Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Maisha na Heshima ya Waislamu Waume na Wake Yatakuwa Salama tu Chini ya Khilafah

(Imetafsiriwa)

Shireen Mazari karibuni aliandika nukuu ya tweet kuhusiana na mauwaji ya kinyama ya msichana anayeitwa Noor Mukaddam ambayo yameogofya nchi nzima. Aliandika tweet “Mauwaji ya kinyama ya mwanamke mchanga, Noor, jijini Islamabad ni ukumbusho mwengine wa kuogofya ambapo wanawake wamekuwa na wanaendelea kufanyiwa ukatili na kuuliwa bila khofu ya kujali sheria. Haya lazima yamalizike. Tunawajibika kuhakikisha kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria na wahalifu wenye ushawishi na nguvu hawawezi “kukwepa” kirahisi rahisi. (Chanzo)

Waziri wa Haki za Binaadamu wa Pakistan Shireen Mazari, ni mmoja wa watu wengi waliotoa maoni juu ya mauwaji yaliotekelezwa karibuni ya Noor Mukaddam, aliyewekwa mateka kwa siku mbili na baadaye kuuliwa kikatili na kukatwa kichwa na rafiki yake, wakati marafiki zao, na walinzi wa nyumba wakiwa wamekusanyika getini. Suala lililohitajika hatua ya kuwaita Polisi lilicheleweshwa na wazazi wake walio na ushawishi waliamua namna ya kuendelea. Tukio hili linaonyesha mgawanyiko wa kitabaka wa jamii ya Pakistan, na namna watu wenye fedha na nguvu wasivyoguswa. Matukio ya vurugu kawaida huja kuonekana wakati muda wa kutoa msaada umeshapita. Je watu wanapenda kuteseka kimya kimya? Hapana. Matukio hayaripotiwi, kwa sababu hawana matumaini ya kupata haki, na kwa kuepuka udhalilifu huamua kuyawacha mambo mikononi mwao, hadi ima maisha yao yaliojaa unyanyasaji yamalizike kimaumbile au yamalizwe na mtu mwengine wa karibu.

[اَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ اَحْسَنُ مِنَ اللّٰهِ حُكْماً لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ]

“Je, wao wanataka hukumu za kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” [Al-Maidah: 50]

Waingereza wameacha nyuma mkusanyiko wa kanuni na sheria ambazo bado zinafuatwa kibubusa. Maongezeo tofauti yametekelezwa kuifanya iwe ya kienyeji zaidi, lakini uharibifu umeendelea, na ndoto ya kuishi chini ya Uislamu nchini Pakistan imechanika. Waislamu wa Bara hili dogo, walio na uchu wa kutawaliwa na Uislamu wamekuwa na ganzi baada ya kudanganywa tena na tena na watu wao wenyewe. Urasilimali kwa kiasi fulani umeingizwa na kutabikishwa juu ya watu na umewafanya kushughulishwa na mapambano yanayoendelea ya kutafuta maisha na kuongezewa na uchumaji wa mali na utawala. Hii imegawa kila kitu kutokea kwenye Elimu, Afya hadi Sheria. Fedha zimekuwa ndio tiketi ya kuelekea njia ya mafanikio na utawala. Elimu na Afya vinanunuliwa. Masikini wanakumbatia ukosefu wa huduma za kimwili na kiakili, na kufikiria kuwa maisha yamekwisha kuwa sio ya haki kwao, kwa hivyo wamenyonga matumaini ya haki, na kisha yote haya kuporwa na tabaka la juu, ambalo limeelimika, linaweza kununua usaidizi wa tiba, lakini likawa bado ni dhalili kwa mamlaka.

Kati ya mamia, hapa kuna kesi chache maarufu “za waliotuhumiwa na bado wapo huru” nchini Pakistan:

1) Mnamo 2010, ndugu wawili waliohifadhi Quran, Mughees na Muneeb Butt, waliuliwa na kundi la watu kwa namna mbaya kabisa, huku Polisi wakiwa wamesimama wanaangalia: mwaka 2018, Mahakama Kuu ilipunguza adhabu ya kifo ya wauwaji kuwa miaka 10 jela.

2) Mnamo 2012, Shahzeb Khan, mwanawe pekee wa kuime wa DSP aliyejaribu kumhifadhi dada yake kutokana na mtu katili, alisakwa kinyama na mhalifu huyu mwenye usemi, na familia yake baadaye ililazimishwa kuchukua diya na kuhamia New Zealand, ambapo baba yake alifariki akikwamilia kumbukumbu za mwanawe

3) Mnamo 2014 katika APS, watoto 150 waliuliwa, na ripoti ya tume ya sheria iliushutumu usimamizi wa Shule kwa uzembe wa hali ya juu. ISPR ilitoa nyimbo mbili kwa ajili yao na wazazi bado wanasubiri kuona wauwaji wakiadhibiwa.

4) Mnamo 2016, msichana Khadija alichomwa na mvulana mara 23 mbele ya Shule, mwanzoni alipigania maisha yake na baadaye kwa ajili ya haki, na mvulana ameachiwa karibuni baada ya kutumikia miaka mitatu na nusu tu.

5) Mnamo 2019, Sallahudin aliyekuwa masikini, taahira aliyejitokeza kwenye kamera za chumba cha ATM, aliteswa na kuonekana kwenye filamu akiwaomba polisi wasimdhuru, baadaye baba yake aliambiwa kuwa alianguka na kufariki.

6) Matukio ya 2020 na 2021 yamepanda kuwa makubwa zaidi, mwanamke alibakwa barabarani, na afisa polisi akatoa maoni kuwa (mwanamke) hakustahiki kuwepo barabarani usiku huo, na karibuni Qurat ul ain aliteswa hadi kufa na mumewe mbele ya watoto wake wadogo wanne. Aliishi katika maisha ya taabu na mateso, na alifariki kwa maumivu, kwa sababu tu kuwa mfumo anaoishi chini yake haukumchukua kama jukumu lake. Ni kwa kuisimamisha Dola ya Khilafah pekee kwa njia ya Utume, ndipo maisha na heshima ya Waislamu itaweza kuhifadhiwa na kuwapatia maisha ambayo khofu pekee itakuwa ni kutomtii Mwenyezi Mungu (swt), “Razzaq”, ambaye ameahidi rizqi kwa kila nafsi.

Wakati wa Hadhrat Umar (ra) Mmisri mmoja alilalamika juu ya mtoto wa Gavana Amr bin Al-Ass ambaye alimpiga. Hadhrat Umar alimtaka Amr bin Al-Ass kuja mwenyewe pamoja na mwanawe. Mmisri huyo alitakiwa kulipiza kisasi na Hadhrat Umar alimwambia Amr: “tokea lini umewaingiza utumwani watu, kwani wamezaliwa kutoka kwa mama zao wakiwa huru”.

Haikuwa vigumu kwa Mmisri masikini kumwendea mkuu wa dola na kutoa taarifa kuwa amekosewa, bila hofu ya kitachotokea. Huu ndio uzuri wa Uislamu.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

انصر أخاك ظالمًا أو مظلومًا” فقال رجل‏:‏ يا رسول الله أنصره إذا كان مظلومًا أرأيت إن كان ظالمًا كيف أنصره‏؟‏”
“قال‏:‏ ‏"‏تحجزه - أو تمنعه - من الظلم فإن ذلك نصره

“Mnusuru ndugu yako, akiwa dhalimu au mwenye kudhulumiwa”. Mtu mmoja akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nitamnusuru ikiwa anadhulumiwa, unaonaje anapokuwa dhalimu vipi nitamnusuru? Akasema (saw), “Mkinge -au Mzuie kutokana na dhulma, kwani huko ndiko kumnusuru kwake”. [Al-Bukhari].

Jamii ya Kiislamu inayotawaliwa na Khalifah anayemuogopa Mwenyezi Mungu (swt), inahakikisha kuwa haki inatendeka kwa watu wote kwenye jamii bila khofu au upendeleo, na huweka mifano mingi ambayo huwa ni matumaini kwa mdhulumiwa, na onyo kwa dhalimu. Unyanyasaji dhidi ya wanawake, ambao ni kielelezo cha dhulma za watawala, utapungua kwa kasi kutokana na khofu ya kuwajibishwa na pia itasaidia kukuuza matendo yao (mema). Wanawake wanaohitajia msaada hawatotelekezwa na watakuwa katika dhima ya dola (kusaidiwa). Uislamu utabadilisha namna ya kufikiri na kuyatathmini mambo. Wanawake hawatotumiwa kama bidhaa, wala wanaume hawatozingatiwa kuwa mashine za ATM. Jinsia zote zitafanya kazi na kuishi maisha ya kumridhisha Mwenyezi Mungu (swt) kwa usawa kwa kufuata maamrisho yake. Hii kwa kiasi kikubwa itapunguza mifadhaiko ya matumaini yasiowezekana ya mfumo wa sasa na italeta amani na utulivu kwa watu na hatimaye kwa Jamii. 

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ikhlaq Jehan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu