Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Kuwait

H.  4 Safar 1438 Na: 1438 H /01
M.  Ijumaa, 04 Novemba 2016

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Nidhamu ya Kidemokrasia Inahukumu Kinyume na Aliyoleta Wahyi Mwenyezi Mungu
﴾وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللهِ حُكْماً لِقَوْمٍ يُوْقِنُونَ﴿
“Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini” [Al-Ma’ida: 50]
(Imetafsiriwa)

Nchi hivi sasa inashughulishwa kuhusiana na mwito wa uchaguzi wa wagombeaji wapya katika Baraza la Ummah, baada ya agizo kutoka kwa amiri kuvunjilia mbali baraza la awali na kuitisha uchaguzi mpya ufanyike mnamo Jumamosi, 26/11/ 2016.

Ilhali watu wanashughulika na masuala ya siasa za ndani, tungependa kuwaelekeza kwa masuala muhimu na kuyaweka wazi:

Kuhukumu kwa Shari’ah ya Mwenyezi Mungu katika mizozo baina ya watu ni wajib. Mwenyezi Mungu (swt) imelihusisha hilo na Imani, Yeye asema: ﴾فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنْفُسِهِمْ حَرَجًا مِمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا﴿ “La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utakayo toa, na wanyenyekee kabisa.” [an-Nisa’: 65]

Suala kwamba Shari’ah inajumuisha hukmu ambazo zinapangilia usimamizi wa watu na mahusiano baina ya mtawala na wanaotawaliwa, ni suala lililoko wazi na lisilokuwa na shaka
Nidhamu ya kidemokrasia inataka ubwana uwe ni wa watu, na haki ya kuhukumu na kutunga sheria iwe ni ya watu, watu wawe na haki ya kumchagua na kumuondosha mtawala, watu wawe na haki ya kutunga katiba na sheria na wawe na haki ya kuzifuta, kuzibadilisha na kuziweka sawa.

Ilhali katika nidhamu ya Kiislamu, Khilafah, ubwana ni wa Shari’ah na sio watu, wala watu au Khalifah hana haki ya utungajisheria, Mwenyezi Mungu (swt) ndiye Mtungajisheria. Watu (Ummah) hawana haki ya kumuondosha mtawala, anaondoshwa na Shari’ah, lakini Ummah una haki ya kumchagua, kwa sababu Uislamu umeyafanya mamlaka kuwa ni ya Ummah, kwa hiyo watu wanachagua mwakilishi (Khalifah) na kumpa Bay’ah.

Kwa mujibu wa nukta hii, tunasisitiza kwamba kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu kunakuja kwanza; utulivu wa kisiasa unaweza kupatikana kwa kufuata Shari’ah ya Mwenyezi Mungu na kupinga nidhamu ya kidemokrasia. Mwenyezi Mungu Azza Wa Jal alisema:﴾وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا﴿ “Na atakaye jiepusha na mawaidha Yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki.” [Ta-Ha: 124]

Kauli mbiu ya kweli inayotakiwa kunyanyuliwa na kila mtu mukhlisina anayetaka suluhisho sahihi la kisiasa lazima iwe: “Ubwana ni wa Shari’ah na Sultan (mamlaka) ni ya Ummah” Naam, ubwana ni wa Shari’ah na kila mtu amefungwa na Shari’ah na sio kinyume chake ambapo Shari’ah inapigiwa kura ya ndio au la!!

Na naam, Sultan (mamlaka) ni ya Ummah, Ummah ndio unaochagua mtawala anayetekeleza Shari’ah na kuiondosha haki hii ni uhalifu kwa sheria ya Kiislamu. Omar Bin Al-Khattab (ra) alisema, “Lau mwanamume atatoa kiapo kwa mwanamume mwengine pasina na kuwashauri Waislamu, ima yule aliyetoa au aliyepewa bay’ah hatakiwi kufuatwa, wamejitia katika hatari ya kuuliwa.”

Kitengo cha Habari cha Hizb ut Tahrir Wilayah Kuwait

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Kuwait
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu