Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  21 Rajab 1445 Na: 1445 / 32
M.  Ijumaa, 02 Februari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watawala Duni Ruwaibidha, Wanasiasa na Makamanda wa Kijeshi Hawana Azma, Uungwana na Uanaume

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 31 Januari 2024, Jenerali Syed Asim Munir, NI (M), Mkuu wa Majeshi (COAS) aliongoza Mkutano wa 262 wa Makamanda wa Vikosi (CCC) uliofanyika Makao Makuu (GHQ), kama ilivyoripotiwa na kitengo cha habari cha jeshi, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Na PR-26/2024-ISPR. Iliripoti kwamba, "Kikao hicho kilisisitiza uungaji mkono usio na shaka kwa Palestina na watu wa Gaza huku kikibainisha matokeo mabaya sana ya mzozo huo na uwezekano wa kusambaa katika eneo hilo kubwa. Haja ya haraka ya usitishaji vita wa kudumu na suluhisho la kudumu la kadhia ya Palestina lilitambuliwa kwa kauli moja. Katika hali hiyo hiyo, azma ya Pakistan ya kuwanusuru watu wa IIOJK (Jammu na Kashmir Zinazokaliwa kimabavu kiharamu na India) kwa ajili ya haki yao ya kujitawala ilisisitizwa tena. Pakistan itaendelea kuwaunga mkono kimaadili, kisiasa na kidiplomasia ndugu na dada wa Kashmir hadi haki ipatikane kwa mujibu wa maazimio ya UNSC." Katika muktadha huo huo, na kinyume kabisa, Waislamu wa Pakistan wanapinga vikali shambulizi la mabomu la "Israel" na kuzingirwa kwa Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi, huku wakilitaka Jeshi la Pakistan litaharaki kuinusuru Gaza.

Kongamano hilo la kijeshi lilifanyika baada ya miezi minne ya mashambulizi ya mara kwa mara ya Mayahudi katika Ukanda wa Gaza, eneo lenye watu wengi zaidi duniani. Lilifanyika wakati Mayahudi wakiinyeshea kwa silaha na risasi mbalimbali za Marekani, pamoja na uhamasishaji wa kurusha makombora, ndege, na meli za kivita. Vita hivyo vimeacha makumi ya maelfu ya mashahidi, na mara nyingi zaidi ya idadi hiyo ya majeruhi. Imesababisha kuhama makaazi kwa watu wengi wa Gaza. Mayahudi wametapakaa ardhini, na wanajaza anga kwa ndege za kivita. Kongamano la kijeshi lilifanyika baada ya sauti za wafiwa kuwa kali kwa kuwaita viongozi na majeshi, hadi zikanyamaza. Hata hivyo, baada ya hayo yote, uongozi wa kijeshi wa jeshi la sita kwa ukubwa duniani bado unasisitiza msimamo wao wa kudhalilisha. Wao sio washindi wala hata kutafuta ushindi. Wanasisitiza kupuuza kwao na kujifungamanisha na adui Mzayuni na waungaji mkono wake, kwa kuendeleza mara kwa mara njama ya Marekani inayoitwa "suluhisho la dola mbili." Hakika hawana maadili yoyote, uungwana wowote, au azma yoyote ya Uislamu. Mtume (saw) amesema,

«مَا مِنِ امْرِئٍ يَخْذُلُ مُسْلِمًا فِي مَوْطَنٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَيُنْتَهَكُ فِيهِ مِنْ حُرْمَتِهِ إِلا خَذَلَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ، وَمَا مِنْ أَحَدٍ يَنْصُرُ مُسْلِمًا فِي مَوْطِنٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَيُنْتَهَكُ فِيهِ مِنْ حُرْمَتِهِ، إِلا نَصَرَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ»

“Hakuna Muislamu yeyote ambaye atamtelekeza Muislamu mwengine, ambaye amekabiliwa na hali ambayo heshima yake inavunjwa na utukufu wake unakiukwa, isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt) atamtelekeza, katika hali ambayo atakuwa na haja ya msaada Wake. Na hakuna Muislamu yeyote ambaye atamnusuru Muislamu mwengine katika hali ambayo heshima yake inavunjwa na utukufu wake unakiukwa, isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt) atamnusuru katika hali ambayo atakuwa na haja ya msaada Wake.” [At-Tabarani]

Makamanda hawa wa kijeshi na wanasiasa hawana ndani yao kuwakilisha Ummah bora zaidi ulioletwa kwa ajili ya wanadamu. Wamekosa uwezo wa umahiri wa kukabiliana na umbile ovu la Kiyahudi, ambalo mnamo tarehe 7 Oktoba lilithibitisha, bila shaka yoyote, udhaifu wake, na kuthibitisha kwamba ni simbamarara wa karatasi tu. Hakika makamanda hawa ni watawala duni wa Ruwaibidhah, ambao hawawezi kuelewa kwamba Ummah una uwezo wa kutosha kuwashinda Mayahudi, na wale waliowaunga mkono katika uvamizi wao. Hawawezi kuona "suluhisho" kwenye upeo wa macho, zaidi ya yale yaliyowasilishwa na mabwana zao wa kikoloni. Hii ni hata baada ya kuthibitika kwa kila mwenye akili timamu kuwa wakoloni ndio adui wenyewe. Imethibitishwa kwa uhakika kwamba Marekani, pamoja na taasisi za kimataifa, Umoja wa Mataifa, Baraza lake la Usalama, na Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ambayo inaongozwa na Jaji wa Marekani, Joan E. Donoghue, zote ni taasisi ambazo wanaegemea upande wa ukafiri na watu wake, wakiwemo Mayahudi. Hawajaunga mkono jambo lolote la Kiislamu tangu kuanzishwa kwao. Hata hivyo, watawala hao wanasisitiza kuendelea kuwaomba, si kwa matumaini yao kwamba taasisi hizo zitaleta ushindi kwa Waislamu katika mambo yao, badala yake ni kuwapotosha wananchi na kuwaondolea wajibu wao. Pia, makamanda hawa wa kijeshi hata hawajioni kuwa wana uwezo wa kuliongoza jeshi litakaloibuka na ushindi katika kulinda matukufu ya Uislamu na Waislamu. Wanajua vizuri kutoweza kwao kufanya hivyo, kwa sababu sio kusudi walilowekwa. Wao ni vibaraka wa nchi za Magharibi, walioteuliwa kutekeleza amri, miradi, na njama zake dhidi ya Uislamu na Waislamu. Hawana mamlaka au uwezo wa kufanya maamuzi kuhusu mambo ambayo yanakengeuka kutoka kwa maagizo ya Magharibi, na madhumuni haya. Hawawezi kamwe kunufaika au kuuokoa Ummah wa Kiislamu.

Enyi Wanajeshi wenye Ikhlasi na Maafisa wa Jeshi la Pakistan! Je! hamna nyoyo mnazoweza kufahamu kwazo, na macho mnayoona kwayo, na masikio mnayosikia kwayo? Je, hamuoni mito ya damu inayotiririka kutoka kwa Waislamu wa Gaza? Hamuoni kuenea kwa mauaji hadi vijijini, mijini na barabara kuu? Je, hamuoni kubomolewa kwa nyumba, kulipuliwa kwa hospitali, na kuzuiwa kwa magari ya kubebea wagonjwa kuwasafirisha majeruhi, au hata kuwatelekeza hadi kuuawa shahidi? Je, hamuoni kwamba ukatili wa umbile ovu la Kiyahudi umewasibu wanadamu, mawe na miti? Udhalimu wa Kiyahudi umeenea hadi Gaza na Ukingo wa Magharibi, na hata Palestina iliyokaliwa kwa mabavu mnamo 1948, kwa hivyo munangojea nini? Bila shaka munaona na kusikia yote yanayoendelea, na yote yanayotokea. Je, hakuna miongoni mwenu mtu mwenye akili timamu, atakayeongoza askari wa Kiislamu na kunusuru Uislamu na Waislamu, kwa kuliangamiza umbile la Kiyahudi linaloikalia kwa mabavu Palestina, na kuiregesha Palestina yote kwenye nyumba ya Uislamu? Ikiwa watawala madhalimu watampinga, atawafukuza kutoka nyuma. Yeyote anayengoja amri ya watawala ni sawa na yule anayenyoosha mikono yake kwenye maji, akiomba yafikie midomoni mwake, lakini kamwe hayawezi kufanya hivyo. Zaidi ya hayo, yeye ni kama mtu anayengoja ngamia aingie kwenye tundu la sindano. Watawala hao wanafuata amri za nchi za kikoloni za kikafiri zilizoanzisha dola ya Kiyahudi na kusalimisha Ardhi iliyobarikiwa ya Palestina kwake. Hakuna matumaini ya kheri kutoka kwao. Hakuna matumaini ya Jihad kutoka kwao.

Ni lazima muipe Nusrah Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Ni lazima mutoe kiapo cha utiifu cha Bayah kwa Khalifa ambaye atakuongozeni kufikia ushindi juu ya Mayahudi na wale waliofungamana nao, ili kwamba moja ya kheri mbili, ushindi au kifo cha kishahidi, iandikwe kwa ajili yenu. Je, hakuna mtu miongoni mwenu mwenye akili, anayeliongoza jeshi la Pakistan kiasi kwamba majeshi mengine yote yanamfuata yakimtukuza Mwenyezi Mungu (swt), huku Umma ikiwafuata, ukimtukuza Mwenyezi Mungu (swt) juu ya ushindi? Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ]

“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi.” [Surah Al-Ghafir 40:51]? Inatosha, enyi askari! Hakuna udhuru uliobaki kwa anayetafuta nyudhuru. Hakuna ubishi kwa mwenye kubishana na Hata ghadhabu na hasira zenu dhidi ya adui yenu hazitakushufaieni, msipochukua hatua. Badala yake, ni lazima mufanye yale aliyokuamrisheni Mwenyezi Mungu (swt), Mwenye nguvu, Mwenye hekima. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ]

“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini.” [Surah At-Tawbah 9:14].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu