Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  28 Safar 1445 Na: 03 / 1445 H
M.  Jumatano, 13 Septemba 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Nyufa na Mizozo Katika Kuchagua Rais Mpya wa Muungano wa Kutengenezwa wa Upinzani

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 12/9/2023, Baraza Kuu la Muungano unaoitwa Muungano wa Upinzani ulimchagua Hadi Al-Bahra kuwa rais wake mpya. sintofahamu hizo zilikuwa zimefikia kilele chake hata kabla ya kuchaguliwa Hadi Al-Bahra, kiasi kwamba baadhi walitangaza kuwa muungano huo umekufa.

Kwa watu wanyoofu katika ardhi ya Ash-Sham: Muungano wa Upinzani si chochote ila ni chombo kilichobuniwa kisiasa, chini ya macho ya mashirika mbalimbali ya kijasusi na waungaji mkono wao. Madhumuni yake ni kuunda uongozi wa kisiasa kwa ajili ya vikosi vya mapinduzi kama chombo cha kutekeleza njama za kisiasa dhidi ya Mapinduzi ya Ash-Sham.

Baadhi ya wanachama wake walichaguliwa kushiriki katika Mapinduzi ya Ash-Sham na walichangia kuyarudisha nyuma kwake baada ya kufika karibu na Damascus. Kutoka miongoni mwao, ujumbe ulichaguliwa kujadili baadhi ya marekebisho ya juu juu ya katiba huku wakidumisha hali ya kisekula ya dola na kuibakisha dini kutengana na dola, bila kujali matakwa ya watu wa Ash-Sham na kanuni za mapinduzi yao, ambayo yanatoa wito wa kupinduliwa kwa utawala wa kihalifu na kusimamisha utawala wa Kiislamu mahali pake.

Na sintofahamu hizo ndani ya chombo hiki kilichobuniwa si chochote ila ni mapambano ya zana kwa ajili ya maslahi na manufaa ya kibinafsi. Ni mashindano tu kati ya mabwana kwa ajili ya watumishi kuwatumikia na kutumikia maslahi ya dola zinazo kula njama dhidi ya Mapinduzi ya Ash-Sham. Wanatafuta kuyamaliza kupitia suluhisho la kisiasa la Marekani na utekelezaji wa masharti ya Azimio la Umoja wa Mataifa 2254. Muungano huu na wanachama wake hawana uhusiano wowote na mapinduzi, kanuni zake, au malengo ya kweli ya vijana na binti zake. Wamesahau kuwa wao ni zana za muda zinazotumiwa na dola zinazo kula njama na wanaweza kubadilishwa kulingana na mahitaji ya jukwaa, wakitupwa jalalani kwa njia tofauti tofauti.

Enyi Wanamapinduzi Wanyoofu katika ardhi ya Ash-Sham: Kujitolea mhanga kwenu kukubwa mlikojitolea na mashujaa wakubwa mliowanakili katika miaka mingi ya mapinduzi kunahitaji uongozi wa kweli wa kisiasa kutoka kwa ndugu na watoto wenu, uongozi unaotokana na imani yenu: “La illah illa Allah, Muhammad Rasuul Allah.” Uongozi unaofanya kazi ya kumridhisha Mwenyezi Mungu pekee, ukisonga mbele kwa busara ili kuregesha udhibiti wa hatma ya mapinduzi yetu. Tunatembea pamoja kwa imani thabiti, tukimtegemea Mwenyezi Mungu peke yake, tukiendeleza mapinduzi yetu hadi tufikie misingi yake, mkubwa  zaidi ni kupinduliwa kwa utawala wa kihalifu, katiba yake, nguzo zake zote na nembo zake, na kusimamisha utawala wa Kiislamu mahali pake. Ushindi huu hautapatikana kwa wale wanaosalimisha maamuzi yetu kwa maadui wa mapinduzi yetu, wakijiingiza katika mipango yao. Badala yake, ushindi wetu utapatikana kwa wenye ikhlasi na wanaofahamu miongoni mwa watoto wetu wa kiume na wa kike wanaoamini kwamba ushindi upo mikononi mwa Mwenyezi Mungu pekee na utashuka tu juu ya mikono na nyoyo safi zilizoshikamana na Mwenyezi Mungu peke yake, kwa imani kamili kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na bishara njema za Mtume wake (saw) kwa yakini zitatimia.

Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[وَعَدَ اللهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [Surat An-Nur:55].    

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu