Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Kuwait

H.  3 Jumada I 1437 Na: 1437H / 02
M.  Ijumaa, 12 Februari 2016

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Watu wetu wa Syria Wametokana na Sisi na sisi tumetokana Nao, sio Fadhla wala hakuna Kufadhiliwa
(Imetafsiriwa)

Mwenyezi Mungu asema:
(إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ) “Hakika Waumini ni ndugu” [Al-Hujuraat: 10]

Na Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema:
«مَثَلُ الْمُؤْمِنِينَ فِي تَوَادِّهِمْ وَتَرَاحُمِهِمْ وَتَعَاطُفِهِمْ مَثَلُ الْجَسَدِ إِذَا اشْتَكَى مِنْهُ عُضْوٌ تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ الْجَسَدِ بِالسَّهَرِ وَالْحُمَّى» “Mfano wa waumini katika mapenzi baina yao, kuhurumiana kwao, kujaliana kwao ni kama kiwiliwili kimoja; pale ambapo kiungo kimoja chauma, basi kiwiliwili chote huumwa, kwa sababu ya kukosa usingizi na homa.” (Haina shaka)

Na (saw) alisema:
«الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ؛ لَا يَظْلِمُهُ، وَلَا يَخْذُلُهُ، وَلَا يَكْذِبُهُ، وَلَا يَحْقِرُهُ» “Muislamu ni ndugu ya Muislamu: hamkandamizi, wala hamuangushi na hamdanganyi, wala hamchukii.” (Muslim)

Na (saw) alisema:
«الْمُسْلِمُونَ تَتَكَافَأُ دِمَاؤُهُمْ، يَسْعَى بِذِمَّتِهِمْ أَدْنَاهُمْ، وَيُجِيرُ عَلَيْهِمْ أَقْصَاهُمْ، وَهُمْ يَدٌ عَلَىمَنْ سِوَاهُمْ» “Damu ya kila Muislamu ni sawa, ni wamoja dhidi ya wengine. Usalama unaopewa wa chini wao katika cheo unawafunga wao (wote), na kurudishwa kunakabidhiwa kwa wa mbali wao.” (Abu Dawoud)

Na (saw) alisema: «من لا يَرْحَمْ لاَ يُرْحَمْ» “Yeyote ambaye hasamehi hatosamehewa.” (Haina shaka)

Na (saw) alisema: «مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤْمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ اَلدُّنْيَا، نَفَّسَ اَللَّهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ يَوْمِ اَلْقِيَامَةِ» “Lau mmoja atamuondoshea Muislamu muumini moja kati ya mazito yake ya maisha ya dunia, Mwenyezi Mungu naye atamuondoshea moja katika mazito ya Siku ya Kiyama.” (Muslim)

Yanayowatokea watu wetu wa Ash-Sham hayakujificha kwa yeyote; njama za kidunia, milipuko, ulengwaji, uharibifu, ukimbizi, ufurushwaji, kudhilalishwa, usafirishaji wa watu ng’ambo na mengine mengi.
Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Kuwait tunazitaka mamlaka za nchi kuondosha vikwazo kuhusiana na makaazi ya watu wa Syria nchini Kuwait na kuwapa kila kinachohitajika katika kukaa kwao kama: nyumba, matibabu, elimu na huduma za umma (sio katika kambi huko jangwani au mipakani!) ili kuwawezesha kupata mahitaji mazuri ndani ya sekta ya umma na kibinfasi ili kufanyakazi na kupiga marufuku hukmu zote walizowekewa. Na pia tunapinga hukmu zote zinazoweka vikwazo kwa wao kubakia ndani ya nchi.

Hayo ndio matakwa yetu na sio mwito wala maombi, bali ni majukumu ya kishari’ah, ambayo (saw) alisema:

«اللَّهُمَّ مَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئًا فَشَقَّ عَلَيْهِمْ فَاشْقُقْ عَلَيْهِ، وَمَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئًا فَرَفَقَ بِهِمْ فَارْفُقْ بِهِ» “Ewe Mwenyezi Mungu, yule atakayekuwa na aina yoyote ya mamlaka juu ya mambo ya watu wangu na akawafanyia uzito, Basi mfanyie uzito juu yake, na yule atakayekuwa na aina yoyote ya mamlaka juu ya mambo ya watu wangu na akawafanyia wepesi na kuwahurumia –kuwa na huruma naye.” (Muslim)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Kuwait

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Kuwait
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu