Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kutokana na Kukosekana kwa Khilafah Hasara ambayo Wanawake Wamekumbwa Nayo ni Kubwa na Mbaya

(Imefasiriwa)

Tunasikia, tunasoma na hata kuishi nazo, ni athari za kukosekana kwa Khilafah na dola ya Kiislamu inayohukumu kwa Uislamu. Na kwa wale wanaoshangaa, ima wanahoji, wanakejeli au kusaka elimu, nini tulikikosa hasa kwa kutokuwepo kwake? Tunasema: Tumekosa mengi katika hatua zote, nyanja na maeneo yote ya maisha. Hapa tutalenga juu ya wanawake waliokosa mengi na kuumizwa katika mambo mengi.

Jambo muhimu zaidi alilolikosa mwanamke kutokana na kutokuwepo Khilafah ni jukumu lake msingi katika maisha, ambalo kwalo huvikwa taji la malkia nyumbani kwake. Kuwa mama na mke nyumbani na mwanamume kuwa na jukumu kwake, katika uangalizi na kumtimizia mahitaji yake. Hivyo halazimiki kuchuma riziki yake yeye binafsi, huku akiruhusika kusoma na kufanya kazi pindi atakapo. Kwa kukosekana Uislamu katika utekelezaji, na utawala wa mfumo wa kirasilimali unaojali manufaa tu, wanawake wanazunguka baina ya majukumu mawili. Baina ya nyumba na majukumu yake na baina ya kazi na ugumu wake, bila mapumziko, utulivu, au kutekeleza majukumu yao msingi kwa ukamilifu, matokeo yake ni kile tukionacho katika uchovu, dhiki, udhalimu na uonevu ambao mwanamke anauhisi wakati anapojitawanya baina ya majukumu yote haya, akilazimika na sio kwa hiyari yake, ili aweze kuyakabili mahitaji yake na ya familia yake, anapokuwa na mume au bila mume. Bila kujali shughuli na kazi zinazokubaliana naye kama mwanamke, ima iwe kwa upande wa aina au mahala. Vile vile, analazimika kuwaachia watoto wake ima walezi wasiofaa nyumbani bila ulezi bora, au hata mitaani hadi arudi nyumbani, inayopelekea kuwa na elimu mbaya, tabia, maadili na misingi mibaya.

Mwanamke amekosa amani na usalama, na hivyo malalamiko yake hayaitikiwi wakati anapokabiliana na machafuko, mauwaji, uhamisho na uvunjwaji wa haki, wala kwa kilio chake akiwa katika jela za madhalimu. Hakuna Mu’tasim anayejibu malalamiko haya na mayowe kwa sababu wale wa kuyajibu au wanaopaswa kuyajibu haya kutoka kwa watawala hawamiliki maamuzi yao, ambayo yanapangwa Washington, London na Paris …

Hata miongoni mwa baadhi, kuna ukiukaji wa haki wa kifamilia ndani ya familia na miongoni mwa familia yake, kuwa wanaume wasiomuogopa Mwenyezi Mungu (swt) na kuwaendesha wanawake kwa ukatili na uonevu, na hivyo wamekuwa ni chanzo cha hofu badala ya kuwa ni amani na utulivu, na kumfanya aombe ulinzi kutoka dhidi yao badala ya kuuomba kutoka kwao, kwa sababu ya kuwa mbali kwao na dini, na kwa sababu hakuna kizuizi kwao kutokana na sheria kwa msingi wa hukumu za Kisharia. Na anaweza kuwa ni mke, msichana, au hata mama ambaye mioyo ya watoto wake imeondolewa huruma, hivyo wamemtupa bila kuwa na mkimu wa familia au msaidizi, na hata hakuna adhabu yoyote kutoka serikalini dhidi ya matendo yao, na hana makaazi ambapo ni tofauti na inapokuwepo dola inayotawala kwa Uislamu, dola ya Khilafah.

Mwanamke amepoteza wepesi katika kupata haki zake na kumuondolea uonevu, ima iwe ni kutoka serikalini, familia, jamaa au kwa yeyote. Wajane wangapi, mayatima, masikini, au wanaodhulumiwa, wanaohangaika wakaipitisha miaka huku wakihama baina ya wanasheria na mahakama, wanammalizia fedha zake kupitia faini na gharama, baada ya kulalamika kwa hakimu akitaka kuchukua haki yake katika kikao kimoja bila gharama, unyonyaji au uchovu. Amepoteza haki zake za urithi katika baadhi ya sehemu na familia, ikiwa pamoja na hukumu zinazohusiana na nidhamu za kijamii, kama ulazima wa ridhaa yake kwenye ndoa, na haki yake ya mahari, na kama mzozo utatokea unaopelekea kuachwa, kuna wale wanaopoteza haki yao ya matunzo au hata sehemu ya mahari iliobakia na haki zake za Kisharia ima kwa sababu ya udhibiti wa mila za kabla ya Uislamu au udhaifu wa mahakama za Kisharia katika kutekeleza hukumu za Kisharia, au upendeleo inapokuwa mshtakiwa anatokea tabaka la watu wakubwa au matajiri.

Hapa nitanukuu Hadith (Gharib Sahih) kutoka kwa Imam Al-Awza’i siku ya Tabouk, wakati Mtume (saw) alipomsifu na kumshukuru Mwenyezi Mungu (swt) na kusema:

 «إِيَّاكم وَالأَقْرَادَ»، قُلْنَا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَمَا الأَقْرَادُ؟، قَالَ: «يَكُونُ أَحَدُكُمْ أَمِيراً أَوْ عَامِلا، فَتَأْتِي الأَرْمَلَةُ وَالْيَتِيمُ وَالْمِسْكِينُ، فَيُقَال: اقْعُدْ حَتَّى نَنْظُرَ فِي حَاجَتِكَ، فَيُتْرَكُونَ مُقَرَّدِينَ، لا تُقْضَى لَهُمْ حَاجَةٌ وَلا يُؤْمَرُونَ فَيَنْصَرِفُونَ، وَيَأْتِي الرَّجُلُ الْغَنِيُّ أو الشَّرِيفُ، فَيُقْعِدُهُ إِلَى جَنِبِهِ، ثُمَّ يَقُولُ: مَا حَاجَتُكَ؟ فَيَقُولُ: حَاجَتِي كَذَا وَكَذَا، فَيَقُولُ: اقْضُوا حَاجَتَهُ وَعَجِّلُوا بها»

“Jiepusheni na Al-Aqra” Tukauliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni nani Al-Aqrad? Akasema: “Anapokuwa mmoja wenu Amir au Amil, akajiwa na mjane, yatima au maskini, huambiwa kaa na usubiri hadi suala lako lishughulikiwe, basi huachwa katika ukimya wa udhalilifu, na mahitaji yao hayatekelezwi, hakuna kinachoamriwa kwao na hivyo huondoka. Anapokuja tajiri au mwenye hadhi, huwekwa karibu yake (Amir au Amil), kisha huulizwa juu ya haja yake na huieleza kadha na kadha, basi husemwa: mtatulieni haja yake na muiharakishe”

Al-Aqrad ni ukimya wa kudhalilika, kama ilivyofasiriwa na Al-Zamakhshari, na hii haitotokea chini ya Khilafah, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Wanawake wamepoteza uwezo wao kutekeleza ibada zao kama wanavyopaswa na wanavyotaka, hasa katika nchi nyingi, ima katika nchi za Waislamu au za Magharibi. Wanawake walipigwa marufuku kuvaa vazi la Kisharia, hawakuhifadhiwa kutokana na madhara, kejeli na dhulma dhidi yao, ima kwa mdomo au kupitia sheria pindi wavaapo hijabu zao, na hata kunyimwa elimu wanapo zuiwa kuingia shuleni au vyuoni kama ilivyotokea Ufaransa na kwengineko! Huenda wakawa kama wengine, huzuiwa kwenda Hajj au Umrah, au hata kwenda msikitini, au kuswali katika maeneo ya kazini.

Huenda pia moja ya mambo muhimu zaidi ambayo mwanamke wa Kiislamu anakumbana nayo kwa kukosekana Khilafah na kuishi kwake katika jamii zisizo za Kiislamu, ni mapambano ya kujilinda yeye binafsi, tabia zake na maadili, jihad katika nafsi yake na mvutano wa kifikra pamoja na wengine, ima iwe katika mazingira ya kifamilia, shule, kazi, au kijamii. Wasiwasi, vipaumbele, kumbukumbu na tabia zinamiminwa ndani ya dimbwi la kuchukiza la usekula na Ubepari, na hivyo anahisi kutengwa ndani ya jamii yake, na uzito na kiwango cha jukumu lake kuielimisha jamii hii na kuwaelimisha watoto wake unaongezeka, juu ya fikra hizi na tabia ambazo zinapatikana kila mahala. Katika mtaa, shule, mitaala, chaneli za setilaiti, njia za mawasiliano, uwazi wa teknolojia na utandawazi, anakuwa na mvutano na binti yake na hivyo hatoki nje bila kujihifadhi, kujipamba (tabarruj) na kuasi, kuchanganyika na wanaume ambako hakujahalalishwa na Sheria, na wimbo kuhusu madai ya uhuru yenye kumtia kasumba yeye na akili yake. Anakuwa katika mgogoro na mume wake na kushughulika na riba katika benki na mikopo, na pia pamoja na mtoto wake na ufinyu wa fikra zake na mapenzi yake na kuasi kwake nyumbani kwao, Dini yake na familia. Kama ingekuwapo Khilafah, mwanamke huyo asingelazimika na haya yote, kwani yote haya yangekuwa ndani ya jamii ya Kiislamu, ima kupitia uchamungu wa watu binafsi au kwa nguvu ya dola inayotekeleza hukumu za Sheria.

Hasara na uharibifu ni mkubwa, na hii ni sehemu ndogo tu … tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kuharakisha Khilafah Rashida ya pili juu ya njia ya Utume, ili tuondokane na yote haya, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt).

#أقيموا_الخلافة
#ReturnTheKhilafah
#YenidenHilafet

 # خلافت_کو_قائم_کرو                                                                                                                                    

# TurudisheniKhilafah

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Muslimah Ash-Shami (Umm Suhaib)

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu