Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  7 Muharram 1443 Na: H.T.L 1443 / 01
M.  Jumapili, 15 Agosti 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mauaji huko Akkar - Mandhari ya Kutisha ya Kuungua Watu - Kwa sababu ya Mamlaka Fisadi na Paka Wanono Wakiritima!!
(Imetafsiriwa)

Jumapili, usiku wa manane, jeshi la Lebanon lililichukua gari moja la mafuta, au magari ya kuhifadhia mafuta yaliyokuwa tayari kusafirishwa kimagendo, katika eneo la At-Tahlil huko Akkar; jeshi liliyagawanyia watu. Inaonekana kana kwamba lori au tangi hilo la kuhifadhi lilipigwa risasi na wasafirishaji magendo, kulipuka na kuua makumi ya watu. Kwa kuzingatia mauaji haya, tunasisitiza yafuatayo:

Mamlaka hii ya fisadi ya kisiasa, kwa sababu ya ukosefu wake wa kujali maswala ya watu, kutawala kwake kwa mfumo ulioundwa na mwanadamu, kuamiliana kwake na riba, wizi wake wa pesa za umma, na ukiritimba wake, unaofanywa na paka wanono, wa nyenzo na bidhaa muhimu kwa watu, imesababisha foleni za watu kudhalilishwa kwenye sehemu za kuoka mikate, hospitali, maduka ya dawa, vituo vya gesi na vituo vya chakula. Haja yao ya mafuta iliwasukuma kuyapata kwa gharama yoyote ile.

Mauaji ya leo yangeweza kuepukwa lau mamlaka hiyo ingekuwa na hisia ya uwajibikaji! Tangu mwanzo wa mgogoro huu, ambao kila mtu anaujua kuwa moja ya sababu zake muhimu ni usafirishaji wa magendo wa bidhaa unaofanywa na paka wanono. Je! Inaingia akilini kwa gari la mafuta kuchukuliwa na kugawiwa kiholela kwa watu bila kuzingatia hatari zinazohusika?! Ni kwa nini hayakumiminwa katika moja ya vituo na kugawiwa kwa watu baada ya hapo?!

Ikiwa umiliki wa lori hili amethibitishwa kuwa mmoja wa mbunge wa jimbo hili, au wengineo, basi lazima akamatwe na awajibishwe, yeyote awaye, kwa sababu yeye ni mwizi, mkiritimba na muuaji. Ikiwa habari za kupigwa risasi kwa lori hilo ni za kweli, mtu aliyeanzisha moto huo lazima ashtakiwe.

Enyi Watu wa Lebanon:

Misiba ilikushukia mfululizo, ni wakati wenu sasa kuepukana nayo kwa kuipindua serikali nzima kuanzia kichwani hadi mguuni, kukiondoa chombo hiki kilichoshindwa na kuirudisha Lebanon kama sehemu ya Ummah, inayotawala kwa Shariah ya Mwenyezi Mungu (swt) na kushughulikia mambo ya watu kwa haki na uadilifu.

 (فَلَوْلَا كَانَ مِنَ الْقُرُونِ مِن قَبْلِكُمْ أُولُو بَقِيَّةٍ يَنْهَوْنَ عَنِ الْفَسَادِ فِي الْأَرْضِ إِلَّا قَلِيلاً مِّمَّنْ أَنجَيْنَا مِنْهُمْ وَاتَّبَعَ الَّذِينَ ظَلَمُوا مَا أُتْرِفُوا فِيهِ وَكَانُوا مُجْرِمِينَ وَمَا كَانَ رَبُّكَ لِيُهْلِكَ الْقُرَى بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا مُصْلِحُونَ)

“Basi mbona hawakuwamo katika watu wa kabla yenu wenye vyeo na wasaa wanao kataza uharibifu katika nchi, isipo kuwa wachache tu, ambao ndio tulio waokoa? Na walio dhulumu walifuata starehe zao, na wakawa ni wakosefu * Wala hakuwa Mola wako Mlezi wa kuihiliki miji kwa dhulma tu na hali watu wake ni watenda mema.” [Hud: 116-117]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu