Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vipi Khilafah Itazuia Dhuluma za Kisiasa?
(Imetafsiriwa)

Demokrasia, uhuru wa rai na haki ya kumchagua na kumhisabu mtawala, ni miito inayo pigiwa debe chini ya serikali za kibinadamu zilizoko leo duniani, lakini, urongo wa miito hii hudhihirika pindi mtu binafsi au kikundi cha watu kinapozikashifu serikali hizi na ufisadi wao, au kinapodai haki ambayo wameipoteza au majukumu ambayo serikali hizi zimefeli kutimiza kwa watu wake. Magereza ya Urusi, mrithi wa Muungano wa Kisovieti, inayo sherehekea siku ya wahanga wa mateso ya kisiasa mnamo 3/10 kila mwaka, wakikumbuka mgomo wa njaa uliofanyika mnamo 30/10/1974 M na ulioanzishwa na wafungwa katika kambi za Mardovia na Perm, ambako wafungwa wa kisiasa walitangaza mgomo wa njaa wakilalamika dhidi ya mateso ya kisiasa yaliyotekelezwa na Muungano wa Kisovieti, magereza haya ni shahidi kwa hili, na magereza ya serikali za kihalifu katika ulimwengu wa Kiislamu, na wauwaji wake nchini Misri, Syria, Libya, Uzbekistan na biladi nyenginezo za Waislamu pia yanathibitisha hili.

Na kwa sababu Khilafah ni ndhamu kutoka kwa Mwenye hekima aliye Mjuzi wa kila kitu, na kwa sababu ndio suluhisho sahihi na sio tu badala kwa serikali hizi za kibinadamu, tutawasilisha katika makala haya mistari mipana inayozuia ukandamizaji na mateso ya kisiasa ambayo tunayashuhudia leo:

1- Dola ya Khilafah sio dola ya kiaskari inayokazanisha mshiko wake juu ya watu na kuwachunguza mienendeo yao, na kuweka kamera ili kuwachunguza sehemu za hadharani na wakati mwengine hata katika sehemu za faragha. Au kufuatilia simu zao au akaunti zao katika mitandao ya kielektroniki, kuwakamata na kuwatesa kwa sababu ya nukuu za tweet au chapisho katika tovuti hizi, au kuwaficha nyuma ya jua “kwa sababu ya mafungamano yao ya kisiasa” kama zifanyavyo serikali hizi katika ulimwengu wa Kiislamu leo. Uislamu umeharamisha kuwachunguza Waislamu kwa nasi ya Aya (وَلَا تَجَسَّسُوا) “Na wala musichunguze” [Al-Hujurat: 12]. Huu ni uharamu jumla wa kuchunguza na ni sharti uendelee kama wa jumla isipokuwa kuwe na dalili maalum. Hii imethibitishwa kupitia riwaya iliyo ripotiwa na Ahmad na Abu Dawud kwa silsila kutoka kwa Al-Miqdad na Abu Umamah pindi waliposema:

«إِنَّ الأَمِيرَ إِذَا ابْتَغَى الرِّيبَةَ مِنَ النَّاسِ أَفْسَدَهُمْ»

“Wakati mtawala anapotaka kuweka uchunguzi dhidi ya watu, basi huwafisidi.”

Hivyo basi, kuwachunguza Waislamu imeharamishwa. Hukumu hii pia inawahusu watu wa Dhimmah miongoni mwa raia wa Dola hii. Hivyo basi, uchunguzaji wa raia ni haramu, Waislamu na wasiokuwa Waislamu.

Uislamu pia ulimharamisha mtawala kuwatesa na kuwadhuru watu. Muslim amesimulia katika Sahih yake kutoka kwa Hisham ibn Hakim ibn Hizam, Amesema: Nimemsikia Mtume (saw), akisema:

«إِنَّ اللهَ يُعَذِّبُ الَّذِينَ يُعَذِّبُونَ النَّاسَ فِي الدُّنْيَا»

“Hakika Mwenyezi Mungu atawaadhibu wale ambao wanawaadhibu watu katika hii dunia”.

Mtume (saw) pia amesema:

«نْفَرَانِ مِنْ أَهْلِ النَّارِ لَمْ أَرَهُمَا، قَوْمٌ مَعَهُمْ سِياطٌ كَأَذْنَابِ الْبَقَرِ يَضْرِبُونَ بِهَا النَّاسَ...»

“Watu aina mbili ni katika watu wa Motoni ambao sijapata kuwaona: watu walio na mijeledi mithili ya mikia ya ng’ombe, wanawapiga kwayo watu ...” (Imesimuliwa na Muslim). Uislamu pia umeharamisha kushambulia matukufu ya Waislamu, heshima zao, na mali zao na kukiuka faragha ya nyumba zao, Mtume (saw) amesema:

«كُلُّ الْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ حَرَامٌ دَمُهُ وَمَالُهُ وَعِرْضُهُ»

“Imeharamishwa kwa Muislamu kumkiuka Muislamu katika damu yake, mali yake, na heshima yake”.

2- Chini ya Khilafah, watu wana haki ya kuzungumza na kutoa rai zao, na kuwahisabu watawala na kuwabadilisha endapo watawanyima raia haki, kushindwa kutimiza majukumu kwao, kupuuza mambo yao, kukiuka hukmu za Kiislamu au kuhukumu kwa hukmu zisizoteremshwa na Mwenyezi Mungu. Watu wana haki ya kufanya hivyo ima kibinafsi binafsi au kwa ujumla wao kupitia Baraza la Ummah au vyama vilivyoko ndani ya Dola. Mwenyezi Mungu (swt) amefanya kuamrisha mema (Ma’ruf) na kukataza maovu (Munkar) ni wajib juu ya Waislamu, Yeye (swt) amesema: 

  (الَّذِينَ إِن مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنكَرِ)

“Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Swala na wakatoa Zakah, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya.” [Al-Hajj: 41].

Na ziko Hadith zinazotaja kumhisabu mtawala haswa. Muslim amesimulia katika Sahih yake kutoka kwa Umm Salamah (ra) kuwa Mtume (saw) amesema:

«سَتَكُونُ أُمَرَاءُ فَتَعْرِفُونَ وَتُنْكِرُونَ، فَمَنْ عَرَفَ بَرِئَ، وَمَنْ أَنْكَرَ سَلِمَ، وَلَكِنْ مَنْ رَضِيَ وَتَابَعَ» قَالُوا: أَفَلا نُقَاتِلُهُمْ؟ قَالَ: «لا، مَا صَلَّوْا»

“Na kutakuweko na viongozi na mutawajua (matendo yao) na mutawachukia, basi mwenye kujua (matendo yao na kujaribu kuwazuia), ataepushwa mbali, na mwenye kuchukia atasalimika, lakini mwenye kuridhia na kufuata ameangamia”. Wakauliza: ‘Je, tuwapige vita?’ Akasema: “Hapana, maadamu wanaswali” na swala hapa ni majazi ya kuhukumu kwa Uislamu.

Mtume (saw), amesisitiza kuwapiga vita watawala madhalimu, licha ya madhara ambayo yatatokea katika kufanya hivyo, hata kama itapelekea mauwaji, ambapo yeye (saw) amesema:

«سَـِّيدُ الشُّهَدَاءِ حَمْزَةُ بْنُ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ وَرَجُلٌ قَامَ إِلَى إِمَامٍ جَائِرٍ فَأَمَرَهُ وَنَهَاهُ فَقَتَلَهُ»

“Bwana wa Mashahidi ni Hamza bin Abdul Muttwalib, na mtu atakaye simama mbele ya kiongozi jeuri akamwamrisha na kumkataza kisha (mtawala huyo) akamuua.”

Haya ni miongoni mwa maneno faswaha katika kubainisha Haki na kuvumilia madhara hadi kifo ili kuwahisabu watawala na kupambana dhidi ya watawala madhalimu.

Kuna dalili nyingi katika historia ya Waislamu kuhusu Waislamu kuwahisabu watawala na kuitisha haki zao pasi na kunyimwa na yeyote. Walimuhisabu Omar ibn al-Khattab, alipokuwa juu ya minbar, juu ya ugawanyaji wa nguo za Kiyemeni. Vile vile, Bilal na Az-Zubayr miongoni mwa wengineo, walipinga na kuzozana naye kwa sababu hakuigawanya ardhi ya Sawad nchini Iraq baada ya kufunguliwa kwake; alijadiliana na kuwashauri maswahaba hadi alipowakinaisha rai yake. Vile vile Ali (ra) alikataa rai ya Uthman (ra), aliyekuwa Kamanda wa waumini, ya kukamilisha Hajj na Umrah.

3- Chini ya Khilafah, Baraza la Ummah litakuwa linawawakilisha watu kikweli na madukuduku yao na sio kwa njia ya kuwahadaa. Litawawakilisha katika kutoa rai kwa niaba yao, likitoa malalamishi yao, na kumhisabu Khalifah na wale walio mamlakani. Waislamu na wasiokuwa Waislamu, wanaume na wanawake, wana haki ya kuwa wanachama wa Baraza hili, ambapo Kifungu cha 107 cha Katiba Kielelezo iliyo tayarishwa na Hizb ut Tahrir kinasema: 

 “Kila raia ambaye ni mtu mzima na mwenye akili timamu, ana haki ya kuwa mwanachama wa Baraza la Ummah au Baraza la Wilaya, awe mwanamume, mwanamke, Muislamu au asiyekuwa Muislamu; mwanachama asiyekuwa Muislamu amefungika na kutoa malalamishi kuhusiana na dhuluma ya watawala au utabikishaji mbaya wa hukumu za Kiislamu.”

4- Chini ya Khilafah, idara ya mahakama haitakuwa ni chombo cha dhuluma na kukandamiza watu, kuwazuia kutokana na kutekeleza haki yao ya kimaumbile ya kuhisabu na kutoa rai, kuwazulia mashtaka ya urongo dhidi yao kwa sababu ya mafungamano yao ya kisiasa na kutoa hukumu za kidhuluma dhidi yao, kama ilivyotokea katika mauwaji ya kinyama ya vijana tisa kutoka Misri mnamo Jumatano asubuhi, 20 Februari 2019, kwa msingi wa kuungama kwao kutokana na kuteswa kwa stima. Badala yake, mahakama zitakuwa ni mwenge wa haki, uadilifu na kuregesha haki kwa wenyewe. Mtawala hatakuwa na kinga wala mfanyikazi yeyote ndani ya dola. Kutakuweko na mahakama maalum ya kusikiza kesi dhidi ya Khalifah au watu walio mamlakani, kwa jina, Mahakama ya Madhalim. Ambapo, Mahakama ya Madhalim inajukumu la “kutoa hukumu ya kisheria kwa njia ya kulazimisha kuhusiana na mzozo wowote utakao kuwepo kati ya raia na Khalifah au yeyote katika Magavana wake au wafanyikazi, au tofauti yoyote iliyoko kati ya Waislamu kuhusu tafsiri ya nasi yote ya kisheria kutumika ili kuhukumu kwazo na kutawala kwa mujibu wake.” (Taasisi za Dola ndani ya Khilafah katika Utawala na Idara). 

Katika historia ya Waislamu, Khalifah wa Waislamu aliketi pamoja na mmoja wa raia wake mbele ya mahakama na kadhi akatoa hukumu upande wa mpinzani na kumshutumu Khalifah. Kisa cha Omar bin al-Khattab pamoja na mtu aliyetaka kununua farasi kutoka kwake ni maarufu mno, kama kilivyo kisa cha kadhi aliyetoa hukumu yake akimtaka Omar bin Abdul Aziz kuliondoa jeshi lake kutoka katika ardhi waliyoifungua kwa sababu hawakuwalingania watu wake katika Uislamu kabla ya kupeleka majeshi hayo, na visa vyenginevyo ambavyo vyaweza kuregelewa.

5- Chini ya Khilafah, kuasisi vyama vya kisiasa ndani ya Dola hii si haramu, maadamu vitasimama kwa msingi wa Uislamu, na kuasisi vyama kama hivyo hakuhitaji idhini ya Dola. Kifungu cha 21 cha Katiba Kielelezo iliyo tayarishwa na Hizb ut Tahrir kinaeleza: “Waislamu wana haki ya kuasisi vyama vya kisiasa ili kuwahisabu watawala au kufikia utawala kupitia Ummah kwa sharti kuwa msingi wake uwe ni Itikadi ya Kiislamu na kwamba hukumu vinavyo tabanni ziwe ni hukumu za Kisheria. Uundaji wa chama hauhitaji ruhusa yoyote. Kikundi chochote kitakachoundwa kwa msingi wa ukafiri ni haramu.” Dalili yake ni maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):

 (وَلْتَكُنْ مِنْكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ)

“Na kuwepo miongoni mwenu kikundi chenye kulingania kheri, na kuamrisha mema na kukataza maovu na hao ndio waliofaulu” [Al-i-Imaran:104].

Mtazamo wa kuitumia ayah hii kama dalili ya kuasisi vyama vya kisiasa ni kuwa Mwenyezi Mungu (swt) amewaamrisha Waislamu kuwa na kikundi kinachobeba Da’wah ya Uislamu miongoni mwao, na vile vile kuamrisha Ma’ruf na kukataza Munkar.

6- Chini ya Khilafah ubwana uko kwa Shariah na utawala uko kwa Ummah. Ummah humchagua mtawala wake na kumpa ahadi ya utiifu juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah ya Mtume (saw) ili kutabikisha Shariah. Mtawala huyo halazimishwi juu yao kutabikisha matakwa ya mabwana zake, kama ilivyo hali leo katika biladi za Waislamu. Dola ya Khilafah ina uwezo wa kisiasa wa kihakika, na hutekeleza siasa kwa sura yake halisi; kuchunga mambo ya watu, na sio kuwatawala juu ya shingo zao na kuwagandamiza na kuwadhulumu. Na chini ya Khilafah, mtawala na raia hufuata hukumu za Shariah na utiifu wa raia kwa mtawala ni sharti juu ya kushikamana kwake na hukumu za Shariah:  

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلاً]

“Enyi mulio amini, mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume na walio na mamlaka miongoni mwenu. Na mutakapozozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa kweli muna muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora na ndiyo yenye mwisho mwema.” [An-Nisa: 59]

Kwa kutamatisha, nitarudi kwa lile nililo anza nalo, kutaja tena kuwa Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume ndio suluhisho sahihi kwa matatizo ya Ummah huu, bali, kwa wanadamu wote. Ni nidhamu ya kipekee kutoka kwa Mwenye hekima aliye Mjuzi wa vitu vyote. Je, haijatosha miaka 98 ya dhuluma, unyanyasaji na mateso bila ya Khilafah?! Je, hatupaswi kuimarisha kujitolea kwetu na kuharakisha kuisimamisha?!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bara’ah Manasrah

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 26 Aprili 2020 11:00

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu