Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vipi Khilafah Itakavyo Linda Heshima ya Wanawake

• Uislamu umeipa hadhi kuu heshima kwa wanawake. Dalili kadha wa kadha za Kiislamu zinawawajibisha wanaume na mujtama kuwatazama na kuamiliana na wanawake kwa heshima na daima kulinda hadhi yao.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَرِثُواْ النِّسَاء كَرْهًا وَلاَ تَعْضُلُوهُنَّ لِتَذْهَبُواْ بِبَعْضِ مَا آتَيْتُمُوهُنَّ إِلاَّ أَن يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ فَإِن كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَى أَن تَكْرَهُواْ شَيْئًا وَيَجْعَلَ اللّهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا﴿

“Enyi mlio amini! Si halali kwenu kuwarithi wanawake kwa nguvu. Wala msiwadhikishe ili mwapokonye baadhi ya mlivyo wapa isipokuwa wakifanya uchafu ulio wazi. Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake.” [An-Nisa: 19]

Mtume (saw) amesema: «إِنَّمَا النِّسَاءُ شَقَائِقُ الرِّجَالِ، مَا أَكْرَمَهُنَّ إِلَّا كَرِيمٌ وَمَا أَهَانَهُنَّ إِلَّا لَئِيمٌ» “Hakika wanawake ni ndugu wa baba na mama kwa wanaume. Hakuna awakirimuye isipokuwa mkarimu na hakuna awafedheheshaye isipokuwa muovu.” [Abu Dawood]

Mtume (saw) amesema: «اسْتَوْصُوا بِالنِّسَاءِ خَيْرًا» “Watendeeni wema wanawake.” [Bukhari na Muslim]

• Hivyo basi, Khilafah itaweka hifadhi ya hadhi na usalama wa wanawake kama nguzo kuu ya sera ya dola. “Mwanamke ni heshima (‘ird) ambayo ni lazima ihifadhiwe.” (Kifungu cha 112, Kielelezo cha Katiba ya Al-Khilafah cha Hizb ut Tahrir)

• Dola itahamasisha uchamungu (Taqwa) ndani ya mujtama unaokuza aqliya ya kujihisabu na uwajibikaji katika namna wanaume wanavyo watazama na kuamiliana na wanawake.

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَلْتَنظُرْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ لِغَدٍ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ] “Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kila nafsi iangalie inayo yatanguliza kwa ajili ya Kesho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari ya mnayo yatenda.” [Al-Hashr: 18]

• Khilafah itatumia nidhamu zake za kisiasa, kielimu na vyombo vya habari pamoja na njia nyinginezo zilizo mikononi mwake ili kuimarisha mtazamo wa heshima kwa wanawake.

• Uislamu umeharamisha ghasia za aina yoyote dhidi ya wanawake – iwe nyumbani au barabarani. Mtume (saw) amesema: «لاَ تَضْرِبُوا إِمَاءَ اللَّهِ» “Msiwapige watumwa wa kike wa Mwenyezi Mungu.” [Ibn Majah]

• Kuupa sura ya ngono mujtama pamoja na aina zote za kuwafanya kuwa vyombo, kuwanyanyasa na kuwadunisha wanawake zitaharamishwa chini ya Khilafah. Dola pia inawaharamisha wanawake kujiingiza katika kazi au huduma yoyote inayoutumia urembo au mwili wake na kumshusha hadhi yake.«وَنَهَانَا عَنْ كَسْبِ الأَمَةِ إِلاَّ مَا عَمِلَتْ بِيَدِهَا وَقَالَ هَكَذَا بِأَصَابِعِهِ نَحْوَ الْخَـبْزِ وَالْغَزْلِ وَالنَّـفْشِ» Rafi bin Rifaa (ra) asimulia, “(Mtume (saw) ametukataza juu ya chumo kutokana na mtumwa wa kike isipokuwa kwa yale aliyo yachuma kwa mkono wake na akasema ‘hivi’ kwa kuashiria kwa vidole vyake, mithili ya kuoka mkate, kushona, na kuchonga.” [Abu Dawud]
“Wanaume na wanawake hawapaswi kufanya kazi yoyote inayo hatarisha maadili au kusababisha ufisadi katika mujtama.” (Kifungu cha 119, Kielelezo cha Katiba ya Al-Khilafah cha Hizb ut Tahrir)


• Nidhamu kamilifu ya kijamii ya Kiislamu imeorodhesha hifadhi ya hadhi ya wanawake kuwa kitovu cha sheria zake na inacheza dori kuu katika kusimamisha heshima kwa wanawake kama msingi mkuu wa mujtama. Sheria hizi za kijamii za Kiislamu hudhibiti maingiliano kati ya wanaume na wanawake, ikiyaelekeza mahusiano ya kijinsia katika ndoa pekee.


“Utenganishaji baina ya jinsia ni wajib, hawapaswi kukutana isipokuwa kwa hitajio ambalo sheria inaliruhusu au kwa lengo ambalo sheria inawaruhusu wanaume na wanawake kukutana kwalo, kama vile biashara au Hajj.” (Kifungu cha 113, Kielelezo cha Katiba ya Al-Khilafah)


“Wanawake wameharamishwa kuwa faragha (khulwah) na wanaume wowote ambao si mahram zao, vile vile wameharamishwa kuonyesha mapambo yao au kufichua miili yao mbele ya wanaume wa kando.” (Kifungu cha 118, Kielelezo cha Katiba ya Al-Khilafah cha Hizb ut Tahrir)


• Nidhamu ya kijamii ya Kiislamu inatoa muundo ambao kwao hulinda kivitendo hadhi ya wanawake: Kwanza, kupitia kutekeleza upya msingi kuwa wanawake sio vyombo vya kuanikwa hadharani ili wanaume kujistarehesha, bali pia kuhifadhi mahusiano safi kati ya jinsia mbili yanayo hakikisha maingiliano yao hayarahisishwi au kuzuiwa kupitia ubabaishaji wa kingono. Hili huasisi ushirikiano wenye matunda, na manufaa kati ya wanaume na wanawake katika nyanja zote za maisha. Na pili, kupitia kuunda mazingira safi na ya kujiepusha na ufuska ambayo matamanio ya kingono hushibishwa kwa namna inayoleta wema katika mujtama badala ya madhara. Yote haya husaidia kudumisha mazingira ya heshima adhimu kwa wanawake, yakipunguza ghasia na uhalifu mwengineo dhidi yao. Natija yake itakuwa kuunda mujtama chini ya Khilafah ambao wanawake wataweza kusoma, kufanya kazi, na kusafiri katika mazingira salama.


• Kupitia nidhamu yake ya kielimu na kimahakama, Khilafah itafanya bidii kuondoa taasubi za kimila zinazowadunisha wanawake au kuwapokonya haki zao za Kiislamu, pamoja na kuondoa tabia dhalimu za kitamaduni kama vile ndoa za lazima na mauwaji ya heshima. Pia itaharamisha kuingia kwa fikra, picha, vitabu, majarida, au mziki wowote ndani ya mujtama wake yanayo dunisha hadhi ya wanawake. 


• Khilafah itatabikisha adhabu kali za Uislamu kwa aina yoyote ya unyanyasaji dhidi ya wanawake ikiwemo ghasia na ubakaji. Kanuni hizi dhidi ya uhalifu ikiwemo upigaji bakora kwa ajili ya uzushi au upigaji mawe hadi kifo kwa ajili ya uhalifu mwengineo dhidi ya hadhi yao. Dola inawajibishwa kuwa na nidhamu barabara ya kimahakama ili kukabiliana haraka na uhalifu kiasi ya kuwa wanawake wataweza kutafuta haki mara moja na kwa wepesi kwa ukiukaji wowote wa heshima au haki zao.   

 [وَالَّذِينَ يَرْمُونَ الْمُحْصَنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَأْتُوا بِأَرْبَعَةِ شُهَدَاء فَاجْلِدُوهُمْ ثَمَانِينَ جَلْدَةً] “Na wanao wasingizia wanawake mahashumu, kisha wasilete mashahidi wanne, basi watandikeni bakora themanini.” [An-Nur 24:4]

عَنْ عَلْقَمَةَ بْنِ وَائِلٍ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّ امْرَأَةً، خَرَجَتْ عَلَى عَهْدِ النَّبِيِّ e تُرِيدُ الصَّلاَةَ فَتَلَقَّاهَا رَجُلٌ فَتَجَلَّلَهَا فَقَضَى حَاجَتَهُ مِنْهَا فَصَاحَتْ وَانْطَلَقَ فَمَرَّ عَلَيْهَا رَجُلٌ فَقَالَتْ إِنَّ ذَاكَ فَعَلَ بِي كَذَا وَكَذَا وَمَرَّتْ عِصَابَةٌ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ فَقَالَتْ إِنَّ ذَلِكَ الرَّجُلَ فَعَلَ بِي كَذَا وَكَذَا ‏.‏ فَانْطَلَقُوا فَأَخَذُوا الرَّجُلَ الَّذِي ظَنَّتْ أَنَّهُ وَقَعَ عَلَيْهَا فَأَتَوْهَا بِهِ فَقَالَتْ نَعَمْ هُوَ هَذَا ‏.‏ فَأَتَوْا بِهِ النَّبِيَّ e فَلَمَّا أَمَرَ بِهِ قَامَ صَاحِبُهَا الَّذِي وَقَعَ عَلَيْهَا فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَنَا صَاحِبُهَا ‏.‏ فَقَالَ ‏«اذْهَبِي فَقَدْ غَفَرَ اللَّهُ لَكِ‏»‏.‏ «وَقَالَ لِلرَّجُلِ قَوْلاً حَسَنًا»‏.‏ قَالَ أَبُو دَاوُدَ (يَعْنِي الرَّجُلَ الْمَأْخُوذَ)، وَقَالَ لِلرَّجُلِ الَّذِي وَقَعَ عَلَيْهَا ‏«ا‏رْجُمُوهُ» (رواه ابو داود)‏

Pindi mwanamke mmoja alipotoka katika zama za Mtume (saw) akitaka kuswali, akakutana na mwanamume mmoja akamshambulia na kumzidi nguvu kisha akakidhi haja yake kwake (akambaka). Akapiga mayowe na mwanamume huyo akaondoka, akatokewa na mwanamume mwengine akamwambia: mtu yule amenifanyia kadha na kadha. Kikatokea kikundi cha muhajirina akawaambia: mwanamume yule amenifanyia kadha na kadha. Wakaenda na kumkamata mwanamume yule ambaye walidhani kwamba ndiye aliyembaka na kumleta kwake. Naye akasema: ndio, huyu ndiye. Kisha wakaja naye kwa Mtume (saw). Na pindi alipotoa amri juu yake akasimama yule mwanamume (halisi) aliyembaka akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi ndiye niliyemtendea hilo. Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia (mwanamke huyo): “Nenda zako, hakika Mwenyezi Mungu amekusamehe”. “Na akamwambia mwanamume huyo maneno mazuri” (Abu Dawud amesema: akimaanisha mwanamume aliyekamatwa kimakosa), na yule mwanamume halisi aliyembaka mwanamke huyo, alisema: “Mpigeni mawe hadi afe”. [Abu Dawud]


Wakati wa Khilafah ya Umar bin Al Khattab (ra), mwanamke mmoja alimtuhumu mwanawe Abu Shahmah kuwa alimbaka. Umar (ra) akamuuliza mwanawe kuhusu uhalifu huo, aliyekiri kutekeleza kitendo hicho. Aliadhibiwa vikali hapo kwa hapo huku mwanamke huyo hakuekewa kosa lolote kwa uhalifu huo.


• Jukumu lililowekwa na Uislamu juu ya wanaume la kuwa wasimamizi wa wake zao na watoto wao huwawajibisha kuwahifadhi na kuwalinda kutokana na madhara. Kuliko tu kuwa na wadhifa wa kuwatawala na kuwaamuru pekee, jukumu hili kubwa la usimamizi (qiwaamah) ni lile la uchungaji wa wake na ndugu wa kike. Hili pia hupunguza ghasia dhidi ya wanawake. ﴿الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاء﴾ “Wanaume ni wasimamizi wa wanawake.” [An-Nisa: 34]


• Uislamu umefafanua haki za mke juu ya mumewe na kunasibisha hadhi ya wanaume katika maisha haya ya duniani na akhera kwa kuwatendea wema wake zao na binti zao. Sheria na kanuni zote hizi hupunguza ukatili na unyanyasaji wa wanawake. ﴿وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ﴾“Na kaeni nao kwa wema.” [An-Nisa: 19]

Mtume (saw) amesema, «أَكْمَلُ الْمُؤْمِنِينَ إِيمَانًا أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا وَخِيَارُكُمْ خِيَارُكُمْ لِنِسَائِهِمْ» “Muumini aliyekamilika imani yake ni yule aliye na tabia njema na wabora wenu ni wale walio wabora kwa wake zao.” [Tirmidhi]


Rekodi za mahakama kutoka kwa Khilafah Uthmaniyya zaonyesha kuwa waume walio wanyanyasa wake zao waliadhibiwa na dola hiyo, ikiwemo kufungwa jela wakati mwengine. Mahakimu aghlabu walimfanya mume kukubali sharti kuwa endapo atamnyanyasa tena mke wake, basi atatalikishwa pasi na mke kusalimisha haki zake za ndoa za kifedha.

“Maisha ya ndoa ni yale ya utulivu na usuhuba. Jukumu la mume juu ya mkewe (qiwaamah) ni lile la uchungaji, na sio la utawala …” (Kifungu cha 120, Kielelezo cha Katiba ya Al-Khilafah cha Hizb ut Tahrir)


• Khilafah itachukua hatua pana za kuhifadhi hadhi ya wanawake wake, ikiwemo hata kuandaa majeshi yake dhidi ya majeshi ya kigeni yanayo chafua au hata kuhatarisha kuchafua heshima yao, kwani hiki ndicho kiwango cha juu cha hifadhi ambayo utawala wa Kiislamu unaimudu kwa wanawake wa dola yake.  

Katika karne ya 9 chini ya Khilafah Abbasiyya, wakati wa utawala wa Khalifah al-Mu’tassim Billah, mwanamke mmoja wa Kiislamu alitekwa nyara na kunyanyaswa na mwanajeshi wa Kirumi nchini Syria. Katika kujibu hujuma hii, Khalifah huyu alipeleka jeshi lenye nguvu hadi mji wa Amuriyyah nchini Uturuki, ngome imara ya Warumi ili kumuokoa mwanamke huyo. Hii ni licha ya makao makuu ya Khilafah kuwa mjini Baghdad wakati huo. Inaashiria umakini ambao Khilafah ilitilia maanani hifadhi ya hadhi ya wanawake wake.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 26 Aprili 2020 10:48

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu