Alhamisi, 14 Sha'aban 1446 | 2025/02/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  10 Sha'aban 1446 Na: HTS 1446 / 47
M.  Jumapili, 09 Februari 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Al-Burhan Anatafuta Kuiga Mfumo Ule Ule wa Kisekula Uliopita
(Imetafsiriwa)

[أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٍ مَرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُونَ]

Je! Hawaoni ya kwamba wanatiwa mtihanini kila mwaka mara moja au mara mbili? Kisha hawatubu, wala hawakumbuki?” [At-Tawba:126].

Katika hotuba iliyotolewa leo na Jenerali Al-Burhan, Mwenyekiti wa Baraza la Utawala na Amiri Jeshi Mkuu, alisema: "Kipindi kijacho kitashuhudia kuundwa kwa serikali ili kukamilisha kazi za mpito. Inaweza kuitwa serikali ya muda. Baada ya kuidhinishwa kwa waraka wa katiba, serikali itaundwa, na waziri mkuu atachaguliwa kutekeleza majukumu yake katika kusimamia baraza la mawaziri la serikali bila kuingiliwa."

Ni wazi kutokana na hotuba hii kwamba Al-Burhan anatafuta kuiga mfumo ule ule wa awali wa kisekula kwa watu mpya. Huu ndio mfumo ule ule ambao ulikuwa sababu ya vita hivi, ambavyo vimeangamiza watu na rasilimali.

Sio yeye wala nguvu za kisiasa zinazomuunga mkono hazijapata somo lolote, kwani wanaendelea kuzalisha tena chanzo kile kile cha vita hivi—kutelekeza hukmu ya Mwenyezi Mungu, kujifungamanisha na madhalimu, na kutekeleza mifumo ya mkoloni kafiri Magharibi, ambayo msingi wake ni kutenganisha dini na maisha na, kutokana na hayo, kuitenganisha na siasa na utawala. Badala yake, wanahukumu kwa mujibu wa matamanio ya watu, bila kujali maamrisho ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ya kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha bila ya kuacha hata moja. Mwenyezi Mungu asema:

[وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَاءهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللهُ إِلَيْكَ]

Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu.” [Al-Ma'ida:49].

Utawala katika Uislamu ni Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume na hivi ndivyo alivyothibitisha Mtume (saw) aliposema:

«كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمْ الْأَنْبِيَاءُ كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ، وَإِنَّهُ لَا نَبِيَّ بَعْدِي، وَسَتَكُونُ خُلَفَاءُ تَكْثُرُ...»

Walikuwa Banu Isra'il wanasiasa wao ni Mitume. Kila mtume mmoja alipofariki, alikuja mtume mwengine, na hakika yake hakutakuwa na mtume mwengine baada yangu. Kutakuweko na makhalifa, na watakuwa wengi.”

Kama Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, na kwa moyo wa ushauri wa kweli na kujiondolea lawama mbele ya Mwenyezi Mungu, tunawasilisha kwa Al-Burhan hasa, na kwa nguvu zote za kisiasa na Waislamu kwa jumla, Rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah. Katiba hii imeegemezwa juu ya wahyi wa Mwenyezi Mungu—Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume Wake (saw)—pamoja na yale waliyoyaongoza, kama vile ijma ya Maswahaba na mlinganisho (qiyas) wenye hoja halali ya Shariah. Kifungu cha kwanza cha katiba hii kinasema: "Aqidah ya Kiislamu ndio msingi wa dola, kiasi kwamba hakuna chochote kinachoweza kuwepo ndani ya muundo wake, taasisi, mifumo ya uwajibikaji, au lolote la mambo yake isipokuwa iwe msingi wake ni Aqidah ya Kiislamu. Wakati huo huo, ndio msingi wa katiba na hukmu zote za Shariah, kiasi kwamba hakuna chochote kinachohusiana nazo kinaruhusiwa isipokuwa kitoke kwenye Aqidah ya Kiislamu."

Badala ya hati ya kikatiba inayoongozwa na matamanio ya wanadamu, tunawasilisha katiba ambayo chanzo chake ni wahyi kutoka kwa Mwenye hekima, Mjuzi wa yote.

Katiba hii tukufu inaainisha mifumo ya utawala na idara kama ilivyoelezwa na kutekelezwa na Mtume (saw) na kufuatiwa na Khulafa ar-Rashideen (Makhalifa Waongofu). Mtume (saw) alituusia kushikamana na njia yao, akisema:

«فَإِنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيَرَى اخْتِلَافاً كَثِيراً، فَعَلَيْكُمْ بِسُنَّتِي، وَسُنَّةِ الْخُلَفَاءِ الرَّاشِدِينَ الْمَهْدِيِّينَ عَضُّوا عَلَيْهَا بِالنَّوَاجِذِ»

“Hakika mwenye kuishi muda mrefu ataona fitna kubwa miongoni mwenu, basi shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Khulafa ar-Rashidin (makhalifa walioongoka), wale wanaoongoa kwenye njia iliyonyooka. Shikamana nazo kwa nguvu [kihalisi: kwa meno yako ya majego].”

Katika haya yamo maisha ya Ummah, na katika kitu chengine chochote kile, umo uharibifu wake.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ]

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal:24].

Linki ya Rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah:

Sehemu ya 1: https://www.domainnomeaning.com/en/index.php/latest-articles/2122.html

Sehemu ya 2: https://www.domainnomeaning.com/en/index.php/latest-articles/2123.html

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu