Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  19 Dhu al-Hijjah 1444 Na: BN/S 1444 / 18
M.  Ijumaa, 07 Julai 2023

 Barua ya Wazi
Kwa Wanahabari na Vyombo vya Habari vya Ndani na vya Kiarabu
(Imetafsiriwa)

Wakurugenzi wa idhaa za satelaiti za Kiarabu zinazofanya kazi katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

Mameneja wa idhaa za ndani katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

Wakurugenzi wa tovuti za habari kwenye Wavuti wa Kilimwengu na mitandao ya kijamii

Wahariri wakuu wa idhaa za ndani na tovuti za habari

Waandishi wa habari wa vyombo vya habari wanaofanya kazi katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

Baada ya Salamu:

Tunakuhutubieni kwa hotuba hii, tukimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu azifungue nyoyo zenu kwa wema na hekima iliyokuja ndani yake, tukitumai kwamba mtaegemea upande wa Ummah wenu na kadhia zake, na muzieleze kadhia zake kwa njia ya inayotumikia umoja na mwamko wake na kupambana na maadui zake. Na kadhia ya Palestina ni jiwe kuu katika kadhia za Waislamu, na tunadhania kwamba munajua kwamba kadhia ya Palestina haina ufumbuzi isipokuwa kwa kuikomboa kikamilifu. Wale walio mbali na karibu wanajua kikamilifu kwamba kile kinachozuia kukombolewa kwake na kinachozuia Umma wa Kiislamu na majeshi yake kutokana na jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ili kuling'oa umbile la Kiyahudi kutoka kwenye mizizi yake ambayo ni watawala na tawala zinazotumishwa na Marekani na Uingereza. Kadhalika, si siri kutokana na ufuatiliaji wa vyombo vyenu vya habari ukubwa wa njama dhidi ya kadhia ya Palestina, na hatua hizo zilikusudia kuitenganisha na Uislamu na Umma wa Kiislamu na kuifanya iwe tegemezi kwa maazimio ya kimataifa na mipango ya kieneo inayoendeleza uvamizi huo na kulihifadhi umbile la Kiyahudi.

Waheshimiwa Ndugu na Dada:

Hapana shaka kwamba suluhisho pekee la kweli na la kivitendo kwa kadhia ya Palestina ni harakati ya Umma na vikosi vyake vya kijeshi ili kuikomboa Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa na kuzitakasa kutokana na najisi ya Mayahudi. Na kwamba mazungumzo yoyote ya masuluhisho mengine ni kurefusha uhai ya ukaliaji kimabavu na kudogosha kwa kufifisha sababu, na kuendeleza masuluhisho ya kufedhehesha ya kusalimu amri, na Magharibi na watu wake na vinywa vyake wanafanya kila juhudi kuwezesha ukaliaji kimabavu katika ardhi hii na kuwapigisha magoti watu wa Palestina mbele ya kiburi chake. Wanafanya kazi kwa bidii ili kuzuia kuwasili kwa sauti au wito wowote unaozungumzia suluhisho la kweli la kadhia ya Palestina, na wanataka vyombo vya habari viwe sauti na jukwaa la kila mzushi na kibaraka, anayezungumza lugha ya Magharibi na istilahi zake chafu, na kushughulika na zana za kujisalimisha na kupuuza kama vile uingiliaji kati wa kimataifa, Baraza la Usalama na vikosi vya kimataifa, na kulikuza kana kwamba ni dawa ya uponyaji kwa watu wa Palestina, na badali yake wanataka vyombo vya habari kuzuia kila sauti inayovuruga amani ya miradi yao au kuharibu mipango yao.

Waheshimiwa Ndugu na Dada:

Tumegundua hofu yenu ya kuficha amali zetu ambazo kwazo tunaulingania Umma wa Kiislamu na majeshi yake kuikomboa Al-Quds, na tunaona kwamba munaogopa kuzungumzia kuhusu majeshi ya Waislamu na wajibu wao wa kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa, na hatuwaoni mukitoa mwanga juu ya wajibu wao na uwezo wao wa kukomboa. Kwa hivyo kwa nini musifanye kazi kuangazia jukumu lake kwenye vyombo vya habari au kuifanya iwe mada ya mazungumzo na majadiliano kwenye majukwaa yenu?! Je, sio jukumu lenu kueneza ufahamu miongoni mwa watu na kufichua ukweli?! Je, kuna ukweli ulio wazi zaidi kuliko umakinifu wa dola kuu juu ya umbile nyakuzi la Kiyahudi na kuutumia kwa nchi za kieneo ili kulihifadhi na kuwakuuza watu kuishi pamoja nalo kama umbile la kiasili?

Inatuumiza sana kwamba vyombo kadhaa vya habari havikuandika amali zetu za hadhara zilizofanywa huko Ramallah, Al-Khalil (Hebron), na Qalqilya zikitoa wito kwa majeshi ya Ummah kuchukua hatua za haraka za kuinusuru Jenin na kuikomboa Palestina. Je, majukwaa yake hayakuweza kupokea sauti yoyote inayoelekeza dira kwenye suluhisho sahihi la ukombozi na wokovu kutokana na uvamizi na uhalifu wake?!

Wapendwa Waandishi wa Habari:

Nyinyi ni sehemu ya Ummah huu na nyinyi ni watoto wake, na mafungamano yenu pekee ni lazima yawe pamoja na Ummah wenu na kadhia zake, na wajibu wenu ni kufikisha kila minong'ono au sauti inayotangaza haki na kutia dawa kwenye kidonda, na kuzika kila tarumbeta au kibaraka anayeendeleza miradi ya kikoloni na kudumu kwa uvamizi huo kwa maneno na misemo mizuri iliyojaa sumu na usaliti.

Jueni kuwa mustakabali ni wa Umma na Uislamu, na kwamba ukoloni unahesabu siku zake za mwisho, hata kama utadai kinyume chake, na utaondoka pamaoj nao mamluki, vibaraka na wafuasi wote kwenda “alipoitupa Umm Qashem” [Motoni pamoja nao], basi iangalieni njia ya mwamko wa Umma kama walivyoiona wengi, na shikaneni na Ummah wenu na wale walio na ikhlasi ndani yake, kwani huu ndiyo haki, basi, baada ya haki ni udanganyifu tu.

Tunakuwekeeni link zile za amali hizo zinazozungumzia utatuzi na kueleza msimamo wa Umma na watu wa Palestina, tukitumai kwamba mutaegemea upande wa Ummah wenu na kutekeleza wajibu wenu wa kuueneza na kuutangaza, na Mwenyezi Mungu akulipeni kwa malipo bora.

-     https://www.youtube.com/watch؟v=GHnFhw38R9o

-     https://www.youtube.com/watch؟v=83FV9CwefSo

-     https://www.youtube.com/watch؟v=emHbuEeC76g

-     https://pal-tahrir.info/hizb-events2/13715

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu