Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  23 Muharram 1444 Na: 1444/01
M.  Jumapili, 21 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ardhi ya Kisiwa cha Warraq ni ya Watu na Wakaazi wake Haijuzu Kuwafukuza wala Kuwalazimisha Waiuze

 (Imetafsiriwa)

Kisiwa cha Al-Warraq ndicho kikubwa kati ya visiwa vya asili katika Mto Nile. Uamuzi ulitolewa mnamo 1998 kukichukulia kama hifadhi ya asili, na mnamo 2017, uamuzi ulitolewa na Waziri Mkuu wa kukiondoa kutoka katika uamuzi wa hifadhi za asili na kukifanya kuwa eneo la uwekezaji, na mnamo 2018 uamuzi ulitolewa kuanzisha jengo jipya la mji kwenye ardhi yake. Kwa mujibu wa maamuzi hayo, polisi na jeshi walifanya kampeni mfululizo za kubomoa nyumba za wakaazi wa kisiwa hicho, na kuchoma mazao yao ya kilimo kwa kile ilichosema ni uvamizi wa mali ya serikali.

Kwa upande mwingine, watu waliandamana kupinga kufukuzwa kwao kutoka kwa ardhi yao, na mapigano yalitokea, na watu kadhaa walikamatwa. Mnamo Disemba 2020, Mahakama ya Upeo ya Usalama wa Dola ya Jinai iliwahukumu wakaazi 35 wa kisiwa hicho kifungo cha gerezani kati ya miaka 5 na 25 kuhusiana na mapigano hayo (Al-Jazeera, 10/8/2022).

Wakati huo, tulichunguza suala hilo pamoja na hakimu ambaye wakati huo alihalalisha hatua ya serikali dhidi ya watu kwa kulazimishwa uwanjani, na kwamba serikali ina haki ya kutetea ardhi yake na kuiregesha pindi inapotokea kushambuliwa, hata kama ilikodishwa kwa baadhi ya watu au kupangiwa wawe na haki ya kuitumia, na akamalizia kwa kusema: Al-Warraq, ambacho baadhi yake kinamilikiwa na Mamlaka ya Wakfu ya Misri, na baadhi ni ya Wizara ya Kilimo na Mamlaka ya Jumuiya za Mijini. Wizara ya Unyunyiziaji maji ilikuwa na haki ya kusimamia nguvu zake na kuhifadhi mto Nile wake mkuu, na ilithibitishwa kutoka kwa nyaraka kwamba baadhi ya maskwota kwenye ardhi hii walijenga juu yake bila leseni, na walijenga kwenye eneo la Mto Nile. ” (Al-Shorouk, 12/27/2020).

Wakili wa haki za binadamu Khaled Ali alithibitisha kwamba watu wa Kisiwa cha Warraq hawakushambulia ardhi za serikali, bali walikuwa na hati miliki za ardhi na nyumba, na alichapisha kwenye ukurasa wake wa kibinafsi wa Facebook picha za mikataba ya mauzo iliyothibitishwa na leseni za ujenzi wa watu wa Warraq. (Al-Jazeera, 10/8/2022)

Kisha, Waziri wa Makao, juu ya maendeleo ya Kisiwa cha Warraq, alisema kwamba serikali inanunua kwa hiari ekari ya Kisiwa cha Warraq kwa pauni milioni 6, akielezea kuwa ubadilishanaji huo ulikuwa ekari moja ya ardhi kwenye Kisiwa cha Warraq kwa ekari 16 katika mji wa Sadat.

Wakati fulani serikali hutangaza kwamba kisiwa hicho ni mali ya serikali na kwamba ina haki ya kukiregesha kama ilivyoelezwa katika mantiki ya uamuzi uliotolewa Disemba 2020 baada ya kukiondoa kuwa hifadhi ya asili na kuwatuhumu watu wake kwa kukiuka milki ya serikali, kisha utawala unatangaza kuwa unanunua kutoka kwa wananchi kile ambacho awali ulidai kuwa ni milki ya serikali! Je, kweli ardhi ya kisiwa hicho ni mali ya serikali, tuchukulie kwamba watu wake hawana nyaraka zinazothibitisha umilikaji wao? Je, inajuzu kwa dola kuwanyang'anya kwa kisingizio cha uwekezaji na maendeleo na kuwalazimisha waiache na kujitenga nayo? Na je, serikali inapaswa kuwafanyia nini?

Kwanza: Kisiwa hiki, kama ardhi zote ambazo watu wa Misri walizihuisha, kuishi na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi chengine, ni mali ya kibinafsi kwao, iliyothibitishwa na kuilima kwao, ujenzi na makaazi yao, kwa mujibu wa Hadith ya Mtume (saw):

«مَنْ أَحْيَا أَرْضاً مَيْتَةً فَهِيَ لَهُ»

Yeyote mwenye kuihuisha ardhi iliyokufa, basi hiyo ni yake.”

Chimbuko la ardhi hiyo ni kwamba kujengwa na kuhuishwa kwake ni moja ya sababu za umiliki wake halali, jambo ambalo halikugusiwa na hakimu aliyedai kuwa ni mali ya serikali, ambayo inaweza kuwanyang’anya wananchi kinyume na matakwa yao, licha ya ukweli kwamba wanaishi juu yake na uhai wao unatokana na mazao yake.

Pili: Haijuzu kuichukua kutoka kwao ima kwa kuwatongoza au kwa nguvu au kuwalazimisha kwa kisingizio cha kuiendeleza jinsi serikali inavyodai.

Tatu: Serikali lazima iwape kila wanachoweza kwa maisha ya staha na utulivu, na ikiwa kweli inataka kuiendeleza ardhi hiyo na kuipatia huduma, ni kipi kinachowazuia kufanya hivyo?! Je, pesa nyingi na kipote cha mabwenyenye wanapaswa kuinunua ili huduma ziifikie?! Je, si wajibu wa dola kuwachunga watu wa Misri na kuwapa huduma zote na kuwapa maisha ya staha, au maisha ya staha yanategemea hadhi kulingana na kile walichonacho katika pesa na kulingana na nafasi zao madarakani na ukaribu wao na watoaji maamuzi?!

Enyi Watu wa Kisiwa cha Al-Warraq: Ni ardhi yenu; ni haki ya halali ambayo hampaswi kuipuuza, na simameni kidete mbele ya kampeni za serikali kama wajibu, na wananchi wa Misri lazima waiunge mkono haki yenu na wakuwalinda dhidi ya serikali na ukatili wake, ili muwe mkono mmoja wenye kuzuia dhulma na ulafi wa utawala huu.

Enyi Watu wa Misri Al-Kinana: Utawala unaofikiria kwa mawazo ya mfanyibiashara na mwanakandarasi hautaishia tu kwenye Kisiwa cha Al-Warraq, bali utapanuka hadi kwenye kila ardhi unaoiashiria, hata kama kuna tofauti na uwezekano wa uwekezaji, kama ilivyofanya kwa Maspero Triangale na Bustani za Al-Mamoura mjini Alexandria, na itazinyakua kwa nguvu na ulazima, na kusimama kwenu mbele ya serikali sasa na kuizuia kutokana na uvamizi na kushambuliwa kwa watu wa Al-Warraq na kuwanyang'anya ardhi yao ni wajibu wa kisheria. Na ikiwa mutawaangusha leo, utawala utakuwa peke yake na nyinyi mmoja baada ya mwingine, na siku hiyo mutasema, "Nililiwa siku ambayo ng'ombe mweupe aliliwa," na tulishambuliwa siku tulipowaacha watu wa Warraq peke yao mbele ya utawala.

Enyi Watu wa Misri, Al-Kinana: Kinachokudhaminieni uadilifu na haki ni kutekelezwa Uislamu ndani ya dola yake, Khilafah Rashida, kwa njia ya Utume. Fikra ambayo serikali inaipiga vita na wafanyikazi wake wanaipiga vita, nayo pekee ndiyo tegemeo lenu na Ummah kwa jumla, na sisi katika Hizb ut Tahrir tunabeba kwa ajili yenu mradi wake wa kihadhara uliokamilika na ulio tayari kwa utabikishwaji mara moja, kwa hiyo fanyeni kazi nasi kutabikisha Uislamu unaoregesha haki kwa watu wake na unaodhamini uadilifu kwa watu wa Al-Warraq na kwa Misri yote.

Enyi Waaminifu katika Jeshi la Kinana: Ibn Taymiyyah, Mwenyezi Mungu amrehemu, alipokuwa gerezani yake jijini Damascus, mnyongaji alimjia na kumwambia: Nisamehe ewe Sheikh, kwani nimeamrishwa. Ibn Taymiyyah akamwambia: Wallahi, lau si kwa ajili yako, wasingeli dhulumu! Naapa kwa Mwenyezi Mungu, lau sio nyinyi, utawala huu usingeliidhulumu Misri na watu wake, wala kuwatenza nguvu, wala kuwafanya watumwa kama inavyofanya hivi sasa. Wallahi mtawajibika Siku ya Kiyama, siku ambayo Mola Mlezi, Mwenye nguvu na Mtukufu atakuiteni:

(وَقِفُوهُمْ إِنَّهُمْ مَسْئُولُونَ * مَا لَكُمْ لا تَنَاصَرُونَ)

 “Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa. Mna nini? Mbona hamsaidiani?” [As-Saffat: 24-25].

Hawatakunufaisheni, sio wao wala pesa zao wala vyeo vyao na fadhila zao wanazokuvutieni nazo na kununua dini yenu, heshima yenu na fahamu zenu, basi jiandaeni siku mutakayokutana na Mwenyezi Mungu na hali watu wananing’inia katika shingo zenu wakisema, Ewe Mola Mlezi, walituangusha na kumpa nguvu adui yako na adui yetu juu dhidi yetu.

Enyi Wanajeshi Waaminifu wa Jeshi la Kinana: Wajibu wenu halali ni kuwalinda watu dhidi ya dhulma za utawala huu, kuwalinda watu kutokana nao, na kuzuia ukandamizaji wake.

Wajibu wenu wa kwanza, unaowadhaminia watu mambo yao na kuhifadhi haki na utu wao, ni kuung’oa mfumo huu kutoka katika mizizi yake pamoja na zana zake zote, nembo na watabikishaji wake, na kuwanusuru wafanyikazi kuregesha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Inayowalinda watu kutokana na ukandamizaji wa kila dhalimu na kuwarudishia utu na ushindi wao. Hii ndio dori yenu na hiyo ndio kazi yenu mtakayoulizwa kuihusu mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi fanyeni hima Mwenyezi Mungu akufungulieni, ili tuione kiuhalisi unayomridhisha Mwenyezi Mungu kwetu sote, na Misri itaangazwa kupitia nyinyi, Mwenyezi Mungu akipenda, Ewe Mwenyezi Mungu iwe haraka iwezekanavyo.

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ)

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele” [Anfal: 24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu