Afisi ya Habari
Tanzania
H. 6 Ramadan 1445 | Na: 1445 / 05 |
M. Jumamosi, 16 Machi 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kampeni ya Ramadhan ndani ya Tanzania
(Imetafsiriwa)
Jana Ijumaa 05 Ramadhan 1445 H / 15 Machi 2024 M wanaharakati wa Hizb ut Tahrir Tanzania katika baadhi ya maeneo walifanya Kampeni Maalum ya Ramadhan chini ya kauli mbiu ya ‘Ramadhan ni Kielelezo cha Umoja wa Ummah’
Maandamano baridi yalifanywa katika jiji la Dar es Salaam na Zanzibar, ambapo ndani ya Dar es Salaam yalifanyika nje ya Masjid Dar us Salaam, Kigamboni, pia yalifanyika nje ya Masjid Idrissa, Kariakoo. Kwa Zanzibar maandamano baridi yalifanyika eneo la wazi karibu na Soko la Darajani.
Kampeni ilifafanua bayana kwamba mwezi wa Ramadhan unawasilisha umoja wa Ummah wa Kiislamu kuwa kitu kimoja, wenye shakhsiya moja, pia wenye muongozo mmoja, ambapo kutokana na muongozo huo ndio imepatikana amri hiyo ya Swaumu ya Ramadhan.
Hata hivyo kampeni hiyo iliwahadharisha Waislamu kwamba umoja wa Kiislamu haupaswi kujifunga katika masuala ya ibada za kiroho tu, bali lazima umoja huo utanuke kwa upana hadi kuwa ni umoja wa kisiasa chini ya dola ya kilimwengu ya Khilafah ambayo itasimamia mambo ya Waislamu.
Kuweza kuufikia umoja wa aina hiyo (wa kisiasa) kampeni imewahamasisha Waislamu kushiriki kikamilifu katika jukumu la kurejesha tena dola ya Khilafah kwa Njia ya Utume inayopaswa kuanzia katika ulimwengu wa Kiislamu. Kwa dola hiyo umoja wa kweli wa kisiasa utafikiwa na utaweza kuhifadhiwa.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
https://domainnomeaning.com/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/tanzania/3835.html#sigProId384d1a1975
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |