Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  29 Rabi' I 1446 Na: 1446 / 11
M.  Jumatano, 02 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Umbile la Kiyahudi Lawaua Waislamu nchini Lebanon na Palestina Kwa Sababu ya Mwaka Mzima wa Kutochukua Hatua kwa Watawala wa Waislamu na Makamanda wao wa Jeshi

(Imetafsiriwa)

Baada ya mwaka mzima wa jinai za umbile la Kiyahudi mjini Gaza, Hezbollah ilitangaza kifo cha kiongozi wake Hassan Nasrallah mnamo 28 Septemba 2024 nchini Lebanon, katika shambulizi la anga lililotekelezwa na umbile la Kiyahudi. Kifo cha Hassan Nasrallah kilifuatia kuuawa shahidi kwa mamia ya Waislamu nchini Lebanon, huku maelfu wakijeruhiwa, katika mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na umbile la Kiyahudi. Jinai za umbile la Kiyahudi yakiwemo mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu wa Palestina na mashambulizi ya anga dhidi ya Lebanon, zimeibua wimbi la hasira na maumivu katika Umma wa Kiislamu. Ummah umetazama kwa hofu. Umeandamana mabarabarani na umehamasisha katika Ulimwengu wa Kiislamu kupinga utepetevu wa watawala wa Waislamu na makamanda wao wa jeshi. Ummah umepinga kukataa kwao kupigana na umbile la Kiyahudi. Ni kukataa huko ndiko kulikolipa ujasiri umbile hilo halifu katika jinai zake dhidi ya Umma wa Kiislamu kwa mwaka mzima sasa.

Enyi Waislamu wa Pakistan! Msidanganywe na taswira ya vyombo vya habari ya uwezo wa kijeshi wa Marekani na umbile la Kiyahudi. Kuua raia na wanachama wa wanamgambo hakuifanyi dola kuwa na nguvu kubwa ya kijeshi, au hata shujaa wa kikanda. Ndege za kivita za Marekani zinaruka kutoka kambi za kijeshi zinazotolewa na watawala wa Waislamu. Ili kulinda umbile la Kiyahudi, manuari za Amerika zinasafiri katika bahari za Waislamu, chini ya ulinzi wa majeshi ya majini ya Waislamu. Ndege za kivita za umbile la Kiyahudi zinaruka katika anga za Waislamu, kwa sababu mifumo ya ulinzi ya anga ya Waislamu haizidengui. Nguvu za jeshi la Kiyahudi hazijapingwa na jeshi hata moja la Waislamu, au hata sehemu ya jeshi moja.

Enyi Maafisa katika Vikosi vya Jeshi la Pakistan! Imepita mwaka mmoja tangu jeshi la watu waoga zaidi katika uso wa dunia kuanza mauaji ya halaiki huko Gaza. Mnawezaje bado kukubali kudhalilishwa, vifo na uharibifu kama huu uliowekwa juu ya watu wenu, mbele ya macho yenu? Vipi bado mnaweza kubaki tuli, ilhali ni kwa kupitia nguvu za mikono yenu ndipo Ummah unatafuta ulinzi wake? Je, mwanajeshi anaweza kukubali ukuu wa kijeshi wa adui yake, bila kufyatua risasi hata moja? Je, askari anawezaje kukataa kupigana na adui yake, na kudumisha Dini yake, heshima na uanaume wake imara?

Enyi Maafisa wa Jeshi la Pakistani! Mcheni Mwenyezi Mungu! Iogopeni Ghadhabu Yake (swt)! Iogopeni Jahannam ambayo Ameitayarisha kwa ajili ya walioasi na waliokataa kupigana na adui. Inukeni! Inukeni sasa! Songeni, mulipize kisasi mauaji ya kaka na dada zenu nchini Palestina na Lebanon! Wang'oeni watawala hawa ambao wamekuweka kwenye njia ya udhalilifu na uasi wa Mwenyezi Mungu (swt)! Waondoeni viongozi ambao wamekufungieni kwenye kambi zenu. Toeni Nusrah yenu kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume. Tengenezeni njia kwa ajili ya Jihad tukufu kwa ajili ya ukombozi wa Palestina na Al-Masjid Al-Aqsa, na kuangamizwa kwa umbile halifu la Kiyahudi, mikononi mwa Khalifa Rashid (Khalifa muongofu) anayekuongozeni kwenye vita. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ]

“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini.” [Surah At-Tawbah 9:14].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu