Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Khilafah ni Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) Juu ya Ardhi Ilioleta Faraja Kwa Karne Nyingi Kutokana na Udhalimu na Ni Pekee Itakayoleta Tena Inshaallah

Imam Malik ametaja katika Muwatta kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«…سَبْعَةٌ يُظِلُّهُمُ اللَّهُ فِي ظِلِّهِ يَوْمَ لاَ ظِلَّ إِلاَّ ظِلُّهُ إِمَامٌ عَادِلٌ» “Watu aina saba Mwenyezi Mungu atawafunika katika kivuli chake siku ambayo hakutakuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake: Imamu muadilifu …” Imamu muadilifu, mtawala wa Waislamu, ndiye wa mwanzo kutajwa kati ya saba ambao wataburudika katika Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) siku ya Kiama, wakati watu wataemewa kwa joto kali na jasho jingi. Mtume wa mwisho na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (saw) amemuelezea mtawala wa Waislamu anayetawala kwa Uislamu, kuwa ni Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) juu ya ardhi. Mtume (saw) amesema,

«السلطانُ ظِلُّ الله في الأرض» ”Sultan (Mtawala) ni Kivuli cha Mwenyezi Mungu juu ya ardhi.” [Imam Sayuti ameiweka daraja ya hadith sahihi katika Al-Jaam’a as-Saghir, kama alivyoiweka Ibn Taymiyyah katika Majmuu’ al-Fatawa].

Faraja ambayo Mtawala anaileta kwa watu wa ardhini ni kwa ajili ya kujifunga kwake na maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Ni Uislamu pekee ambao unawazuia wenye nguvu dhidi ya walio dhaifu, wengi huwadhulumu wachache au wanaume huwadhulumu wanawake. Mtu wa mwanzo kutawala baada ya Mtume (saw), Khalifah wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), Abu Bakar as-Sidiq (ra), ametamka, وَالضّعِيفُ فِيكُمْ قَوِيّ عِنْدِي حَتّى أُرِيحَ عَلَيْهِ حَقّهُ إنْ شَاءَ اللهُ, وَالقَوِيّ فِيكُمْ ضَعِيفٌ عِنْدِي حَتّى آخُذَ الحَقّ مِنْهُ إنْ شَاءَ اللهُ" “Aliye dhaifu kwenu ni mwenye nguvu kwangu hadi niirejeshe kwake haki yake inshaallah, na aliye na nguvu kwenu ni dhaifu kwangu hadi niichukue haki kutoka kwake inshaallah.”

Hakika, wakaazi wa mbinguni na ardhini wameshuhudia uadilifu mkubwa wa kuhukumu kwa Uislamu katika zama za Uislamu. Utawala wa Kiislamu ulipatwa na msiba, kusita kuliko refuka kwa kuvunjwa kwa Khilafah mwezi Rajab 1342 Hijri, Machi 1924 Miladi, miaka mia moja iliyopita. Kupotea kwa Khilafah kunahisika zaidi wakati watu wote duniani, bila kujali dini, utajiri, jinsia na uasili, wanahitaji faraja kutokana na ukandamizaji mkubwa wa mfumo wa sasa wa kiulimwengu.

Katika Uislamu, mtawala hawezi kuwanyonya au kuwakandamiza watawaliwa kwa kuwa wote wanajifunga na Uislamu. Uislamu pekee ndio chanzo cha hukumu kwa Waislamu na hakuna maoni au mapatano ya mwanaadamu yanayoweza kutengua Hukumu za Mwenyezi Mungu (swt) katika jambo lolote. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

(وَأَنِ ٱحْكُم بَيْنَهُمْ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَآءَهُمْ وَٱحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ إِلَيْكَ)

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliokuteremshia Mwenyezi Mungu” [Surah Al-Maida 5:49]. Hivyo Mtawala sio dikteta wala mwana demokrasia. Hatawali kwa mtazamo wake binafsi wala kwa mtazamo wa Bunge. Anatawala kwa mujibu wa Quran na Sunnah na anawajibika kwa Sheria za Mwenyezi Mungu (swt) katika kila mzozo na wale anaowatawala. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

(فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ)

“Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho.” [Surah an-Nisa’a 4:59].

Ndivyo tunashuhudia Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) katika zama za Khalifah Rashid wa pili, mmoja ya waliotabiriwa Pepo, Amiir ul-Mu’miniin, ‘Umar ibn al-Khattab (ra). ‘Umar al-Faruuq (ra) alitamka akiwa mtawala, لَا تُغَالُوا فِي مُهُورِ النِّسَاءِ" “Msifanye mahari ya wanawake kuwa makubwa mno.” Kutoka miongoni mwa watawaliwa, mwanamke mmoja akatafautiana naye na kusema,

لَيْسَ ذَلِكَ لَكَ يَا عُمَرُ إِنَّ اللَّهَ يَقُولُ وَآتَيْتُمْ إِحْدَاهُنَّ قِنطَارً “Hilo sio lako ewe Umar, kwani Mwenyezi Mungu amesema: (وَآتَيْتُمْ إِحْدَاهُنَّ قِنطَاراً) “Na hali mmempa mmoja wao chungu ya mali” [TMQ 4:20]. Akiwa ni Mtawala anayetatua mizozo kupitia Uislamu, Umar mara moja alikiri na kutengua amri yake, akatamka, "إِنَّ امْرَأَةً خَاصَمَتْ عُمَرَ فَخَصَمَتْهُ" “Hakika, mwanamke ametafautiana na Umar na yuko sahihi katika kutafautiana naye.” Hivyo mtawala wa Ummah wote amekiri juu ya rai ya mtawaliwa, kwa kuwa ana uzito wa Wahyi upande wake.

Hata hivyo, bila ya Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) juu ya ardhi, Waislamu kote katika Ulimwengu wa Kiislamu wanatiwa magerezani au kutekwa nyara, kwa sababu tu ya kulingania haki yao ya Uislamu. Hivi leo, hata maelezo ya Uislamu katika masuala ya siasa yanaangukia chini ya sheria za kupambana na ugaidi.

Chini ya Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) juu ya ardhi, madhaifu na masikini wamepewa haki zao, bila ya matajiri kupewa uhuru kwa utajiri mwingi wa taifa. Mwenyezi Mungu (swt) amesema, (كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاء مِنكُمْ) “Ili (mali) isizunguke baina ya matajiri wenu tu” [Al-Hashr 59:7]. Sheria nyingi za Uislamu zinahakikisha usambazaji sawa wa utajiri, zikiruhusu ueneaji wa utajiri kote katika jamii.

Imepokewa katika Kitabu cha Mali, cha Imam Abu ‘Ubaid al-Qasim, kuhusiana na Khalifah ‘Umar bin ‘Abdul-Aziz,

كتب عمر بن عبد العزيز إلى عبد الحميد بن عبد الرحمن وهو بالعراق أن أخرج للناس أعطياتهم، فكتب إليه عبد الحميد إني قد أخرجت للناس أعطياتهم وقد بقي في بيت المال مال، فكتب إليه أن انظر كل من أدان في غير سفه ولا سرف فاقض عنه، قال: قد قضيت عنهم وبقي في بيت المال مال، فكتب إليه أن زوج كل شاب يريد الزواج، فكتب إليه: إني قد زوجت كل من وجدت وقد بقي في بيت مال المسلمين مال، فكتب إليه بعد مخرج هذا أن انظر من كانت عليه جزية فضعف عن أرضه، فأسلفه ما يقوى به على عمل أرضه، فإنا لا نريدهم لعام ولا لعامين

“Umar bin Abdul-Aziz aliandika kwa Abdul-Hamid bin Abdur-Rahman aliyekuwa Iraq. “Chukua mali kwa ajili ya watu na uwape wao.” Abdul Hamid akaandika, “Kwa hakika nimechukua kwa ajili ya watu na kuwapa, na kilichobaki kiko katika baytul maal.” Umar akamuandikia, “Angalia kwa kila mwenye deni, lisilotokana na upumbavu au israfu na umlipie.” Akasema, “Nimewalipia madeni yao na imebakia mali katika baytul maal.” Umar akamuandikia, “Muozeshe kila kijana anayetaka kuoa.” Akajibu, “Nimemuozesha kila niliyempata na mali imebakia katika baytul maal katika mali ya Waislamu.” Umar akamuandikia, “Baada ya kutoa hayo, angalia yule mwenye Jizya na aliyedhoofu kuhusiana na ardhi yake, basi mpe kile kitakachomtia nguvu kwenye kazi zake juu ya ardhi yake, na kwamba hatuhitaji kutoka kwao kwa kipindi cha mwaka au miaka miwili.”

Hata hivyo, bila ya Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) juu ya ardhi, kunakuwa na mrundikano mkubwa wa mali katika mikono ya kipote teule cha wenye nguvu, kupitia taratibu za Urasilimali wenyewe na mbinu za ufisadi. Matajiri wakubwa zaidi katika ulimwengu wameongeza utajiri wao kutoka 27.5% kufikia $10.2 trilioni kutoka Aprili hadi Julai 2020, kwa mujibu wa ripoti kutoka benki ya Uswizi UBS. Kinyume chake, umasikini wa kutupwa umeongezeka kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili, imeripoti Banki ya Dunia tarehe 7 Oktoba 2020. India imeyumbishwa na maandamano ya wakulima waliofukarishwa chini ya Demokrasia, ambapo Bara dogo la India chini ya Uislamu lilikuwa na mgao wa asilimia 23 ya uchumi wa dunia, uliofikia kilele cha asilimia 27 katika kipindi cha Aurungzeb Alamgir.

Ni Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) juu ya ardhi ambacho, inshaallah, kitaipatia dunia afueni kutokana na mkusanyiko mkubwa wa utajiri chini ya mikono ya kipote cha wenye mabenki kupitia uovu wa riba. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ * فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِّنَ اللَّهِ وَرَسُولِهِ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ)

“Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizobakia, ikiwa nyinyi ni Waumini. Basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilimali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe.” [Baqarah 2:279]. Kwa hakika, Khilafah itaipa faraja Pakistan ambapo mapato ya kodi yanayovunja mgongo yanatumika kulipia riba za madeni ya ndani na nje.

Ni Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) juu ya ardhi, ambacho, inshaAllah, kitaipatia dunia faraja kutokana na mrundikano mkubwa wa utajiri katika mikono ya kipote cha mashirika, kwa kuhakikisha kuwa nishati na madini ni mali ya ummah ambayo haitomilikiwa na dola au kubinafsishwa, bali lazima itumike kwa ajili ya mahitaji ya watu wote. Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

   «الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ الْمَاءِ وَالْكَلَإِ وَالنَّارِ» “Waislamu ni washirika katika vitu aina tatu, maji, malisho na moto (nishati).” (Ahmad). Neno ‘moto’ hapa linakusanya aina zote za nishati zinazotumika kama mafuta kwenye viwanda, mashine na mitambo pamoja na mitambo inayotumia gesi au makaa ya mawe kama ni mafuta. Vyote hivi vipo chini ya kundi la umiliki wa ummah. Ni hakika, Khilafah itazalisha mali nyingi kwa ajili ya kuangalia raia wake, bila kujali dini zao, jinsia au asili.

Ni Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) juu ya ardhi ambacho, inshaAllah, kitaipatia dunia faraja kutokana na urundikaji mkubwa wa mali katika mikono ya maafisa walafi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«مَنِ اسْتَعْمَلْنَاهُ عَلَى عَمَلٍ فَرَزَقْنَاهُ رِزْقًا فَمَا أَخَذَ بَعْدَ ذَلِكَ فَهُوَ غُلُولٌ» “Yeyote tunaempatia wadhifa katika kazi na tukampatia malipo, basi chochote anachochukuwa zaidi ya hicho huwa ni ghuluul (wizi).” [Abu Dawud]. Imepokewa kuwa Umar bin Khattab (ra) kwamba alikuwa akihesabu mali za ma’amil wake kabla ya kuwateuwa, pia baada ya kumalizika muda wao. Alikuwa akiichukuwa kila mali iliozidi katika aliokuwa nayo (yenye shubha). Pia alihoji umiliki wa baadhi ya maWali na kuchukuwa sehemu ya mali zao, kwa sababu ya shaka kuhusiana na njia za uchumaji wao, kama kutumia vibaya nafasi zao na ushawishi wao. Huchukuwa umiliki wa mali hizo na kuzitia katika Bayt ul-Maal.

Chini ya Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) juu ya ardhi, wanawake inshaAllah watahifadhiwa kutokana na udhalimu wa wanaume. Haya yatakuwa hivi wakati katika nchi za Magharibi, mama wasio na waume sio tu hujichumia wenyewe mahitaji yao, lakini hujifungua na kulea watoto peke yao. Haya pia yatakuwa hivi wakati katika nchi za Mashariki, wanawake hunyimwa haki zao za msingi ambazo Uislamu umewapatia tokea karne ya kumi na nne zilizopita zinazohusiana na ridhaa kwenye ndoa, umiliki wa mali na kuwajibishwa kwa watawala. Haki za wanawake katika Uislamu zinahakikishwa na Mwenyezi Mungu (swt), sio kwa uzuri wake, utajiri au nasaba yake, bali kwa mazingatio yake ya kuwa ni mwanaadamu, mja wa Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) amesema,              

  (وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللَّه وَرَسُولَهُ ۚ أُولَٰئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ اللَّهُ ۗ إِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ)

“Na Waumini wanaume na waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika Swala, na hutoa Zaka, na humtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hikima.”  [Surah at-Tawbah 9:71]. Mtume (saw) amesema, «نَعَمْ. إِنَّمَا النِّسَاءُ شَقَائِقُ الرِّجَالِ» “Ndio, Hakika wanawake ni nusu ilioshikamana na wanaume.” [Abu Dawuud]. Mtume (saw) amesema katika hutuba ya kuaga, «اسْتَوْصُوا بِالنِّسَاءِ خَيْرًا» “Watendeeni wema wanawake.” [Ibn Majah]. Wanawake na wanaume wanafanya kazi pamoja kulingana na haki na majukumu ambayo Uislamu umewapangia, bila kuruhusu uonevu kwa kila jinsia. Mume amewajibishwa kutoa matumizi (nafaqa) kwa mke wake, ima awe Muislamu, Mkristo au Yahudi, na kupuuzia ni dhulma, ambayo itaondolewa na Mtawala. Lazima amsaidie mke wake kwa kuwa anazaa watoto wao na atumie kutoka udogoni kwake katika ulezi (Hadaanah). Hivyo, Waislamu wanaume na wanawake washirikiane katika maisha ya kifamilia, kwani familia ni ngome ya jamii ya Kiislamu.

Wakiwa wamehifadhiwa na Uislamu, wanawake katika Uislamu ni wale wanaofanya kazi kusimamisha Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) juu ya ardhi. Sayyidat Khadijah (ra) alitowa usaidizi kwa Mtume (saw) muda wote wa Utume wake. Sumaiyyah (ra) alikuwa shahidi wa mwanzo katika Uislamu, aliyebeba Da’wah, mkakamavu aliyevumilia vikwazo vyote. Umm Ammarah na Umm Munii’a waliotoa bay’ah kwa Mtume (saw) katika Bay’ah ya Pili ya ‘Aqabah ambayo ni bay’ah ya Nussrah na utawala. Na wanawake katika Uislamu ni wale waliong'ara chini ya Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt). Sayyidat Aisha (ra) alikuwa ni Faqiha (Mwanachuoni) na A’limah (Msomi) aliyepokea Hadithi za Mtume (saw). Rafidah al-Aslamiyyah alikuwa ni muasisi wa sayansi ya tiba katika Uislamu. Umm Salamah, Mama wa Waumini alitoa rai nzito katika Hudaybiyah. Fatima al-Zahraa (ra) aliwakuza na kuwatunza viongozi wawili wa Peponi, Hassan na Hussain (ra). Zaynab bint al Hussain aliibuka kutoka katika msiba wa Karbala na kumkabili Yazid, akimrushia kauli nzito kwa kupora mamlaka na kumuuwa Hussain (ra).

Chini ya Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) juu ya ardhi, raia wasio Waislamu watalindwa kutokana na kila aina ya dhulma kutoka kwa watawala wao Waislamu, kwa kuwa Uislamu wenyewe unaamrisha kuangaliwa haki za wasio Waislamu kuwa zisikiukwe. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«أَلا مَنْ قَتَلَ نَفْسًا مُعَاهِدًا لَهُ ذِمَّةُ اللَّهِ وَذِمَّةُ رَسُولِهِ فَقَدْ أَخْفَرَ بِذِمَّةِ اللَّهِ، فَلا يُرَحْ رَائِحَةَ الْجَنَّةِ، وَإِنَّ رِيحَهَا لَيُوجَدُ مِنْ مَسِيرَةِ سَبْعِينَ خَرِيفًا»

Yeyote anayemuua Mu’ahid mwenye dhimma ya Mwenyezi Mungu na dhimma ya Mtume Wake hakika amekhini Dhima ya Mwenyezi Mungu, basi hatohisi harufu ya Pepo, na hakika harufu yake inafikia mwendo wa kharif sabiini” [Tirmidhi]. Hivyo, Uislamu umemuhakikishia hifadhi kamili raia wa Khilafah asiye Muislamu, hifadhi kwa ajili ya mali na nafsi zao, na Uislamu umemkinga na ukandamizaji wowote unaohusiana na matendo yao ya kidini ya kibinafsi. Mara tu baada ya Upanga wa Mwenyezi Mungu, Khalid Ibn al-Walid (ra), kuifungua al-Hira kusini mwa Iraq, aliandika barua kwa Khalifah Abu Bakar (ra) akimwambia namna alivyoitekeleza kodi ya jizya lakini amewaengua wasio Waislamu masikini, wazee na walemavu, akisema, "طُرِحَتْ جزيتُه وعيلَ من بيت مال المسلمين وعياله" “Imesamehewa Jizya yake, na kutajirishwa kwa Baytul Maal ya Waislamu, pamoja na familia yake.”

Pindi Khilafah ikikosa uwezo wa kujifunga na mkataba wa kuwalinda wasio Waislamu, haitoruhusika kukusanya Jizya. Ash-Sham imekombolewa kwa mikono ya Waislamu, lakini Wakristo wa Roma walipokusanya vikosi kuichukuwa tena, Sahaba mkubwa Abu Ubaidah (ra), hakuweza kuwahakikishia ulinzi wasio Waislamu. Hivyo Jizya ilirejeshwa, pamoja na tamko,

"وَإِنَّمَا رَدَدْنَا عَلَيْكُمْ أَمْوَالَكُمْ لِأَنَّا كَرِهْنَا أَنْ نَأْخُذَ أَمْوَالَكُمْ وَلَا نَمْنَعَ بِلَادَكُمْ"

“Tumekurejesheeni fedha zenu, kwani tunachukia kuchukuwa mali zenu wakati hatuihifadhi ardhi yenu.” Badala ya kujiweka upande wa Wakristo wa Roma, Wakristo wa ash-Sham walitamka,

"رَدَّكُمُ اللهُ إلينا، ولَعَنَ اللهُ الذين كانوا يملكوننا من الروم، ولكن والله لو كانوا هم علينا ما ردُّوا علينا، ولكن غصبونا، وأخذوا ما قدَرُوا عليه من أموالنا، لَوِلايتُكُم وعدلُكم أحبُّ إلينا مما كنا فيه من الظلم والغُشْم"

“Mwenyezi Mungu aturudishe kwenu, na awalaani wale waliotumiliki kutoka Roma. Wallahi lau wao wangelikuwa juu yetu, wasingeturudishia, bali wangetupora na kuchukuwa kila wanachoweza katika mali zetu. Usimamizi wenu na uadilifu wenu ni wenye kutupendeza zaidi sisi kuliko kuwa katika dhulma na mateso.” Hivyo Khilafah itarudi kuwa mshindi na kuwahifadhi wasio Waislamu wa ash-Sham kwa karne nyingi chini ya kivuli chake.

Huku watu wa dini walio wachache wakiteswa kote duniani, Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) juu ya ardhi kwa hakika kimekosekana kweli. Usiku wa manane Agosti 2, 1492, manuwari za Columbus ziliondoka kutoka bandari zisizotambulika za Palos kwa sababu njia za meli za Cadiz na Seville zilizozibika kwa Mayahudi wa Sephardic  waliofurushwa kutoka Uhispania kwa Amri ya Malkia Isabella na Mfalme Ferdinand wa Uhispania. Mayahudi walilazimishwa ima kuingia kwenye Ukristo au kuondoka nchini bila mali zao. Kwa kutambua ufukuzwaji wa dhulma wa Mayahudi kutoka Uhispania, Khalifah Bayezid II alituma manuwari za Khilafah kuwachukuwa Mayahudi kwa usalama katika ardhi za Dola ya Khilafah, zaidi katika miji ya Thessaloniki na Izmir, huku akitamka, “Mnathubutu kumwita Ferdinand Mwenye Busara, yeye ambaye ameidhoofisha nchi yake mwenyewe na kuistawisha yangu!”

Nini kitachomaliza dhulma kwa watu hivi sasa bila ya Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) juu ya ardhi? Waislamu na wasio Waislamu katika ardhi ya ash-Sham hawajahifadhiwa na wanasumbuka kwa kiasi kikubwa chini ya mikono ya umbile la Kiyahudi na utawala dhalimu wa Bashar. Wakaazi madhlumu wa ash-Sham wanakimbilia pembe zote za dunia kuomba hifadhi, wakizama baharini wakiwa njiani au wakikaribishwa kwa dharau, na kuwekwa kama kuku waliowachwa kwenye banda chakavu. Nje ya ash-Sham, misiba iko sawa. Vilio vya Wauighur katika Turkistan ya Mashariki na Rohingya wa Burma vinaangukia kwenye uziwi wa watawala Waislamu, huku watawala wa Pakistan hata kukataa vilio wao wenyewe. Waislamu wanaokimbia uvamizi wa kigeni Afghanistan kuelekea Pakistan wanaamiliwa kwa dharau na kubezwa na Watawala wa Pakistan, wanaowazingatia kuwa ni mzigo badala ya utajiri. Waislamu wa Kashmir Iliokaliwa Kimabavu wametelekezwa kwa dhalimu Modi, wakati watawala wa Pakistan wakiwazuia mamia ya maelfu ya vikosi vilivyotayari na uwezo kupigana na dola ya Kibaniani kuikomboa Kashmir. Waislamu wa ardhi zilizokaliwa wameachwa wakielemewa na maadui, ijapokuwa Mwenyezi Mungu (swt) amesema,   (وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ) “Wanapokutakeni msaada katika dini, ni juu yenu kuwanusuru.” [Surah Al-Anfal 8:72] Majeshi hayapelekwi kuwakomboa kutokana na dhulma, ijapokuwa Mwenyezi Mungu (swt) ametutaka,

(وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ وَالْفِتْنَةُ أَشَدُّ مِنَ الْقَتْلِ)

“Na wauweni popote muwakutapo na watoeni popote walipokutoweni; kwani fitna ni mbaya zaidi kuliko kuuwa.” [Surah al-Baqarah 2:191].

Zaidi ya hayo, kwa kukosekana kwa Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) juu ya ardhi, watawala wa sasa wa Waislamu hudiriki hata kuwapatia nguvu madhalimu kwa kukimbilia kufanya mikataba ya kijeshi na maafikiano ya kiuchumi pamoja nao ijapokuwa Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

(إِنَّمَا يَنْهَاكُمْ اللَّهُ عَنْ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الظَّالِمُونَ)

“Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanaofanya hao marafiki basi nao ndio madhaalim.” [Surah al-Mumtahina 60:9]. Ndio wanawepesisha maelewano ya kawaida na wavamizi makruseda wa Amerika katika Afghanistan, umbile la Kiyahudi na Dola ya Kibaniani, wakiwadhalilisha Waislamu, juu ya kwamba Hukmu ya Mwenyezi Mungu (swt) ni kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt) hadi wavamizi watimuliwe. Ikiwa ni sehemu ya mikataba yao na maadui, watawala Waislamu sio tu wanazuia majeshi ya Waislamu, bali wanawasaka Waislamu mmoja mmoja wanaopigana na maadui, ijapokuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ameonya, «مَا تَرَكَ قَوْمٌ الْجِهَادَ إلاّ ذُلّوا» “Hawaachi watu kupigana Jihad isipokuwa watadhalilishwa.” [Ahmad]

Hakika, Enyi Waislamu, dunia iko katika hasara kubwa bila ya Kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) juu ya ardhi. Ni juu yetu sote kujifunza na kuukumbatia urithi wetu tajiri wa Kiislamu. Ni juu yetu sote kufahamu wajibu wetu, tukichukuwa majukumu kwa ukamilifu kwa kurejesha utawala wa Kiislamu. Ni juu ya kila mmoja wetu kufanya kazi ya kurejesha tena Khilafah kwa Njia ya Utume sambamba na kuilingania Khilafah hadi isimamishwe. Ni miaka mia moja tokea kuvunjwa kwa Kivuli cha Mwenyezi Mungu juu ya ardhi, Enyi Waislamu, basi irejesheni! Hakika, Mwenyezi Mungu (swt) amewaahidi wale walioamini na kutenda matendo mema kuwa watapata ukhalifah (utawala) juu ya ardhi,

  (وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ)

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya Makhalifah katika ardhi kama alivyowafanya Makhalifah wa kabla yao.” [Surah An-Nur 24: 55].

أقيموا_الخلافة#
#ReturnTheKhilafah
#YenidenHilafet
خلافت_کو_قائم_کرو#

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Musab Umair – Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu