Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Khilafah na Mfumo wa Ulimwengu

Tunapoiangalia dunia, tunaona makundi ya nchi washirika yakiwa yanapingana kila moja, na tutashangazwa juu ya tofauti itayokuwepo kama kutakuwa na Dola ya Khilafah katika mchanganyiko huo. Kwanza tuchukulie Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislam (OIC) haimo katika mjadala, kwa kuwa kimsingi itakuwa imeshajitoa yenyewe. OIC imejiweka yenyewe kuwa ni chombo cha sera za kigeni za Saudia, na kwa sababu Saudi Arabia imejitiisha yenyewe kikamilifu kwa Amerika, imekuwa ni aina tu ya usaidizi kwa sera za kigeni za Amerika.

Pindi mtu akiizingatia nadharia ya Samuel P. Huntington ya ‘Mgongano wa Hadhara’ (Clash of Civilizations), angekumbana na pengo. Angedai kuwa Wamagharibi ndio wenye nguvu, lakini angeona ikikumbana na ushindani kutoka kwa hadhara za Kichina (Konfyushasi) na Kiislamu. Hata hivyo, wakati kuna dola kiongozi ya Magharibi, Amerika, na Dola kiongozi ya Konfyoshasi, China, kihakika hakuna dola ya Kiislamu kwa maana ya kuwa itaweza kushindana na Amerika, hata kwa kiwango ambacho China inakiweza. Uchambuzi wa Huntington umekosolewa vikali, na kwa hakika unaweza kukosolewa. Lakini pia ni kweli kuwa Dola ya Khilafah itahalalisha kwa kiwango cha kwamba hivi sasa hakuna dola inayowakilisha hadhara ya Kiislamu, au kuwa kama ni kiini chake. Dola ya Khilafah haipaswi kuja kwa sababu lazima ishindane, lakini mara itaposimama, italazimika kushindana ili iweze kufikia vigezo vya msingi vya kuwa na usalama wake wenyewe, na wa kutekeleza nidhamu za Kiislamu.

Mbali na fadhaa yoyote inayoweza kuletwa na ukataaji wa Khilafah juu ya mfumo wa kirasilimali, lengo la wazi la dola ni Da’wah na Jihad. Itakuwa ni kuvunjika moyo kwa watetezi wa mfumo wa ulimwengu unaoegemea usimamishaji wa amani (pindi tu amani hiyo ikiwa inakwenda sambamba na matakwa ya baadhi ya nchi za kirasilimali), kwa sababu itaengua msingi wa kutoingilia mataifa mengine. Inaweza kuonekana ni mshangao, lakini dola kama hiyo haitokuwa ni ya kinafiki kwa kudai kutoingilia wakati inaingilia kuongeza maslahi yake. Dola ya Khilafah itakuwa rahisi kufahamika maeneo mengine duniani, kwa kuwa itakuwa na sera za wazi kabisa kuelekea maeneo mengine. Nchi za Waislamu, zilizotawaliwa na Waislamu katika kipindi chochote cha nyuma, zitajumuishwa na Khilafah. Nchi zisizo za Waislamu, kama mataifa ya kibeberu mfano Amerika, Uingereza au Ufaransa, yatachukuliwa kama ni nchi tulioko vitani nazo (kafir harbi), na ijapokuwa vita kamili vitaamuliwa na Khalifah akiwa ni Amir wa Jihad, amani na mataifa hayo itategemea tu juu ya mambo mawili: uwepo wa mkataba, na maamiliano yao na Waislamu ndani na nje ya mipaka yao.

Inaweza kutabiriwa kuwa Dola ya Khilafah itakuwa ya ufanisi zaidi kuliko muundo wa sasa wa mataifa 56 ya OIC katika kushughulikia matatizo yanayozuka kwa Waislamu. Suala la mwanzo ambalo dola ya Khilafah itajifunga nalo ni kushughulikia nchi za Waislamu ambazo haziitii. Nchi zisizoikubali Khilafah na hazitekelezi nidhamu za Kiislamu zinazingatiwa kuwa zimeasi, na ni lazima zipigwe vita hadi zisalimu amri. Zitakapojisalimisha, zitaamiliwa tofauti na ardhi za makafiri, ambazo mapambano yataendelea hadi Waislamu wasimamishe nidhamu humo.

Tatizo la Waislamu wakati ambapo Khilafah ilipokuwa inavunjwa ni ukoloni. Idadi kubwa ya Waislamu nje ya Khilafah ilikuwa nchini India (ambamo walikuwa ni wachache), Indonesia na Asia ya Kati, ambapo mtawalia zilikuwa ni koloni za Uingereza, Uholanzi na Urusi. Khilafah iliyasalimisha maeneo mengi katika Balkan, lakini kujitenga kwa ardhi za Waarabu chini ya Mkataba wa Sykes-Picot, ambapo Uingereza na Ufaransa zilikubaliana kuzigawa ardhi za Kiarabu baina yao, huku ikisubiriwa Vita vya Kwanza vya Dunia na kuvunjwa kwa Khilafah. Kushindwa kwa Uturuki katika Vita vya Kwanza vya Dunia kumepelekea matatizo mawili kwa Waislamu. Kwanza ni kuvunjwa kwa Khilafah. Kisha ni Mkataba wa Sykes-Picot, ambao pamoja na mambo mengine, uliipeana Palestina - ambayo ilikuwa ni sehemu ya Wilaya ya Syria - kwa Uingereza, sehemu pekee ya Wilaya hiyo ambayo haijaenda kwa Ufaransa, na ambapo ilimaanisha ni kwa ajili ya kuisimamisha dola kwa ajili ya Mayahudi. Khalifah wa mwisho aliyekuwa na nguvu wa Uthmaniya, Abdul Hamid II, alikataa kuwapa Mazayuni ardhi yoyote katika Palestina. Badala yake, Uingereza ilifanya iwezekane.

Wakati Uingereza ikiondoka Palestina mwaka 1948, iliyopelekea An-Nakba, ambayo yalikuwa ni maafa makubwa ya kibinaadamu baada ya Vita vya Pili vya Dunia, ilikuwa tayari imeshaipatia uhuru India mwaka 1947, na kuikata ndani yake Pakistan (ambamo ndani yake ilikuja kuzaliwa Bangladesh mwaka 1971) ikiwa ni nchi ya Waislamu. Utoaji uhuru ulifuatia haraka baada ya hapo, na sio tu katika ardhi za Waarabu, lakini pia nchi za kusini mwa jangwa la Sahara zimepata uhuru moja baada ya moja, zikiwemo nchi za Waislamu. Kuundwa kwa OIC mwaka 1969 iliokusudiwa kusimamia utanukaji wa eneo hili kubwa la nchi za Waislamu ambazo zimekuwa huru (angalau kimbinu) kutokana na utawala wa kikoloni. Hili limekuja muda mchache baada ya matokeo mawili muhimu: Vita vya Siku Sita 1967, ambapo Masjid Al-Aqsa uliingia katika udhibiti wa umbile la Kiyahudi, baadaye tukio la moto katika Masjid Al-Aqsa, ambalo lilisababisha hasira katika Ummah wote. Serikali, ambazo mara nyingi huwa za kifalme au za kidikteta, zote zimekuwa na jukumu la utiifu ima kwa Amerika au Usovieti, zikihitajia kuonyesha kuwa zinafanya kitu. Hata hivyo matatizo kwa Waislamu yameongezeka sana. Matatizo ya baada ya Khilafah, ya Palestina na Kashmir, hayajatatuliwa, na juu ya hayo yameongezeka ya Cyprus Kaskazini, Timor Mashariki, na Sudan Kusini, wakati  Warohingya na Wauighur wanakumbana na mzunguko mpya wa ukandamizaji. Nchini India, Waislam wanakumbana pia na mzunguko mpya wa ukandamizaji.

Sababu moja kwa nini mfumo wa sasa hauendani na hisia za Waislamu ni kuwa dola hizi mpya za kitaifa katika ardhi za Waislamu zilianza kufuata maslahi yao yenyewe. Watawala wengi wanaodhibiti mataifa haya wana mvutano wa kimaslahi. Mfano mzuri ni Saudi Arabia, ambayo imejiingiza kwenye uwekezaji wa $15 bilioni katika mradi wa viwanda vya usafishaji mafuta. Hii imeleta ushawishi kwa Saudi Arabia kwa kuendeleza mahusiano mazuri, bali mazuri zaidi pamoja na India. Serikali ya Saudi Arabia lazima iweke uwiano baina ya hili na wale wanaotaka Saudi Arabia kuipa changamoto India kwa matendo yao kwa watu wa Kashmir. Kwa namna hii, serikali zote lazima ziweke uwiano kwa msukumo unaowekwa na raia wake, na kuja na sera moja. Katika hilo, Khilafah itakuwa kama dola nyengine yoyote. Serikali itaunda sera kulingana na namna Khalifah atavyotatua matakwa ya Ummah, kwa kuwa kutakuwa na dhamira moja inayofanya kazi kote ndani ya Dola, na Khilafah itakuwa na nguvu zaidi ya dola nyingi, kama sio zote, ambako matatizo huzuka kwa Waislamu, Khalifah huenda hatokuwa na kusita sita katika kushughulikia masuala haya kwa haraka, na hivyo kung'arisha sifa zake ndani ya Ummah.

Moja ya uhuru muhimu atakaokuwa nao Khalifah katika kushughulikia masuala ya Ummah ni kwamba atakabiliana na uchaguzi (kwa ajili ya Bay’ah), lakini sio kustaafu (angalau, sio kwa lazima kwa kuwekewa kipindi maalum). Kwa kuwa kipindi chake kimefungika na muda wa uhai wake, haelewi kama asivyoelewa mtu mwengine yeyote juu ya kumalizika kwake, na hakuna utendaji wa matendo yatayosaidia kuchaguliwa tena. Hakuna nguvu yoyote ya kigeni itayoweza kumpatia msaada wowote katika uchaguzi wowote, kwa sababu hautokuwepo wowote kwake. Hakutakuwa na chochote cha kumpatia katika kukaa kwake madarakani. Anaweza kuhofia ukosoaji kutoka nje, lakini kama hautojengewa msingi mzuri, kama mfano ukosoaji wa rekodi ya haki za binaadamu katika serikali yake, ataupuuza. Hatoshawishika kufuata ajenda yoyote ya kigeni. Kwa sababu ya hayo, Ummah utakuwa kwenye utulivu zaidi kwa viongozi katika Dola ya Khilafah kuliko hali ilivyo leo. Moja ya masuala muhimu yaliojificha ambayo Khalifah itabidi ayashughulikie ni idadi kubwa ya Waislamu wanaoishi nje katika nchi za kigeni. Ni kadirio lisilo na shaka kuwa wengi watarejea kwenye Khilafah wakati itaposimama tena, lakini vile vile ni kadirio la kweli kuwa wengi watabakia mahala walipo. Suala muhimu katika kuamua muelekeo wa Khalifah kwao ni muelekeo wake kwa nchi wanayoishi, ambao huamuliwa na uhuru walionao Waislamu katika kufuata Shariah. Khalifah pia atalazimika kuzingatia msukumo unaotolewa na raia hawa juu yake kupitia jamaa zao walioko ndani ya Khilafah, na uwezekano wa kuwa msukumo huo unatokana na hatua za serikali ya nchi wanazoishi. Wakati huo huo, nchi hiyo itatakiwa izingatie mbinyo unaoelekezwa kwake ili iruhusu Shariah kutawala maisha ya Waislamu.

Raia wa dola ya Khilafah wataona kuwa na mtu anayeongoza serikali anayejizingatia kuwa amefungika na hukmu za kisharia kuwa ni hatua nzuri dhidi ya yule ambaye ima ni dikteta au anayetunga sheria kama anavyotaka. Taasisi ya Madhalim itaonekana kuwa ni kifungua macho kwa raia, atakayeiona Khilafah kuwa ni hatua nzuri dhidi ya dola za leo za kirasimu. Hata Wamagharibi wataweza kunufaika, au angalau mtu wa kawaida, kama sio serikali. Serikali zinaweza kuhoji kuwa hazina tena udhibiti juu ya watawala, lakini watu mitaani yumkini watakaribisha utawala uliowekwa chini ya makao makuu juu ya masuala yote ya Waislamu. Kwa mfano, tunatarajia kuona mwisho wa vikundi vya wanamgambo kuyaweka mambo mikononi mwao, kwa sababu Khalifah ndio Amir wa Jihad, na hivyo ndio mtu pekee atakayetangaza Jihad, wakati katika hali ya sasa mtu mmoja mmoja au makundi hutangaza Jihad, na hili halitowezekana. Hii itatatua suala la kijeshi katika ardhi za Waislamu kwa kiasi kikubwa. Hivi sasa, ikumbukwe kuwa uungwaji mkono mkubwa kwenye mapambano ya kijeshi katika ardhi za Waislamu ni kwa sababu ya kukosekana mamlaka inayoweza kutangaza juu ya uhalali wake. Ikumbukwe kwamba Khalifah sio tu huamua ima kundi la watu lazima lipigwe vita, lakini pia muda gani. Anaweza kukubaliana na Wapiganaji Waislamu kuwa Waamerika, au Wafaransa, au Watimor Mashariki, kwamba wanastahili kupigwa vita, lakini kama ataona kuwa muda sio muwafaka, hawatoweza kupitisha uamuzi wao wenyewe. Zaidi ya hivyo, Jihad inayoratibiwa na Dola inamuelekeo mzuri zaidi wa kupata matokeo ambayo mengi ya makundi ya wanamgambo katika Ulimwengu wa Kiislamu yanayatamani lakini mengi yanashindwa kuyafikia.

Huenda ni kutokana na faida za namna nyingi ambazo Khilafah inazileta kwa Uislamu na Waislamu ndio mataifa ya Ulaya yalifanya juhudi kubwa kwa kuangushwa kwake. Kurejeshwa kwa Khilafah kwa Njia ya Utume sio tu ni faradhi, lakini ndio jukwaa pekee ambalo Waislamu wanaweza kukamilisha malengo yao muhimu zaidi na yanayohitajia uharaka.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Afzal Qamar – Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu