Afisi ya Habari
Uingereza
H. 27 Dhu al-Qi'dah 1441 | Na: 1441 H / 25 |
M. Jumamosi, 18 Julai 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kesi ya Shamima Begum Inafichua Mfilisiko wa Kifikra Nchini Uingereza
Vyombo vya habari vya Uingereza vimepata ubabaishaji mpya kutokana na hali mbaya ya uchumi wa Uingereza.
Msichana wa shule wa umri wa miaka kumi na tano, Shamima Begum, alipewa mafunzo na wakala wasiojulikana, akasafirishwa hadi Syria, kisha akaolewa na mpiganaji wa kundi la ISIS jijini Baghdad. Yote haya yalitokea bila ya ridhaa ya familia yake au watu wazima walio pambizoni mwake. Baadaye alipatikana na mwanahabari mmoja katika kambi moja ya wakimbizi, hivyo vyombo vya habari vya Uingereza vilikuwa na siku mwanana ya kuitumia kesi yake ili kuchapisha chuki yao iliyo wazi dhidi ya Uislamu na Waislamu, kama ilivyo ada yao. Waziri wa Ndani wa Uingereza Sajid Jayid wakati huo alimvua Uraia wake wa Uingereza katika uamuzi ambao bila shaka ulichochewa kisiasa. Mahakimu wakuu katika Mahakama ya Rufaa wamehukumu kwamba Shamima anaweza kurudi Uingereza kupinga kitendo cha serikali kuwa si cha halali.
Vikiendelea na ada yao ya utoaji ripoti zinazo egemea upande mmoja za habari kuhusu Waislamu, runinga, magazeti na majukwaa ya mtandaoni za mashirika makubwa ya habari zimeangazia umakini wote juu ya ghasia za kundi la ISIS katika jaribio lao dhaifu la kuuzulia uongo Uislamu na Waislamu wote. Kila mmoja anajua kwamba kundi hili haliwakilishi Uislamu wala haliufanyii kazi Uislamu na Waislamu. Washirika na vibaraka wa Kimagharibi hawatajwi ambao ndio waliochochea ghasia nchini Syria ili kulinda serikali ya Assad. Huo ndio unafiki wa watetezi wa mfumo wa kisekula.
Sakata ya Shamima Begum kwa mara nyengine tena inaonyesha kuwa serikali ya Uingereza, vyombo vya habari, na masekula wameshindwa kupambana fikra kwa fikra. Badala yake, wanatumia uongo, upotoshaji, habari zisizo sahihi, ubabaishaji, na uungaji mkono aina zote za serikali na makundi maovu; yote ni kwa ajili ya kumzuia yeyote kupambana na msingi wa uongozi wao wa kirasilimali.
Uislamu kama imani ya kifikra inawakilisha mapambano makali kwa itikadi ya kisekula, ambayo haina ithbati wala msingi, hivyo kuwepo ulegevu wa kujadili fikra dhidi ya fikra. Uislamu kama mfumo kamili wa maisha na mujtamaa, pindi unapotabikishwa katika Khilafah halisi kwa njia Utume, huwakilisha mapambano makali kwa dhulma na mateso ambayo Urasilimali umeleta ulimwenguni. Licha ya hili, daima huwa tunasikia tu mauwaji ya kutengezwa ya wale ambao wametumiwa kutumikia ajenda za Kimagharibi, waziwazi, lakini kikweli kamwe sio kwa jina la Uislamu.
Waislamu nchini Uingereza hawapaswi kuwekwa nyuma kupitia sintofahamu ya Shamima Begum. Dola ya Uingereza waziwazi imemvunja moyo, kama inavyo wavunja moyo mamilioni ya vijana kila siku. Ukoloni wa Kiingereza na wa Kiamerika waziwazi unawavunja moyo watu wa Iraq na Syria, kama ambavyo unavunja moyo sehemu nyingi duniani. Mfumo wa kisekula hauna chochote cha kuupa ulimwengu isipokuwa mateso yanayo halalishwa na uongo.
Yahya Nisbet
Mwakilishi Kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Uingereza
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uingereza |
Address & Website Tel: +44 (0) 7074 192400 www.hizb.org.uk |
E-Mail: media@domainnomeaning.com / press@hizb.org.uk |