Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  27 Shawwal 1444 Na: BN/S 1444 / 16
M.  Jumatano, 17 Mei 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuhuisha Sheria ya Hifadhi ya Jamii ni Uhalifu na Kunyima Riziki ya Watu na Mfereji Mpya Ulioongezwa na Mamlaka ya Palestina Kushambulia Ukakamavu na Uchumi wao
(Imetafsiriwa)

Kwa ujanja na hila, siku hizi Mamlaka ya Palestina (PA) inatafuta kufufua Sheria maarufu ya Hifadhi ya Jamii, ambayo watu walisimama imara dhidi yake miaka iliyopita, kukataa kushambuliwa kwa mali zao, matunda ya juhudi zao na riziki zao kwa kisingizio cha "kuwadhamini!" Leo, inafanya kazi ya kurudia yaleyale kwa mara nyingine tena kwa marekebisho rasmi ambayo hayabadilishi dhati ya sura ya awali au athari zake mbaya isipokuwa kwa kuificha, ili watu wapate janga jipya katika uchumi kwa kile kinachojulikana kama sheria ya Hifadhi ya Jamii.

Ama hili kuwa ni balaa jipya lililoongezwa na PA, hii ni kwa sababu kile watu watakachohisi kutokana na utekelezwaji wa sheria hii si chochote bali madhara yake ya kiuchumi, na hasara ni zaidi ya faida, kwani hakuna manufaa. Hii ni kwa sababu kwanza mishahara ya sasa haitoshi kwa wamiliki wake hata kabla ya kukatwa, vipi basi wanapokatwa kwenye mishahara, hasa kwa kuzingatia mmomonyoko mkubwa wa mishahara kutokana na bei za juu. Kwa upande wa masoko, kukatwa fedha za mishahara na kuzitoa kwenye mzunguko wa matumizi kutaongeza mdororo hasa kwa yale yanayojiri katika suala zima la ukosefu wa fedha na kupunguzwa kwa mishahara na PA na utendaji mbovu kwa kuzingatia kuzingirwa na umbile la Kiyahudi. Ama kuhusu biashara, maslahi, na taasisi ambazo pia zinakabiliwa na shida ya soko, matumizi ya sheria hiyo yatawaongezea tu mizigo na gharama, na gharama hizi za ziada hazitapata njia kwao isipokuwa kuongezwa kwenye bei ya bidhaa na huduma zinazotolewa kwa watu, hivyo kuongeza bei kwa gharama kubwa zaidi, vyenginevyo nyingi zao zitafungiwa au kutoroka kutoka kwa mazingira ambayo hufukuza uwekezaji na kutouzalisha.

Hivyo basi, kuletwa upya kwa Sheria ya Hifadhi ni hatari kwa watu, na unyonyaji mpya juu ya kile ambacho watu wa Ardhi Iliyobarikiwa wanakabiliwa nacho cha kuzingirwa na uchovu, kana kwamba hali ya kuzorota kwa uchumi ambayo watu wako ndani yake inakusudiwa kuongezwa kina chake kuwafanya watu kuishi katika ugumu wa maisha na kuwazuia wasifikirie juu ya ardhi yao inayokaliwa kwa mabavu na Aqsa yao inayo najisiwa.

Kuhusu mambo mengine, hazina hii haina mdhamini halisi, na hiki ndicho kiini cha msiba. PA sio dhamana, wala haiko katika utendaji wake wala katika historia yake iliyojaa ufisadi, bali hata katika uhai wake, mbali na kuwa mdhamini, na fedha za Mfuko wa Kitaifa wa Palestina, Mfuko wa Pensheni, na Mfuko wa Hospitali ya Al-Hasan kwa ajili ya Saratani na "Msimamo kwa ajili Izza" ni ncha tu ya mlima wa barafu na mifano ya hatima ya fedha zinazokusanywa na hatima yao. Hakika, uzoefu wa fedha za dhamana hata kati ya wale ambao wana uzoefu zaidi kuliko mamlaka, kama vile Jordan, kwa mfano, na nchi nyingine za Kiarabu zinaonyesha kuwa wao ni mazalia ya ufisadi, na uwanja wa hasara za fedha za watu na kutojitosheleza. Ama kuhusu suala la kuwekeza fedha za mfuko, historia ya uwekezaji huo mara nyingi husababisha kufilisika, madeni, na wizi unaofanywa na mamlaka, juu ya kuwa ni uwekezaji ambao hauwezi kumilikiwa au kuingizwa katika uwekezaji wa kigeni ambao kwao uchumi wa ndani haunufaiki kwa namna yoyote ile.

Madhumuni ya fedha kama hizo sio kuwalinda wafanyikazi au waajiri au kuwawekea watu maisha yenye staha, kwani mamlaka hiyo iko mbali na hilo. Bali, jambo sio lolote zaidi ya jaribio la Mamlaka ya Palestina kutaka kutwaa rasilimali mpya ili kujifadhili yenyewe, kwani haina vipengele vya kudumu na haina vyanzo isipokuwa mifuko ya watu, na pia inafadhili kutokuwa na uwezo wa kutumia katika mradi wake uliofeli unaotumia rasilimali, mradi huo ambao kiini na kazi yake haikuwa ila ni ulinzi wa umbile la Kiyahudi na usalama wake, na hapo ndipo huduma za usalama zilipopandishwa bei kwa ajili hiyo, hivyo hazina zikafilisika na kutumia kila kitu, na sasa wanataka kufanya makato kutoka kwenye mishahara ya wafanyikazi kugharamia hayo yote, na kauli mbiu za dhamana si chochote ila ni udanganyifu na kutia vumbi machoni, kana kwamba wao, kama mamlaka iliyo chini ya uvamizi, wana amri yao au wanaweza kudhamini hata kitu kimoja.

Mamlaka ya Palestina imezoea kufinika sheria zake kwa kupitisha kile kinachoitwa amri kwa sheria, na kwa hivyo, kwa mwandiko wa kalamu kwa "uamuzi wa sheria", ilijihalalishia yenyewe wizi wa pesa za watu na kuzihatarisha au kuzila bila haki, na kwa njia hii ni ya kwanza kutoa sababu ya "ukosefu wa dhamana" kwa fedha hizi kwa mwandiko wa kalamu yenyewe pia kwa mabadiliko katika sheria au marekebisho. Kwa hiyo, ilikuwa ni lazima kwa watu, na hali na vilevile wale wanaochezea pesa zao na kuguguna ukakamavu wao, wasimame dhidi ya mamlaka hii na sheria zake, zinazowapeleka kutoka mporomoko mmoja hadi mwingine, na kutoka kwenye hatari moja hadi nyingine, na kuzidisha matesso yao juu ya utawala wa umbile la Kiyahudi.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu