Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 29 Rajab 1444 | Na: HTS 1444 / 35 |
M. Jumatatu, 20 Februari 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan Wakutana na Mkurugenzi wa Vipindi katika Televisheni ya Taifa (Omdurman)
(Imetafsiriwa)
Katika muendelezo wa mikutano ya wajumbe wa Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan na viongozi wa serikali, na ndani ya wigo wa kampeni ya hizb ya kupambana na mihadarati, ujumbe kutoka hizb, ukiongozwa na Ustadh Muhammad Jami (Abu Ayman)- Msaidizi wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, akiandamana na ndugu wawili, Ustadh Abd Al-Khaleq Abdoun na Ustadh Ibrahim Musharraf - Wanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, walikutana na Ustadh Al-Nour Maana - Mkurugenzi wa Vipindi katika Televisheni ya Taifa ya Sudan (Omdurman), mbele ya uwepo wa Mkurugenzi wa Vipindi vya Michezo, na Mkurugenzi wa Kipindi cha Asubuhi.
Abu Ayman aliwasilisha maelezo ya kampeni inayofanywa na Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan ya kupambana na mihadarati, ambayo iliizindua katika Shirika la Habari la Sudan (SUNA) mnamo tarehe 22/1/2023. Kampeni hiyo ilifanywa katika miji mingi ya Sudan; katika viwanja vya umma, vilabu, masokoni, shuleni na misikitini. Watu wa Sudan waliingiliana na kampeni hii na kuisifu. Hayo ikiwa ni pamoja na ziara na mikutano ya wajumbe wa Hizb kwa wanasiasa, wanahabari, wataalamu na wengineo, ambapo walieleza mtazamo wa hizb kuhusu suala la dawa za kulevya, na kwamba hiyo ni njia mojawapo ya vita vya kisasa, ambavyo kupitia kwavyo vinakusudiwa kuwaangamiza vijana wa Sudan, na kwamba vita hivi vinahitaji dola ya kimfumo ili kukabiliana navyo. Dola hii ni Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo umejengwa juu ya Aqidah ya Ummah, na ndio maana kauli mbiu ya kampeni hiyo ilikuwa “Mihadarati ni Vita, kwa Khilafah Tunashinda”.
Mkurugenzi wa Vipindi na wasaidizi wake walieleza kupendezwa kwao na kampeni hiyo, na kuisifu hizb kwa kutabanni kwake suala hili muhimu, na kusisitiza utayari wao kamili wa kushirikiana na Hizb ut Tahrir kufanikisha kampeni hii ili kulinda nchi na watu wake dhidi ya hatari zake.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
https://domainnomeaning.com/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/sudan/3106.html#sigProId6a852fac16
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: |