Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhalifu wa Bunduki ni Kadhia Kubwa nchini Amerika

(Imetafsiriwa)

 

- Mnamo 2022, kumekuwa na matukio 213 ya ufyatuliaji risasi ambapo watu 4 au zaidi wamepigwa risasi au kuuawa kutokana na ufyatuliaji huo.

- Mnamo 2021, kulikuwa na ufyatuliaji risasi 692 wa watu uliorekodiwa.

- Mnamo 2020, kulikuwa na ufyatuliaji risasi 610 wa watu. (Chanzo: Guardian)

Ufyatuliaji risasi huu kwa kawaida hufuatiwa na maandamano makubwa- hasa yanapotokea shuleni. Lakini hakujawahi kuwa na mabadiliko makubwa - raia wa Marekani bado wangali na "haki ya kubeba silaha" isiyoweza kushtakika, haki ambayo inalindwa na baraza la mawaziri, bunge na mahakama.

Wanaweza kubadilisha sheria - Seneti inao uwezo wa kufanya hivyo. Ilhali bado hawajafanya hivyo. Badala yake, wamefanya kinyume chache- badala ya kuruhusu sheria kubadilika, hawajapitisha sheria inayolinda maisha kwa kuweka mipaka ya umiliki wa bunduki.

"Tangu mauaji ya 2012 ya watoto 20 na wafanyikazi wanne katika Shule ya Msingi ya Sandy Hook huko Newtown, Connecticut, sheria iliyoletwa katika kukabiliana na mauaji ya watu wengi imeshindwa kupita Seneti mara kwa mara." (The Conversation)

Na hivi majuzi, uamuzi wa Mahakama ya Upeo ulitupilia mbali sheria ya New York ambayo ililazimisha masharti ya leseni ya kumiliki silaha zilizofichwa - hii inafanya iwe vigumu kwa majimbo na miji mingine kulazimisha vikwazo vyao wenyewe kwa silaha.

Kwa nini Amerika haijaweka vikwazo zaidi?

Kulikuwa na nchi nyingine ambazo hapo awali zilitiwa moyo kuwapa raia wao haki ya kubeba silaha - ikiwa ni pamoja na Bolivia, Costa Rica, Colombia, Honduras, Nicaragua, Liberia, Guatemala, Mexico, na Marekani. Isipokuwa Marekani, Mexico na Guatemala, tangu wakati huo wamebatilisha haki hii.

Huko Uswizi, baada ya kuona jinsi uhalifu wa kutumia bunduki ulivyoenea zaidi walipoongeza haki za raia wao za kumiliki bunduki, waliongeza vifungu zaidi kwenye sheria zao (kuweka idadi inayoongezeka ya mipaka juu ya umiliki wa bunduki nchini).

- Mamlaka za Uswizi katika ngazi ya ndani ya nchi huamua iwapo itawapa watu vibali vya kumiliki bunduki, na huweka rekodi ya wale wanaomiliki bunduki katika eneo lao (ingawa bunduki za kuwinda na baadhi ya silaha ndefu za nusu-otomatiki hazijumuishwi katika masharti ya kibali)

- Watu ambao wamehukumiwa kwa uhalifu au wana uraibu wa pombe au dawa za kulevya hawaruhusiwi kununua bunduki nchini Uswizi.

- Sheria pia inasema kwamba mtu yeyote "anayeonyesha tabia ya vurugu au hatari" hataruhusiwa kumiliki bunduki.

Kwa hivyo kwa nini Amerika inapinga mabadiliko?

Kuna ukosefu wa utashi wa kisiasa kwa mabadiliko

"Wabunge hawajakaza sheria za shirikisho za kumiliki bunduki kwa njia ya maana tangu 1994. Ikiwa watapitisha sheria sasa itakuwa ni kwa kuona haya. Ingawa Waamerika wengi (wanaoendelea kupungua) wanataka vizuizi vikali, hatua kabambe haziko mezani. (The Economist)

 Mnamo 1994, kufuatia mfululizo wa ufyatuliaji risasi, kulikuwa na jitihada za kuunda vikwazo kwa silaha za mashambulizi katika ngazi ya shirikisho. Marufuku hiyo ilizuia umiliki wa "silaha za mashambulizi ya nusu otomatiki" na "vifaa vikubwa vya kujazia risasi. Marufuku hiyo ya miaka 10 sasa imemalizika muda wake.

Lakini baada ya mswada huo kupita, wabunge walioupigia kura walipoteza viti vyao katika uchaguzi mwaka huo. Na baadhi ya wanaRepublican waliripotiwa kupokea vitisho vya vurugu.

"Mwakilishi wa GOP Fred Upton wa Michigan alisema 'alilazimika kuwa na ulinzi wa polisi kwa miezi sita' baada ya kupigia kura mwaka wa 1994 marufuku ya silaha za shambulizi."

 Tangu wakati huo, licha ya majaribio ya kuimarisha sheria za umiliki wa bunduki, miswada (kama ya kupanua uhakiki wa usuli wa mtu) ilishindwa kupita kizuizi cha Seneti (ambacho kinawaruhusu watunga sheria kusitisha au kuzuia upigaji kura kwa mswada), kwani Wanarepublican wengi na baadhi ya Wanademocrat wanaipinga sheria hiyo.

Moja ya sababu za ukosefu huu wa hatua ni ukweli kwamba hakuna msukumo kutoka kwa umma wa Amerika. Kwa kweli, utafiti umeonyesha kwamba, kufuatia matukio ya ufatuliaji risasi wa watu wengi, hamu ya kudumisha "haki yao ya kubeba silaha" inaimarika.

“Katika nyakati za mara kwa mara wakati tahadhari ya taifa inapowekwa kuhusu ufyatuliaji risasi wa watu wengi ndio wakati wenye uwezekano mdogo kwa watu kuweza kufikiria kwa busara kuhusu jinsi ya kudhibiti bunduki. Katika nyakati hizo, wamiliki wa bunduki wanahisi kutishiwa na wanamiminika kwenye maduka ya bunduki kununua bunduki zaidi…”

Utafiti umeonyesha kuwa katika muongo mmoja uliopita kumekuwa na ongezeko kubwa la kitakwimu sawia katika mauzo ... katika miezi mara baada ya kila tukio baya zaidi la ufyatuliaji risasi...

Na katika majimbo yanayounga mkono bunduki, wabunge wa chama cha Republican wakati mwingine wamefuatilia matukio ya ufyatuliaji risasi kwa kulegeza sheria za kumiliki bunduki. (Politico)

And in pro-gun states, Republican lawmakers have sometimes followed mass shooting events with a loosening of gun laws.” (Politico)

Kuzingatia haja ya kubadilisha sheria (kufuatia janga) kwa kawaida ni ya muda mfupi, na haitafsiri kuwa kura za uchaguzi. Wakati wa uchaguzi, umma unazingatia uchumi na huduma za afya, miongoni mwa mambo mengine, na sheria za bunduki hupita katikati ya nyufa.

NRA (Chama cha Kitaifa cha Bunduki) ndicho kitovu cha haya yote

"Baada ya mswada (wa kupekua ukaguzi wa usuli wa watu) kushindwa, aliyekuwa Rais Barack Obama alitoa hotuba kali akilaumu kushindwa kwa Chama cha Kitaifa cha Bunduki, ambacho kilipinga vikali sheria hiyo na kuapa kufanya kampeni dhidi ya seneta yeyote anayeiunga mkono." (Guardian)

NRA ni chama kilichoanzishwa mwaka 1871, na kundi la Maafisa wa Muungano ambao walitaka kuboresha umahiri wa askari wao. Na mwaka wa 1934, walitoa ushahidi wa kuunga mkono sheria ya kwanza ya shirikisho ya bunduki mwaka wa 1934, ambayo ilifanya msako wa bunduki za mashini zilizopendwa na Bonnie na Clyde na wezi wengine wa benki.

“Wakati mbunge alipouliza kama pendekezo hilo lilikiuka Katiba, shahidi wa NRA alijibu, "Sijafanya utafiti wowote kutoka kwa mtazamo huo." Chama hicho kilishawishi kimya kimya dhidi ya kanuni ngumu zaidi, lakini lengo lake kuu lilikuwa uwindaji na uchezaji michezo: kuwinda kulungu, sio kuzuia sheria.” (Chanzo: Brennan Centre)

Lakini mnamo 1977, kufuatia mabadiliko ya uongozi katika shirika hilo, wanaharakati kutoka Wakfu wa Marekebisho ya Pili na Kamati ya Raia ya Haki ya Kuweka na Kubeba Silaha walisukuma njia yao kuingia madarakani. Tangu wakati huo, ushawishi uliweka Marekebisho ya Pili kuwa kotovu cha wasiwasi wake.

Kutabanni Sheria ya Pili ya Marekebisho

Leo, watu huzingatia kifungu maalum ndani ya Marekebisho ya Pili ya Katiba ya Marekani badala ya taarifa nzima, ambayo inasomeka:

"Wanamgambo waliodhibitiwa vyema, ambalo ni muhimu kwa usalama wa Dola huru, haki ya watu kushika na kubeba Silaha, haitakiukwa."

Kuna mijadala mingi inayozunguka upeo wa Marekebisho 'yaliyokusudiwa', kwani mkazo katika sehemu ya mwisho ya kifungu cha ibara "haki ya watu kushika na kubeba Silaha" huunda haki ya mtu binafsi ya kikatiba ya kumiliki silaha, na kuzuia uwezo wa vyombo vya kutunga sheria kupiga marufuku umiliki wa silaha (kwani itakuwa kinyume cha katiba). Ingawa Marekebisho hayo kwa ujumla yanazuia Bunge la Congress kutunga sheria mbali na haki ya nchi kujilinda, hivyo basi kuhakikisha ufanisi wa jeshi.

Hadi kufikia karne ya 21, Katiba ya Marekani haikuwapa watu binafsi haki isiyoweza kushtakika ya kubeba silaha. Kwa kweli, walikuwa na sheria za bunduki.

Walisimamia “kila kitu kuanzia ambapo baruti zingeweza kuhifadhiwa hadi kwa nani angeweza kubeba silaha—na mahakama ziliunga mkono vizuizi hivyo kwa wingi sana. Haki za bunduki na udhibiti wa bunduki zilionekana kwenda sambamba. Mara nne kati ya 1876 na 1939, Mahakama Kuu ya Marekani ilikataa kutoa uamuzi kwamba Marekebisho ya Pili yalilinda umiliki wa mtu binafsi wa bunduki nje ya mazingira ya wanamgambo.”

Hili lilibadilika mwaka wa 2008, wakati Mahakama ya Upeo ilipokagua upya suala hilo katika kesi nyingine na kuchagua kutabanni ufahamu wa wananchi kwamba mtu binafsi ana haki ya kubeba silaha. Walisema kwamba uamuzi wa 1939 ulikuwa wa kipekee, ambapo Wamarekani hawakuruhusiwa kumiliki silaha maalum na walipendekeza kuwa Katiba ya Marekani haitakataza kanuni zinazokataza wahalifu na wagonjwa wa akili kumiliki silaha.

Kando na kuonyesha dosari katika sheria iliyotungwa na mwanadamu, utafiti kuhusu suala hilo umeonyesha jinsi NRA ilifanya kazi nyuma ya pazia kubadilisha mtazamo wa Marekani kwa Haki za Marekebisho ya Pili- katika kila ngazi.

NRA ilianza na elimu na utafiti

Hadi kufikia 1960, vifungu vya marekebisho ya sheria vilihitimisha kuwa Marekebisho ya Pili hayakuhakikisha haki ya mtu binafsi ya bunduki. Mwanafunzi wa sheria William na Mary walizungumza vyenginevyo mwaka wa 1960, akinukuu katika jarida la NRA's American Rifleman. Baada ya hapo, idadi ya mawasilisho ambayo yaliunga mkono hisia hii ilikua; ikisaidiwa na kutiwa moyo na NRA ambao pia walitoa dolari milioni 1 ili kumtawaza Patrick Henry uprofesa katika sheria ya kikatiba na Marekebisho ya Pili katika Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha George Mason.

Yote haya yalikuwa na athari, ambayo ilichuja hadi kwa mashirika ya serikali.

Mnamo 1981, Wanarepublican walichukua udhibiti wa bunge la Seneti la Amerika kwa mara ya kwanza katika miaka 24. Seneta wa Utah Orrin Hatch alikuwa mwenyekiti wa jopo muhimu la Kamati ya Mahakama na akaagiza utafiti kuhusu "Haki ya Kuweka na Kubeba Silaha".

“Yale ambayo Kamati Ndogo ya Katiba ilifichua yalikuwa wazi—na yamepotea kitambo—uthibitisho kwamba marekebisho ya pili ya Katiba yetu yalikusudiwa kama haki ya mtu binafsi ya raia wa Marekani kushika na kubeba silaha kwa njia ya amani, kwa ajili ya kujilinda yeye mwenyewe, familia yake, na uhuru wake.”

Tamko hili lilitanguliwa na tangazo la jukwaa la GOP mnamo 1980, na ridhaa ya kwanza ya rais ya NRA kwa Ronald Reagan.

Jukwaa la GOP lilitangaza kuwa “Tunaamini haki ya raia kushika na kubeba silaha lazima ilindwe. Ipasavyo, tunapinga usajili wa shirikisho wa silaha."

Kisha baadaye mwaka wa 2000, wanaharakati wa bunduki walimuunga mkono sana Gavana George W. Bush wa Texas. Baada ya kuchaguliwa kwake, mwanasheria mkuu mpya, John Ashcroft, aliunga mkono zaidi msimamo huu alipobadilisha msimamo wa Idara ya Sheria, na kuweka wazi kwamba.

"Maandiko na dhamira asilia ya Marekebisho ya Pili yanalinda kwa uwazi haki ya watu binafsi kushika na kubeba silaha."

Hii ni mifano michache tu muhimu inayoonyesha jinsi NRA imeshawishi serikali kuunga mkono ajenda yake. Wamefadhili wabunge, wengi wao wakiwa Republican, kwenye Capitol Hill na katika majumba ya serikali kote Marekani, kwa nia ya kutibua juhudi za kuimarisha sheria za udhibiti wa bunduki.

"NRA inadumisha ushawishi mkubwa, na wa kina mifukoni wa silaha jijini Washington ambao unahusika katika kushinikiza wanachama wa Congress kupinga sheria yoyote ambayo inaweza kuzingatiwa kama kupinga kihafifu bunduki. Katika robo ya kwanza ya 2022, kwa mfano, NRA ilitumia zaidi ya dolari za Kimarekani 600,000 (karibu pauni 500,000) katika ushawishi. Idadi hiyo inatarajiwa tu kuongezeka katika nusu ya pili ya mwaka huu huku uchaguzi wa katikati ya muhula wa 2022 ukikaribia pamoja na madai mapya ya marekebisho ya bunduki na wanaliberali.” (Chanzo: France24)

Na wametumia mamilioni ya dolari kushawishi uchaguzi wa majaji wa Mahakama ya Upeo na wanasheria wakuu kote nchini. Kwa hivyo, NRA ina ushawishi juu ya viti vya maisha kwenye benchi la shirikisho.

"Rekodi za ushuru na faili za kampeni zinaonyesha NRA "imeingiza mamilioni ya dolari kwa kikundi cha mbele ambacho kinatumia pesa zake kuchagua majaji" (Chanzo: NBC)

Zaidi ya hayo, pia wameonyesha msimamo wao juu ya rai jumla.

“Mnamo 1959, kulingana na kura ya maoni ya Gallup, asilimia 60 ya Waamerika walipendelea kupiga marufuku bunduki; hiyo ilishuka hadi asilimia 41 kufikia 1975 na asilimia 24 mwaka 2012. Kufikia mapema 2008, kulingana na Gallup, asilimia 73 ya Waamerika waliamini Marekebisho ya Pili “yalihakikisha haki za Waamerika kumiliki bunduki” nje ya wanamgambo.” (Chanzo: Brennan Center

Ubaguzi huu umewaruhusu kuwaondoa wanasiasa walio madarakani kwenye sanduku la kura.

"Ikiwa Wanarepublican (au Wanademocrat wenye msimamo wa wastani) watayumba juu ya suala la bunduki, NRA - haswa katika kura ya mchujo - itamwaga pesa na rasilimali katika kampeni za wapinzani ambao wanaunga mkono mamlaka ya uzembe zaidi ya bunduki. Hata tishio la changamoto hiyo mara nyingi linatosha kuwatisha wanasiasa wengi dhidi ya kukaidi ajenda ya NRA.” (Chanzo: France24)

Ushahidi huu wa ushawishi wa NRA juu ya sera ya Marekani hauwaondolei wanasiasa au watunzi wa sheria uwajibikiaji wale wanaoumizwa au kuuawa kutokana na ghasia za bunduki nchini Marekani. Inaonyesha tu kiwango cha upotovu ndani ya mfumo, na dosari ndani ya sheria iliyotungwa na mwanadamu.

Hasa, unapozingatia ukweli kwamba sababu ya kuwa Haki ilijumuishwa (pamoja na marekebisho mengine ya Kukazanisha) ni matokeo ya shinikizo la kisiasa.

“Mnamo Juni 8, 1789, James Madison – Mtetezi shupavu wa Shirikisho ambaye alishinda uchaguzi wa Congress baada tu ya kukubali kushinikiza mabadiliko ya Katiba mpya iliyoidhinishwa - alipendekeza marekebisho 17 juu ya mada kuanzia ukubwa wa wilaya za bunge la congress hadi malipo ya bunge hadi haki ya uhuru wa kidini.” (Chanzo: Brennan Center)

Ufisadi ni asili ya mfumo wa Kirasilimali

Ufisadi ni tatizo linalokubalika katika mfumo wa kidemokrasia wa kirasilimali- lengo la wanasiasa ni kuhakikisha kwamba wanasalia madarakani, hata kama hili litafikiwa kwa hasara ya ustawi wa raia.

Wafanyabiashara hujitahidi kutumia dosari hii, wakitumia kiasi kikubwa cha pesa ili kuhakikisha kwamba ni ndani ya maslahi ya mwanasiasa kuunga mkono maslahi ya kampuni yao na kutunga sheria zinazowanufaisha.

Tatizo hili si mahususi kwa washawishi wa kutumia bunduki pekee nchini Marekani- ufisadi upo duniani kote na mifano inaweza kupatikana katika kila sekta. Wote mara kwa mara huweka manufaa ya kimada na faida juu ya ulinzi na mahitaji ya watu.

Wafuasi wa mfumo huu watasema kwamba tunahitaji kuwa wa kidemokrasia zaidi, na hiyo ndiyo itapunguza ufisadi – kamwe haitafanya hivyo. Wanasiasa, na wafanyibiashara wanaofanya kazi ndani ya mfumo huu watarekebisha tu jinsi wanavyofanya kazi, wakipata rai jumla na kuhakikisha kuwa wanaendelea kufaidika kutokana na watu.

Katika Uislamu, makampuni hayatapewa kiwango hiki cha ufikiaji rasilimali za Ummah, au kuwa na uwezo wa kushawishi sheria kwa njia hii. Nguvu na ushawishi wao utakuwa na mipaka, kupitia utabikishaji wa sheria za Mwenyezi Mungu. Hii itatusaidia kuepuka ufisadi ambao ndio asili ya sheria zilizotungwa na mwanadamu, na kuwalinda watu katika kila nyanja ya maisha yao.

Imepokewa kutoka kwa Al-Ghazali: Hatim al-Asamm, Mwenyezi Mungu amrehemu, amesema: “Muumini anaamrisha na anaharamisha kwa ajili ya utawala na anaweka mambo sawa. Mnafiki anaamrisha na anakataza kwa ajili ya madaraka na anasababisha ufisadi.”

(إنَّما الإمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِن ورَائِهِ ويُتَّقَى به، فإنْ أمَرَ بتَقْوَى اللَّهِ وعَدَلَ، فإنَّ له بذلكَ أجْرًا وإنْ قالَ بغَيْرِهِ فإنَّ عليه منه)

“Imam ni ngao watu hupigana nyuma yake na hujilinda kwayo, basi akiamrisha kwa taqwa na akawa mwadilifu hakika ana malipo kwa hilo, na akiamrisha kinyume na hilo basi ni juu yake mwenyewe.” (Muslim)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Fatima Musab

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahri

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu