Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 8 Sha'aban 1446 | Na: HTS 1446 / 46 |
M. Ijumaa, 07 Februari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Watu wa Sudan, Komesheni Mambo Matatu ya Marekani ambayo Yanahusisha Uhalifu Mkali: Vita, Kuitenga Darfur, na Uhalalishaji Mahusiano na Umbile la Kiyahudi
(Imetafsiriwa)
Kila mtu anashangaa juu ya siri iliyoko nyuma ya kuongezeka kwa kasi hii katika operesheni za kijeshi za jeshi hivi karibuni, kama vile vita vilivyokuwa hapo awali, na kwa zaidi ya mwaka mmoja, vimekuwa vikifanyika ndani ya duara lililofungwa, huku kukiwa na kusonga mbele na kurudi nyuma, bila ya kuwepo na uamuzi wa kijeshi kutoka upande wowote.
Ili kujibu hilo, tunasema yafuatayo:
Kwanza: Jeshi lilianza kukomesha sera ya subira ya kimkakati na ya muda mrefu, bila kusababisha ukosefu mkubwa wa usawa katika mizani ya kijeshi. Tangu mwanzo wa vita, lilikuwa na uwezo wa kuamua na halikufanya hivyo.
Pili: Vikosi vya Msaada wa Haraka vinapata hasara huko Al-Jazeera na Khartoum, lakini vinaondoka kuelekea Darfur, ambako wanadhibiti majimbo manne, huku jeshi likiwafungulia njia kuelekea Darfur, badala ya kuwalazimisha kujisalimisha. Hili pia linathibitisha kuwa mambo yanasimamiwa kwa njia fulani, na kwamba nyuma ya hatua hii ni pande zinazosimamia mandhari hii kwa niaba yao.
Hakuna shaka kwamba hili linasababisha mgawanyiko halisi wa nchi! Vikosi vya Msaada wa Haraka vinadhibiti Darfur yote isipokuwa Al-Fasher, na sasa wanajipanga baada ya kuondoka kutoka Sudan ya kati, na kuelekea Darfur.
Haya yote yanasadifiana na kuwasili kwa Trump katika ikulu ya White House, jambo ambalo linachukua mtazamo mpya; anataka vita vya Sudan viishe kwa jeshi kudhibiti Sudan ya kati, kaskazini na mashariki, na kuacha eneo la Darfur upande wa magharibi kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka. Hii ina maana kwamba kwa sera hii, anataka kushinikiza serikali kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi. Uhalalishaji huu wa mahusiano ulianzishwa na Burhan wakati wa urais wake uliopita. Kinachothibitisha hayo ni kile Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Ali Youssef, alichofichua kuhusu kuwepo kwa ruwaza na programu za kuhakiki sera ya Marekani nchini Sudan baada ya utawala mpya kuchukua madaraka. (Gazeti la Al-Sharq, 23/1/2025) Kisha kukawa na mkutano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, ambao walijadili kuhusu maendeleo ya Sudan, ambapo walisisitiza haja ya kushinikiza pande zinazozozana kukomesha uhasama na kupanua wigo wa misaada ya kibinadamu (Sudan News, 25/1/2025). Kwa hivyo, ni wazi kabisa kwamba Trump anataka Sudan kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi, na anataka Darfur itenganishwe kama Sudan Kusini ilivyotenganishwa, na vita hivi vya dhambi ni jambo la tatu ya mambo matatu ya uhalifu ambavyo Amerika inayachochea ili kuharibu muundo wa makubaliano na kuwaondoa vibaraka wa Ulaya kutoka uwanja wa kisiasa nchini Sudan.
Kila mtu lazima afanye kazi kukomesha machafuko haya ya Amerika katika nchi yetu, na atambue uhalifu huu. Nchi hii inapaswa kuwa na jeshi moja, linaloelekeza silaha zake dhidi ya adui; makafiri wakoloni, na katika hilo kuna ushindi na wokovu duniani na mafanikio kesho Akhera.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |