Afisi ya Habari
Uingereza
H. 8 Muharram 1442 | Na: 01 / 1442 H |
M. Alhamisi, 27 Agosti 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ripoti Mpya: Kuzama kwa Kina - Ulimwengu Baada ya COVID-19
Hizb ut Tahrir / Uingereza imetoa ripoti kwa anwani "Kuzama kwa Kina - Ulimwengu Baada ya COVID-19", ambayo inanakili kufeli kwa ulimwengu wa Kirasilimali kulikabili kwa ufanisi janga la maambukizi la kiulimwengu. Ripoti hii inaonyesha jinsi gani kasoro za utaratibu wa mfumo wa kirasilimali zinafanya kufeli huko kuwa ni jambo lisilo na budi, huku nidhamu yake ya kidemokrasia imehakikisha kuwa serikali za leo zinatumikia kipote cha watu wachache cha asilimia moja pekee.
Ripoti hii inatamatisha kuwa mfumo wa kiliberali wenye kuangazia watu binafsi na uhuru wao umekuwa mzuri kwa wachache lakini wenye mateso kwa waliobakia. Urasilimali na demokrasia zimefeli vibaya mno, tena na tena. Nidhamu hii ambayo watetezi wake wanasema kuwa ni nzuri kwa wengi, kiuhalisia ni nzuri kwa wachache pekee. Fikra za kisiasa kutoka kwa uliberali zimeundwa kwa ajili ya matajiri na zinawadharau pakubwa masikini. Baadhi wanaendelea kuutetea Urasilimali, lakini baadhi ya wafasiri
Baadhi ya wachambuzi hawaelezi tena hoja za jinsi Urasilimali ulivyo mkuu bali wanautetea kuwa ndio mfumo bora ulioko kwa sasa. Muktadha wa kisiasa kote duniani ni ule wa kutojali na kukata tamaa, bila ya kuzingatia aina ya serikali ambayo watu wanaishi chini yake; ima ya kidemokrasia, ya kidikteta au watawala waliozuka, hamu ya mabadiliko imejaa nyoyoni mwa watu wote bila ya kuzingatia rangi au dini. Licha ya Urasilimali kueneza uongozi wake kote duniani, mfadhaiko wa watu unakua kwa haraka kuliko uongozi wake. Hamu ya mabadiliko itaongezeka pindi hali ya kiuchumi ikizidi kuwa mbaya duniani na gharama msingi ya maisha kwa wengi zaidi ikishindwa kumudiwa.
Katika mazingira haya ya mabadiliko, ni wajibu wetu kama Waislamu kuchukua fursa hii na kutoa mtazamo badali kwa walimwengu. Mwenyezi Mungu Muumba wa Dunia na mfumo wake wa ikolojia uliounganishwa. Kwa Rehma Zake Zisizo na Mwisho, alitupa sisi wanadamu Uislamu ulio na masuluhisho ya kina na makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kimazingira ambayo yanawiana na sayari yote iliyo salia. Ni jukumu letu kama Ummah wa Kiislamu kuchukua hatua na kufanya kazi kusimamisha uongozi wa Kiislamu duniani huku ulimwengu wa Kiislamu ukiwa kama nukta kianzilishi kupitia kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume.
Ili kuisoma ripoti hii kwa ukamilifu tafadhali zuru:
http://www.hizb.org.uk/wp-content/uploads/2020/08/Deep-Dive-The-World-After-COVID-19.pdf
Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uingereza |
Address & Website Tel: +44 (0) 7074 192400 www.hizb.org.uk |
E-Mail: media@domainnomeaning.com / press@hizb.org.uk |