Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  23 Jumada I 1443 Na: BN/S 1443 / 05
M.  Jumatano, 08 Disemba 2021

 Tanzia ya Aliyekuwa Imamu wa Msikiti wa Ibrahim, Mmoja wa Wanachama wa Hizb ut Tahrir

 (مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُواْ مَا عَاهَدُواْ اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبْدِيلاً)

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab: 23]
(Imetafsiriwa)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina inamuomboleza aliyekuwa Imam wa Msikiti wa Ibrahimi, mmoja wa wanachama wema wa Hizb ut Tahrir, Hajj Salih Abdul-Jawad Al-Razem (Abu Dhia), aliyefariki mnamo Jumatano alasiri, 8/12/2021, baada ya kuvumilia kwa subra maradhi yaliyomsababishia maumivu na kupooza, na twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kuwa itakuwa ni kafara kwake siku ambayo haitafaa mali wala watoto.

Sheikh alijulikana kwa tabia yake nzuri, mazungumzo na majadiliano ya ufasaha, na kwa mapenzi yake kwa Dawah na kujitolea kwa ajili yake. Uzee wala maradhi hayakumvunja moyo kuendelea kuamrisha mema na kukataza maovu. Alikuwa na misimamo inayojulikana sana katika kukabiliana na maadui wa Ummah na makubaliano ya hila ya CEDAW, na alikuwa jasiri katika kutabanni kadhia za Ummah; alitetea wakfu wa swahaba mtukufu Tamim bin Aws al-Dari, na akasimama upande wa wafanyakazi katika kutetea pesa zao na kuzuia wizi wake kwa jina la Sheria (ya Usalama wa Jamii). Na yeye, Mwenyezi Mungu (swt) amrehemu, alikuwa Imam wa zamani wa Msikiti wa Ibrahimi, alioupenda, na kuupenda mji mkongwe wa Al-Khalil (Hebron) na alipenda kuulinda, na alikuwa akiwapenda watu wa Al-Al-Khalil (Hebron) Khalil, na walimpenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Hivi ndivyo tunavyomwona, na Mwenyezi Mungu anamjua zaidi.

Sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarika, tunatoa rambirambi zetu kwa familia yake na jamaa zake na watu wa mji wa Al-Khalil ambao walikuwa wanamfahamu vyema Sheikh huyu. Kizazi chake miongoni mwa wazee kinakumbuka jinsi alivyokuwa akimcha Mwenyezi Mungu (swt) pekee tangu ujana wake. Siku moja alitoa Khutba juu ya mateso ya watu wa Al-Khalil, umbile la Kiyahudi ndilo lililokuwa mtawala wa moja kwa moja wa Al-Khalil wakati huo, kwa hiyo alifungwa miezi 6 kwa ajili hiyo, na akabaki hivyo baada ya kuwasili kwa Mamlaka; kwa hivyo, aliihesabu na kufichua maovu yake, na wala hakuiogopa. Mabaraza ya Marekebisho yanakumbuka uongofu wake. Mwenyezi Mungu (swt) amrehemu Sheikh Salih, na ayajaalie mabustani mapana kuwa makaazi yake. Twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aijaalie kazi yake ya kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kuwa ni mlango wa yeye kuingia peponi, na amkusanye pamoja na manabii, wakweli, mashahidi, wema na hao ndio maswahaba bora. Tunasema tu yale yanayomridhisha Mola wetu Mlezi pekee, “sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake Yeye hakika tutaregea”, na ni cha Mwenyezi Mungu alichokitoa na ni chake Yeye alichokichukua, na Mwenyezi Mungu (swt) amekipa kila kitu muda wake.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestin

Rambirambi kutoka Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/ Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina kwa Sheikh Salih Al-Razem

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu