Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  11 Rabi' I 1446 Na: 1446 / 09
M.  Jumamosi, 14 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Marekani Yazipatia India na Umbile la Kiyahudi Silaha za Kisasa, Huku Ikiweka Vikwazo kwa Mpango wa Makombora ya Ballistiki wa Pakistan

(Imetafsiriwa)

Huku ikilipatia umbile la Kiyahudi silaha zenye thamani ya mabilioni ya dolari kutekeleza mauaji ya halaiki huko Gaza, Marekani inaweka vikwazo kwa dola pekee ya kinyuklia katika Ulimwengu wa Kiislamu, Pakistan. Mnamo tarehe 12 Septemba 2024, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Matthew Miller, alitoa taarifa kwa vyombo vya habari yenye kichwa, “Marekani Inaendelea Kuweka Vikwazo kwa Wasambazaji wa Mpango wa Makombora ya Ballistiki wa Pakistan.” Sera ya Marekani kwa Ulimwengu wa Kiislamu ni sera ya kuwatiisha na kuwadhalilisha Waislamu, kwa kuungwa mkono na kuwatia nguvu maadui wa Ummah. Kuhusu Pakistan haswa, Marekani inataka kuidhoofisha Pakistan ili kuruhusu India kuinuka, ili Dola hiyo ya Kibaniani iweze kukabiliana na Waislamu na China kwa niaba yake. Kwa uwazi, chini ya uongozi wa sasa wa Waislamu, mradi wa muungano na Marekani unawadhuru Waislamu na Dini yao. Kwa hivyo, je, haujafika wakati wa kuutoroka mfumo wa ulimwengu wa Marekani, kupitia mradi mpya, Khilafah Rashida, chini ya uongozi mpya, Hizb ut Tahrir?

Enyi Watu Wenye Nguvu na Ulinzi nchini Pakistani! Kwa uwazi, muungano na Amerika ni mradi wa mbaya. Ni wazi, wale wanaoshirikiana na Amerika ni uongozi mbaya. Tunakukumbusheni kuhusu vibaraka wa awali wa Marekani katika uongozi wenu Jenerali Musharraf, ambaye aliimarisha mradi wa muungano na Marekani. Mnamo tarehe 19 Septemba 2001, saa 20:30 Saa za Kawaida za Pakistan, Jenerali Musharraf alitoa hotuba kwa watu, aliyopeperushwa kupitia Televisheni ya Pakistan na Redio Pakistan. Kwa kuzingatia maandalizi ya uvamizi wa Marekani dhidi ya Afghanistan, Musharraf aliiomba Pakistan kushirikiana na Marekani. Musharraf alisema, “Katika hali hii ikiwa tutafanya maamuzi yasiyo sahihi yanaweza kuwa mabaya sana kwetu. Wasiwasi wetu muhimu ni ubwana wetu, pili uchumi wetu, tatu mali yetu ya kimkakati (nyuklia na makombora), na nne kadhia yetu ya Kashmir. Yote manne yatadhurika ikiwa tutafanya uamuzi mbaya.” Walakini, muungano na Amerika haukuiweka “Pakistan Kwanza.” Uliiweka Amerika kwanza, na Uislamu na Waislamu, mwisho. Vibaraka wa mfumo wa ulimwengu wa Amerika wameangamiza ubwana wetu na uchumi wetu. Vibaraka wa Amerika wameisalimisha Kashmir kwa Dola ya Kibaniani. Vibaraka wa ukoloni sasa wanafanya kazi ili kuunyima Ulimwengu wa Kiislamu kizuizi chake pekee cha nyuklia.

Enyi Watu Wenye Nguvu na Ulinzi nchini Pakistani! Je, Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan haikuwaonya juu ya hatari za muungano na Amerika, kwa wakati? Mnamo tarehe 22 Septemba 2001, Naveed Butt, Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan, alionya juu ya kuudhoofisha Ummah kupitia muungano na Amerika. Alisema, “Kauli mbiu za aina ya ‘Pakistan Kwanza’ zimetumika kutoa msaada kwa Marekani, kwa jina la maslahi ya kitaifa... simamisheni Khilafah ambayo itaunganisha Afghanistan na nchi nyinginezo ili Waislamu wawe Ummah mmoja kivitendo... Khilafah hii yenye nguvu haitawapinga tu maadui makafiri, itawaweka chini ya Uislamu.” [Nambari ya Toleo la Taarifa kwa Vyombo vya Habari pk01023pr]. Je, vibaraka wa Amerika waliitikia vipi onyo kuhusu muungano na Amerika, katika miaka iliyofuata? Walikawakamata Mashababu (Shabab) wa Hizb ut Tahrir. Waliwahangaisha wafanyikazi wao hadi wakawatoa kazini, wakavamia nyumba zao na kuwatesa kwa kipigo na shoti za umeme. Ama Naveed Butt walimteka nyara na amesalia kutoweka tangu Ijumaa tarehe 11 Mei, 2012. Hivyo basi, vibaraka wa Marekani wanafanya kila wawezalo kuzuia kutoroka moja kwa Waislamu kutoka kwa madhara ya mfumo wa ulimwengu wa Marekani, kusimamishwa kwa Khilafah Rashida, chini ya uongozi wa Hizb ut Tahrir.

Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Ni wakati wenu sasa wa kuachana na mradi wa muungano na Amerika, na kuzitakasa safu zenu kutokana na vibaraka wa Amerika. Imepita robo karne tangu Jenerali Musharraf aingie madarakani, Oktoba 1999, ili kuimarisha udhibiti wa Marekani nchini Pakistan. Tangu Jenerali Musharraf, vibaraka mtawalia katika uongozi wenu wameimarisha utawala wa Marekani hata zaidi. Kila mwaka unavyopita, hali ya usalama na uchumi wa Pakistan imekuwa mbaya zaidi. Jiulizeni, ni kwa kiasi gani zaidi ya ushirikiano na Amerika Pakistan inaweza kudumu? Je, hamutazingatia onyo la Mwenyezi Mungu (swt),

[إِنَّمَا يَنْهَاكُمْ اللَّهُ عَنْ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الظَّالِمُونَ]

Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” [Surah Al-Mumtahina 60:9]? Hakika, Marekani inatupiga vita na inazikalia ardhi zetu. Hakika, Marekani inawasaidia Mayahudi na Mabaniani katika kupigana nasi na kuzikalia ardhi zetu. Kwa hivyo, zingatieni onyo la Mwenyezi Mungu (swt), Mjuzi wa yote, Mwenye hekima, na chukueni hatua ya kwanza ya kivitendo ya kukata aina zote za muungano na Marekani.

Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Kateni mafungamano na makafiri na muwaunganishe waumini chini ya Khilafah Rashida. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ أَيَبْتَغُونَ عِندَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا]

Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.” [Surah An-Nisa'a 4:139]. Mradi wa Khilafah Rashida hautafuti nguvu kutoka kwa makafiri. Khilafah Rashida inaunganisha nguvu ya waumini kama dola yenye nguvu zaidi duniani. Je, Mwenyezi Mungu (swt) hakuubariki Umma wa Kiislamu kwa mamilioni ya askari, akiba kubwa ya nishati na madini, watoto wa kiume na wa kike mahiri, njia ya kufikia bahari kuu na njia muhimu za maji, na ardhi kubwa ya kilimo? Je, Mwenyezi Mungu (swt) hakutayarisha Ummah kwa ajili ya mabadiliko kupitia mtihani wa Gaza? Ummah mzima umetambua uovu wa mfumo wa ulimwengu wa Marekani. Ummah mzima unazungumza kuhusu haja ya Uislamu na umoja. Wito wa Khilafah unasikika kuanzia Indonesia hadi Morocco. Je, sio wakati muafaka kwenu kuchukua hatua ya kwanza ya kivitendo kumaliza mateso ya Ummah mikononi mwa Amerika?

Enyi Watu Wenye Nguvu, Ulinzi na Nusrah nchini Pakistan! Ni wakati sasa wa mradi mpya, Khilafah Rashida, na uongozi mpya, Hizb ut Tahrir. Uongozi wenu wa sasa unakupeni tu udhalilifu zaidi mikononi mwa Amerika. Hata hivyo, Khilafah Rashida iliangusha utawala dhalimu wa ulimwengu wa Warumi na Wafursi. Khilafah ilitawala dola zengine za ulimwengu kwa karne nyingi, ikiweka mfumo wa kimataifa kwa kuzingatia Shariah adilifu. Sasa munahitaji uongozi utakaosimamisha Khilafah Rashida, Hizb ut Tahrir. Hizb ut Tahrir imetayarisha katiba nzima yenye vifungu 191 kwa ajili ya Khilafah, ikiambatana na dalili za kiwahyi kutoka katika Quran na Sunnah. Imetayarisha maktaba ya vitabu vinavyofafanua juu ya masuluhisho ya kisiasa ya Uislamu na njia ya utekelezaji. Imetoa vikosi vya wanaume na wanawake wenye uwezo, wanaofahamu na waliojitolea katika Ulimwengu wote wa Kiislamu, waliotayarishwa kuwashauri na kuwahesabu watawala wa Khilafah. Inaongozwa na Amiri wake mmoja wa kimataifa, mwanasiasa mwenye uwezo na mwanafiqhi mkubwa, Sheikh Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah. Basi chukueni hatua ya kwanza ya kivitendo ya kuuchana mfumo wa ulimwengu wa Marekani, mupate Radhi za Mwenyezi Mungu (swt). Ipeni Nusrah yenu Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu