Mgogoro wa Kiuchumi wa Misri, kwa kweli, ni Mgogoro wa Kimfumo Ndio Mzizi wa Maradhi na Chanzo cha Mateso
- Imepeperushwa katika Misri
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Umaskini uliokithiri, ukosefu wa ajira uliogubika, machafuko ya kisiasa na kiuchumi, utajiri wa kupindukia kwa wachache kwa gharama ya watu wengi, kushuka kwa thamani ya pauni dhidi ya fedha za kigeni kusikokuwa na kifani, kula akiba za watu, kushuka kwa kiwango kikubwa cha maisha, kuongezeka kwa kasi kwa deni la umma, kupanda kwa bei kusiko na kifani, kupuuza rasilimali za kiuchumi na kimkakati kwa ajili ya maadui wa Ummah...