Katiba ya Madina kwa mfano, iliasisi kuwa wasio Waislamu wote ndani ya dola inayotawaliwa na Uislamu kuwa na haki ya kutekeleza imani zao za kidini bila ya bughudha, unyanyasaji, au udhalilishaji. Hakika, Mtume wetu (saw) amesema:

«أَلَا مَنْ ظَلَمَ مُعَاهِدًا، أَوِ انْتَقَصَهُ، أَوْ كَلَّفَهُ فَوْقَ طَاقَتِهِ، أَوْ أَخَذَ مِنْهُ شَيْئًا بِغَيْرِ طِيبِ نَفْسٍ، فَأَنَا حَجِيجُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ» 

“Yeyote anayemdhulumu Mu’ahid (raia wa dola asie Muislamu), au kumpunguzia haki zake au akamkalifisha zaidi ya uwezo wake, au akachukua kitu kwake bila ya ridhaa ya nafsi yake, basi mimi nitapambana naye Siku ya Kiama”

Hii ndio sababu waandishi na wanahistoria wengi wasio Waislamu wa zama za nyuma wameisifu nidhamu ya Khilafah ya Kiislamu – ambayo kusimamishwa kwake tena mnaopinga – kama mwandishi wa Kiingereza, H. G. Wells, aliyeandika kuhusiana na uadilifu wa Khilafah: “Wameanzisha desturi tukufu za uvumilivu wa kiuadilifu. Wamehamasisha watu kuwa na moyo wa ukarimu na uvumilivu, na ulio na utu na wa kivitendo. Wameunda jamii ya ubinaadamu ambayo ni nadra kuona ukatili na ukosefu wa haki, kinyume na jamii yoyote iliyokuja kabla yake”, na Will Durant, mwandishi wa Kiamerika na mwanahistoria, aliye elezea katika kitabu chake, ‘Hadithi ya Hadhara – Zama za Imani’: “Wakati wa Khilafah ya Umayyah, watu wa dhimmi, Wakristo, Majusi, Mayahudi, na Wasabai, wote walifurahia kiwango cha uvumilivu ambao hatuuoni hata leo katika nchi za Kikristo. Walikuwa huru kutekeleza ibada za dini zao na makanisa yao na mahekalu yalihifadhiwa. Walifurahia mamlaka ambapo walikuwa chini ya sheria zao za kidini za wanachuoni na mahakimu.” Hakika, Khilafah sio tu iliwahifadhi raia wake wasio Waislamu, bali ikiwa kama dola ya kiutu iliostaarabika, iliwaokoa na kuwapatia mahali salama watu wa dini nyengine waliokumbana na udhalimu, kama inavyoonekana katika matendo ya Khalifah Bayezid II, ambaye katika karne ya 15, chini ya utawala wa Khilafah Uthmani, alipeleka kikosi chote cha jeshi la wanamaji ili kuwaokoa Mayahudi wa Ulaya 150,000 waliokuwa wakiteswa na watawala wa Kikristo wa Uhispania na kuwaweka katika ardhi za Waislamu.

Bw, Macron! Hifadhi gani nyengine ya nguvu ya kifikra uliyonayo mikononi mwako? Utadai kuwa usekula ni fikra iliozalika kutoka kwenye uongofu…. wakati chimbuko lake limeegemea juu ya mapatano ya kumtenganisha Mungu na dola, ambayo imepuuza suala la  mfumo upi ni wa imani sahihi kiakili, na umeweka kando mjadala wa yupi anayestahiki kutawalisha sheria kwa wanaadamu – Muumba au kiumbe Wake? Na vipi unaweza kudai kuwa usekula unategemea uongofu, wakati unawalazimisha Waislamu kukubali imani kupitia kuamini kibubusa kwa kutumia sheria kandamizi na vikwazo na kujenga khofu, badala ya hoja za kiakili? Hata hivyo, imani yetu ya Uislamu, inapingana na imani ya kibubusa na inahitaji watu waufuate kupitia imani thabiti ya kiakili na sio ya kulazimishwa, kwa kuwa ukweli wake unategemea dalili za kiakili zilizo wazi. Quran inaeleza:

   [وَمَا يَتَّبِعُ أَكْثَرُهُمْ إِلاَّ ظَنًّا إَنَّ الظَّنَّ لاَ يُغْنِي مِنَ الْحَقِّ شَيْئًا]

“Na wengi wao hawafuati ila dhana tu. na dhana haifai kitu mbele ya haki.” [Yunus: 36]. Pamoja na hayo, hukumu katika Uislamu ni tofauti na hukmu katika usekula, unakataza kila aina ya matumizi ya nguvu katika kukubali imani yake, kwani Quran iko wazi:

[لاَ إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ]

“Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani uongofu umekwisha pambanuka na upotofu.” [Al-Baqara: 256]

Huenda Bw. Macron, utatetea kuwa suala la kuitenga dini kutokana na dola ni njia ya kutengeneza jamii njema zilizo imara. Kama ni hivyo, basi kwa nini, ripoti ya Shirika la Afya Duniani ya 2011 imeiweka Ufaransa kuwa ni taifa lililo na mfadhaiko zaidi duniani, huku 1 kati ya watu 5 wanakiugua kutokana na mfadhaiko wa kimatibabu, na kutangazwa kuwa ni “bingwa wa dunia wa mateso” na vyombo vyake vyenyewe vya habari? Nafasi ya pili imezawadiwa Amerika, taifa jengine kuu kiongozi la kisekula duniani. Na kama mfumo wa kimaisha wa kiliberali wa kisekula ndio njia ya kuridhika na furaha, basi kwa nini kuna majaribio 220,000 ya watu kujiuwa nchini Ufaransa kila mwaka (Eurostat)? Jibu ni rahisi. Kuongezeka kwa suala la kuitenga dini na Mungu kutokana na maisha na jamii chini ya usekula kumeleta ombwe katika maisha ya watu, ikiwa ni pamoja na kutengeneza milima ya matatizo ya kiuchumi, kijamii, maadili na mengineyo ambayo watu hawawezi kuyashughulikia kwa ufanisi. Tunaona kwa mfano, vipi Ufaransa licha ya kuwa ni moja ya nchi tajiri zaidi duniani, lakini hata kabla ya COVID, mtu 1 kati ya 7 (milioni 9) walikuwa wanaishi chini ya mstari wa umasikini(Statista), mtu 1 kati ya 5 hakuweza kumiliki milo mitatu kwa siku (Secours Populaire (French Popular Relief), na kuna viwango vikubwa vinavyoongezeka vya ukosefu wa ajira, deni kubwa na matatizo ya kifedha kwa watu. Hali ya sasa ni janga zaidi, na linaangaliwa katika mataifa ya kisekula duniani kote. Zaidi ya hayo, uhuru wa kiliberali na mfumo wa kisekula wa kirasilimali umekuza ubinafsi, starehe na aina ya maisha ya kimada ambayo yamesababisha majanga katika ulevi na uraibu wa madawa ya kulevya pamoja na uhalifu. Nchini Ufaransa, mtu 1 kati ya 10 ana tatizo la ulevi (The Independent), wakati zaidi ya watu 110 hufariki kila siku kutokana na ajali au hali zinazohusiana na ulevi (Sante Publique France).

Kinyume chake, Uislamu unatoa dhumuni la wazi la maisha pamoja na msingi wa kiroho ambao kupitia kwake unaendana na matatizo na mazito, unasaidia kuepuka na kupunguza wasiwasi na mfadhaiko. Hii ni ikiongezea na ubinafsi, unyanyasaji, kupenda vitu vya kimada, ulevi na utumiaji wa madawa ya kulevya na ubinafsi haribifu wa kutafuta matamanio ya mtu binafsi bila kujali matokeo yake. Badala yake Uislamu umejenga akili ya kuwajibika inayobeba hisia ya kuwajibika katika matendo ya mtu na katika kuwashughulikia wengine kwa mujibu wa viwango vya juu vya kimaadili vilivyowekwa na Muumba. Pamoja na haya, nususi za Kiislamu zinaweka wazi masuluhisho mapana na sahihi kwa matatizo yote ya mwanaadamu, yenye kujenga jamii patanifu ilio na uhalifu wa kiwango cha chini iliobarikiwa na neema yenye kuwafaidisha wote, na sio watu wachache wa tabaka teule. Hii imedhihirishwa ndani ya karne nyingi za utawala wa Khilafah. Hivyo wakati uvamizi wa Ufaransa wa Afrika Kaskazini ukiacha urithi wa umasikini na kufeli kwa uchumi katika eneo hilo, utawala wa Kiislamu ndani ya maeneo yayo hayo chini ya Khilafah ya Umar bin Abdul Aziz, uliwanyanyua watu kutoka kwenye umasikini kupitia utekelezaji wa mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu, kiasi cha kuwa hakuna yeyote aliyehitajia zaka. Gavana (Wali) wa Afrika Kaskazini wa wakati huo, Yahya bin Said, amesema: “Nilipelekwa na Umar bin Abdul Aziz kukusanya zaka kutoka Afrika. Baada ya kukusanya, nilikusudia kuwapa watu masikini. Hata hivyo, sikumpata yeyote.”

Bw. Macron! Unadai kuwa imani za Kiislamu za kihafidhina huwa zinazalisha fujo na mauwaji ya raia, huku ukipiga mbiu ya kupuuzi kuwa usekula haukuuwa hata mtu mmoja. Hata hivyo, Waislamu hawahitaji mafunzo yoyote katika kuzuia umwagikaji wa damu, kutoka kwa nchi za kisekula ambazo zimezaliwa kutokana na mapinduzi yaliojengewa juu ya vitisho na mauwaji. Wala hatuhitaji mihadhara juu ya kuzuia uhalifu kutoka taifa la kikoloni ambalo mikono yake imejaa damu za mamilioni ya wasio na hatia, na ambalo sera zake za kigeni zimeleta makaburi kwa mataifa, yakiwemo Algeria na Rwanda. Kinyume chake, Uislamu unachukia machafuko ya kikatili na kumwaga damu za wasio na hatia, hata kama ni katika vita. Khalifah wa mwanzo wa Uislamu, Abu Bakar As-Sidiq (ra) aliwaagiza wanajeshi wake juu ya mipaka ya umwagaji damu wakati wa mapigano, akisema: Msifanye usaliti na msivuke mipaka, msije mkawa makhaini, na msikatekate maiti, msiuwe watoto, wala wazee, wala wanawake, msikate wala kuchoma miti, na msiikate miti ya matunda, msiuwe mbuzi, wala ngombe, wala ngamia, isipokuwa mnapohitajia kwa kula, mtawapitia watu waliojifunga na utawa, waachieni kwa kile walichojifunga nacho.” Hivyo wale wanaouwa wasio na hatia kwa dhamira ya kufikia malengo ya kisiasa, huchukuwa matendo yao kutoka kwenye fikra za kisekula za kirasilimali, na sio za Kiislamu!

Bw. Macron, huenda unahisi kuwa unaweza kushinda vita hivi vya kifikra vya kisekula dhidi ya Uislamu katika uwanja wa mapambano ya ‘Mwanamke’ na haki zake. Huenda unafikiri kuwa unaweza kuendelea kueneza hadithi zilizopitwa na wakati, zinazoratibiwa na wakoloni, zenye kudanganya kuwa eti usekula unaheshimu wanawake na kwamba Uislamu unawakandamiza, ukitegemea kuwa dunia itapuuza maandamano ya maelfu ya wanawake wa Kifaransa kwenye mitaa yako wakikasirishwa na maambukizi ya uovu wanaokumbana nao chini ya mfumo wa kisekula wa kiliberali? Unafikiri kuwa unaweza kuficha mbele ya watu, hali ya kuwa kila mwaka nchini Ufaransa zaidi ya wanawake 219,000 wanakumbana na unyanyasaji wa kijinsia (Euronews) na kwamba mwanamke mmoja anauawa kila siku tatu chini ya mikono ya mshirika wa sasa au wa zamani (France24), au ukweli kuwa zaidi ya nusu ya wanawake wa Ufaransa wamekuwa wakinyanyaswa kingono (Statista) na zaidi ya 1 kati ya 10 wamebakwa (Foundation Jean Jaures thinktank), au ukweli kuwa bunge la Ufaransa – kitovu cha utawala wa kisekula – limejawa na vitendo vya kingono? Na unaona kabisa kuwa takwimu hizi zinaakisiwa, kama sio mbaya zaidi, katika dola nyenginezo za kisekula duniani kote. Zaidi ya hivyo, vipi unaweza kudai, kwa macho makavu, kuwa mfumo wa kisekula unaheshimu wanawake, wakati ugeuzaji wao kuwa vyombo na utumwa wao wa kingono katika sekta za urembo, matangazo, filamu za ngono, na ukahaba yanatekelezwa katika dola za kisekula chini ya uhuru wa ngono wa kiliberali, zikiruhusu makampuni kufaidika kutokana na kuwashusha hadhi wanawake? Na unahisi ni uhuru wa aina gani kwa wanawake kuwa walezi wasio na waume, waking'ang'ana kuwalea na kuwapatia mahitaji watoto wao wakiwa peke yao, kutokana na kuvunjika kwa ndoa na maisha ya familia inayosababishwa na kuranda randa katika mahusiano kunakotokana na uhuru wa ngono wa kiliberali?

Wakati huo huo, masekula kwa kejeli wanaishutumu hijab au jilbab kwa kuwakandamiza wanawake, wakati kihakika wanaunda sehemu ya mfumo wa nidhamu ya kijamii inayoshirikisha mkusanyiko mpana wa sheria ambazo zinaendesha kwa ufanisi mahusiano baina ya wanaume na wanawake ili kuhakikisha ushirikiano baina ya jinsia katika nyanja zote za maisha kwa kuelekeza ukamilishaji wa matamanio ya kingono kupitia ndoa tu. Kwa hiyo ndio nidhamu ambayo, inakataza moja kwa moja udhihirishaji wa waziwazi na ashiki ya kingono kwa wanawake, pamoja na unufaikaji wa uzuri wao kwa dhumuni lolote, pamoja na tendo jengine lolote linaloshusha hadhi zao katika jamii.  Yote haya yanaleta mazingira ya kuheshimika kwa wanawake ndani ya jamii ambapo wanaweza kuyaendea maisha amma (ya hadharani), yakiepukana na usumbufu au unyanyasaji, ambapo pia inahifadhi utukufu wa ndoa, uadilifu wa kitengo cha familia, na haki za watoto. Na wakati usekula ukisherehekea yote ambayo ni uasherati na uchafu, na kuyafanya ni uhalifu yale ambayo ni ya staha na ya maadili, Uislamu umeyachukua yale mema na ya kuheshimika, hata kutamka neno moja tu linalokiuka heshima ya wanawake, kuwa ni uovu mkubwa. Hakika, Mtume Muhammad (saw), ambaye unamvunjia heshima na kumchafua, ameeleza kuwa hadhi ya mtu ipimwe kulingana na kiwango chake cha uzuri wa matendo yake kwa mkewe. Amesema SAW,

«إِنَّمَا النِّسَاءُ شَقَائِقُ الرِّجَالِ، ما أكرمهن إلا كريم وما أهانهن إلا لئيم»

“Wanawake ni vipande (sehemu) ya wanaume, hakuwa isipokuwa mkarimu anayewatendea wema wanawake, na hakuwa isipokuwa muovu anayewadhalilisha wanawake.” Na pia SAW amesema,

«أَكْمَلُ الْمُؤْمِنِينَ إِيمَانًا أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا وَخِيَارُكُمْ خِيَارُكُمْ لِنِسَائِهِمْ»

“Aliye mkamilifu zaidi wa imani ni yule mwenye tabia nzuri zaidi kati yenu, na mbora wenu ni yule aliye mbora wenu kwa wake zake”

Baada ya yote haya Bw. Macron, vipi unathubutu kudai kuwa Uislamu uko katika mgogoro, wakati Usekula ndio uko katika mmomonyoko? Ukweli ni kwamba huna silaha za kifikra za kuushambulia Uislamu, ndio sababu kwa nini umejielekeza hali ya kukata tamaa - kwenye uongo, matusi, na sheria kandamizi na kuzuia kupigana vita hivi vya kifikra, ukijua kuwa usekula umeshapoteza mapambano ya fikra za kiakili kwa Uislamu. Kwa hakika, wengi katika Wamagharibi wameshapoteza imani juu ya maadili ya demokrasia na usekula, wameona kupitia unafiki wa ahadi na madai yake ya uongo. Hii ndio sababu kwa nini unagoma hata kuridhia mjadala na Waislamu juu ya maadili na mfumo wao wa Kiislamu na kwa kile wanachotoa kwa wanaadamu na ulimwengu, na kuchagua badala yake kukaripia na kunyamazisha uelezaji wa imani yao.

Lakini sisi tukiwa Waislamu hatutoachana na imani yetu ya Kiislamu, hata kwa uongo na madongo kiasi gani unayoturushia…. hii si tu kwamba imani hizi zimejengwa juu ya ukweli, lakini pia kwa sababu dunia ambayo iko kwenye mgogoro hivi leo kutokana na usekula na mifumo mengine iliobuniwa na mwanaadamu, inahitaji maadili adhimu na sheria za Uislamu zaidi! Kwa hivyo Bw. Macron, unaweza kupambana vita hivi kama unahitaji….lakini tambua hiki….ni vita ambavyo hutoweza kushinda!

]أَفَمَنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَى تَقْوَى مِنَ اللّهِ وَرِضْوَانٍ خَيْرٌ أَم مَّنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىَ شَفَا جُرُفٍ هَارٍ فَانْهَارَ بِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ وَاللّهُ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

“Je mwenye kuweka msingi wa jengo lake juu ya kumcha Mwenyezi Mungu na radhi zake ni bora au mwenye kuweka msingi wa jengo lake juu ya ukingo wa shimo linaloburugunyika, na likaburugunyika naye katika Moto wa Jahannamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu.” [At-Taubah: 109]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Dkt. Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu