Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  12 Jumada II 1442 Na: H.T.L 1442 / 06
M.  Jumatatu, 25 Januari 2021

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi

[كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ]

 “Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kaamili Siku ya Kiyama. Na atakaye epushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu.” [Al-i-Imran:185]

 (Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Lebanon inaomboleza kifo cha mmoja wa wanaume wake miongoni mwa wabebaji ulinganizi, Hajj Majid Zaid (Abu Rami), mkazi wa mji wa Tyre, aliyefariki alfajiri ya leo, Jumatatu, 12 Jumada al-Thani 1442 H, sawia na 25/1/2021, baada ya kuambukizwa maradhi yasiyotibika.

Na tunapojifariji sisi wenyewe, familia yake na wapendwa wake, tumwombe Mwenyezi Mungu (swt), Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu, amsamehe na amrehemu, na kumfinika kwa ukarimu na fadhila zake, kutokana na kile alichokijua Mwenyezi Mungu (swt) cha ubebaji da'wah kwa ujumla, na kazi yake katika mji wa Tyre haswa katika kuunganisha safu za Waislamu, akijitolea katika njia hiyo nafsi, wakati na juhudi zake.

Na tunamwomba Mwenyezi Mungu (swt), ayaruhusu macho yetu yashuhudiye hivi karibuni lile ambalo Hajj Abu Rami amelifanyia kazi; Dola ya uadilifu na uongofu, Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo huwaunganisha Waislamu na kuzikusanya safu zao chini ya bendera moja, bendera ya “La Ilaha Illah Allah Muhammadun Rasulullah.”

وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ * الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ * أُوْلَئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِنْ رَبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ وَأُوْلَئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ]

“…Na wabashirie wanao subiri * Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea* Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka!” [Al-Baqara: 155-157]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu