Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Bishara Njema Kwako Naveed Butt: Kuwa Na Subira Nzuri Kwani Muda wa Khilafah Umewadia

(Imetafsiriwa)

Kwa muda wa miaka kumi, hakuna anayejua Idara ya Usalama ya Pakistan (ISI) imemuweka wapi Ndugu Naveed Butt, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir Wilaya ya Pakistan, au wapi ameshikiliwa.

Miaka kumi imepita tokea 11/5/2012, na Hizb ut Tahrir, na tokea kuanza kwake, imeharakisha hatua miongoni mwa Ummah wa Kiislamu kusimamisha jengo kubwa la Khilafah; jengo lenye kuwahifadhi wanaadamu kutokana na mateso ya mfumo wa kirasilimali na watekelezaji wake.

Huenda mambo yanakwenda bila kusema kuwa kundi lenye utambuzi lipo katika kipindi cha maisha ya Makkah, likiwa na mazingira yake ya joto (magumu) na baridi (afueni), ambalo mpango wake umechorwa na mpendwa wetu Muhammad (saw) wakati Mwenyezi Mungu (swt) alipomwambia:

[فَٱصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ ٱلْمُشْرِكِينَ]

"Basi wewe tangaza uliyoamrishwa, na jitenge na washirikina." [Al-Hijr: 94].

Hivyo, Mtume (saw) alianza kuwasiliana na watu kujenga jengo juu ya msingi wa mfumo mtukufu wa Kiislamu. Yeye (saw) alijenga jamii yenye ufahamu wa kisiasa ambayo imeuonyesha Uislamu katika uelewa wa ndani wa kisiasa, ili kwa jamii hii, Mtume (saw) aweze kuunda rai jumla kwa fikra za Uislamu kuwa ni mbadala wa fikra za watu wa Makkah na njia yao ya maisha ya ufisadi inayoendeleza dhulma na uovu. Hatua ya kipindi cha Makkah ilikuwa ni amali ilionyanyuliwa ya kisiasa ilio mbali na amali yoyote ya kinguvu. Ulikuwa ni mstari wa wazi na uliofafanuliwa vizuri ambao unachambua ukubwa wa amali ya kifikra ambayo inawanyanyua wabebaji Da’wah kwenye hatua kubwa, na kuwafanya wenye kujenga utukufu wa Ummah kupitia Uislamu. Kwa hivyo, lazima tuamini kikweli ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na bishara za Mtume (saw) kuwa suluhisho lipo karibu, na kuwa muda umeshakuja kutangaza Dola ya Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume.

Hatua ya kipindi cha Makkah inakusanya siri za kazi ilio makini, kunyanyua kifikra, na kujenga shakhsia ya Kiislamu na kifikra, yaani, kujenga wanasiasa wa kuweza kupambana na hali ngumu na mazingira mazito zaidi ya kuogofya na kufahamu namna ya kukabiliana na hali ya joto na kutengeneza njia ya kuvuka.

Hatua ya kipindi cha Makkah imeuzunguka Ummah hivi sasa kwa namna ya kuonyesha Ummah wa Kiislamu unavyojengwa na kutengenezwa, kwa jengo la kifikra juu ya msingi wa Uislamu na kuufanya Uislamu kuwa kiongozi wa kifikra kwa ajili ya Ummah, na kuwavunja moyo maadui zake.

Kile ambacho ndugu yetu Naveed Butt, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Pakistan, alieswekwa jela na kuwekwa mbali na watoto wake na kuzuiwa kufanya Da’wah, katika kupambana dhidi ya fikra chafu, na kufichua njama za kimataifa dhidi ya Ummah wa Kiislamu, ni jambo la kusikitisha kwa vipimo vya kibinaadamu. Tunapata maumivu kwa kutengana naye kwa miaka, lakini amri za Mwenyezi Mungu ni zenye kunufaisha zaidi kwetu na kwake, hatujui, huenda Mwenyezi Mungu (swt) atatuonyesha mazuri zaidi kwa kukaa kwake mahabusu, kuweka taadhima kwa hatua ya kipindi cha Makkah na kuwa imara juu yake, bila kukengeuka hata kwa inchi moja; kuwa hakuna kazi ya utumiaji nguvu. Licha ya uzito ambao madhalimu hujaribu kuwatwisha kundi la walio na ufahamu juu ya mfumo wa Uislamu, ukiwa ni fikra na njia, kuwatoa japo kwa shubiri moja, hawakufanikiwa kabisa, na hili ndilo lililowashangaza na kuwaogofya. Mtume (saw) alisema kwa familia ya Yasir: «صَبْراً آلَ يَاسِرٍ فَإِنَّ مَوْعِدَكُمُ الْجَنَّةُ» “Kuweni na subira enyi watu wa Yasir kwani makazi yenu ni Jannah”

Majaribu na mateso kwa Ammar bin Yasir na wazee wake, Yasir na Sumayyah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, yalikuwa makali. Sumayyah alikuwa ni shahidi wa kwanza katika Uislamu wakati alipochomwa mkuki na Abu Jahl, laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake. Na Khabbab bin Al-Aratt, aliposema kumwambia Mtume (saw): «أَلَا تَسْتَنْصِرُ لَنَا، أَلَا تَدْعُو لَنَا؟» “Je hututakii nusra sisi, je hutuombei kwa Mwenyezi Mungu?” Ni maombi yenye kuonyesha uzito wa adhabu walizokabiliana nazo, yanayotoka kwenye nyoyo zilizochoshwa kwa manyanyaso na mateso, wakitaka nafuu ya haraka na ushindi wa karibu.

Sisi hivi sasa tupo katika kipindi cha Makkah, tukimuomba Mwenyezi Mungu (swt) kutufanyia haraka kwa ushindi kama alivyofanya haraka kwa ushindi wa kizazi cha mwanzo baada ya kupata manyanyaso makubwa. Hivi sasa tupo katika maumivu kwa sababu ya maafa ya Wa-Rohingya, Waislamu wa Uyghur, hali mbaya ya Naveed Butt na ndugu zake, watu wetu katika Kashmir na Palestina, ukandamizaji wa Al-Sisi nchini Misri, njaa na mateso nchini Syria, Iraq, Lebanon, Tunisia, Yemen, Sudan na Somalia, kama mwili wetu umechanwa chanwa. Hivyo na tumuombe Mwenyezi Mungu (swt) atusaidie kwa ufunguzi mkubwa wa Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume.

Mtume wetu mtukufu (saw) alifanya maombi aliporudi kutoka Taif, baada ya kile kilichomtokea kwa ndugu watatu wa Thaqif, Abd Yalil bin Amr bin Omair, Masoud na Habib, walipowashawishi wapumbavu wao na watumwa wao kumtukana Mtume (saw) na kumfukuza, kumvurumishia mawe hadi visigino vyake kuenea damu na kuishia kwenye bustani, na akaomba dua: «اللَّهُمَّ إِلَيْكَ أَشْكُو ضَعْفَ قُوَّتِي وَقِلَّةَ حِيلَتِي وَهَوَانِي عَلَى النَّاسِ، يا أَرْحَمَ الرَّاحِمِينَ، أَنْتَ رَبُّ الْمُسْتَضْعَفِينَ وَأَنْتَ رَبِّي، إِلَى مَنْ تَكِلُنِي، إِلَى بِعِيدٍ يَتَجَهَّمُنِي، أَوْ إِلَى عَدُوٍّ مَلَّكْتَهُ أَمْرِي، إِنْ لَمْ يَكُنْ بِكَ عَلَيَّ غَضَبٌ فَلَا أُبَالِي، وَلَكِنَّ عَافِيَتَكَ هِيَ أَوْسَعُ لِي، أَعُوذُ بِنُورِ وَجْهِكَ الْكَرِيمِ الَّذِي أَشْرَقَتْ لَهُ الظُّلُمَاتُ، وَصَلَحَ عَلَيْهِ أَمْرُ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ مِنْ أَنْ يَنْزِلَ بِي غَضَبُكَ أَوْ يَحِلَّ عَلَيَّ سَخَطُكَ، لَكَ الْعُتْبَى حَتَّى تَرْضَى وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِكَ»، “Ewe Mwenyezi Mungu! Nakushtakia udhaifu wa nguvu zangu na uchache wa rasilimali zangu, na kudhalilishwa na watu. Ewe mwingi wa Rehema mwenye kurehemu. Wewe ni Mola wa walio madhaifu na ni Mola wangu. Kwa nani unanikabidhisha? Kwa mtu wa mbali anayenipokea kwa uadui? Au kwa adui uliyemmilikisha mambo yangu? Kama hujanighadhibikia basi mimi sijali. Lakini afwa yako ndio kitulizo kikubwa kwangu. Ninajikinga kwa Nuru ya Uso wako mkarimu ambao unang'arisha viza vyote, na yanatengenea mambo ya dunia na akhera, kutokana na kuteremsha kwangu ghadhabu zako au hasira zako. Ninahitaji radhi na ridhaa zako hadi uniridhie. Hakuna hila wala nguvu ila kwako.” 

Dua inayoweka wazi ukubwa wa hatua ya kipindi cha Makkah katika mapambano ya kifikra na kisiasa, hivyo faraja ikaja miaka michache baadaye wakati Mtume (saw) alipokutana na Aws na Khazraj mjini Makkah, ambapo alitawalishwa baada ya miaka mitatu tu ikiwa nukta ya kumakinika ni Madinah; dola ya mpendwa wetu Al-Mustafa (saw).

Ndugu yetu Naveed Butt amekuwa ni mfano wa alama ya ushujaa ya kufuatwa, katika dhana ya kazi ya jumuiya ya kifikra ambayo imejifunga katika njia yake, hivyo Ummah unaelewa kuwa kuna wanaume wasiobadilisha misimamo yao na kufungwa katika Ummah wa Kiislamu ukubwa wa kushikamana na hukmu za Sharia. Mwenyezi Mungu (swt) amesema katika Sura Al-Ahzab aya 23:

[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُواْ مَا عَاهَدُواْ اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu waliotimiza waliyoahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab:23]

Mamlaka ya Pakistan imetekeleza uovu huu mkubwa dhidi ya mhandisi Naveed Butt, na kuonyesha duara la uovu katika kuzuia ubebaji wa Da’wah, na kuhakikishwa kwa kitendo hiki ushawishi mkubwa wa Hizb ut-Tahrir nchini Pakistan na Afghanistan. Serikali ya Pakistan haifanyi kazi kwa manufaa ya watu wa Pakistan, vivyo hivyo haitambui upeo wa fikra ambayo Hizb ut Tahrir inao. Kuwekwa ndani kwa Naveed Butt kumejenga rai kuwa serikali ni ndumila kuwili, na kile ilichokifanya kitaigeukia na kuwa ni balaa kwake na kuwa ni mpinzani asiye na mkopo. Na kimaumbile ni kuwa iwe upande wa Uislamu na sio adui kwa wale wanaokwenda kwa ajili ya Ummah kwenye umoja wake, juu ya msingi wa Dini yake, Dola ya Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume.

Ni jambo la kushtua kuwa Serikali ya Pakistan imemuweka ndani Ndugu yetu Naveed Butt kwa miaka kumi, huku ikiwaona Waislamu wa Kashmir kwa miongo saba wakikumbana na kitisho katika maisha na mabadiliko ya kimfumo ya kidemografia, kupitia hatua za kisheria na kijeshi za India kwa kuiunganisha Kashmir kwa nguvu.

Ni jambo la kushtua kuwa Serikali ya Pakistan imemfunga Ndugu yetu Naveed Butt kwa miaka kumi, na kuna ripoti za kiutafiti zilizofanywa na mashirika ya kimataifa zinazoeleza kuwa asilimia ya watu masikini nchini Pakistan imefikia 40%, na kuwa eneo la Balochistan lipo juu zaidi kwa umasikini pamoja na maeneo ya makabila!

Ripoti zimeeleza kuwa Wapakistan 191 wanajiua ndani ya mwaka kukwepa umasikini, mateso, na hali ngumu ya maisha, na kuwa umasikini unawasukuma masikini wengi nchini Pakistan kuuza figo zao, kwa lengo la kuondokana na madeni yanayowagubika. Wakati hospitali za kibinafsi zinazofanya operesheni za upandikizaji zinatoza dolari alfu 15 kwa uwekaji wa kila figo moja, anayeuza figo lake anapokea dolari alfu moja tu! Ripoti zinaeleza kuwa adesi ni zao la kimkakati nchini Pakistan, linajumuisha mlo wa watu masikini zaidi walio chini ya mstari wa umasikini, wanaofikia kiasi milioni 70 nchini Pakistan. (Al Jazeera Net).

Ni ajabu, kunapatikana hali hii huku serikali ya Pakistan ikimfunga Ndugu yetu Naveed Butt, ambaye ameelezea wazi ukweli na kufichua huduma mbovu na kujidhalilisha kwa Pakistan kwa Amerika, na mateso kwa kila anayetangaza ukweli huu!

Haki ya kisharia ya Mwenyezi Mungu (swt) itabakia, na Mwenyezi Mungu (swt) atalipa kisasi kwa wale madhalimu wanaoendelea katika udhalimu wao kwa waja, haswa wale walio mbele katika ngazi za kufichua njama zao na usaliti kwa Ummah wa Kiislamu, na kuchukua nafasi ambayo Mwenyezi Mungu (swt) anairidhia. Ni jambo moja tu la kusemwa kwenu: muacheni huru ndugu yetu, mhandisi Naveed Butt, mara moja. Wale wanaotenda uovu huu dhidi ya Ndugu Naveed Butt, watawajibishwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt), kwa kusimamishwa Dola ya Khilafah karibuni, ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt), ambaye havunji miadi Yake.

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Sheikh Muhammad As-Sammani – Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu