Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kuihusu Hizb ut Tahrir: Kazi Yetu na Ruwaza Yetu

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir [HT] ni chama cha kisiasa cha kilimwengu ambacho fikra yake ni Uislamu na lengo lake pekee ni kurejesha njia ya maisha ya Kiislamu kwa kuirejesha tena Khilafah. Tokea kuanzishwa kwake mnamo 1953, katika Al-Quds (Jerusalem), fikra yake na njia yake ya kufikia lengo hili zimechimbuka katika ufahamu wa ndani wa Uislamu, Aqida yake na nidhamu zake.

Katika wakati ambapo ulimwengu wa Kiislamu, zaidi katika Mashariki ya Kati ulipokuwa umezama katika fikra ya Utaifa, hasa ya Umoja wa Waarabu wote na utaifa wa Kiarabu, wakati walipozugwa na Ujamaa, na kuingia katika harakati za kieneo za kisekula za kupinga ukoloni, nuru ya mwangaza iliibuka kwa kuundwa Hizb ut Tahrir na Sheikh Taqiuddin Nabhani (rh).

Ni matumaini ya nuru yenye fikra angavu zilizo wazi, fikra za ndani na usadikishaji wa kuwa ina suluhisho la sawa kwa Ummah na njia ya kulifikia.

Hizb ut Tahrir, chama cha ukombozi, kimekuwa mbele ya muda wake. Fikra zake zilionekana kuwa ngeni wakati wa zama ambapo ukombozi ulikuwa umefinyika katika kukomboa ardhi kutoka kwa wavamizi wa kikoloni. HT ilifafanua wazi kuwa ukombozi wa kweli ni wa akili; ni ukombozi kutokana na dhana, fikra, maadili na njia ya maisha pamoja na mfumo wake ambao wavamizi wameuweka juu ya Ummah. HT ilisisitiza kuwa ukombozi wa kweli ulikuwa ni kuiepusha akili na uongozi wa kifikra (Al-Qiyadatul Fikriyyah) ya Kimagharibi, yaani kuitenganisha Dini kutokana na masuala ya maisha.

Imesemwa kuwa ukombozi wa kweli ni kuivua aqida ya Usekula na kuweka badala yake usadikishaji katika Aqida ya kiroho na kwa upande wa kisiasa wa Uislamu. HT imesisitiza kuwa ukombozi wa kweli hauwezi kukamilika hadi mifumo ya Kikafiri, Urasilimali au Ukomunisti uwe umesambaratishwa na mfumo wa Uislamu umetekelezwa.

Hivyo, inazugumzia juu ya Nahdha (uhuishaji). Kuihuisha akili. Na inasemwa, “Mwanadamu anahuika (yanhadhu) kulingana na kile anachokibeba katika fikra kuhusiana na ulimwengu, mwanadamu na maisha, na kuhusiana na mahusianao yao, kiujumla, kwa kile kilichotangulia katika maisha ya dunia na kile kinachokuja baada yake.

Kwa hivyo, ili mwanaadamu ahuike (yanhadh), ni lazima abadilike kimsingi na kwa ukamilifu juu ya fikra zake za sasa na azalishe fikra nyengine.”

(إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا۟ مَا بِأَنفُسِهِمْ)

“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yalioko kwa watu  mpaka wabadilishe wao yaliomo  nafsini mwao” (Ar-Rad 11).

Hii inaelezea kuwa mabadiliko katika jamii yanapatikana kwa kubadilisha fikra na hisia za watu na nidhamu inayowaongoza na kuwatawala.

Inaufafanua Uislamu kuwa ni njia ya maisha, yenye Aqida, fikra iliyokamilika, Aqida katika siasa na kiroho ambapo mfumo huchipuza. Mfumo alioshushiwa Mtume wetu mpendwa (saw). Unaainisha kukataliwa kuigawanya Dini katika mambo ya kimaisha na ya kidini.

Tokea kuanzishawa kwake, mnamo 1953, Hizb ut Tahrir imeunda katiba ya nidhamu hii ya Uislamu, Khilafah. HT imefafanua na kuelezea muundo, utawala na nidhamu mbali mbali za dola ya Khilafah kama uchumi na nidhamu ya utawala kama unavyosikia hivi leo.

Ina nyenzo zilizofafanuliwa vyema juu ya namna gani Khilafah itafanya kazi, muongozo wa uoni wake, dondoo zake baadhi kama unavyozisikia hivi leo. Hizi sio nyenzo za kitaaluma zinazoeleza juu ya umbile la upande la ki-Ungu la Dini hii, au kuuhami Uislamu kutokana na ukosolewaji wake, na wala sio tafakuri za wanafalsafa wa nadharia za kisiasa.

Bali, fikra tunazoziwakilisha hivi leo na nyenzo zilizofafanuliwa kwa uwazi ni kwa ajili ya urejeshaji wa kivitendo wa njia ya maisha ya Kiislamu. Ni kwa ajili ya kuirejesha tena Khilafah. Ni kwa ajili ya suluhisho la kivitendo kwa kadhia zetu hivi leo. Fikra hizi ni kwa ajili ya uoni wa kesho mpya, uoni wa dunia mpya, mpango mpya, dola mpya ilio na nguvu kubwa, Khilafah Rashidah ya pili, inshaAllah.

Wanazuoni 

Kwa upande wa utaalamu wetu, tunachukua msimamo wa kimsingi wa kutosifia vyeo au sifa za utaalamu wetu. Hii ni kuunyanyua Ummah kuangalia zaidi ya sifa na kushughulika zaidi juu ya maudhui na vyanzo yaani Quran na Sunnah.

Mtu anaweza kudai kuwa hii ndio inayokusudiwa na wanazuoni wote. Lakini, kama ambavyo baadhi wanaweza kushuhudia, vita dhidi ya Uislamu vinalenga kuugeuza Uislamu ili ulingane na fikra za kisekula za kiliberali na maadili yake. Bila ya kuwepo fikra na uoni wa wazi, wanazuoni na Waislamu wa kawaida hawasalimiki na ushawishi wa maadili ya kisekula na ni walengwa wa uingiliaji wa fikra za Kimagharibi katika Dini yetu. Utaalamu na vyeo vimekuwa vikitumika kama sehemu ya ajenda ya kuugeuza Uislamu.

Kazi ya HT ya kuirejesha Khilafah inahitaji utaalamu ambao Hizb wanao. Majaribio yoyote makini kuchunguza nyenzo zetu yatapelekea kuuonyesha zaidi ukweli huu. Hata hivyo, msimamo msingi wa kusifia vyeo ni mlima mrefu kuupanda lakini matokeo ya muda mrefu ya kuzikuza fikra za Kiislamu ni mapambano yenye thamani.

Hata hivyo, nitazungumza kwa uchache kuhusu viongozi wa Hizb ut Tahrir kama ni mfano.

Hizb ut Tahrir iliundwa na Sheikh Taqiuddin Nabhani (rh) pamoja na idadi kadhaa ya Wanazuoni, wengi wao walikuwa ni wahitimu kutoka Chuo Kikuu cha Al-Azhar. Wanachama waasisi wakiwemo Nimr Al-Masri, Dawud Hamdan, Ghanim Abdu, Sheikh Ahmed Daur, Sheikh AbdulQadiim Zallum pamoja na wanachuoni wengine.

Sheikh Taqi alizaliwa mwaka 1911, katika mji wa Ijzim maili chache kutoka Haifa. Ametokana na familia ya wanachuoni. Baba yake ni Sheikh Ibrahim alikuwa ni mwanasheria na mwalimu katika Sharia, na mama yake ni Taqiyya alikuwa hafidha katika Hadith. Babu yake upande wa mama ni Sheikh Yusuf al-Nabhani alikuwa maarufu katika Khilafah ya Uthmaniya na alikuwa Qadhi katika mahakama za Dola ya Uthmaniya.

Sheikh Taqi akawa ni hafidh wa Quran katika umri mdogo. Mnamo 1928 alikwenda Misri kwa masomo na aliweza kujiunga kwa wakati mmoja katika Chuo cha al-Azhar na Dar al-Ulum. Alihitimu kwa pamoja mwaka 1932 katika daraja ya juu katika digrii nne – Cheti cha elimu ya sekondari ya juu cha al-Azhar, digrii katika Sharia, digrii katika lugha ya kiarabu na fasihi na Ijaza ya kuwa qadhi katika Sharia.

Kutokana na taarifa zote kutoka kwa walimu wake na wanafunzi wenzake, Sheikh Taqi alikuwa ni mwenye kipaji akiwa na upana katika fikra zake, uzito katika hoja zake na alikuwa mwenye shakhsiya imara. Kabla ya kuiunda kwake HT, alifanya kazi ya uqadhi Jerusalem. Sheikh Taqi aliandika jalada nyingi za thaqafa zikiwemo vitabu, makala, uchambuzi wa kisiasa na Fatawa katika mawanda mengi.

Vivyo hivyo, Amir wa pili wa HT, Sheikh Abdul Qadiim Zallum (rh) alitokana na familia ya kidini. Alihitimu kutoka Al-Azhar na kutunukiwa Shahada tal ‘Alamiya na alibobea kwenye Sharia ambayo ni sawa na kiwango cha sasa cha Ph.D. Alikuwa ni faqihi na ameandika vitabu kadhaa, vikiwemo Al-Amwaal fii Dawla til-Khilafah (Mali katika Dola ya Khilafah).

Amir wa sasa na wa tatu, Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah mwanzoni alikulia na kusoma katika kambi ya wakimbizi karibu na Hebron na hatimaye alihitimu akiwa mhandisi mjenzi kutoka Chuo Kikuu cha Cairo Misri. Alikuwa msemaji wa mwanzo wa Hizb ut Tahrir na alikuwa akiwekwa kizuizini mara kwa mara na serikali ya Jordan. Kitabu chake, Taysir fi Usul at-Tafsir na msururu wa Maswali na Majibu katika kadhia tafauti inaonyesha kiwango chake kikubwa katika elimu yake. Kitabu cha Taysir fi Usul at-Tafsir, kimekusanya tasnifu juu ya misingi ya tafsiri inayofuatwa na utekelezaji wake kupitia tafsiri ya Surah Al-Baqara. Aliandika kitabu hiki akiwa gerezani Jordan.

Kujitoa muhanga

Hizb ut Tahrir imemwagika damu na machozi kwa ajili ya fikra zake na malengo yake ya kusimamisha Khilafah. Kutokea mwanzo katika 1953, imekuwa ikiteswa kote katika ulimwengu wa Kiislamu na kufungiwa. Wanachama wake wameendelea kuteswa, kuwekwa chini ya uchunguzi, kufukuzwa, kufungwa, kuteswa na kuuliwa. Hufanyiwa yote haya licha ya kuwa ni kundi lisilotumia nguvu kabisa.

Mwaka 1953, baada ya tangazo rasmi la kuasisiwa kwake, wanachama waanzilishi waliwekwa ndani. Walitakiwa kuachana na harakati hizo na hata kurubuniwa. Chama kilipigwa marufuku kama ilivyotakiwa huku harakati nyengine zikiruhusiwa kuendelea kutokana na mtazamo wao wa kifalsafa kuelekea serikali ya Jordan.

Sheria zilipitishwa kuzuia harakati za HT na kipindi chote cha miaka ya 1950 na 60 ukamataji wa wanachama ulikuwa ni kawaida. Katika kuonyesha nukta hii Mashababu huchukua mabegi yao yaliowekwa pajama na nakala ya tamko linalokusudiwa kutolewa ikiwa ni Msikitini, chuo kikuu au mtaani kwa kujua kuwa punde watakamatwa na mamlaka. 

Abdul Ghani al-Mallah alikuwa mwanachama wa mwanzo wa Hizb ut Tahrir kuuliwa kutokana na mateso na utawala wa Baath wa Iraq mnamo 1963.

Sheikh Abdul Aziz al-Badri, aliyekuwa mwanachama mashuhuri na mwanachuoni maarufu aliteswa na kuuliwa mnamo 1969 na chama cha Baath cha Iraq.

Sheikh Taqi aliwekwa ndani na kuteswa na serikali ya Iraq mnamo 1972; kwa muda wa miezi 3 alikuwa akipatiwa mlo mmoja mchache kwa siku.

Mnamo 1980, Muhammad Mustafa Ramadhan aliuliwa na Gaddafi nje ya Msikiti wa Regent Park mjini London. Gaddafi alibeba mapambano binafsi dhidi ya Hizb ut Tahrir. Mwaka 1983, aliwauwa wanachama kumi na tatu; walinyongwa katika vyuo vikuu na mashuleni mbele ya walimu wao, wanafunzi na familia. Mmoja wao alikuja chini akiwa hai, akanyongwa tena mara ya pili, kisha wakamfunga mwili wake nyuma ya gari iliyoendeshwa kwa kasi ikionekana na wanafamilia wake. Muhammad Muhathab Haffaf, baada ya kunyongwa, wafuasi wa utawala waliendelea kuupiga mwili wake. Mnamo April 2012, kumbukizi ya waliouliwa miaka 30 iliyopita ilifanyika katika Chuo Kikuu cha Tripoli kwenye uwanja ambapo mashahidi hao waliuliwa iliyopewa jina la “Shahidi Muhammad Muhathab Haffaf”.

Mwaka 1984, Saddam Hussein aliwauwa wanachama 60 wakiwemo maafisa wa kijeshi.

Mwaka 1999, Farhad Usmanov aliuliwa na Islam Karimov nchini Uzbekistan. Unyama uliofanywa na Islam Karimov dhidi ya Hizb ut Tahrir hauna kikomo. Baadhi ya wanachama wa Hizb walichomwa wakiwa hai. Hata wanawake hawakusalimika. Kwa mfano, Musharaf Usmanov, mke wa Farhad aliwekwa ndani pia. Aliolewa baadaye na Ismat Hudoyberdiyev ambaye naye pia aliuliwa mnamo 2002.

Mnamo 2005, katika mji wa Andijan, Uzbekistan, inakisiwa Waislamu kati ya 500 hadi 700 waliuliwa na Islam Karimov wakiwemo wanaume, wanawake na watoto, wakiwa wengi wao ni wabebaji da’wah wa Hizb.

Mwaka 2010, takriban wanachama 8,000 wa Hizb ut Tahrir walifungwa jela Uzbekistan.

Mwaka 2012, Naveed Butt, Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir nchini Pakistan alitekwa nyara na idara za kijasusi mchana kweupe na hadi sasa hajulikani hali yake wala wapi alipo. 

Pamoja na hayo, ndani ya miaka hii 20 iliopita, maelfu ya wanachama wake waliswekwa ndani nchini Tunisia, Misri, Tanzania, Yemen, Palestina, Lebanon, Jordan, Syria, Kuwait, Uturuki, Pakistan, Bangladesh, Uzbekistan, Kyrgyzstan, Tajikistan, Kazakhstan, Urusi, na Crimea. Hupewa vifungo virefu hasa katika nchi za Asia ya Kati na Urusi.

Hii ni mifano michache ya kujitoa muhanga kwa wanaume na wanawake wa HT kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) na kwa kazi ya kurejesha Khilafah. Ni sehemu ya Ummah huu ambao unateseka pamoja kwa ajili ya Uislamu. Uovu wao si mwengine isipokuwa ni kusema neno la Haqq dhidi ya watawala waovu na kulingania utabikishwaji wa Uislamu. Mwenyezi Mungu azinyanyue daraja zao Akhera, awasahilishie mateso yao, awarejeshe kwa familia zao wale waliofungwa na awanyanyue kwenye daraja ya Mashahidi, ishaAllah. Amiin

Welekevu wa Kisiasa

Kazi ya kuhuisha na kusimamisha Khilafah ni kazi ya kisiasa ambayo inaongozwa na Uislamu. Welekevu wa kisiasa ni kuwa na fikra ya wazi, uoni, mtazamo wa kifikra, umahiri katika kufikiri, ufahamu wa siasa za ndani na za kimataifa na ufahamu wa maumbile ya jamii. Bila ya kuwa na sifa hizi, harakati zitashindwa na kumilikiwa na mikono ya maadui zao na hawatoweza kufuata njia ya mwamko.

Kuna “kampeni ya kuwatenga Waislamu na siasa…imefikia hatua ya kuisawiri siasa kuwa yenye kukinzana na utukufu na hali ya kiroho ya Uislamu. Kwa hivyo, Ummah unapaswa kuelewa siri iliyo nyuma ya vita vinavyopiganwa na dola za kikafiri na watawala vibaraka dhidi ya makundi ya Kiislamu yanayofanya kazi ya kuwahuisha Waislamu …Ni muhimu kuulea Ummah kwa thaqafa ya Kiislamu na kuendelea kuupenyezea fikra za kisiasa za Kiislamu na hukmu na kuelezea namna ambavyo fikra hizi na hukmu zinavyotokana na Aqida ya Kiislamu…Ni lazima pia kuimakinisha thaqafa hii kutokana na upande wake wa kiroho katika hadhi yake kama maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu (swt)” – (kitabu): Fikra za Kisiasa.

Hizb imeendelea kuelezea ufahamu wake ulio sahihi wa siasa za kilimwengu na werevu wake katika fikra za kisiasa kiujumla. Kwa kuifafanua nukta hii, nitapitia mifano ifuatayo.

Mnamo miaka ya 1950 wakati Mashariki ya Kati yote imebanwa na fikra ya Umoja wa Waarabu na kuvutiwa na Gamal Abdel Nasser, kuwa mkombozi mkuu, Hizb ut Tahrir ilisema hakuwa chochote isipokuwa ni kibaraka wa Marekani. Kwa wakati ule hili halikufikirika kabisa. Hizb ilisumbuka sana kutokana na msimamo wetu wa kisiasa imara na usio maarufu. Wanachama sio tu waliteswa na mamlaka za utawala bali hata watu jumla kwa wakati ule.

Zaidi ya hivyo, tulisema kuwa uundwaji wa Umoja wa Jamhuri ya Kiarabu (UAR) baina ya Misri na Syria ilikuwa ni sehemu ya mipango ya Amerika katika eneo wakati Umoja wa Kiarabu (Arab Union) baina ya Jordan na Iraq ilikuwa ni jaribio la Uingereza kuweka udhibiti wake. Miongo kadhaa baadaye msimamo wetu ulishuhudiwa kuwa ni sahihi.

Mfano mwengine ni ule uliotokea July 1966 tulionya kuwa Ukanda wa Ghaza utawekwa chini ya udhibiti wa umbile la Kiyahudi na usawazishaji wa mahusiano utafanyika baina ya ‘Israel’ na Jordan. Ujumbe ulipelekwa kumuonya Waziri Mkuu wa Jordan Wasfi Al-Tall dhidi ya hatua hiyo. Alikataa madai haya na kusema jambo kama hilo halitotokea wakati yeye ni waziri mkuu. Mwaka uliofuata, mnamo June 1967, wakati wa Vita vya Siku Sita, hili ndilo hasa lililotokea. Tukatangaza Mfalme Hussein kuwa ni msaliti na bila shaka ukamataji ulifuatia kama ilivyotarajiwa.

Vile vile, tulimuwajibisha Khomeini, kupinga katiba yake na mwaka 1979 kusema kuwa mapinduzi yalisaidiwa na Amerika. Bila shaka kwa wakati huo hili halikuaminika. Watu wengi zikiwemo harakati nyingine za Kiislamu wakati huo walikuwa waungaji mkono kwa ukamilifu na/au hawakuwa wenye kumkosoa Khomeini na Mapinduzi ya Iran. Hata hivi sasa, tunaendelea kusema kuwa Iran ni kibaraka wa yule anayeitwa “shetani mkuu” Amerika. Haya yamedhihirika hivi sasa kwa kutolewa nyaraka zinazoonyesha mawasiliano baina ya Khomeini na CIA. Kwa kusema tu kuwa hakuna mvutano baina ya Iran na Amerika.

Miongo kadhaa baadaye msimamo wetu ulithibitika kuwa sahihi.

Mnamo 1999, wakati General Pervaiz Musharaf alipoingia madarakani Pakistan, wengi wa watu na harakati nyengine za Kiislamu ziliunga mkono mapinduzi. Hata hivyo, tulisema wazi alikuwa ni kibaraka wa Amerika akiwa na mipango ya kumaliza harakati za upinzani katika Kashmir na kuiruhusu India kuimarisha mamlaka yake Kashmir. Alikuwa mshiriki muaminifu wa vita dhidi ya ugaidi na mipango ya Amerika katika eneo. Miaka ishirini baadaye, mnamo 2019, Kashmir hatimaye imeingia kwa ukamilifu chini ya mamlaka ya India, na Pakistan kuridhia kimya kimya, ikithibitisha ufahamu wetu wa hali ya kisiasa.

Wakati wa machafuko ya Syria tulisisitiza tena kuwa Bashar Al-Assad alikuwa ni kibaraka wa Amerika, na Amerika ni mchezaji muhimu aliyeileta Urusi, Iran, Uturuki, wanamgambo wa Kikurdi na ISIS kuzuia mapinduzi.

Mfano mwengine, mnamo 1996 na 1997 tulichapisha vitabu vinavyoitwa Njama ya Marekani ya Kuuangamiza Uislamu na Fikra Hatari. Katika vitabu hivi tulielezea maneno kama Ugaidi, Demokrasia, Uhuru, Dini mseto, Vyama Vingi nk. kuwa ni fikra katika vita dhidi ya Uislamu.

Tulisema, “njama za sasa za Amerika zina lengo la kuuangamiza Uislamu kwa kuwafanya Waislamu waikatae itikadi yao na kuukumbatia usekula na kuufanya Urasilimali kuwa “Dini” mpya kwao kama msingi wa fikra zao…ikimaanisha kuuweka Uislamu mbali kabisa na maisha yao ambapo hakuna kinachobakia isipokuwa ibada za kiroho tu zinazotekelezwa kwenye nyumba za ibada.

Ushahidi wa wazi wa hili ni kuwa Amerika, wakati ikifanya kampeni ya kuufanya Urasilimali kuwa wa kilimwengu, imeanzisha kampeni ya kuupiga vita Uislamu ima kwa kuwabambikia wale wanaoshikamana na Uislamu kuwa ni magaidi, au kwa kuwalazimisha watawala waovu katika ardhi za Waislamu kuwakandamiza wale wanaofanya kazi kwa ikhlasi ya kuuhuisha Ummah juu ya msingi wa Uislamu, pamoja na kuharibu fikra ya Uislamu kwa msaada wa vibaraka na wandani wao.”

Hiki ni sawa kabisa na kile tunachokiona hivi leo juu ya vita dhidi ya Uislamu. Vile vile fikra zetu na maoni ya kisiasa yamethibitika kuwa sahihi.

Mwisho, mnamo Disemba 2021, kabla ya vita kuanza baina ya Urusi na Ukraine tulisema, “kuwa Urusi inajiburuza yenyewe kwenye mzozo … na Amerika inaweza … kuichokoza Urusi ili isiwe na upenyo au chaguo ila kuivamia Ukraine, [ambapo] itazama ndani ya matope ya Ukraine na kuwa matatani na Ulaya. Ukraine sio mwanachama wa NATO ambapo Amerika haitoweza kuilinda kijeshi [bali itaweza kutumia vikwazo vya kiuchumi tu]. Pindi Urusi ikifanya makosa na kuivamia Ukraine, itaipatia Amerika uhalali wa kuzitiisha nchi za Ulaya na kuzirejesha kuwa chini ya guo la Amerika kwa kisingizio cha kusimama pamoja dhidi ya uchokozi wa Urusi, ambao hauendani na ugawanyaji sawa wa nguvu baina ya mataifa unaotetewa na Urusi. Kuna mtazamo ambao Urusi hauuoni. [Kwa kuongezeka] mbinyo dhidi ya Urusi [na] katika tukio la uvamizi wake Ukraine, Amerika itakuwa na zana mpya ya kuubomoa muungano baina ya Urusi na China…pindi Amerika itaamua kuiingiza Urusi hatarini na kuisukuma kwenye vita na Ukraine, basi Urusi itaangukia au kunasa katika mpango wake.” 

Zaidi ya kile tulichokisema juu ya suala hili, hivi sasa tunaona limekuja kutokea. Yote hayo ni kuvuta nadhari juu ya ukweli wa kuwa Hizb iko vizuri kabisa katika uwerevu na utambuzi wa kisiasa. Hivyo, inao Wanasiasa weledi ambao inshaAllah wataongoza Khilafah ijayo.

Misingi, Uthabiti na Kutobadili Msimamo

HT imekuwa mkweli na shujaa katika siasa licha ya ukandamizaji wanaopatiwa duniani kote. Tokea kuasisiwa kwake, imesimama kwenye misingi, isiyoyumba na isiyobadilika. Siasa za kifalsafa, siasa za kimanufaa au Maslaha sio sehemu ya DNA yake. Licha ya unyanyasaji, kutiwa mbaroni, mateso na kuuliwa wanachama wake, Hizb ut Tahrir haikuondoa hata chembe ya msimamo kwa madhalimu wake.

Haikubadili jina lake, haikuyeyusha fikra zake na wala haikulegeza msimamo juu ya njia yake ya kuirejesha Khilafah. Njia iliyoivua kutoka katika Quran, Sunnah na Serah ya Mtume wetu (ﷺ) pekee. Njia inayoiamini kuwa ni Hukmu Shar’i.

Kimsingi, hatushiriki kwenye siasa za chaguzi za kisekula. Kimsingi, hatushiki nafasi za uongozi kwenye serikali za kisekula. Kimsingi, hatuwanyenyekei madhalimu wetu. Kimsingi, hatupigi picha za kibinafsi na wale wanaotupiga mabomu. Kimsingi, tunaamini yote haya ni Haramu.

Kimsingi, hatuwabembelezi watawala Waislamu madhalimu. Kimsingi, hatuna makubaliano nao. Kimsingi, hatubebi ajenda zao.

Kimsingi, tunazungumza Haqqi bila kujali matokeo juu ya Hizb au kwa mtu binafsi. Kimsingi, tunaizungumza Haqqi licha ya kuwa haina umaarufu.

Kimsingi, hatubadilishi fikra sanifu za Uislamu wakati zinapowafikiana na mazingira ya kisiasa au kwenda sambamba na ajenda za Wamagharibi kuurekebisha Uislamu.

Kimsingi, hatufungamani na waliberali au wahafidhina. Kimsingi, hatuurekebishi Uislamu kuwiana na usasa, uliberali au usekula.

Kimsingi, hatuzihafifishi fikra za Khilafah, Sharia, Jihad, Amr bil Ma’ruf wa nahyu anil Munkar, Hijab, ndoa, Hudud nk.

Kimsingi, tunashikamana na njia ya siasa ya Mtume na sio fikra za kifalsafa au siasa za kimanufaa. Kuwa washikiliaji wa misingi ni kufuata Dini ya Uislamu kwa ukamilifu wake kwa kufahamu dalili husika. Kuwa wenye kushika misingi ni kushikilia msimamo, ukakamavu na kutolegeza msimamo katika utiifu wa Dini, utiifu kwa Mwenyezi Mungu (سبحانه وتعالى), utiifu kwa Maamrisho Yake: (وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا) “Wala usiuze aya zangu kwa thamani chache” (Al-Maida 44)

Ruwaza Yetu

Hivi leo tumekuonyesheni mpango makini wa uoni wetu kwa ajili ya kesho mpya kwa Ummah na dunia kwa jumla. Uoni wetu ni kwa fikra hizi kuwa zenye uwazi na uhalisia ili ziweze kubadilisha maisha ya walimwengu. Hivyo, ni jambo la muhimu kuuangalia Uislamu kwa uoni wake wenyewe wa kilimwengu na kwa elimu ya ufahamu. Mara nyingi, baadhi ya wasomi, wanafikra, na harakati zinajihusisha na kuusawazisha Uislamu katika usasa, kuufinyanga ulingane na kiwango cha hisia cha Kimagharibi na “kuwepesisha” uwepo wetu katika ardhi za Magharibi. Uoni umekomea katika kutafuta uwepo wa hali njema katika usekula wa Kimagharibi ambapo tutakuwa “tupo huru” kutekeleza dini yetu na “kukubaliwa”. Udadisi wa ndani juu ya hili utagundua kuwa “uhuru na kukubalika” huko ni dhana ya hadaa tu. Bila shaka, tuna masuala maalum ya kushughulika nayo tukiwa kama ‘wachache’ katika nchi za magharibi lakini fikra kama hiyo ya uchache na Uislamu wa kisiasa wa kieneo sio njia ya Mtume wetu (ﷺ).

Mtume wetu mpendwa (ﷺ) na kundi dogo la Waislamu Makkah walikuwa wachache. Hata hivyo, yeye  (ﷺ) tokea mwanzoni alipingana na hali ilivyo, akilingania kuun’goa mfumo uliyopo ambao yeye (ﷺ) alizaliwa ndani yake na akipigia mahesabu dola kubwa ambayo itaikomboa Roma na Fursi. Ni msimamo wenye msingi wa kishujaa na uoni bora ulioje.

Hivyo, tunahitaji kupanua upeo wetu. Kile kinachohitajika ni kuiangali dunia kwa mtazamo wa Kiislamu kwa uoni wa kesho ambao unahitaji kuondoa kiza cha Usekula na kuing’arisha dunia chini ya utawala wa Kiislamu yaani Khilafah.

Ummah umeishi bila ya Sheria za Mwenyezi Mungu (سبحانه وتعالى) kwa miaka 101 ya Hijria tokea kuvunjwa kwa Khilafah, ukikumbana na udhalilifu, udhalimu, uvamizi, ufisadi, vita, kutokuwa na umoja, ukoloni na ukatili dhidi ya mwili wake.

Chama Kisiasa cha Kilimwengu

Kujiunga na Kazi Hii

Hapa tunaonyesha chama cha Kiislamu cha kisiasa kilichojitoa kwa ajili ya kuuhuisha Ummah na kurejesha njia ya maisha ya Kiislamu. Chama cha Kilimwengu, kilichoenea katika nchi 40 kutokea hapa Amerika hadi Australia kikiwa na uthabiti wa kifikra, ustahamilivu dhidi ya mateso na msimamo madhubuti na nguvu ya utashi wa kulifikia lengo lake. Licha ya mateso na kuzuiwa taarifa zake kwenye vyombo vya habari, kimeweza kuhamasisha watu duniani kwa ajili ya lengo hili.

Kwa mfano, mnamo mwaka 2007, wakati wa kampeni yake ya Rajab nchini Indonesia, wahudhuriaji 100,000 waliujaza uwanja wa michezo wa Gelora Bung wa Jakarta, wengi wao walikuwa wanawake. Mwaka uliopita, katika kumbukizi ya miaka 100 ya Hijria ya kuanguka kwa Khilafah, HT iliendesha kampeni ya kilimwengu kutoka Amerika hadi Australia, kutoka Uzbekistan hadi Afrika Mashariki, na hata kufikia Afghanistan.

Katika kutilia nguvu, huu sio tu wito kwa Khilafah bali, kazi yetu inahitaji kubomoa mifumo iliyopo sasa katika ulimwengu wa Kiislamu na kutoa suluhisho la kivitendo kwa ajili ya kadhia zetu hivi leo. Katika muktadha wa Amerika, HT ilichukua msimamo wa kimsingi usio wa maridhiano juu ya kadhia mbali mbali zinazoathiri Ummah hapa Amerika, hasa baada ya 9/11 wakati wengi wakifanya mgeuko wa ghafla juu ya masuala nyeti.

Kutokea kuionya jamii juu ya hatari ya ushiriki katika siasa (zilizo kinyume na Uislamu), mipango ya CVE (Countering Violent Extremism),  simulizi za Vita dhidi ya Ugaidi, siasa za kitambulisho na hata katika masuala yahusuyo kuigawanya Aqida yetu iwe ya upande wa dini na ya upande wa dunia, ‘Uislamu wa Kiamerika’ na masuala ya fiqh kama kuonekana kwa mwezi na ‘fiqhi ya wachache’, Hizb imeendelea kujihusisha na kadhia za Ummah licha ya vikwazo vinavyowekwa mbele yao. Haijafungamana na ajenda za upande wowote uwe wa ‘kiliberali’ au ‘mrengo wa kulia’ wala haijaingia kwenye mchezo wa simulizi za ‘Muislamu mzuri / Muislamu mbaya.

HT imeshikilia misingi ya kijasiri ya Kiislamu na rai kwenye masuala kama hayo hata kama hayakuwa maarufu bila ya kulegeza msimamo kwa muda wote huo. Imekuwa mbele ya wakati. Imekuwa mbele ya mpindo. Imefanya hayo bila kutaka chochote cha heshima za kidunia, hata pongezi, bali ipo moja kwa moja kwa ajili ya kuufikiria Ummah na kutaka radhi za Mwenyezi Mungu (سبحانه وتعالى).

Hizb ut Tahrir imekuwa mbele ya juhudi hizi na utambuzi wa Ummah kwake ni kutokana na kuzifunua akili za Waislamu katika kulifikia lengo la kusimamisha Khilafah.

Hata kwa mkosoaji wake mkubwa, Zeyno Baran amekuja kukiri juu ya nukta hii. Ameelezea, “Mafanikio makubwa ya Hizb ut Tahrir hadi sasa ni kuwa imehamisha kadhia za mjadala ndani ya ulimwengu wa Waislamu. Hadi miaka michache iliopita, makundi mengi ya Kiislamu yaliichukulia dhana ya kusimamisha Khilafah mpya ni jambo la kindoto. Hivi sasa, idadi kubwa ya watu wanalizingatia kuwa ni lengo muhimu linalohitaji mazingatio. Na baada ya miongo kadhaa ya kutia mkazo upatikanaji na umoja wa jamii ya Kiislamu ya kilimwengu (Ummah), Hizb ut Tahrir inaweza kupata heshima katika hisia zinazoongezeka miongoni mwa Waislamu ambapo kitambulisho chao msingi kina simama, na uaminifu wao msingi umepatikana kutokana na dini yao zaidi kuliko kwenye asili zao, makabila, au utaifa.” (Fighting the War of Ideas – Zeyno Baran)

Kusimamishwa kwa Khilafah ni “fikra ambayo muda wake umewadia.”

Patrick Buchanan ameeleza, “Uislamu umeweza kuvumilia karne mbili za kushindwa na kudhalilishwa za Himaya ya Ottoman na kuvunjwa kwa Khilafah na Ataturk. Umevumilia vizazi vya utawala wa Wamagharibi. Umedumu kwenye kipindi cha falme za mwanzoni za Wamagharibi nchini Misri, Iraq, Libya, Ethiopia na Iran. Uislamu ulijihifadhi na ukomunisti, ulisalimika na kushindwa kwa Unassiriya (fikra za Abdel Nassir) mnamo 1967, na umeonyesha uvumilivu zaidi ya utaifa wa Arafat au Saddam. Hivi sasa, unakataa kusalimu amri kwa dola kuu ya mwisho. Ikiwa utawala wa Kiislamu ni fikra iliokita miongoni mwa Umma wa Kiislamu, vipi basi jeshi bora zaidi duniani litauzuia?” (An idea whose time has come – Patrick Buchanan) 

Khilafah ni miongoni mwa misingi ya Uislamu. Sio “siasa kali” bali ni sehemu ya Uislamu iliyo ya kawaida. Kusimamisha tena Khilafah ni wajibu/fardhi juu yetu sote.

Uwe unaungana na juhudi hizi au uwe mtazamaji au mpingaji, lazima mtu atambue kuwa muelekeo wa safari ya Ummah ni kuelekea kwenye lengo hili na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt) itasimama pamoja nawe au bila ya wewe.

Swali ni je, wewe uko wapi katika njia hii?

Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

(يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱسْتَجِيبُوا۟ لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ)

“Enyi mlioamini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapokuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele” [Anfaal: 24]

Uislamu na utabikishaji wa Uislamu ndio unaupa uhai kwa Ummah wetu.

Angalia kila upande, huoni na kuhisi uchungu na maumivu makali ya Ummah? Angalia kila upande, husikii mayowe na vilio vya wanawake na watoto? Angalia kila upande, husikii ubakaji kwa kina mama na dada zetu nchini India na kufungwa vizazi wanawake nchi China. Hivyo huhisi maumivu yanayopitia Ummah huu? Mpaka lini, ndugu zanguni, mpaka lini? Macho yatalia mpaka lini? Moyo utabeba maumivu haya mpaka lini? Enyi Ummah, suluhisho ni lipi kama sio kusimamisha Khilafah.

Jiungeni na kazi hii, ndugu zanguni. Jiungeni na juhudi hizi pamoja na Hizb ut Tahrir. Chama kilichosimama juu ya misingi, kisichoyumba na kisichobadili misimamo. Chama chenye wanasiasa mahiri na uoni kwa ajili ya dunia mpya, mfumo mpya, Khilafah Rashida mpya, kwa njia ambayo haijailegezea msimamo hata shubiri moja. Fanyeni kazi na Hizb ut Tahrir kusaidia kusimamisha tena Khilafah, ala- Minhaj an-Nubuwah, kwa njia ya Mtume (ﷺ).

Hatimaye, kumbukeni ahadi ya Mwenyezi Mungu (سبحانه وتعالى):

(يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِن تَنصُرُوا۟ ٱللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ)

“Enyi mlioamini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad 7]

#ReturnTheKhilafah   #YenidenHilafet 
 #الخلافة_101  #أقيموا_الخلافة  
 #TurudisheniKhilafah

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdur-Rafay

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu